Baljurashi
JF-Expert Member
- Dec 30, 2017
- 1,310
- 2,174
Sasa hiyo ni sababu ya kuacha mke kweli?Baada ya kuinasa amekuwa akijirushia 5,000-10,000 mara mbili kila mwezi na muda wa maongezi wa tshs 1,000-2,000 kila siku.
Mume anataka amuache sasa hivi na mimba yake akilalamika kuwa ni mwizi na asiye na shukrani kwani amekuwa akimtunzia ndugu zake na mtoto aliyemkuta kwa miaka mingi tu huku huduma akizitoa.
Lakini pia anadai kuna cases nyingi tu za ye kupoteza hela kila mara bila kuelewa, ingawa alidhani ni yeye mwenyewe tu anazipoteza lkn kwa hali hii anahitimisha kuwa itakuwa ni huyo mke aliyekuwa anamchezea michezo hiyo.
Kwakuwa siku za mwizi ni arobaini amegundua hilo juzi tu baada ya kutumiwa hela ya mtu huku salio likiwa hilo tu, sasa kila akijaribu kutoa anaambiwa salio halitoshi. Alipowapigiwa huduma kwa wateja wakawa wanamwambia mbona umetoa hela mwenyewe. Sasa alipochukua taarifa za miamala ndipo alipokutana na hayo. Mke alikuwa anafuta jumbe zote anazofanya miamala mume asione.
Mimi nimemwambia amwache, tena leo usiku huu huu kwani sio mtu wa kawaida huyo dada.......huwezi kujua ameshamdanganya mangapi na amepanga mangapi dhidi yake! Vipi wadau nimeshauri vibaya?!!!!!