Mjadala: Gharama na njia nafuu za kujenga nyumba ya kuishi Tanzania

Hapana mkuu, ulijibu vizuri sana, niliona watu wanavunja wengine moyo pasi na hoja yenye mashiko, ulijibu vyema sana vipi ulishamaliza hiyo project yako?
Yeah, kuna watu wanatuogopesha kwa kutoa figures ambazo kwa kweli kijana anajiuliza hivi nitashika lini 30m nianze kujenga, kumbe mtu anaweza kufanya kwa steps tu; foundation, walls then anapaua. Ujenzi hauishi, nipo mahali navuta pumzi, uzuri niko na bright lady Patience123.
 
Salaam jf.
Leo nimeona nilete hiki kitu huenda ndio kwanza nimewashtua watu kutoka katika usingizi mzito wa kusahau kutokana na presha za kisiasa na misukosuko ya kiuchumu, hasira za kugongwa na nyoka wa kijani na uchovu wa kuzuia ukuta uliotaka kuanguka.
Wito wangu wote kwa wale waliojisahau kununua kieneo hata cha mguu mmoja ili wazibe njia wapate hata mahala pa kujiegesha. Na uzi huu ni hasa kwa wale vijana wetu ambao wengi sana ni wale ambao wameajiriwa au hata kujiajiri wenyewe na hasa wale wanaokaa maeneo ambayo viwanja hakuna mfano Kinondoni,o'bay,msasani, sinza na yanayofanana na hayo ambao wale pesa wanapata japo kidogo lakini huzitumia kwa sababu maeneo yanawaruhusu (wasio taka kuhama kisa anakaa na msanii jirani).

Wito:
Vijana tafuteni vijieneo jamani huko mbele mambo magumu itafika kipindi hali ya kimaisha itakuwa mbaya mtu unawezashindwa hata shilingi 500 kwa siku. Haya mambo ya nywele nyeupe na kijani yapo tu miaka yote mtafanya.View attachment 398692
Boss..point yako ni ipi? Umeongea the obvious. Sawa na kusema mtu akifa hapumui.
 
Yeah, kuna watu wanatuogopesha kwa kutoa figures ambazo kwa kweli kijana anajiuliza hivi nitashika lini 30m nianze kujenga, kumbe mtu anaweza kufanya kwa steps tu; foundation, walls then anapaua. Ujenzi hauishi, nipo mahali navuta pumzi, uzuri niko na bright lady Patience123.
Nyumba ni stages tu kama unavyosema ila vijana wengi huwa wanafikiria mpaka awe na milion 10 ndo anaanza na hapo ndio wengi hukata tamaa maana anashangaa milioni 10 inayeyuka fyuuuuuu alafu anarudi kuwatisha watu, lakini mzee wa kumwaga mchanga, anavuta anamwaga kokoto analeta tofari alafu analeta fundi hata kama atatumia 10 milion kwa hatua flani akirudi atatia watu moyo tofauti na aliejengea bank alaf akaibuka kitu kikawa level ile ile
 
Kwa mfumo mbadala wa majitaka waone kampuni ya Riflo. Unaweza kugoogle kwa maelezo zaidi. Mfumo salama, hutakaa unyonye majitaka wala kusikia harufu yoyote na bei zao za vifaa na ufundi kama utanunua mawe lori 1 na kuchimba mashimo mwenyewe haizidi milion 1.
 
Watanzania bwana wanachowaza ni jambo moja kwa wote ndo maana maendeleo yanachelewa hiv ni nani aliotuambia kujenga ndio maendeleo au mtu kuwa na kiwanja ndo maendeleo. Unaweza ukawa na nyumba na ukawa maskini mkubwa au usiwe nayo pia ukawa maskini vile vile. Wafundishe watu mbinu za kupata pesa kuenga au kuto kujenga first ni hobbi ya mtu but sec ni matter of time. Viwanja au kadhalika sio utajiri. Kikubwa ni uwezo wa kujisaidia na kusaida ndugu zako pale wanapoitaji msaada wako so poloopolojo tu kla ukiombwa pesa na huku unajisifu unanyumba. Miaka ya kuishi tu ni tatizo. Upendo kwa ndugu umepungua. Wape watotowako uridhi usiohamishika na wao wanaweza kufanya yao kwa usahh zadi kuliko nyumba.

Mtazamo tu sio ugomvi.
 
Ni jambo jema sana kwa kijana kufikiria kujenga. Kwa hali ya maisha inavyokwenda sasa, kujenga ndio mpango wa BUSARA zaidi.
Kijana anza na chochote, tafuta kiwanja hata kama ni kipande kidogo sana.

Kumbuka kuwa gharama za kununua kiwanja leo na kujenga nyumba ni Nafuu zaidi kuliko itakavyokuwa Kesho. Hii ni kanuni ya kudumu.
 
Naweza kukubaliana na wewe iwapo utanipa uwekezaji mbadala wa ardhi na nyumba, baada ya hapo nami nitajenga hoja kwanini uwekezaji wa ardhi na nyumba ni muhimu
utakuwa hujamuelewa jamaa. Huo uwekezaji wa nyumba ni mzuri kama tayari umeshakamata hela na una uwezo wa kuendesha maisha bila tatizo. kibaya hapa ni mtu ambae bado hajaiona future yake itakuwaje halafu inatokea anapambana kupata Milioni 60 either kwa kukopa au namna nyingine halafu anajenga nyumba ya milioni 60 then anapata kodi ya sh laki mbili kwa mwezi na anakosa hata hela ya kuishi vizuri au hata kulipa ada ya watoto wapate elimu bora. Ndio maana tunasema sisi watanzania tunapaswa kujua namna bora ya kupata hela ya uhakika kabla ya kukimbilia kuwekeza. unawekeza nini mkuu wakati huna kitu? kama tungekuwa na elimu bora ya kujiajiri wenyewe pamoja na kujiamini milioni 30 mtu anaweza akaizungusha na ndani ya miaka miwili huyu mtu anageuka kuitwa tajiri mtaani na mafanikio yake yanaonekana. wewe na nyumba yako ya milioni 60 unabaki unapiga mahesabu ya kuikarabati kama sio kuiuza.
 
Nimemuelewa sana, nami niliomba anipe mbadala wa nyumba anaofikiria ni investment bora zaidi.
 
Huyo mzee kuna uwezekano mkubwa hajajenga kwasababu ya hao hao watoto, leo hii wanamuona mzigo. Huo ni ubinafsi tu. Kuna wazee waliwekeza kwenye vibanda badala ya elimu ya watoto,sasa hivi watoto mateja/vibaka wanawasubiria wafe wauze nyumba!

Na hapa ndipo wengi wnapo fail, yani shule watotto hawajenda na kibanda hakijaisha, chezea maisha ewe, masha ni timing kwa nini ulazimishe?
 
Nimemuelewa sana, nami niliomba anipe mbadala wa nyumba anaofikiria ni investment bora zaidi.

Nyumba kibongo bongo ni Liabilitie, gaharama za kuitunza kwa vyovyote ni kubwa, pili inategemea na kipato chako, kma ni cha kuunga unga ni bora ukawezkeza kwenye Elimu yako au ya wanao, afya yako ay ya familia, hakika matunda utayaona mbeleni,

Pia kwa mtazamo wangu, maisha yalivyo sio lazima Ubutue wewe, ni bora leo kuweka misingi Imara ya wanokuja kuja kubutua vizuri, kuliko wewe kulazimisha kubutua maisha huku ukiawa na msingi mbovu, siku ukifa nyuma unaacha mateja, cha kwanza ni kuuza hiyo nyumba na kuuana.
 
Kwa mfumo mbadala wa majitaka waone kampuni ya Riflo. Unaweza kugoogle kwa maelezo zaidi. Mfumo salama, hutakaa unyonye majitaka wala kusikia harufu yoyote na bei zao za vifaa na ufundi kama utanunua mawe lori 1 na kuchimba mashimo mwenyewe haizidi milion 1.

Thanx NANDERA, ngoja niwaangalie..
 
Nyumba kibongo bongo ni Liabilitie, gaharama za kuitunza kwa vyovyote ni kubwa, pili inategemea na kipato chako, kma ni cha kuunga unga ni bora ukawezkeza kwenye Elimu yako au ya wanao, afya yako ay ya familia, hakika matunda utayaona mbeleni,

Pia kwa mtazamo wangu, maisha yalivyo sio lazima Ubutue wewe, ni bora leo kuweka misingi Imara ya wanokuja kuja kubutua vizuri, kuliko wewe kulazimisha kubutua maisha huku ukiawa na msingi mbovu, siku ukifa nyuma unaacha mateja, cha kwanza ni kuuza hiyo nyumba na kuuana.
Ninasikitika sana kuwa hamjaelewa hoja yangu, nilitaka mnipe mbadala wa uwekezaji mbadala wa nyumba.
Duniani kote uwekezaji wa ardhi na majengo ya biashara au hata makadhi ndio wa uhakika zaidi.
Unajaribu kuniaminisha kuwa kusoma ndio uwekezaji lakini hujaniambia ni nini itasapoti elimu yako na wanao kama huna uwekezaji wa uhakika wa kulipa hizo ada?
Tanzania sio sawa na nchi za scandnavia useme utafadhiliwa masomo yako.
Narudia ukia na nyumba nzuri na za kisasa, mahali sahihi huwezi kukosa pesa zitokanazo na kodi au fremu za maduka.
Mkuu najua wengi wana nyumba za kupangisha na hazijawasaidia, hii ni kwa sababu hawajajenga kwa viwango, so wapangaji walio nao ni walala hoi na wasio na uwezo wa kulipa kodi kwa wakati;
Nisome hivi kwa mfano;
1) jenga viself vyako vyenye single
room, mikoa kama Mwanza,
na dar huwezi kukosa
150,000/@month...kumbuka
Kila kukicha thamani ya ardhi
na nyumba thamani yake inaongezeka na kodi inapanda.
Huu ni mfano mdogo sana, je ni biashara gn bongo ambayo ni ya uhakika na inaweza kufanywa na watu wa kawaida ukiacha matajiri na inayoweza kuwa ya uhakika na yenye financial security zaidi ya hii?
Nikipata muda nitaandika kwa urefu
 
Back
Top Bottom