Mh. Livingstone Lusinde akimwaga Sera za CCM Arumeru

Nina mashaka makubwa kama kweli kiongozi anaweza kupanda jukwaani na kutamka maneno kama hayo. Huo ni uwongo wa hali y juu kwa mleta maada.

Mleta mada katufanya sisi watoto wadogo. Ni kweli wakati wa kampeni huwa kuna vijembe na kashfa. Lakini si kwa maneno aliyoyaweka hapa.
 
MODs, naona hii thread mmehamishia jukwaa la chaguzi ndogo. Nadhani jukwaa la siasa panastahili zaidi ili wadau wengi watoe maoni yao. Hii topic ni muhimu kujua 'afya' ya siasa zetu kwa sasa. Na maadam watu wanasubiri Audio basi ingerudi jukwaa la siasa.
 
Inawezekana mleta mada ndiye mwenye tatizo kuliko lile la Lusinde. Kahama hapa, kaanzisha uzi mwingine akidai amepata video tayari lakini huko nako hajaiweka. Haeleweki!
 
Hatari sana,sipendi kuamini kama chuo cha siasa na propaganda pale Kigamboni kinaweza kutoa product dizaini ya Lusinde,na kama ana majukumu ya malezi katika jamii,jamii ana tegemea itajifunza nini kutokana na kalu zake.Mbona tunakitukanisha chama hususani katika kipindi hiki cha ushindani wa kisera.Tulitegemea ukongwe wake usio pungua miaka 35 ungetoa mafundisho kwa vyama vichanga.Kama baba nadni ya familia anafikia kutoa matusi ya nguoni hadharani mbele ya watoto wake unategemea familia hiyo kimuundo itakuwa ni familia ya aina gani. Jambo jingine nisilopenda kuliamini,ni kitendo cha timu nzima ya kampeni ndani ya chama kuafiki aina ya sera mpya walizoamua kuzinadi kwa kutofautisha ilani ya uchaguzi 2010 iliyoelezea sera za chama na kugeuka sera za maneno machafu na matusi mbele ya jamii ya wana wa Arumeru.Ukomavu huu wa kiumri si kigezo cha kuamini unapozeeka unashindwa kutambua lipi zuri na lipi baya.Tena mbaya zaidi timu hii inaongozwa na rais mstaafu mabye alizindua kwa matusi,tukadhani wameteleza kumbe ni aina mpya ya kunadi sera za chama kwa mtindo wa matusi.Kmamkuna ombwe la fikra ndani ya CCM ni bora basi wangeachana na siasa za ushindani na kusajil chama kama danguro na pango la wahuni. Pia sipendi amini kuwa timu hii yote ya kampeni ina baraka zote za m/kiti aliyeridhia matusi kama sera mpya katika kuelekea ushindi wa kisiasa katika uchaguzi ujao wa 2015.Ndani ya chama hiki wameanzisha baraza la ushauri loa wazee,je hiindiyokazi yao na malezi kwa vijana na UVCCM ambayoiliaminika kama chombo cha kuanda viongozi wa vadilifu ndani ya chama na serikali.Ukosefu huu wa hekima unasababishwa na kukataliwa ongezeko la posho au nini,N akama ni ugumu wa maisha si sababu ya kuzalisha Chama Cha Matusi.Ingependeza kama mkibanana kwa sera na hoja zenye mshiko kuliko hiikadhia mliyoamua kama njia mujarabu
 
Tokea tumeanza kusikia habari za kampeni za kugombea ubunge wa Arumeru mashariki gumzo kuu limekuwa ni lugha ya matusi ya CCM(a.k.a Chama Cha Matusi).Tokea awali tungetegemea kukemewa na kuonywa kwa CCM kutumia lugha lakini halikutokea. Pia tungetegemea wazee wanaozunguka mikutano ya ccm wangekemea lugha ya matusi lakini wapi. Mshangao zaidi ni wa CCM kumleta mtukanaji aliyebobea kwa uhuni na kichwa kibovu LUSINDE. Ninachojiuliza hivi ccm ni wehu kiasi gani hadi watumie muda mwingi kutukana badala ya sera? haiwezekani kwamba lugha ya matusi ndiyo watu wa arumeru wanaielewa zaidi? hebu watu wa arumeru tujulisheni MATUSI NI LUGHA YENU ADHIMU YA MAWASILIANO?
 
mimi siamini mpaka video iletwe
juzi hapa kuna mtu alianzisha thread ya JK na Bilal na Pinda
wametoka msoga kwa bibi mganga kufanyiwa makafara
it turn out kumbe walikuwa kwenye mazishi ya mkuu wa wilaya huko Kibaha
na saa mbili ilioneshwa taarifa ya habari.......
 
I see.......

Ninachoona hapa ni mleta thread(Yplus) kaamua kuwatukana wabunge wa CHADEMA na viongozi wengine wa CHADEMA kwa mgongo wa Lusinde......

Kama ni kweli Lusinde ameyatamka haya mleta thread ni kwa nini ameshindwa kuleta Audio ama Video ya kauli hizi za Lusinde?..

Haiingii akili kwa mtu mzima na akili zake(hata kama hana adabu) kutamka maneno ya aina hii kwenye mkutano wa hadhara,tena wa kampeni za uchaguzi wenye ushindani kama huu wa AM....Kama angeyatamka haya nina imani wananchi wote waliohudhuria mkutano huo wangeondoka na kumuacha yeye na wana CCM wenzake katika mkutano huo.....

Mods ondoeni thread hii mpaka mletaji thread atakapoleta uthibitisho/ushahidi wa Video ama Audio ya kauli hizi...Kuendelea kuiacha thread hii ni kuendelea kuwadhalilisha viongozi na wabunge wa CHADEMA ambao mleta thread amewataja....
 
To proof otherwise chungulia kwenye youtube lusinde ccm matusi.

Kama ipo YouTube na umeiona kuna ugumu gani wa wewe kuweka link ya hiyo video hapa? Au mnamaanisha haya?

CCM yamwaga matusi

Katika hali isiyo ya kawaida mkutano wa kampeni wa mgombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM ) Sioi Sumari ulitawaliwa na maneno ya matusi na vijembe dhidi ya viongozi wa CHADEMA.

Hali hiyo ilijitokeza jana wakati mgombea wa CCM , Sioi Sumari, alipokuwa akihutubia jukwaani aliporwa kipaza sauti na Meneja wa Kampeni hizo, Mwigulu Mchemba, ambaye alianza kumshambulia Katibu Mkuu wa CHADEMA , Dk. Willibrod Slaa kwa matusi akimwita kichaa.

Hatua hiyo ilitokana na kitendo cha helikopta ya CHADEMA kupita juu kwa mbali na ulipokuwa ukifanyika mkutano wa CCM, na kusababisha wananchi wengi waliokuwa kwenye mkutano huo kushangilia kwa kutumia salamu ya CHADEMA ya "Peoples Power" huku wakionyesha vidole viwili juu.

Hata hivyo ilibainika baadaye kuwa waliokuwa ndani ya ndege hiyo ni Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe , mgombea wa CHADEMA, Nassari, na kiongozi wa kampeni hizo Vicent Nyerere ambao walikuwa wakielekea kwenye mkutano wao wa mwisho eneo la Maji ya Chai.

Naye mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani aliwalalamikia makada wa CHADEMA kwa kumsakama kuwa ni mganga wa kienyeji wakati yeye ni muumini mzuri wa Kanisa la Anglikana.

http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=34264
 
but if not mistaken Mh. Mwigulu Nchemba alisema hii ndio style yao ya kuwin Arumeru sasa labda walifanya research wakagundua WAmeru wanapenda matusi na cyo sera za maendeleo! Hii ni dharau kubwa kwa wanaArumeru!
 
Si kila kitu cha kuamini hapa JF. Nimejifunza jambo hili, kuna ID Zikitupia thread nasoma kwa uhakika bila ya shaka yoyote. Lakini kuamini kuwa upo uwezekano wa mtu kutamka maneno kama haya hadharani, tena kwenye kampeni. Tusifikie huko, ushabiki wa mambo ya kisiasa usifike hapa. Wakati wa kampeni ni kweli huwa kuna vijembe vingi tu. Lakini kwa matusi aliyoweka huyu bwana hapa, anataka kutufanya akili zetu punguani. Tuachane na aina hii ya ushabiki. Uchaguzi utapita, wanachama wa CHADEMA, CCM na vyama vingine pamoja na sie tusio na vyama. Wote tunaishi katika jamii moja, tunachangia misikiti, makanisa, mahosptali nk. Propaganda za aina hii zitupishie mbali.

Kuna Video na Audio zitawekwa hapa, stay tuned! Tumpe muda mleta mada
 
Mbona mleta uzi karudi mikono mitupu? Wamepotea! Ndadhani wanaisaka hiyo video. Acha tuvute subira.
Kwani ulimpa nauli, kwanza hana haja ya kuleta video Lusinde anajulikana kama wewe humjui hiyo ni shida yako, na shida yako usituhusishe wengine.
 
mimi ndio mtoa mada YPlus
Huwa naogopa sana kutoa mada nisiyokuwa na ushahidi nayo,kwa hili nawahakikishia ni kweli kwa asilimia zote,nimehangaika sana ku upload hii kitu bado sijafanikiwa lakini nashukuru mpaka sasa ninesha wapatia watu kwa njia ya cd na pale kambini cdm cd zinagawiwa kwa kila anaye hitaji,bado naendelea na zoezi la kuupload hadi nifanikiwe,nitatoa link hapa.
Haya matusi ya Mh Lucinde sio siri nawahakikishia mtayasikia tu labda msifuatilie ila ninauhakika kila sehemu Tz hii yatafika.
 
mimi ndio mtoa mada YPlus
Huwa naogopa sana kutoa mada nisiyokuwa na ushahidi nayo,kwa hili nawahakikishia ni kweli kwa asilimia zote,nimehangaika sana ku upload hii kitu bado sijafanikiwa lakini nashukuru mpaka sasa ninesha wapatia watu kwa njia ya cd na pale kambini cdm cd zinagawiwa kwa kila anaye hitaji,bado naendelea na zoezi la kuupload hadi nifanikiwe,nitatoa link hapa.
Haya matusi ya Mh Lucinde sio siri nawahakikishia mtayasikia tu labda msifuatilie ila ninauhakika kila sehemu Tz hii yatafika.
yplus, wewe endelea na shughuli zako hawa anaokuomba video wanajulikana ma tomaso, kwanza wamekupa pesa ya ku upload? kama wanataka wawasiliane na jamaa zao kambi ya CDM Arumeru watapata usuumize kichwa bure wakati tayari CD ziko mitaani Arusha.
 
Kwani ulimpa nauli, kwanza hana haja ya kuleta video Lusinde anajulikana kama wewe humjui hiyo ni shida yako, na shida yako usituhusishe wengine.

We naye na hoja zako za kitotoo! Haya bwana. Nimekusikia, najisikia uvivu kujibu post zako kwani naona hazijibiki zaidi ya kukoroga ubongo tu. Acha nikuache na utoto wako huo.
 
We naye na hoja zako za kitotoo! Haya bwana. Nimekusikia, najisikia uvivu kujibu post zako kwani naona hazijibiki zaidi ya kukoroga ubongo tu. Acha nikuache na utoto wako huo.
Huna hoja umeambiwa CD ziko mitaani wewe unalazimisha uletwe who are you katafute huko...ala.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom