Ladslaus Modest
JF-Expert Member
- Jun 27, 2008
- 635
- 20
Angalia hapa:
http://www.cms.ccmtz.org/doc/KATIBA.pdf
http://www.cms.ccmtz.org/doc/KATIBA.pdf
Acheni kumtetea fisadi namba moja wa Tanzania aliyeigeuza Ikulu kuwa soko la kufanyia biashara zake za kifisadi!
Hapa mtu hanishawishi hata kama ni kwa data kutoka kuzimu! Matatizo yote tunayoyapitia Watanzania kwa kwa sasa yamesababishwa na Mkapa. Kama Mtanzania unategemea nini kama mafisadi wote wakiongozwa na kinara wao Mkapa walikuwa wamehodhi uchumi wote wa nchi?
Kesi zote za ufisadi zilizoko Mahakamani zinamgusa Mkapa moja kwa moja. Anzia kwa kina marehemu Balali na wapambe wake kina Liumba na sakata la EPA na Twin Towers mpaka madudu ya Mgodi wa Kiwira. Njoo kwa kina Mramba,Yona na madudu ya Sterwat.Njoo kwa kina Kagoda na Meremeta na Deep Green(CCM). Njoo kwa kina Chenge na vijisenti vya Rada na Ndege ya Rais Mkapa ambapo Watanzania tuliambiwa tule nyasi ili ndege ya Mkapa inunuliwe!
Njoo kwenye mikataba mabomu ya madini yetu,mbuga zetu za Wanyama na upuuzi mwingine wote ambao amabo ulifanywa na Mkapa na wote tu mashahidi!!
Naamini kabisa kama Mkapa alikuwa kiongozi makini Tanzania kwa sasa uchumi wetu ungelikuwa mbali sana. Anagnlieni jamani wenzetu pale BOTSWANA. Wao wa nini cha zaidi kuliko sisi? Uchumi wa Botswana ni wa kupigiwa mfano katika Afrika nchi ambayo inategemea ALMASI NA NG'OMBE tu. Tanzania tuna DHAHABU kwa wingi,tuna TANZANITE(madini pekee duniani yanayopatikana Tanzania),tuna ALMASI,tuna GESI,n.k na n.k.
Lakini kutokana na sera na mikataba mibovu alizotengeneza Mkapa akisaidiana na Chenge madini yote haya hayatusaidii Watanzania kwa lolote.Leo nimesikia wale jamaa Kampuni ya Resolute wanaochimba madini kule Tabora wameshaanza kujiandaa kuondoka baada ya kuona Dhahabu zimeanza kwisha!!!!!
Mwaka 2012 wanaondoka na kutuachia MASHIMO!!!Hayo ndiyo matunda aliyoyuletea Njomba Nkapa mnayetaka kumtetea kuwa alifanya mazuri!!!Yaapi hayo????
Nitaendelea.
Ndicho ninachokisema kwenye post yangu hapo juu!
BOTSWANA WAO WAMEWEZAJE? KWANINI SISI HATUWEZI?..BOTWASNA NI NCHI NDOGO SANA, INA RASILIMALI CHACHE UKILINGANISHA NA SISI, IWEJE WAO WAWEZE KUWA HAPO WALIPO?
SOLUTIONS PLEASE - WE ARE TIRED OF ANALYSIS!
Rais mstaafu Benjamin Mkapa.
Rais mstaafu Benjamin Mkapa, amesema yote yanayosemwa juu yake, anamwachia Mungu.
Alisema lakini yeye (Mkapa) katika siku za karibuni, hajawahi kusemwa kwa mazuri wala kusifiwa lakini yote anamwachia Mungu.
Mkapa amekuwa akituhumiwa kutumia vibaya madaraka yake kwa kujimilikisha mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya bila kufuata taratibu na kwa bei ya kutupa.
Inadaiwa kuwa alishirikiana na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini katika serikali yake, Daniel Yona, kujimilikisha mgodi huo kwa Sh. milioni 700 badala ya thamani yake halisi ya Shilingi bilioni nne.
Hata hivyo, licha ya kujimilikisha kwa gharama ndogo, pia inadaiwa kuwa waliishia kulipa Sh. milioni 70 tu.
Chanzo: IPP Media Web
Wewe makaye hata wewe uliwa rais huwezi kupitia kila kitu cha nchi hii unless uvunje safari na kila kitu ukae tu ofisini,mkapa tries his best lakini wasidizi wake nao walimuangusha na mjue mkapa sio mwanasheria hawezi kuelewa kirahis legal tems unless sahivi ajiriwe mwanasheria special na mwaminifu kwaajili ya kumtafsiria rais mikataba na kila kitu cha kisheria.wewe mwenyewe mkeo anaweza akawa analala na houseboy wako au mdogo wako na usijue sembuse mambo ya mikataba.simtetei mkapa ila tuongea vitu vya maana sometime ndio maana hata habari za kiwila siongelei kwasababu hiyo ile kweli alafanya makusudi.
Halafu mi nadhani baada ya kupiga kelele nyingi ohoo mkapa sasa tukubali yameshatokea tunafanya nini sasa????kama inawezekana kuvunja hito mikataba kwa gharama yeyote tufanye natujue vipi tunaingia mikataba yenye tija kwetu sio kila siku mara mkapa sofia simba sijui rostam mi naona ni kupoteza muda viongozi wetu ni kama sikio la kufa jamani.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Kidumu Chama Tawala hadi miisho ya Nyakati
CCM ni Nambari Wani.
Wewe makoye hata wewe uliwa rais huwezi kupitia kila kitu cha nchi hii unless uvunje safari na kila kitu ukae tu ofisini,mkapa tries his best lakini wasidizi wake nao walimuangusha na mjue mkapa sio mwanasheria hawezi kuelewa kirahis legal tems unless sahivi ajiriwe mwanasheria special na mwaminifu kwaajili ya kumtafsiria rais mikataba na kila kitu cha kisheria.wewe mwenyewe mkeo anaweza akawa analala na houseboy wako au mdogo wako na usijue sembuse mambo ya mikataba.simtetei mkapa ila tuongea vitu vya maana sometime ndio maana hata habari za kiwila siongelei kwasababu hiyo ile kweli alafanya makusudi.
Halafu mi nadhani baada ya kupiga kelele nyingi ohoo mkapa sasa tukubali yameshatokea tunafanya nini sasa????kama inawezekana kuvunja hito mikataba kwa gharama yeyote tufanye natujue vipi tunaingia mikataba yenye tija kwetu sio kila siku mara mkapa sofia simba sijui rostam mi naona ni kupoteza muda viongozi wetu ni kama sikio la kufa jamani.
Baba unaamini MABADILIKO yataletwa na masanduku yetu haya ya kura?
NANYI MTAIFAHAMU HIYO KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU
.........yataletwa na sisi wenyewe nna wala sio maboksi yetu
Ukiangalia Tanzania Tunalipa kodi kubwa sana na Hasa sisi wafanyakazi, ukitaka kujua kodi tunazolipa usiangalie kwenye mshahara peke yake, angalia na kwenye matumizi. Ki msingi wengi kama mjuavyo kwenye mfumo wa kodi wa kitanzania upo kwa ajili ya kumnyonya mfanyyakazi zaidi kuliko Mfanyabiashara. Wafabiashara wanakwepa kodi,wafanyakazi hawana ujanja wa kukwepa kodi.
Mkuu hebu jaribu ufanye biashara , hata ukiweka kiduka, ndo utamjua PILATO.
Hivi wafanyakazi nchi nzima wa sekta zote wako wangapi?
Hivi wanafika milioni 2? kati ya waTanzania 40 million