Rais Dkt. Mwinyi ahimiza kuhifadhi Quran na kufundisha

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
742
479
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Waumini wa Dini ya kiislamu kuendelea kuhifadhi Quran Tukufu na kufundisha watoto wao kuisoma na pia wazidishe kutoa sadaka kwa watu wenye mahitaji hususani katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo katika fainali za 24 za Mashindano ya Quran Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al Hikma Foundation kwa kushirikisha nchi mbalimbali 22 za Afrika na nje ya Afrika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam tarehe 24 Machi, 2024.

Aidha Rais Dk. Mwinyi amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano na kuzidi kupiga hatua za maendeleo nchini.

Kwa upande mwingine Rais Dk. Mwinyi ameipongeza Taasisi ya Al Hikma Foundation kwa kuandaa mashindano hayo makubwa ambayo yanaitangaza Tanzania kwa kushirikisha nchi mbalimbali. Pia ameipongeza Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa kuyadhamini mashindano hayo kila mwaka.

Mshindi wa kwanza wa Mashindano hayo ni Ibrahim Sow wa Ivory Coast aliyepata shilingi milioni 27, mshindi wa pili Haafith Abdulkariim Kabiito kutoka Uganda shilingi milioni 17.2 , mshindi wa tatu Kamil Almin Swaleh kutoka Tanzania shilingi milioni 11.6, mshindi wa nne Kamilou Koura kutoka Togo shilingi milioni 8.1 na mshindi wa tano Idris Nshimwe kutoka Burundi shilingi milioni 4.5
IMG-20240324-WA0029.jpg
IMG-20240324-WA0026.jpg
IMG-20240324-WA0025.jpg
IMG-20240324-WA0024.jpg
IMG-20240324-WA0027.jpg
IMG-20240324-WA0023.jpg
 
Faida yake huwa ni nini? Hv nchi kama Pakistan, Afghanistan, Iran, Morocco huwa zinafanya haya Mambo?
Morocco nchi ya kiarab inaongoza Afrika kwa kuuza na kutengeneza magari na vipuri, sasa badala ya zenj kuomba na wao watengenezewe viwanda, vya kutengeneza vipuri tu, hata TAA za mbele za landcruser, zote zitoke Zenj, wao wanaomba Masada wa kukalili msaafu!
Ukitaka kujua balaa, Pendekeza kwa china na wao wafanye mazoezi ya kukalili msaafu! Ndio utajua mchina ni nani!
 
Kukariri ,ku cram . Shule tulikatazwa mfumo wa kukariri sio mfumo wa elimu hauupi.ubongo uwezo wa kujitegemea
 
Faida yake huwa ni nini? Hv nchi kama Pakistan, Afghanistan, Iran, Morocco huwa zinafanya haya Mambo?
Morocco nchi ya kiarab inaongoza Afrika kwa kuuza na kutengeneza magari na vipuri, sasa badala ya zenj kuomba na wao watengenezewe viwanda, vya kutengeneza vipuri tu, hata TAA za mbele za landcruser, zote zitoke Zenj, wao wanaomba Masada wa kukalili msaafu!
Ukitaka kujua balaa, Pendekeza kwa china na wao wafanye mazoezi ya kukalili msaafu! Ndio utajua mchina ni nani!

nilijua tu mtakuja kumwaga mapovu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom