aliye waambia 'District Medical Officer' = Mkuu wa Idara ya Afya ni nani?
Nziku, idara ya afya ina nyanja mbali mbali sawa lakini "DMO" anayezungumziwa na mwandishi anatakiwa kuwa na taaluma ya udaktari wa binadamu, sio wa falsafa au utaalamu mwingine wa sekta ya afya. Wananchi watakapotambua haki zao na wanasheria watakapohamia mahospitalini ndio umuhimu wa hizi allocation za kazi na maadili ya kazi utakapoonekana.
Thadeo alipoulizwa kuhusu suala hilo alikiri kwamba hana taaluma ya udaktari, lakini alikanusha kwamba amepewa nafasi ya kukaimu nafasi hiyo kwa makosa. "Ni kweli mimi si daktari.
Nilikaimishwa ofisi hii baada ya daktari aliyekuwepo kwenda masomoni na kabla ya kurudi akafariki dunia akiwa huko na baada ya hapo nikaendelea kuwa DMO kwa sababu nina taaluma ya usafishaji 'cleanliness' na hii ilitokana na utaratibu wa ofisi hii kuwa na vitengo viwili ambavyo ni kitengo cha kinga na tiba ambalo ndilo eneo la daktari na eneo jingine ni la usafishaji ambalo ndilo eneo langu, hivyo mimi nikawa kama msimamizi wa masuala ya usafi na si masuala ya kinga na tiba," alisema Thadeo na kuongeza
Huyu si ameshikilia kwa muda tu hadi hapo mwenye taaluma hiyo atakapofika,au vipi?
Nziku,
Majibu ya Meya bado sijaridhika nayo, najua unajua vizuri sifa za mganga mkuu ziko wazi meya ameshindwa kuwasiliana na mkoa au hata wizara kupata mtu wa kuja kukaimu hiyo nafasi. jamaa huyo anaweza kukaimu kwa kipindi fulani dhen kuna suala la kuwa confirmed kuwa mganga mkuu kasheshe hapo. Tuwe makini na utendaji wetu, ni sawa na kumpa mtu cheo cha kukaimu urubani mkuu, wakati yeye ni injinia wa tairi. Kweli tutafika hivi? Mimi hapo ni mala 100 kumpa mtu aliye na elimu ya mganga msaidizi ambaye anaweza kudeal na majanga.
anyway Mkuu Shadow, ninasema ninachokijua kwani nimeshawahikufanyakazi na Serikali za Mitaa kwa miaka mingi tu. Hivyo ninaelewa shida iliyopo katika kutofautisha vyeo vya maofisa na Mkuu wa Idara.
Nimewahi kusoma kwamba Mfumo wa Maboresho wa Serikali za Mitaa utapitiwa upya, mpangilio na majina ya vyeo vya maofisa hasa wakuu wa idara ili uwe mmoja kwa taifa zima. Sijui kwasasa mfumo huo ulishafanyika au bado.
Sio suala la kushikiria kwa muda utashangaaaaaaaaaaaaa atamaliza mwaka miaka.
Alafu ata kama ni utawala ni lazima awe Dr ili aweze kuendana na mahitaji ya wenzake otherwise wenzake watataka iki yeye atasema mbona sioni kama kina umuhimu.
Chukua mhasibu akawaongoze maingeneer utaona mziki wake.
Si lazima ila ni vyema uongoze watu ambao mnaoana kiprofessional so that u can all be in the same wavelength interms of problem solving,setting goals,team work etc
sawa kabisa Mkuu Masatu, tupo ukurasa mmoja hapa kuna mtu ananyatia cheo hicho anashindwa kukitafuta kwa taaluma na uzoefu sasa anatumia media.
mwandishi huyu wa Mwananchi hajui kabisa mfumo wa Serikali za Mitaa ulivyo. Hivi nani aliye mwambia kwamba Mkuu wa idara ya afya lazima awe daktari? Katika idara ya afya kuna Madaktari, Ma-Bwana afya, Ma-afisa ustawi wa jamii, wahandisi wa usawi (sanitation engineers). Wote hawa wanahaki sawa kuwa wakuu wa idara endapo elimu yao na uzoefu unaruhusu.
Sambamba na idara ya afya ni hivyo hivyo kwa idara zingine kama vile Ujenzi. Kuna wahandisi wa majengo (Arctects), mitambo (mechanical), bara bara na halmashauri zingine kuna mhandisi wa maji. Yeyote kati ya hawa anweza kuwa Mhandisi wa wilaya.
The same way kwenye idara ya Mipango miji, kuna Ma-afisa mipango miji, Ma-afisa ardhi, Wadhamini (valuers), ma-surveyor na Ma-afisa misitu/mazingira. Pia yeyote anaweza kuwa Mkuu wa Idara ya Mipango Miji.
Idara ya kilimo kuna Ma-daktari wa mifugo, Ma-afisa kilimo, Ma-land use planners au soil specialists, ma-afisa ushirika nk. Idara ya elimu kuna afisa elimu taaluma, takwimu, elimu ya watu wazima, utamaduni nk.
Tofauti ipo katika idara za fedha, utumishi, vitengo vya mwanasheria na mkaguzi wa ndani kwani hawa taaluma yao ni moja.
Mkuu Mtindiowaubongo, let me make a summary.
Katika Idara ya afya kuna maafisa/wataalamu wafuatao:-
Ma-daktari, Ma- Bw./Bi. Afya, Ma- afisa ustawi wa jamii na Ma-sanitary engineer.
Katika hizo clusters kuna wakuu wa section wafuatao
1. Daktari wa Wilaya (Mkuu wa section ya Tiba)
2. Bw./ Bi./ Afisa afya wa Wilaya (Mkuu wa section ya Kinga)
3. Afisa Ustawi wa Jamii wa wilaya (Mkuu wa section ya ustawi wa jamii) na
4. District sanitation engineer (Mkuu wa sanitation section)
Kati ya hawa wakuu wa section yeyote anaweza kuwa Mkuu wa idara ya afya. Sasa kwa Shinyanga nafasi hiyo inakaimiwa na sanitation engineer.
Tatizo hapa ni kasumba yetu ya kumwita Rais ni Nyerere. Kwamba huyu jamaa, mwandishi wa habari husika, wewe nk, mnamwita Mkuu wa idara ya afya ni DMO. Hili ni tatizo kwa nchi nzima na idara zote. Ndo maana maboresho ya Serikali za mitaa yalitaka ku-harmonize hilo. sijui wamefikia wapi.
Wewe kama unataka uuhakika wasiliana na watu wa Shinyanga wakueleze vizuri kama huyo Mhandisi ni Mkuu wa section ya Tiba au mkuu wa idara. Wenyeji wa Shinyanga tunalijua hilo vizuri.
anyway, nimejitahidi sana kulieleza kwa upana na mifano mingi tu. Ni vema pia kupitia makala za Karugendo juu ya Mfumo wa Serikali za Mitaa. Otherwise, pitia ripoti za Halmashauri mbalimbali na uwahoji wahusika.
You can't fool me that a sanitary engineer awe subordinate milele katika idara yake tena awe chini ya watu wasio na degree na yeye anadegree eti kwasababu tu kitengo chake kipo ndani ya idara ya afya yenye madaktari au Medical Officers na Assistants wao. LOL
Labda nikuulize, Mganga Mkuu wa Manispaa ni mkuu wa cluster au idara..tutaendelea kuanzia hapo..