Mijadala gani hufungwa au kufutwa kabisa katika JamiiForums?

Status
Not open for further replies.
Mimi jana nimeweka uzi hapa juu ya matukio mapya ambayo yamepangwa Zanzibar kufanya uhujumu, hata kuuwa, lakini uzi huo umefutwa, jamii Forum haina uhuru tena, tumekwisha
 
Kila kitu kwenye nchi hii Kwa sasa kinaendeshwa kibabe babe tu so tuvumilie kipindi hichi cha mpito
 
wanazo..unadhani hujulikani!!..pole
Hazijui kama wanazujua itakuwa mwenye hii website ya JF kazipeleka.....hawana uwezo huo,na ndio maana walimpeleja mahakamani huyu huyu jamaa mwenye hii JF kumlazimisha atoe password za watu fulani
 
JF siku hizi hakuna uhuru kabisa. Siku hizi tunazidiwa na.magazeti ya udaku kwa ubora! Kama mmekasirika siogopi kupigwa ban maana hamnilishi wala kunijazia mafuta kwenye gari. Tumbaku!
Kweli kabisaaa siku hizi jf imekuwa ya kiduwanzi sanaa ,,jamaa anatumika sanaa nà kitengo,,usikute hata taarifa zetu anazitoa kimya kimya .
Jf ya sasa sio kama ya zamani.
 
Sijawahi kuweka thread hapa isifutwe, na sitoweka tena, sasa hizi nipo hatua za mwisho mwisho kuweka forum yangu niandike ninavyopenda mwenyewe, hata niwe peke yangu, nitaandika Halafu nitajisomea mwenyewe na kujijibu mwenyewe, nyote mnakaribishwa.
 
Mkuu Invisible, kwa awamu hii ya utawala tuliokuwa nao,utawala unaonyima haki zote za msingi za kumfanya mtanzania ajisikie huru, JF ndio sehemu pekee kwa Tanzania ya sasa kuwa mtanzania anaweza kutoa dukuduku lake la mayoni hasa kuhusu hizi siasa za vitisho,siasa za ketekana na kupigana risasi..

Nimeona kuna nyuzi nyingi zinazohusu Zanzibar hasa kama zile za Mungano huwa hazichukuwi dakika tano hufutwa wakati kwenye mitandao ya kijamii ya wazanzibari zinajadiliwa kama kawaida,binafsi uwazi na majadiliano naamini ndio njia pekee ya kuondoa tafauti..

Naamini kama tunakuwa wawazi na kuweka vitu mezani na kuanza kuvijadili mapigano,utekaji,kutokuelewana itakuwa hamna,siasa za makongamano,siasa za yakujadiliana ndio zinazofanywa na nchi za Ulaya,Marekani na zile nchi zilizopiga hatua kimaendeleo..

Kama JF mmedhamiria kuwa mabigwa wa uhuru wa kuongea,uhuru wa kujadili,uhuru wa kutoa mawazo na maoni basi wacheni watanzania watoe maoni na mawazo yao kwenye JF kwani hii naamini ndio sehemu pekee mtanzania anajisikia huru,,, kama hamuwezi kufanya hivyo basi bora hii "option" ya "jukwaa la siasa" iondoeni....Nawakilisha
 
Siku hizi kule jukwaa la siasa pamepoa, kumbe sababu ni nyuzi kufungwa!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom