Sheria haioni ndani kweli pesa. Mawakili wetu wanajua kuchangamkia fursa. Ndio maana Magu alikuwa hataki ujinga
Jamaa walikuwa wanavuta muda kidogo watanzania wasahau
Tafuta pesa sana Utaipenda hii nchi. Kesi ni Biashara nzuri Tanzania
Sasa mngefanyaje kwa mfano?
 
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemkuta hana hatia Miriam Steven Mrita, mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha, bilionea Erasto Msuya hivyo ameachiwa huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yake.

Miriam pamoja na mshitakiwa mwenzake, Revocatus Everist Muyella, maarufu kama Ray, walikuwa wanakabiliwa na shitaka la mauaji ya kukusudia, wakidaiwa kumuua kwa kumchinja Aneth Elisaria Msuya ambaye ni wifi yake Miriam.

Miriam na mwenzake Muyella walidaiwa kutenda kosa hilo la mauaji ya kukusudia Mei 26, 2016 huko nyumbani kwa Aneth Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Hukumu ya kesi hiyo ya jinai namba 103 ya mwaka 2018, imetolewa leo Februari 23, 2024 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Pia soma:
Hakimu anapomuachia mtuhumiwa hua anataja na "grounds“ alizotumia to make such decisions. Yaan vipengele vilivyompa doubt ni vipi.

Huyu wa hii kesi alisemaje kwani?
 
Hakimu anapomuachia mtuhumiwa hua anataja na "grounds“ alizotumia to make such decisions. Yaan vipengele vilivyompa doubt ni vipi.

Huyu wa hii kesi alisemaje kwani?
Huo ndo ulipaswa kuwa mjadala, watu wanaongozwa na hisia!
 
Shida sio kakolaki.

Kakolaki ni mzoefu kwenye kesi za jinai kafanya miaka mingi tangia akiwa wakili aa serikali , kapitia pia tume ya kupambana na madawa ya kulevya, huko ndiko anakopajua.

Tatizo lipo kwenye upepelezi, haufanyiki vizuri, niliwahi kushauri hapa na pia tume ya haki iliyoundwa na kumpa ripoti Rais Samia ilikuja na maoni kama hayo kuwa iundwe taasisi maalum ya upelelezi wa makosa ya jinai.

Bila kufanya hivyo tutarudi hapa kulaumiana kila siku.
Kesi ya Mbowe afande Kingai na wenzake wapelelezi wabobezi yaani ndio wanategemewa na jeshi ila waligeuka kituko mbele ya mahakama
 
Back
Top Bottom