Elimu ya Tanzania ina shida gani? Eti Physics, Kiswahili na Geography nayo ni combination moja

Nesi mkunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2022
701
1,842
Lengo ni nini? Haya maamuzi yamefanyika kwa kushirikisha wataalamu kweli? Tunakusudia kujenga taifa la aina gani? Mtu akisoma Physics, Kiswahili na Economics (PKE) anaadaliwa kuwa nani? Au anayesoma Chemistry, Comerce na Mathematics (CCM) mnamuandaa kuwa nani kama sio kuwa chawa?

Nadhani idadi ya combination haijawahi kuwa tatizo katika elimu. Tatizo kubwa ni namna ya kuimpact knowledge kwa wanafunzi. Yani mwanafunzi akipata A ya History ukiongea nae uione hiyo A imekaa kichwani. Kwa sasa mwanafunzi anaweza kupata A ya History lakini hajui chochote kuhusu Chief Kimweri wala Maumau war. Unajiuliza hiyo A kapataje?

Au mtoto kapata A ya English lakini hajui hata SVOCA analysis ni kitu gani. Kuna mmoja alikua na B ya Biology lakini haelewi kitu kuhusu Cross genetics. Nikawa nazungunza nae kuhusu autosomal dominant na autosomal recessive akawa ananiangalia kama vile naimba tenzi za rohoni. Haelewi.

Kwahiyo serikali ingejikita kuimpact knowledge kwa vijana. Kuhakikisha vijana wanasoma na kuelewa na sio kukariri. Kuongeza idadi ya combinations ni kuwapotezea watoto focus. Mtoto akichagua kusoma History, Biology na Comerce (HBC) anajiandaa kuwa nani, kama sio kumpotezea focus? Nani aliwaambia tatizo la elimu nchi hii ni idadi ya combination? Acheni kucheza na alimu ya nchi kwa sababu za kisiasa?

Mungai alifuta michezo mashuleni, hadi leo athari zinaonekana. Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISETA hayana tena msisimko kama enzi zamani. Wakati ule wachezaji wanachukuliwa kutoka UMISETA na kusajiliwa ligi kuu saivi hakuna tena. Kawambwa akaunganisha Physics na Chemistry kuwa somo moja. Mwingine akaja akafuta masomo ya biashara na kilimo Olevel. Sasa mmekuja na combinations 65 A Level. Yani kila Waziri anachezea elimu vile anavyojisikia.

Shughulikeni na matatizo ya msingi ya elimu. Ajirini walimu wa kutosha, walipeni vizuri, jengeni madarasa ya kutosha, boresheni mitaala ya elimu, wekeni usimamizi mzuri kuhakikisha elimu inampact knowledge kwa mwanafunzi. Hayo ndio mambo ya msingi yanayoweza kumsaidia mtoto kitaaluma, sio kuongeza combination. Acheni kushohiya.!
 
Back
Top Bottom