kaangwa
JF-Expert Member
- Jan 30, 2011
- 644
- 192
kuchukua tahadhali siyo woga,mabo yaliyotokea mwanza na Arusha Arumeru ambapo m/kiti wa CDM aliuawa na wabunge wa CDM kule mwanza kuumizwa linanipa picha kwamba hata hizi tetesi zinaweza kuwa kweli.Ni kosa kubwa mlinzi wa duka kuambiwa kuwa kuna watu wamesikika wakipanga kuvamia duka akapuuza na baadaye wezi wakaja kweli na kumdhuru,lakini akichukua tahadhari hata wasipokuja haina madhara maana kuimarisha ulinzi ni jukumu lake hata asipoambiwa.
Angalia mkakati uliopo wa kuwazulia kesi makamanda wetu,Kama usalama wataifa ni kweli wako pamoja na CDM kesi ya makongolo na Mpendazoe jimbo la segerea matokea yamekuwaje? Vipi kesi ya Lema? Angalia kesi nyingine za kizushi kama ile iliyomkabili Tundu Lisu,Mnyika N.K: mimi naomba wakati huu sio wa kupuuza jambo lolote kila jambo lichukuliwe kwa umakini mkubwa na hata kama jambo litakuwa si la kweli lithibitishwe na utafiti na siyo maneno tu.Jamvi hili ni la watu wote,wenye nia njema na CDM na hata wenye nia mbaya.Huenda wanaokanusha niwale wenye nia mbaya ili uhaini huu usifanyiwe kazi na hatimaye lengo la uhalibifu litimie namna ya kuwatambua ni kwa utafiti na si vinginevyo.Nani alijua kuwa wabunge watano tu CCM ndio wanaopinga ufisadi kiukweli kwa kusaini karatasi ya zito,Wakati wanaochangia miswada kwa jaziba mpaka wanatokwa na povu wako lukuki.kama siyo kipimo cha MH,Zitto tulidhani tuna makamanda wengi lkini ikathibitika kuwa wengi wao ni maneno tu walipopewa changamoto ya kuchukua hatua ya kuiwajibisha serikali.
Ni kweli wapo watumishi wengi serikalini wenye mapenzi mema na CDM lakini hilo lisifanye idara za usalama za CDM kulala ndiyo maana kuna msemo unaosema "KUVAA VAZI LA KONDOO KUMBE NDANI NI MBWA MWITU WAKALI".uzushi na ukweli ubainishwe na utafit na si vinginevyo
Mungu ibariki tanzania na wote wenye nia safi kwa nchi hii.