Mjadala: Gharama na njia nafuu za kujenga nyumba ya kuishi Tanzania

Kinacho tucost ni kampani zetu au makundi ya marafiki au maswahiba, mi nakueleza marafiki ndio kila kitu ukipata wala bata basi swala la kujenga kukumbuka itakuwa shida.

Nyumba ni maamuzi tu, sababu nyumba haizuii wewe kufanya mambo mengine. Unapunguza starehe huku nyumba unajenga kidogo kidogo.

Pia usitake kujua gharama ya mwisho ya ujenzi mtu alitumia, we amua kwa kuchukua hatua kusema nataka kujenga. Utajenga na hadi utakapo fika uwezi amini ulipo toka.

Namshukuru Mungu nna miaka 28 nna kakibanda ambacho nitakaa na kuwaza hela ya kula tu.
 
hahaha umenichekesha sana

Hapa ni Tanzania, siyo ughaibuni ingawa hata wao uchumi ukienda mrama kidogo wengi hujikuta hawana pa kuishi kutokana na kushindwa kulipa mortgage tofauti na Mtanzania aliyejenga mwenyewe. Sekta ya nyumba za kupanga haieleweki kabisaa hasa kwa sisi wa daraja la chini la kati (lower middle) na la chini. Kodi ya nyumba inategemea hali ya mwenye nyumba. Akipata mchepuko au akitaka kucheza binti anapandisha kodi. Akitaka kupangisha nyumba yake kwa laki 4 madalali wanamwambia laki 6 ili 10% yao iwe kubwa. Acha huko uswahili kwenye mazingira machafu, nyumba mbovu, vyoo vya kushea..... Bado utakiwe kulipa kodi ya mwaka mzima mara moja wakati wewe kipato unaingiza kwa siku au kwa mwezi. Kesho tingatinga au tetemeko likipitia nyumba au ukapata uhamisho huwezi kurudishiwa hela yako. Watanzania wenye uchumi mdogo kujenga hatupendi, bali tunalazimishwa na mazingira. Kutokuwepo kwa usalama kwenye nyumba za kupanga ni sababu kubwa mojawapo. Lakini pia Mtanzania hata mwenye take-home ya milion 3 hatoshelezi vigezo vya kununua nyumba ya kueleweka ya NHC labda zilizojengwa madongo kuinama. Kwa kipato chake hicho anaweza kujijengea nyumba yake kwa savings na personal loans akamaliza. Sasa mwambie mtanzania ambaye hana hakika na mahali pa kulala kuhusu uwekezaji wa hela yake. Umwambie afanyeje, aishi wapi wakati anaikuza hela yake imzalishie faida ndo ajenge au kununua nyumba.

ma-injinia wana bei za ajabu ajabu wakati fundi juma bei poa ukiwa 7m unajenga nyumba ya sebule, jiko, vyumba viwili vya kulala na parking ya gari.
 
Salaam jf.
Leo nimeona nilete hiki kitu huenda ndio kwanza nimewashtua watu kutoka katika usingizi mzito wa kusahau kutokana na presha za kisiasa na misukosuko ya kiuchumu, hasira za kugongwa na nyoka wa kijani na uchovu wa kuzuia ukuta uliotaka kuanguka.
Wito wangu wote kwa wale waliojisahau kununua kieneo hata cha mguu mmoja ili wazibe njia wapate hata mahala pa kujiegesha. Na uzi huu ni hasa kwa wale vijana wetu ambao wengi sana ni wale ambao wameajiriwa au hata kujiajiri wenyewe na hasa wale wanaokaa maeneo ambayo viwanja hakuna mfano Kinondoni,o'bay,msasani, sinza na yanayofanana na hayo ambao wale pesa wanapata japo kidogo lakini huzitumia kwa sababu maeneo yanawaruhusu (wasio taka kuhama kisa anakaa na msanii jirani).

Wito:
Vijana tafuteni vijieneo jamani huko mbele mambo magumu itafika kipindi hali ya kimaisha itakuwa mbaya mtu unawezashindwa hata shilingi 500 kwa siku. Haya mambo ya nywele nyeupe na kijani yapo tu miaka yote mtafanya.View attachment 398692
kwanza vijana shida yao kubwa ni kupata ajira iwawezeshe kupata mkate wao wakila siku na pesa yakulipia pango la chumba kw kila mwezi, ambaye ni vigumu kumudu vitu hivyo na ukisema wajiajiri, sekta ya kujiajiri sasa hivi wadau wamekuwa wengi wanunuzi ni wachache, sasa kwa mantiki hiyo ya kununuwa viwanja, ni vigumu kwao kumudu kununua hata ukubwa wa sentimiter moja kutokana pesa hawana
 
Hii imekaa sawa kweli? ina maana kwa nyumba ya vyumba 5 alioulizia mkuu inaweza kuwa around Tzsh 25 - 30 Million?.

Hii ukikadiria kwamba kila chumba kitakuwa na ukubwa wa 10 square meters. ((10 x 5) x 500,000) = 25,000,000.

Kwa utaratibu huu mbona gharama zitakuwa ni ndogo ukilinganisha na gharama tunazozisikia kila siku?
kabisa mkuu
 
utakuwa hujamuelewa jamaa. Huo uwekezaji wa nyumba ni mzuri kama tayari umeshakamata hela na una uwezo wa kuendesha maisha bila tatizo. kibaya hapa ni mtu ambae bado hajaiona future yake itakuwaje halafu inatokea anapambana kupata Milioni 60 either kwa kukopa au namna nyingine halafu anajenga nyumba ya milioni 60 then anapata kodi ya sh laki mbili kwa mwezi na anakosa hata hela ya kuishi vizuri au hata kulipa ada ya watoto wapate elimu bora. Ndio maana tunasema sisi watanzania tunapaswa kujua namna bora ya kupata hela ya uhakika kabla ya kukimbilia kuwekeza. unawekeza nini mkuu wakati huna kitu? kama tungekuwa na elimu bora ya kujiajiri wenyewe pamoja na kujiamini milioni 30 mtu anaweza akaizungusha na ndani ya miaka miwili huyu mtu anageuka kuitwa tajiri mtaani na mafanikio yake yanaonekana. wewe na nyumba yako ya milioni 60 unabaki unapiga mahesabu ya kuikarabati kama sio kuiuza.
Nimekuelewa sana mkuu
 
Bora niendelee kupanga, na ningejua ndivyo hiyo pesa ningeongeza mtaji kwa biashara yangu ningepata pesa zaidi ambazo zingenipa uhakika wa kilipa kodi, leo nimezika pesa chini, nabaki na hasira kama vile nilitumwa kumbe ni dhamira nzuri ila mipango mibovu
 
Ni bora uwashauri vijana kutafuta hela na vyanzo vya uhakika vya mapato. kujenga nyumba sio issue ni utamaduni tu wa muafrica kwa vile waafrica wengi huko mbele ni giza maana watu hawataki kuwa na vyanzo vya uhakika vya kukupa hela uile hadi siku unakufa. hata ukijenga nyumba kama huna hela huko mbeleni utaiuza tu na usipoiuza wewe wataiuza wanao! ukiwa kinganganizi hutaki kuiuza watakuua kwaza ili waiuze. :)
..... duuuuu umeongea maneno frani kuntu ambayo watu wachache wameelewa... usipouza wewe watauza watoto.. so inabidi uandae mazingira yako na ya watoto wako...
 
Hii estimate ni sahihi??!

Stucture yangu ni 10x11=110sqm. X500,000=55,000,000. This isn't realistic in a Tz context. Mimi nimejenga kwa 15mil tu. Kama hizo ndo estimate mnazofanya kwenye miradi ya serikali ndo maana hatuendelei.
Wew kama una uhalisia ivi zingine naona promo na kukatishana tamaa
 
Wakuu msaada bei ya tofali zuri la kuchoma kwa Arusha ni kiasi gani?
 
Hii imekaa sawa kweli? ina maana kwa nyumba ya vyumba 5 alioulizia mkuu inaweza kuwa around Tzsh 25 - 30 Million?.

Hii ukikadiria kwamba kila chumba kitakuwa na ukubwa wa 10 square meters. ((10 x 5) x 500,000) = 25,000,000.

Kwa utaratibu huu mbona gharama zitakuwa ni ndogo ukilinganisha na gharama tunazozisikia kila siku?
MKUU NAONA KAMA ITAKUA ((10X10X5)X500,000) JIBU SILIJUI
 
Back
Top Bottom