Mijadala gani hufungwa au kufutwa kabisa katika JamiiForums?

Status
Not open for further replies.
Husika na kichwa tajwa.
Kama member wa Jf, nasikitika kuona kuwa threads zangu zinafutwa muda mfupi baada ya kuziweka hapa, sijawahi kuandika kwa kutukana yeyote kwa namna yeyote ile na pia sijawahi pewa sababu zozote kwa njia yoyote zinazoeleza sababu za ama kunitaka nirekebishe kasoro ama kusudio la moderators kutaka kuzifuta.

Jana niliweka mada yenye kichwa " waache waandamane ujinga wao...CCM mbele kwa mbele na huku mnaogopa maandamano" ili futwa muda mfupi baadaye, sijajua nini sababu japo kuna threads zipo kwa muda hata tija kwa jamii siioni.

Mapendekezo; ni vyema mods. wakamtaarifu mtoa mada juu ya kasoro zilizopo kwenye threads husika kabla ya kuchukua maamuzi ya kujifutia threads ya member, naamini kufuta na hatua kali karibu na kufunguwa uanachama kwa muda bila mhusika kujua sababu. Ni hayo tu mods nimeona nimevumilia kwa muda sasa.

JF the home of great thinkers and not threads deleting thirsts!
 
Moods wa JF mna rohoo mbaya na ngumu kama ya shetani, Niweka uzi wangu hapa muda si mrefu uliobeba madokezo juu ya kifo cha aliyekuwa jabali la siasa nchini Reverend Mtikila, matokeo yake hata nusu saa haijaisha moods mmeufuta, mnaweza nipa sababu za kuufuta? Au kuna habari za watu flani hazitakiwi humu ndani? Naihitaji maelezo tafadhali
 
Nimeweka uzi wangu kuhusu habari zilikuwa na mweelekeo wa ukweli kwani sio muda mwingi kama wiki moja hivi kulitokea matokeo fulani Zanzibar kuhusu kusachiwa ofisi za vyama vya siasa na vyombo vya dola..

Uzi niliupata kwenye mtandao,katika uzi ule yalikuwemo majina fulani ya wahusika wa huo mpango,majina ya watu kutoka Zanzibar na mengine kutoka Tanganyika,mawazo yangu ile habari ni ya kweli kwasababu sio rahisi mtu kutoa majina tu na kuanza kuwasingizia habari za uongo watu

Madhumuni ya kuweka uzi ule ni kuleta majadiliano yenye manufaa na Taifa letu,labda wako watu wachache wenye mawazo kama yale,Uzi ule haukufika dakika tano hewani umefutwa,sifahamu kwanini au kwa manufaa ya nani,tunazungumzia uhuru wa kuzungumza "Freedom of speech" sasa kweli moderator ulichofanya kuufuta ule uzi ni uhuru wa kujadiliana?!! ni "Freedom of speech"....??

Najua kuna profile iliandika moja kwa moja kwa moderator na kumwamrisha afute ule uzi....je Fb imekuwaje,Je ni nani mwenye ile profile iliyomuamrisha moderator afute na yeye moderator hapo hapo akafuta ule uzii...??
 
Nimeweka uzi wangu kuhusu habari zilikuwa na mweelekeo wa ukweli kwani sio muda mwingi kama wiki moja hivi kulitokea matokeo fulani Zanzibar kuhusu kusachiwa ofisi za vyama vya siasa na vyombo vya dola..

Uzi niliupata kwenye mtandao,katika uzi ule yalikuwemo majina fulani ya wahusika wa huo mpango,majina na ya watu kutoka Zanzibar na mengine kutoka Tanganyika,mawazo yangu ile habari ni ya kweli kwasababu sio rahisi mtu kutoa majina tu na kuanza kuwasingizia habari za ongo watu

Madhumuni ya kuweka uzi ule ni kuleta majadiliano yenye manufaa na Taifa letu,labda wako watu wachache wenye mawazo kama yale,Uzi ule haukufika dakika tano hewazi umefutwa,sifahamu kwanini au kwa manufaa ya nani,tunazungumzia uhuru wa kuzungumza "Freedom of speach" sasa kweli moderator ulichofanya kuufuta ule uzi ni "Freedom of speach"....

Najua kuna profile iliandika moja kwa moja kwa moderator na kumwamrisha afute ule uzi....je Fb imekuwaje,Je ni nani mwenye ile profile iliyomuamrisha moderator afute na yeye moderator hapo hapo akafuta ule uzii...??
Kwahiyo hapo tatizo ni aliyeamrisha au aliyefuta?!
 
Hivi taratibu au vigezo vya moderator kufuta bandiko/post ya mwana JF ni zipi/vipi?
 
wazee wa kitengo wapo @ mahali,usimlaumu sana Mods

Yaweza kuwa hata Mods hajui nani kaufuta huo uzi
 
Hebu kama unayo tupia tena, muda huu wako baa wanakamua bia kwa kodi zetu. Kabla pombe hazijawaisha kesho asbh ss tutakuwa tumeishasoma na kujua content yake.

Fanya fasta basi, muda unaenda. Najua hata kesho watakuwa busy kuzuga na issue ya gazeti la Musiba maana nimesikia ameitwa. Tupia madini muda huu mkuu.
 
:D:D
 
JF siku hizi hakuna uhuru kabisa. Siku hizi tunazidiwa na.magazeti ya udaku kwa ubora! Kama mmekasirika siogopi kupigwa ban maana hamnilishi wala kunijazia mafuta kwenye gari. Tumbaku!
 
Kuna mtu humu ashawahi suggest kuwa hili jamvi linamilikiwa ama kuwa influenced na mukhabarat
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom