Mitsubishi Pajero iO inanitesa

jamani nimenunua mitsubishi pajero io ina kama miezi kumi tu, lakini imeanza kusumbua hasa misi zimekua nyingi na wakati mwingine inanizimikia kwenye foleni hapa mjini.

Nimejaribu mara kadhaa kuipeleka gereji mafundi washanilamba mara kibao lakini tatizo lipo palepale, nimebadilisha kwa maelekezo ya mafundi hadi plug (ambazo zote nne ni kama laki moja) mara mbili lakini bado tatizo lipo palepale.

Nishaurini wazee tatizo ni nini nimechoka sasa​


tatizo la kuzima mara nyingi linazababishwa na sensors inapo hisi kitu kwenye engine.hizi gari zina mfumo wa computer ambazo kupia sensor zinafanya mawasiliano na engine.nakushauri uifanyie diagnosis ya engine then mtambo utakujulisha ni sensor gani ambayo inasababisha error code,hapo utabadilisha kifaa kingine.plug sio sababu ya hizo miss na kuzima bali sensor ndo zinaiamuru engine kuzima hasa zinapo hisi kitu ambacho sio cha kawaida...........
 
Pole sana ndugu yangu....
mimi nina gri hiyo nimeinunua 2009 mwishoni, mwanzoni ilikuwa inamiss mpaka nilipopeleka kwa fundi mmoja yupo kinondoni karibu na hospitali ya mifupa anaitwa bakari then akanichekia kwenye computer na kubadilisha plugs na vitu vingine na akanishauri nitumie mafuta ya unleaded tu na kuna dawa inauzwa total alinishauri niwe naweka kila ninapoweka mafuta inasaidia kusafisha....nilifanya hivyo mpaka leo haijawahi nisumbua,watu wengi wanakuja niuliza but nikiwaambia hainisumbui hawaamini....na sikuhizi naweka mafuta yoyote tu na haina tatizo...nakushauri umtafute huyo fundi atakusaidia.......
 
Na wewe unaelekea kulekule ...achana na mitsubishi hata ikiandikwa nini. mi ni mtaalam wa magari nakushauri endesha toyota yoyote au suzuki yani ni bora ununue rav 4 hata ya 95 kuliko mitsubishi ya 20011.
ndugu baada ya kupokea ushauri wa wanajamii umetatua tatizo lako?si vibaya ukatuambia wengine tatizo ni nini kwani wengine tuko mbioni kumiliki hizo Mitsubishi!

kwa wale walio na ujuzi,hii Mitsubishi airtrek mnaionaje?kuna anayeitumia hii?ina tatizo lolote Cronic?

natafuta kagari kadogo,nimetazama Rav4,Honda,Escudo,Vitara,landrover freelander..,hii mitsubishi airtrek ndio gari pekee iliyonipendeza kwa bei yake.nategemea kutumia 12M max.
 
Na wewe unaelekea kulekule ...achana na mitsubishi hata ikiandikwa nini. mi ni mtaalam wa magari nakushauri endesha toyota yoyote au suzuki yani ni bora ununue rav 4 hata ya 95 kuliko mitsubishi ya 20011.
<br />
<br />
mh! Mitsubish vimeo. Dont ever try! Ushauri wa huyo jamaa hapo juu ni wa kweli.
 
pajero I0 ni gari nzuri ila tatizo huwa ni mafuta jitahidi kuweka mafuta ya BP tatizo la miss litaisha .. pia kuwa makini na oil inayotumika
 
Waswahili tunachekesha tuna po judge UBORA wa gari(USED) bila history lilipitiwa na nani,muarabu au mswahili au ndg zetu wa TZ kaskazini.
Nunua gari brand new hayo mambo utayasikia redioni wala hao mafundi hutawa jua/sikia.
Lakini ukiishakwenda kwenye used tegemea lolote na uwe na list ya mafundi na kila fundi ukienda kwake anamponda wa zamani.
Mitsubishi Center its the best solution ila kama ni salary worker kama mimi nenda huko mwisho wa mwezi,ila huwa wana huduma ya check up ni kama 65,000Tshs wanaku
ambia kila ubovu uliomo halafu unaweza kuamua kwenda mtaani au kumuita chemba huyo fundi.
 
Mimi ninaitumia toka 2008 mpaka leo ilikuwa na km 35000 mpaka sasa ina km 105000. Tatizo ninalo liona ni ughali na upatikanaji wa spea, kama utapata fundi mzuri wa pajero haikupi taabu ila usitumie mafuta ambayo yenye lead. ukiweka kitu cha BP miss kwako utazisikia tu. Mimi iliwahi kunisumbua mara moja nikabadilisha plugs na nozzle zote mpaka sasa haijasumbua tena.
Ila yote kwa yote ni gari expensive kuiendesha kwani inatumia mafuta mengi na spea zake ni ghali mno mfano plug moja ni kati ya 20000-25000 wakati ya toyota mpaka za 4000 zipo.
 
HA HA HAAAAAAAAAA hawa ndio wabongo bwana! wanaletewa clean modern technology hawaitaki kwa sababu wamezoea kuchakachua. Pajero ni gari za kisasa zenye shape nzuri zinapendeza! Ilahazitaki magumashi. Fundi aliyefeli darasa la saba kwa vyovyote vile usimpelekee hii gari atakuulia jumla. spare zake hakuna za kufoji kama za toyota zinazochongwa mitaani. mafuta lazima yawe safi si ya kuchanganywa na mafuta ya taa. Ulaya hizi gari zinatumika mno na ndo maana wazungu wengi hapa dar wanazo. Kwa hiyo naomba ieleweka tatizo si gari bali ni sisi. Hivi mjapan hana akili wenye akili ni sisi. Nyie endeleeni kulialia yeye anawauzia wenye akili tena kwa bei mbaya. Mimi mwenyewe nina unifomu yangu (toyota) nataka nibadilike kidogo ninunue pajero wala hamniambii kitu. Nitakuwa napeleka kwa dealers kuservice no problem!
 
Mistubishi pajero GDI my best car ever!!! Using it for the 3rd year now
 
Achana na mitsubish ndugu, hata kama inaitwa mitsubish obama,au jk, or mitsubish slaa. Zote hazifai
ndugu baada ya kupokea ushauri wa wanajamii umetatua tatizo lako?si vibaya ukatuambia wengine tatizo ni nini kwani wengine tuko mbioni kumiliki hizo Mitsubishi!

kwa wale walio na ujuzi,hii Mitsubishi airtrek mnaionaje?kuna anayeitumia hii?ina tatizo lolote Cronic?

natafuta kagari kadogo,nimetazama Rav4,Honda,Escudo,Vitara,landrover freelander..,hii mitsubishi airtrek ndio gari pekee iliyonipendeza kwa bei yake.nategemea kutumia 12M max.
 
Ni kweli, waone mafundi walio specialize kwenye Mitsubishi, tatizo ni kwamba mafundi wetu wengi hapa Bongo niwa babaishaji na wamezoea cheap and simple engines of toyota, wakati mitsubishi ni more advanced na ukizipatia ni nzuri zaidi kuliko toyota. Wao ndio wakongwe huko Japan walianza 1870. That's why specialized more in Banks and heavy machines like marine, jet engines etc
 
MImi nina kiminiPajero Mitsubishi, mwaka wa 6 sasa japo of late kime-develop tatizo la kuslip clutch. Gari hili ni automatic lakini ukiliwasha unasikia linapumulia/ngurumia kifuani/kwenye injini na linakuwa zito sana kutoka hadi utembeee kilomita kama 3 ndo unasikiaa linapick-up. Niliambiwa kuwa nisafishe gearbox na kuweka BP oil na mengine mengi nimefanya hadi nimechoka. Mambo mengine ni kizuri, nakitumiaga kwenda Arusha na kurudi same day without matatizo na kiko vizuri hapa Dar na mambo ya parking huangaki sana. Mwenye ushauri kuhusu hiyo gear box/kuslip kwa clutch naomba anijuze..au ambaye anajua fundi mzuri
 
kitu vitz tu mazee,lita 8 dar hiyo,mi nipo moro,yaani kinanusa tu,chezea vitz wewe,pole bro,jaribu kuweka wese la bp tatizo linaweza kuisha kabisa,mbona zima hiloo
 
ndugu baada ya kupokea ushauri wa wanajamii umetatua tatizo lako?si vibaya ukatuambia wengine tatizo ni nini kwani wengine tuko mbioni kumiliki hizo Mitsubishi!

kwa wale walio na ujuzi,hii Mitsubishi airtrek mnaionaje?kuna anayeitumia hii?ina tatizo lolote Cronic?

natafuta kagari kadogo,nimetazama Rav4,Honda,Escudo,Vitara,landrover freelander..,hii mitsubishi airtrek ndio gari pekee iliyonipendeza kwa bei yake.nategemea kutumia 12M max.

Kiukweli Mitsubishi sio kwamba ni Gari baya, tatizo kubwa la haya magari ya siku hizi ni service. I am expert in that field nikiwa na time nitakuja kueleza vizuri zaidi juu ya magari yote from Toyota, Honda, Audi, BMW, Mitsubishi, nk matatizo yake na namna ya kuyatatua, pia Engine tofauti like VVT-i, Dual VVT-i, D4, GDI, EFI nk.
kwa haraka peleka gari lako kwa Dealer wa Mitsubishi, atatatua tatizo kwa urahisi sana. From maelezo yako tatizo la gari yako sio plug bt i guess its either MAF, au Oxygen Sensor.
Gud luck mkuu wala usikate tamaa. waweza ni PM kwa maelezo zaidi na ushauri zaidi wa gari lako.
 
Peleka kwa good tech mimi ninae mmoja anaitwa Denis 0754594076 atafanyia computerised diagnosis na kuspot tatizo, then atafix pia unatakiwa kutumia genuine plugs za Mitsubishi au nyingine ambazo ziko na good quality, tumia unleaded fuel, ukiweka mafuta machafu kaka hii gari iko very sensitive, mimi ninayo for 3 yrs now iko kama mpya I maintain it very well.
 
Back
Top Bottom