Miaka ya themanini Wazo Hill, Bunju, Boko na Tegeta kulikuwa na swala, digidigi na sungura wengi sana. Sasa hivi hawapo

Machudaa

Senior Member
Jan 22, 2018
124
311
Nakumbuka tukiwa wadogo miaka ya themanini kulikuwa na mapori makubwa sana kuanzia Tegeta, Bunju, Mbezi Beach, Wazo Hill, Kunduchi, Mbweni, Boko. Kulikuwa na swala na sungura wengi sana. Siku moja mimi na marehemu mjomba wangu tulienda Madale kuwinda Swala.

Hili suala la Ngorongoro lichukuliwe sana kwa uzito. Lazima tuangalie future.

Serikali ijitahidi sana ili wamasai wenyeji wapate ufumbuzi.
 
Binadamu ni kiumbe hatari sana kwa maisha ya viumbe wengine
 
Nakumbuka tukiwa wadogo miaka ya themanini kulikuwa na mapori makubwa sana kuanzia Tegeta, Bunju, Mbezi Beach, Wazo Hill, Kunduchi, Mbweni, Boko. Kulikuwa na swala na sungura wengi sana. Siku moja mimi na marehemu mjomba wangu tulienda Madale kuwinda Swala.

Hili suala la Ngorongoro lichukuliwe sana kwa uzito. Lazima tuangalie future.

Serikali ijitahidi sana ili wamasai wenyeji wapate ufumbuzi.
Sasa hivi Kuna Panya road
 
Nimeishi umasaini nikagundua kwamba ile jamii ipo tofauti sana na makabila mengine.

Kwanza, Masai anapenda sana pori. Akiona nyumba ya bati imejengwa karibu yake, anafikiria kuhama. Masai anapenda sana uoto, majani vichaka n.k kwa sababu vinampatia dawa na malisho.

Pili, Masai hali ndege iwe wakufugwa au wa porini. Sijawahi kusikia au kuona Masai anakula nyama pori.

Tatu, masai akijenga boma hahitaji kufyeka eneo. Sana sana atahitaji kupruni mti na siyo kuukata.

Kwa hiyo, ukilinganisha maeneo yaliyoharibiwa na waswahili na kudhani kwamba Masai naye ataharibu the same siyo mlinganyo sahihi.

NB; kama wataalamu wameona kwamba Masai anaweza kuishi na wanyama katika baadhi ya maeneo, mimi naunga mkono.
 
Kweli kuna mabadiliko,sehemu zilizokuwa vichaka na mapori hivi sasa ni sehemu ya makazi tena holera.
Mwaka 1976 nilipanda basi la UDA wakati huo,likifanya safari ya Kariakoo-Africana kupitia Magomeni.
Kuanzia Makumbusho, Mwenge, Lugalo hadi Mbezi kulikuwa na mashamba ya mpunga na korosho.
 
Shua kabisa mzee wangu aliwahi nunua pori sinza ss hivi kila akinipigia story hizo namuona fala kwa nini alinunua sehemu ndogo akati alikua na uwezo wa kununua ekari kabisa.
 
Hata sasa bunju baadhi ya maeneo ni pori tupu na hao digidigi na sungura wapo!
2049507646.jpg
1719534750.jpg
822637106.jpg
 
Nakumbuka tukiwa wadogo miaka ya themanini kulikuwa na mapori makubwa sana kuanzia Tegeta, Bunju, Mbezi Beach, Wazo Hill, Kunduchi, Mbweni, Boko. Kulikuwa na swala na sungura wengi sana. Siku moja mimi na marehemu mjomba wangu tulienda Madale kuwinda Swala.

Hili suala la Ngorongoro lichukuliwe sana kwa uzito. Lazima tuangalie future.

Serikali ijitahidi sana ili wamasai wenyeji wapate ufumbuzi.
Kumbe wewe na mjomba wako mlikwenda kuwinda swala, na yule na shangazi yake alikwenda kuwinda sungura, Justina na ankle Ben walikwenda kuwinda sungura, mlikuwa wawindaji wengi hivyo mliwamaliza hao wanyama.
 
Pili, Masai hali ndege iwe wakufugwa au wa porini. Sijawahi kusikia au kuona Masai anakula nyama pori.

Mbona Edward Lowassa, marehemu Edward Sokoine na Ole Sendeka tulikuwa tunapiga nao "vyuku" kwa sana tu?

"Vyuku" is a plural of KUKU.
 
Swala la wafugaji Nomadic one lazima lifanyiwe mpango mkakati wakutosha.

Tunawahitaji sana hawa jamaa vinginevyo bei ya nyama itakuwa ni anasa kwa wananchi wengi wa TZ kuliko ilivyo sasa.

Kwa sasa tu nyama imekuwa ni anasa kutokana na umaskini wa kutupa wa waTZ wengi.

Sembuse tahadhari isipochukuliwa ya kuwatengenezea mazingira mazuri ya ufugaji hawa wamasai mnazani itakuwaje?
 
Tusiwachukulie Poa na kuwa-ignore na kuwaona wakorofi n.k

Serikali kazi yao ni kuwatafutia maeneo kwa kushirikiana nao mweneo ambayo ni rafiki kwa ufugaji.

Kazi ya kufuga ni ngumu sana,

Wanaendelea kufuga wenyewe na kujikimu wenyewe haja yao ni Uhuru wa maeneo.
 
Back
Top Bottom