Mjadala wa Elimu Live Nkhrumah leo

Waridi

JF-Expert Member
Mar 30, 2008
1,025
172
Naam wakuu,
Mjadala kuhusu elimu na mustakabali wa Taifa unaendelea sasa hivi katika ukumbi wa Nkrumah. Vile vile uko live ITV na radio one. Tufuatulie
 
katibu wa udasa bwana faraja amemkaribisha mwenyekiti wa udasa kwa ajili ya kufungua. ameomba siasa zisitawale mjadala, bali maslahi ya taifa.
 
mwenyekiti wa udasa Dr. Francis kafungua tayari kwa kumkaribisha mtoa mada wa kwanza Prof. Mosha mtaalam wa mipango ya elimu
 
mgogoro uliokao katika elimu ni mgogoro wa kimfumo. mtaala ungetolewa na kusambazwa, vitabu wa kiada na ziada vingekuwa bora, ukaguzi ufanyike na mitihani iendane na mtaala - mosha
 
waliopata three na four wapewe remedial sasa hivi- mosha
 
mgogoro wa pili ni kuporomoka kwa ubora. anatoa takwimu za kila mwaka
 
tatizo letu nini
1. upungufu wa walimu (anatoa takwimu) msingi hadi vyuo vikuu
 
Nimesikia serikali ina mpango wa kupunguza pass mark ya kwenda kidato cha tano kutoka div 1-3,na badala yake sasa hivi mpaka div 4 wenye div 4 ya pts 26-29 wanaweza kupata nafasi ya kidato cha tano.
 
tunapeleka wenye ufaulu wa chini kwenye mafunzo ya ualimu - mosha
 
Namuona Professa Mosha anashusha data hapo, alikua Mwalimu wangu huyo kwenye Masters
 
walimu wa shule ya msingi wanafundisha masomo yote hata yale waliyofeli
 
mishahara ni midogo, licha ya udogo inacheleweshwa na wana madeni yao hayalipwi
 
walimu wana mazingira magumu sana ya kazi. ofisi zao ni chini ya miti na wengine kwenye corridor
 
Back
Top Bottom