Millard Ayo ana tatizo gani na habari za Upinzani?

Congressman

JF-Expert Member
Jun 2, 2020
732
2,154
Kijana huyu baada ya kupata mafanikio kupitia sisi vijana, ghafla ameanza kujisahau. Zaidi ya 90% ya followers wake instagram pamoja na subscribers wake ni wafuasi kindakindaki wa CHADEMA na hilo analijua.

Katika video zinazohusu Siasa, kwa miaka yote zile zenye maudhui ya CHADEMA na viongozi wake ndio zimekuwa zikiongoza kwa views, hivyo tangia mwaka 2015 amewatumia vya kutosha wafuasi wa CHADEMA lakini kutokana na kujipendekeza leo kawapiga kapuni.

Haiingii akilini hata kidogo kurusha Live matangazo ya CCM katika kila hatua za chaguzi zao, Mkutano mkuu CCM, UVCCM, mpaka umoja wa wazazi, ikiwemo na matamko ya kipuuzi ya kina Polepole, Jaji Kaijage na mpwa wao Dr. Abbas vyote vimekuwa vikipata coverage ya kutosha, lakini leo hii hata kurusha habari za CHADEMA na tundu Lissu hakuna.

Hapa tunapoongea Millardayo hana habari kuwa CHADEMA na Lissu walikuwepo Singinda, Shelui, Igunga, kahama, Shinyanga na leo wapo Musoma. Mpaka leo habari iliyopo kwake ni ile ya Lissu kupokelewa JK Airpot. Hili halikubaliki hata kidogo, hata kujipendekeza basi ni lazima uwe na aibu.

Hujuma za Millardayo anazozifanya leo zina mwisho, Tukiamua kukupuuza utabakia huna dira, kawaulize TBC watakupa habari. Siku tukiamua kuja na petition ya kukupuuza ndio utajua maana ya nguvu ya umma.
 
Huyo kijana ni miongoni mwa "WATAPIA TUMBO", anajifanya mjanja wa kukwepa lawama za TCRA, au pengine kaishapigiwa simu na Profesa Polepole asiandike chochote kuhusu upinzani.

Ila anafeli, kama wanavyofeli waimbaji wa bongo fleva kujihusisha na vyama vya siasa (hasa CCM), hawajifunzi kwa nchi zilizoendelea (Huwezi ukamkuta Eminem, Lil Wayne, Rihanna, Beyonce, Jay Z, DJ Khaled wanaimba "MAPAMBIO YA KIPUUZI YA SIASA AU VYAMA VYA SIASA - Hawajui wanapoteza FANS wengi walioupande wa pili kisiasa, wao wanajionesha hawajali hilo kundi la pili la FANS wao").
 
Kijana si mwanaharakati, anatazama maslahi yake kwa mapana, ebu anayeona millard anakosea aingie kazini ajazie pale alipokosa yeye. Kama BBC na DW wametimuliwa unataka Millard wamfanyeje au umesahau yaliyowapata wengine?

Ila na vyama pinzani miaka yote vinalalamika kuwa havipati jukwaa la usawa toka TV za ndani lakini hata hawajisumbui kuanzisha vyombo vyao vya habari hadi wamezidiwa mbinu na WCB kijana hata hajafika chuo kaona anabaniwa kwingine kaja na mbinu ya kuwa na chombo chake cha habari.
 
Kijana huyu baada ya kupata mafanikio kupitia sisi vijana, ghafla ameanza kujisahau. Zaidi ya 90% ya followers wake instagram pamoja na subscribers wake ni wafuasi kindakindaki wa CHADEMA na hilo analijua...
Atavuna anachopanda
 
Unamuonea bure, kwani wewe ni mgeni hapa bongo?
Hata picha huioni?

Unataka afunge biashara yake sababu ya kuridhisha kila mtu? Si afadhali abakiwe na hao wachache lakini abaki kwenye biashara?
Brother hujawazoea tu Keyboard warriors!!

wanahubiri mabadiliko ila hawataki kuwa part ya kuyaleta hayo mabadiliko, wanatamani watu wengine wajitoe kafara kwa ajili yao ila wao wapo relaxed mbele ya screens. sio fair
 
Kijana si mwanaharakati, anatazama maslahi yake kwa mapana, ebu anayeona millard anakosea aingie kazini ajazie pale alipokosa yeye. Kama BBC na DW wametimuliwa unataka Millard wamfanyeje au umesahau yaliyowapata wengine?...

Hata wangeanzisha vingefungiwa kama yalivyofungiwa magazeti na baadhi ya tv online zenye mwelekeo wa demokrasia
 
Kijana huyu baada ya kupata mafanikio kupitia sisi vijana, ghafla ameanza kujisahau. Zaidi ya 90% ya followers wake instagram pamoja na subscribers wake ni wafuasi kindakindaki wa CHADEMA na hilo analijua.

Katika video zinazohusu Siasa, kwa miaka yote zile zenye maudhui ya CHADEMA na viongozi wake ndio zimekuwa zikiongoza kwa views, hivyo tangia mwaka 2015 amewatumia vya kutosha wafuasi wa CHADEMA lakini kutokana na kujipendekeza leo kawapiga kapuni...
Mkuu siasa zinawafanya mkose Akili kabisa Yaani account yake binafsi unataka umpangie cha kupost?

Sasa si Kama umeona hakidhi maudhui yako una unfollow tu halafu unakaa kimya.
Ile siyo account ya clouds, ITV Wala TBC Ila Ni ya Millard Ayo so usitake kuingilia Uhuru wake.
 
Hata wangeanzisha vingefungiwa kama yalivyofungiwa magazeti na baadhi ya tv online zenye mwelekeo wa demokrasia
sasa kama vyama vyenyewe vinafungiwaonline TVs na magazeti wadhani Millard akiwa mlengo wakushoto atafanywaje na palendipo kula yake ilipo hana ruzuku.

Kama Kabendera yalimkuta yale unadhani Millard hana hofu? Si kila mtu anaweza kuwa mwanaharakati na wala haina haja ya kumlaumu maana kila mtu ana haki ya kuwa na hofu
 
Back
Top Bottom