Mkapa: Yote yanayosemwa juu yangu namuachia Mungu

Acheni kumtetea fisadi namba moja wa Tanzania aliyeigeuza Ikulu kuwa soko la kufanyia biashara zake za kifisadi!

Hapa mtu hanishawishi hata kama ni kwa data kutoka kuzimu! Matatizo yote tunayoyapitia Watanzania kwa kwa sasa yamesababishwa na Mkapa. Kama Mtanzania unategemea nini kama mafisadi wote wakiongozwa na kinara wao Mkapa walikuwa wamehodhi uchumi wote wa nchi?

Kesi zote za ufisadi zilizoko Mahakamani zinamgusa Mkapa moja kwa moja. Anzia kwa kina marehemu Balali na wapambe wake kina Liumba na sakata la EPA na Twin Towers mpaka madudu ya Mgodi wa Kiwira. Njoo kwa kina Mramba,Yona na madudu ya Sterwat.Njoo kwa kina Kagoda na Meremeta na Deep Green(CCM). Njoo kwa kina Chenge na vijisenti vya Rada na Ndege ya Rais Mkapa ambapo Watanzania tuliambiwa tule nyasi ili ndege ya Mkapa inunuliwe!

Njoo kwenye mikataba mabomu ya madini yetu,mbuga zetu za Wanyama na upuuzi mwingine wote ambao ulifanywa na Mkapa.Watanzania wote tu mashahidi!! Naamini kabisa kama Mkapa alikuwa kiongozi makini Tanzania kwa sasa uchumi wetu ungelikuwa mbali sana. Angalieni jamani wenzetu pale BOTSWANA. Wao wana nini cha zaidi kuliko sisi? Uchumi wa Botswana ni wa kupigiwa mfano katika Afrika nchi ambayo inategemea ALMASI NA NG'OMBE tu. Tanzania tuna DHAHABU kwa wingi,tuna TANZANITE(madini pekee duniani yanayopatikana Tanzania),tuna ALMASI,tuna GESI,tuna MBUGA ZA WANYAMA,tuna MIFUGO n.k na n.k.

Lakini kutokana na sera na mikataba mibovu alizotengeneza Mkapa akisaidiana na Mwanasheria wake Chenge madini yote haya hayatusaidii Watanzania kwa lolote.Leo nimesikia wale jamaa wa Kampuni ya Resolute wanaochimba madini kule Tabora wameshaanza kujiandaa kuondoka baada ya kuona Dhahabu zimeanza kwisha!!!!!

Mwaka 2012 wanaondoka na kutuachia MASHIMO!!!Hayo ndiyo matunda aliyoyuletea Njomba Nkapa mnayetaka kumtetea kuwa alifanya mazuri!!!Yaapi hayo????

Nitaendelea.
 
Acheni kumtetea fisadi namba moja wa Tanzania aliyeigeuza Ikulu kuwa soko la kufanyia biashara zake za kifisadi!

Hapa mtu hanishawishi hata kama ni kwa data kutoka kuzimu! Matatizo yote tunayoyapitia Watanzania kwa kwa sasa yamesababishwa na Mkapa. Kama Mtanzania unategemea nini kama mafisadi wote wakiongozwa na kinara wao Mkapa walikuwa wamehodhi uchumi wote wa nchi?

Kesi zote za ufisadi zilizoko Mahakamani zinamgusa Mkapa moja kwa moja. Anzia kwa kina marehemu Balali na wapambe wake kina Liumba na sakata la EPA na Twin Towers mpaka madudu ya Mgodi wa Kiwira. Njoo kwa kina Mramba,Yona na madudu ya Sterwat.Njoo kwa kina Kagoda na Meremeta na Deep Green(CCM). Njoo kwa kina Chenge na vijisenti vya Rada na Ndege ya Rais Mkapa ambapo Watanzania tuliambiwa tule nyasi ili ndege ya Mkapa inunuliwe!

Njoo kwenye mikataba mabomu ya madini yetu,mbuga zetu za Wanyama na upuuzi mwingine wote ambao amabo ulifanywa na Mkapa na wote tu mashahidi!!
Naamini kabisa kama Mkapa alikuwa kiongozi makini Tanzania kwa sasa uchumi wetu ungelikuwa mbali sana. Anagnlieni jamani wenzetu pale BOTSWANA. Wao wa nini cha zaidi kuliko sisi? Uchumi wa Botswana ni wa kupigiwa mfano katika Afrika nchi ambayo inategemea ALMASI NA NG'OMBE tu. Tanzania tuna DHAHABU kwa wingi,tuna TANZANITE(madini pekee duniani yanayopatikana Tanzania),tuna ALMASI,tuna GESI,n.k na n.k.

Lakini kutokana na sera na mikataba mibovu alizotengeneza Mkapa akisaidiana na Chenge madini yote haya hayatusaidii Watanzania kwa lolote.Leo nimesikia wale jamaa Kampuni ya Resolute wanaochimba madini kule Tabora wameshaanza kujiandaa kuondoka baada ya kuona Dhahabu zimeanza kwisha!!!!!

Mwaka 2012 wanaondoka na kutuachia MASHIMO!!!Hayo ndiyo matunda aliyoyuletea Njomba Nkapa mnayetaka kumtetea kuwa alifanya mazuri!!!Yaapi hayo????

Nitaendelea.


Ndicho ninachokisema kwenye post yangu hapo juu!
BOTSWANA WAO WAMEWEZAJE? KWANINI SISI HATUWEZI?..BOTWASNA NI NCHI NDOGO SANA, INA RASILIMALI CHACHE UKILINGANISHA NA SISI, IWEJE WAO WAWEZE KUWA HAPO WALIPO?
SOLUTIONS PLEASE - WE ARE TIRED OF ANALYSIS!
 
Ndicho ninachokisema kwenye post yangu hapo juu!
BOTSWANA WAO WAMEWEZAJE? KWANINI SISI HATUWEZI?..BOTWASNA NI NCHI NDOGO SANA, INA RASILIMALI CHACHE UKILINGANISHA NA SISI, IWEJE WAO WAWEZE KUWA HAPO WALIPO?
SOLUTIONS PLEASE - WE ARE TIRED OF ANALYSIS!

Tuwaige GHANA yule kiongozi alitumia mbinu nzuri kupambana na rushwa na ni nchi inayosifika Africa. Mawaziri wao wanapanda hadi daladala ili kupata adha watu wanayoipata ili wajue namana ya kutatua tatizo hilo kwa haraka.
 
Hakuna mtu hata mmoja anamtetea mkapam kweli amefanya makosa lakini mkapa ni moja ya marais bora waliowahi kutawala africa sio hutu vasco dagama wenu kila siku safarini ndio maana anaanguka jukwaani.mimi nadhani hiyo kusema aseme anaiachia mahakama na sio mungu nadhani siyo jukumu lake ni la serikali kumkamata na kumfikisha mbele ya vyombo vya sheria,halaf hivi watu kama huyu mwanakijiji huwa nadhani wanaandika vitu bila kufikiria na kama kweli unauchungu na nchi yako ungerudi huku huko kwa watu unafanya nini au ndio dalili za kuvua uzalendo mzee tuambie?????
 
Wewe makaye hata wewe uliwa rais huwezi kupitia kila kitu cha nchi hii unless uvunje safari na kila kitu ukae tu ofisini,mkapa tries his best lakini wasidizi wake nao walimuangusha na mjue mkapa sio mwanasheria hawezi kuelewa kirahis legal tems unless sahivi ajiriwe mwanasheria special na mwaminifu kwaajili ya kumtafsiria rais mikataba na kila kitu cha kisheria.wewe mwenyewe mkeo anaweza akawa analala na houseboy wako au mdogo wako na usijue sembuse mambo ya mikataba.simtetei mkapa ila tuongea vitu vya maana sometime ndio maana hata habari za kiwila siongelei kwasababu hiyo ile kweli alafanya makusudi.

Halafu mi nadhani baada ya kupiga kelele nyingi ohoo mkapa sasa tukubali yameshatokea tunafanya nini sasa????kama inawezekana kuvunja hito mikataba kwa gharama yeyote tufanye natujue vipi tunaingia mikataba yenye tija kwetu sio kila siku mara mkapa sofia simba sijui rostam mi naona ni kupoteza muda viongozi wetu ni kama sikio la kufa jamani.
 
Mkapa%285%29.jpg

Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Rais mstaafu Benjamin Mkapa, amesema yote yanayosemwa juu yake, anamwachia Mungu.


Alisema lakini yeye (Mkapa) katika siku za karibuni, hajawahi kusemwa kwa mazuri wala kusifiwa lakini yote anamwachia Mungu.

Mkapa amekuwa akituhumiwa kutumia vibaya madaraka yake kwa kujimilikisha mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya bila kufuata taratibu na kwa bei ya kutupa.

Inadaiwa kuwa alishirikiana na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini katika serikali yake, Daniel Yona, kujimilikisha mgodi huo kwa Sh. milioni 700 badala ya thamani yake halisi ya Shilingi bilioni nne.

Hata hivyo, licha ya kujimilikisha kwa gharama ndogo, pia inadaiwa kuwa waliishia kulipa Sh. milioni 70 tu.

Chanzo: IPP Media Web

Huyu BWM kweli kwenye oungozi wake kuna mazuri aliyofanya. Lakini kwa yale maovu aliyo fanya itabidi tu awajibike tu na asimshirikishe Mungu katika hili kwani akumhusisha katika maovu yake.
Abebe Msalaba wake mwenyewe.
 
Wewe makaye hata wewe uliwa rais huwezi kupitia kila kitu cha nchi hii unless uvunje safari na kila kitu ukae tu ofisini,mkapa tries his best lakini wasidizi wake nao walimuangusha na mjue mkapa sio mwanasheria hawezi kuelewa kirahis legal tems unless sahivi ajiriwe mwanasheria special na mwaminifu kwaajili ya kumtafsiria rais mikataba na kila kitu cha kisheria.wewe mwenyewe mkeo anaweza akawa analala na houseboy wako au mdogo wako na usijue sembuse mambo ya mikataba.simtetei mkapa ila tuongea vitu vya maana sometime ndio maana hata habari za kiwila siongelei kwasababu hiyo ile kweli alafanya makusudi.

Halafu mi nadhani baada ya kupiga kelele nyingi ohoo mkapa sasa tukubali yameshatokea tunafanya nini sasa????kama inawezekana kuvunja hito mikataba kwa gharama yeyote tufanye natujue vipi tunaingia mikataba yenye tija kwetu sio kila siku mara mkapa sofia simba sijui rostam mi naona ni kupoteza muda viongozi wetu ni kama sikio la kufa jamani.

1st bold - hapa umenichekesha sana. Kutokujua sheria is not an excuse.Kuteua AG aliyemuamini na hatimaye kumuingiza mkenge- the blames falls in him squarely.
2nd bold - tuko pamoja.
 
Anabakia Kuwa Raisi imara zaidi katika kuleta maendeleo ya kuonekana hapa nchini.

Kuanzia barabara, afya, elimu, mawasiliani, uchumi mkuu, maji, na ujenzi wa taifa la kujisimamia kimaendeleo..

Kikubwa ni KIONGOZI MWENYE UTHUBUTU KATIKA KUAMUA NA KUTEKELEZA..Alizungukwa na wasaidizi na jamii isiyotambua dhana ya kuona mbali na kutenda kwa uthubutuuu..

Nitamuheshimu DAIMA KAMA KIONGOZI WA WAKATI WAKE ALIYETUWEKA KATIKA RAMANI YA KIMATAIFA KIMAENDELEO.
 



Kidumu Chama Cha Mapinduzi

Kidumu Chama Tawala hadi miisho ya Nyakati

CCM ni Nambari Wani.

Ladi mkuu, sisi sote ni wana CCM, lakini hii yako imepitwa na wakati.
Inaitwa parroting, kasuku.
Hii mwachie Komba, he is paid for that.Kama na wewe unalipwa kwa hilo ,fine.
Ukumbi huu weka argument na mantiki ya argument hiyo, full stop.
 
Tatizo la watanzania wengi hawafahamu nini wajibu wa kiongozi, tunapoona baadhi ya mambo yamefanyika tunafikiri kwamba ile ni favour au ni jitihada ya kiongozi mmoja peke yake , siyo kweli.Tunapomchagua kiongozi tunatarajia kwamba atafanya kwa kiwango kinachotakiwa, na wala siyo afanye baadhi ya mambo na mengine hayaache.Kwa mfano suala la ujenzi wa barabara ni la muhimu na ndiyo maana tuna wizara ya ujenzi na idara kama TANROADS. LENGO LAKE NI KUWA NA MIPANGO YA KUENDELEZA MIUNDO MBINU. Ukiangalia Tanzania Tunalipa kodi kubwa sana na Hasa sisi wafanyakazi, ukitaka kujua kodi tunazolipa usiangalie kwenye mshahara peke yake, angalia na kwenye matumizi. Ki msingi wengi kama mjuavyo kwenye mfumo wa kodi wa kitanzania upo kwa ajili ya kumnyonya mfanyyakazi zaidi kuliko Mfanyabiashara. Wafabiashara wanakwepa kodi,wafanyakazi hawana ujanja wa kukwepa kodi. Kwa hiyo turitarajia kuwa tunachagua kiongozi wa kutuletea maendeleo,Ni kwa Vipi ujenzi wa barabara viwanja vya michezo na kadhalika uwe favour? Siyo favour bali ni wajibu uliotufanya tuwachague.Wanapoingia mikataba mibovu gharama yake tunalipa sisi wafanyakazi wa Tanzania wenye mishahara midogo yenye kodi nyingi. Msisahau kuwa manufaa makubwa wanayapata wageni kuliko Watanzania, serikali haijaweka mazingira mazuri ya mfanyakazi wa kitanzania ulkilinganisha na wale Wageni wanaoingia akwa kivuli cha jina la EXPERT wakati hakuna hiyo expert ndani yake, Ni viongozi hao hao ndio wanashirikiana na wageni kuwanyanyasa watanzania wenzao halafu mnasifia hapa mnasifia kitu gani? Ubabe wa Mkapa na Kauli zake tata? Nakubaliana na alichosema askofu Mokiwa leo atubu kwa Watanzania.
 
Na Waandishi wetu
20th November 2009
B-pepe
Chapa
Maoni
Sasa aomba Watanzania wampime
Ajigamba alichapa kazi akiwa Ikulu
Aambiwa aombe radhi asamehewe
Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.

Kuna kila dalili kwamba Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, ameanza kulegea juu ya msimamo wake wa kutokujibu tuhuma dhidi yake za kupoteza uadilifu akiwa madarakani.

Hatua ya Mkapa kujitokeza hadharani juzi kwenye mkutano wa taasisi yake ya Benjamin William Mkapa HIV/Aids Foundation na kusema kwamba yote anayotuhumiwa kwayo anamwachia Mungu, na jana kuibuka tena kusema kwamba wananchi wanapaswa kupima wenyewe kama alifanya kazi au la, ni mwendelezo wa kusaka suluhu ya makombora ambayo yameelekezwa kwake kwa takribani miaka minne sasa.

Jana Mkapa aliendeleza wimbi la kujisafisha baada ya kuwataka Watanzania wapime wenyewe kama alifanya kazi nzuri katika uongozi wa miaka 10 ama alivurunda.

Kadhalika, aliwashambulia wanasiasa wanaosema kwamba Tanzania haina dira.

Mkapa, kiongozi aliyekuwa akitoa kauli kali za kutisha si kwa viongozi wenzake tu akiwa madarakani bali hata wananchi huku akijinasibisha kuwa ni kiongozi mkweli, jana alijitetea tena baada ya kuulizwa swali kama alisimamia misingi tisa ya maadili ya uongozi akiwa Rais wa nchi.

Mkapa alisema anaona kuwa alifanya kazi nzuri, lakini Watanzania wanaweza kupima wenyewe kuhusu utendaji wake.

Swali hilo liliulizwa na Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ambayo ipo chini ya Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Nicholas Kingazi.

Mkapa alisema: “Huwezi kuzuia masikio kusikia lakini unaweza kuzuia mdomo kuzungumza.”

Kabla ya kuanza kuzungumza katika mkutano huo, Mkapa aliuliza kama kulikuwa na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam ambako mkutano wa Taasisi yake ya Benjamin Mkapa Foundation ulikuwa ukifanyika kuanzia juzi hadi jana.

Baada ya kuuliza swali hilo, watu walicheka na yeye akasema kuwa kicheko hicho kiliashiria wapo.

Akizungumza na washiriki wa mkutano huo, Mkapa alisema kiongozi makini ni lazima ajue mahitaji muhimu ya watu wake anaowaongoza katika nchi yoyote duniani.

Kuhusu wanasiasa wanaosema Tanzania haina dira, alisema madai hayo hayana ukweli.

Mkapa alisema Tanzania ina dira ya maendeleo ya mwaka 2025 tofauti na wanasiasa wanavyosema.

Akizungumzia suala la ugonjwa wa Ukimwi ambao taasisi yake inapambana nao, alisema bado fedha zinazotengwa na serikali katika sekta ya afya hazitoshi.

Alisema azimio la Abuja linasema ifikapo mwaka 2025 kila nchi katika bara la Afrika iwe na uwezo wa kutenga asilimia 15 ya bajeti yake katika afya ambapo hivi sasa serikali inatenga silimia 11. Alifafanua kuwa taasisi yake imejiwekea malengo ya kupambana na Ukimwi kwa vitendo nchini na kwamba kila mmoja anahusika katika kupambana nao.

Mkutano huo wa siku mbili uliomalizika jana ulihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa, wasomi, vijana na wanaharakati wa masuala ya Ukimwi.

Juzi jioni, akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, alisema kuwa mambo yote yanayosemwa juu yake anamwachia Mungu.

Hii ni mara ya tatu Mkapa kujitokeza hadharani kujitetea dhidi ya tuhuma zake. Miaka miwili iliyopita akiwa kijijini kwake, Lupaso, Mtwara, Mkapa alisema habari zote zinazoandikwa na magazeti dhidi yake ni za uongo na aliwataka wananchi wazipuuze ikiwa ni pamoja na kuyachanachana magazeti hayo.

Hata hivyo, mbinu hizi mpya za Mkapa zimepingwa na Mbunge wa Kishapu, (CCM), Fred Mpendazoe na Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Willbroad Slaa.

Wabunge hao wamemweleza Mkapa kuwaomba radhi Watanzania kwa maovu yaliyofanyika chini ya utawala wake.

Akizungumza jana na Nipashe, Mpendazoe alisema Mkapa akiomba radhi anaweza kusamehewa na Watanzania ambao wengi wanaendelea kuathiriwa na maamuzi yaliyofanywa na serikali yake.

"Naamini nusu ya Watanzania bado wanampenda sana Mkapa, nilishamshauri ajitokeze na kuomba radhi ili apate heshima maana ni kawaida mtu akiomba msamaha anasamehewa, lakini kusema unamwachia Mungu tu haitoshi," alisema.

Mpendazoe aliorodhesha baadhi ya madudu yaliyofanywa na serikali ya Mkapa iliyoanzia 1995-2005, kuwa ni pamoja na uuzwaji wa Benki ya NBC, wizi wa Sh. bilioni 133 katika Akaunti ya Malipo ya Mapeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kampuni iliyochota mabilioni BoT ya Kagoda, mikataba mibovu ya madini na uuzwaji holela wa nyumba za serikali.

Alitaja tuhuma nyingine kuwa ni pamoja na uuzwaji wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira ambapo yeye (Mkapa), alishirikiana na aliyekuwa Waziri wake wa Nishati na Madini, Daniel Yona kujiuzia.

Alisema hivi sasa Watanzania wanayajua hayo yote hivyo akitaka yaishe na kusahaulika ni vyema akasimama hadharani na kukiri kuwa yalitokea kimakosa na aombe radhi.

"Asipofanya hivyo hata wajukuu zetu watampa shida kwa maana watakapowaona wajukuu wa Mkapa na wenzake walionunua nyumba zile wanaishi maisha mazuri wanaweza hata kuwapiga mawe maana watasema nyumba hizo waliuziwa kifisadi," alisema.

Mpendazoe alisema wanaosema Mkapa aachwe apumzike hawamtakii mema maana maamuzi aliyofanya akiwa madarakani bado yanawaumiza Watanzania wengi.

Kwa upande wake, Dk. Slaa alisema msimamo wake kuhusu Mkapa ni ule ule kwamba awaombe msamaha Watanzania kwa aliyoyafanya akiwa Ikulu.

"Anasema anamwachia Mungu? Mbona Mungu yuko mbali, kwa nini asianze na sisi wa karibu yake kwa kutuomba msamaha kwa maovu aliyotufanyia?” Alihoji na kuongeza: “Hata Mungu anasema mpende jirani yako kama nafsi yako.”

Dk. Slaa alisema kuna usemi kuwa: “msema kweli ni mpenzi wa Mungu hivyo kama kweli Mkapa ni mpenzi wa Mungu anapaswa kueleza ukweli wa maovu yake akiwa Ikulu ndipo asamehewe.”

"Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere wakati akimnadi Mkapa mwaka 1995, alikuwa akisisitiza kuwa watu wasikimbilie Ikulu maana lile si pango la walanguzi sasa huyu (Mkapa) aliyempeleka akaigeuza Ikulu pango la walanguzi," alisema Dk. Slaa, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chadema.

Alisema baadhi ya watu wanaweza kudhani kuwa Mkapa anaonewa, lakini kinachotafutwa hapo ni uadilifu wa viongozi wanapokabidhiwa dhamana ya kuongoza nchi.

Mkapa alisema juzi kuwa mlolongo wa tuhuma zinazotolewa dhidi yake anamwachia Mungu.

Aliyasema hayo wakati akimkaribisha Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein, kufungua mkutano wa pili wa mwaka wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/AIDS, unaofanyika jijini Dar es Salaam.

"Ninashukuru kwa yote yanayosemwa juu yangu na wanaotamka hayo ni watu makini wenye kufanya hivyo kwa tafsiri zao," alisema na kuongeza kuwa hahitaji kufafanua jambo hilo.

Kiutendaji mkapa ni better off kuliko Kikwete kwasababu alikuwa na msimamo na akichapa kazi tatizo ni kwamba haya madudu alikwiba au hajakwiba??? na kutuomba msamaha haitoshi arudishe hela zetu ndio tutamsamehe na sio msamaha tu haitoshiiii!!!! mkubwa
 
Wewe makoye hata wewe uliwa rais huwezi kupitia kila kitu cha nchi hii unless uvunje safari na kila kitu ukae tu ofisini,mkapa tries his best lakini wasidizi wake nao walimuangusha na mjue mkapa sio mwanasheria hawezi kuelewa kirahis legal tems unless sahivi ajiriwe mwanasheria special na mwaminifu kwaajili ya kumtafsiria rais mikataba na kila kitu cha kisheria.wewe mwenyewe mkeo anaweza akawa analala na houseboy wako au mdogo wako na usijue sembuse mambo ya mikataba.simtetei mkapa ila tuongea vitu vya maana sometime ndio maana hata habari za kiwila siongelei kwasababu hiyo ile kweli alafanya makusudi.

Halafu mi nadhani baada ya kupiga kelele nyingi ohoo mkapa sasa tukubali yameshatokea tunafanya nini sasa????kama inawezekana kuvunja hito mikataba kwa gharama yeyote tufanye natujue vipi tunaingia mikataba yenye tija kwetu sio kila siku mara mkapa sofia simba sijui rostam mi naona ni kupoteza muda viongozi wetu ni kama sikio la kufa jamani.

Ikivilinge,

Kwenye management kuna kitu kinaitwa MBWA(Management By Walking Around). Kama Rais unapaswa kupitia kila sehemu siyo kukaa ofisini na kusubiri kuletewa rushwa,posho na hongo ili kutoa vibali vya kuuza nchi kama alivyofanya Rais wako Mkapa. Bado kuna maeneo Mkapa alikuwa akienda anapoona kuna ulaji(ufisadi)!

Tunaona Kikwete ana-practice hiyo MBWA. Mkapa alishindwa nini? Mbona alikwenda kule Bulyanhulu akapewa pande la Dhahabu?Mkapa hawezi kujitetea kwa lolote wala wale mnaomtetea haitasaidia. Mkapa ni FISADI tu mpaka kufa.

Sana sana wanaomtetea ni wale wakereketwa wa CCM au wale walionufaika na ufisadi kutoka kwake kwa namna moja au nyingine.
CCM yafaa tuibatize na kuipa jina la CHAMA CHA MAFISADI. Hili ni jina linalowafaa sana hawa jamaa kwa sasa.

Kwa taarifa yako Mkapa hana ubora wowote wa Urais katika karne hii hata Mo Ibrahim analijua hilo ndiyo maana alimtema kwenye kuteua Rais bora katika Afrika. Ninashangaa sana mtu anaposema eti Mkapa ni mojawapo ya Marais bora Afrika!! Kwa ubora upi hasa? Kama hata jumuia za Kimataifa zinashindwa kumtambua kama Rais Bora wewe unayosemaje kuwa ni Bora???

Kama kuna jumuia zingine za kimataifa wanaomuona Mkapa ni bora ni wale waliofaidika na utawala wake. Makampuni ambayo yamewekeza kwenye madini ili kuvuna Dhahabu na Almasi zetu ndo wanaomwona ni kiongozi bora, nje ya hapo Mkapa ni Rais BOMU kabisa katika kizazi hiki na karne hii.

The Way forward au kile tunachotakiwa kufanya ni kuipiga chini CHAMA CHA MAFISADI-CCM! Ili tuweze kuweka utawala wa chama kingine chenye mtazamo hasi na CCM. Haiwezekani CCM tangu TANU waendelee kuitawala nchi hii kana kwamba wana hati miliki ya Nchi hii. HAIWEZEKANI asilani.

Kumbukeni kuwa chama chochote kikishakaa madarakani kwa muda mrefu kinabweteka na kujisahau. CCM sasa hivi wamefulia wamebaki jina tu. Lazima waondoke Ikulu wapishe vyama vingine vyenye sera na mwelekeo tofauti ili kuikwamua nchi hii kutoka katika lindi la ufisadi na umaskini uliokthiri.

Lazima tujifunze toka kwa nchi zilizoendelea kama Uingereza, Marekani,Ufaransa,Ujeremani n.k.kuwa kila baada ya Chama kuongoza kwa muda fulani lazima chama kingine kichukue nafasi ili kuleta mabadiliko katika nyanja tofauti tofauti ambazo chama kilichotangulia kilishindwa kuleta mabadiliko na hasa mabadiliko ya kimaendeleo. Kosa tunalofanya Wa-tz ni kung'ang'ania kuchagua CCM kila mwaka. Chama ambacho kina sera na mipangi ileile ya miaka nenda rudi! Viongozi walewale,sera zilezile,sura zilezile,ufisadi uleule,ngojera ni zilezile hakuna jipya.

Sasa tunatakiwa Wa-tz tusema kuwa CCM basi imetosha. WE NEED CHANGE WHICH WE CAN BELIEVE IN kama alivyokuwa akitamka Rais wa Kwanza mweusi katika Taifa kubwa lenye nguvu duniani yaani USA mheshimiwa Barack Obama Onyango.

Kwa situation tuliyofikia Watanzania kwa sasa Change is inevitable and Change is a must. Nguvu ya sanduku la kura inatakiwa iamue na ituletee mabadiliko katika uchaguzi huu unaokuja wa 2010.
 
Nadhani Mkapa anaomba msamaha kiutu uzima. Tuzipime tu kauli zake, tuangalie na mengine mazuri aliyotufanyia kama Taifa. Mama Anna Mkapa amechangia pakubwa kumbomoa Rais wetu Mstaafu.
 
Baba unaamini MABADILIKO yataletwa na masanduku yetu haya ya kura?


















NANYI MTAIFAHAMU HIYO KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU
 
Ukiangalia Tanzania Tunalipa kodi kubwa sana na Hasa sisi wafanyakazi, ukitaka kujua kodi tunazolipa usiangalie kwenye mshahara peke yake, angalia na kwenye matumizi. Ki msingi wengi kama mjuavyo kwenye mfumo wa kodi wa kitanzania upo kwa ajili ya kumnyonya mfanyyakazi zaidi kuliko Mfanyabiashara. Wafabiashara wanakwepa kodi,wafanyakazi hawana ujanja wa kukwepa kodi.

Mkuu hebu jaribu ufanye biashara , hata ukiweka kiduka, ndo utamjua PILATO.
Hivi wafanyakazi nchi nzima wa sekta zote wako wangapi?
Hivi wanafika milioni 2? kati ya waTanzania 40 million
 
Its pity kati ya yote mema aliyo yafanya Mkapa watu wameona uwanja mpya wa taifa tu!

Huu ni upofu usio yumkinika lakini si shangai hilo kwani hao wanaodai hayo wapo Detroit kwenye comfort zone zao.

Wataonaje barabara za viwango vya lami, vituo vya afya, maboresho ya maslahi serikalini (zamani watu walikimbia kufanya kazi serikalini siku hizi kila mtu anataka) maboresho ya vitendea kazi serikalini magari, samani nk. Miradi mikubwa ya kama daraja la Mkapa, mradi wa maji kutoka ziwa Victoria Shinyanga, uchumi kuimarika. Inflation to go down to single digit, mipango ya MMES, TASAF, MKUKUTA, MKURABITA nk if you know them.

Na mengine kadhaa wa kadhaa lakini ma pundit wa JF wameona uwanja wa taifa tu loo shame on you! Mkapa atabaki kuwa miongoni if not only the best President taifa letu limepata kuwa nae.
 
Mkuu hebu jaribu ufanye biashara , hata ukiweka kiduka, ndo utamjua PILATO.
Hivi wafanyakazi nchi nzima wa sekta zote wako wangapi?
Hivi wanafika milioni 2? kati ya waTanzania 40 million


Nimeshawahi kufanya biashara nyingi , Na nimeshakuwa kwenye Makampuni , hili ninalokuambia ndiyo hasa Mtaji wa Wafanyabiashara wengi na hata juzi nilikuwa nazungumza na mmoja wa marafiki zangu ambaye ni mfanyabiashara mzuri. Kwamba udanganyifu ndio mtaji wa Wafanyabiashara wengi. Haijalishi Idadi ya Wafanyakazi kiasi cha kodi ni kikubwa na hilo ni dhaili kabisa. Na haina longolongo Taxed at Source thats all.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom