Mgongano: Serikali Vs. Mwanahalisi - Mipaka ya Maoni?

Yaap,safi sana na ndilo nililotarajia kusikia. Sasa walichokua wanahangaikia polisi kwa fujo zoote ni ni hasa?
 
Halisi,
Mku shukran..turushie habari zaidi..

Mwanakijiji,
Mkuu navyofahamu mimi Polisi wanaweza kukuita Kituoni kwa ajili ya kuchukua maelezo yako kuhusiana na swala fulani bila warrant kwa sababu haupo chini ya usalama (under arrest). Na unaposhindwa kufika ndipo wao huchukua warrant na kuja ofisini ama nyumbani kukutafuta, hivyo hapa tulipo hakuna kati yetu anayefahamu kama sasa hivi wanayo hiyo warrant ama hawana. Kumbuka tu Bongo warrant inaweza kutolewa kama cheti cha ndoa halmashauri ya jiji...

Mimi kinachonikosha zaidi ni jinsi swala hili lilivyochukuliwa kuwa kubwa kiasi hicho... kwani kuna sheria inayokataza viongozi wa ndani wa CCM kutojenga kundi jingine dhidi kiongozi aliyepo ili uchaguzi ujao waweze kumweka mtu wao?..

Hadi hapa sioni kama Kina Lowassa walikuwa na mbinu ya KUPINDUA serikali ya Kikwete isipokuwa kumwondoa kama mgombea wa kiti cha CCM ktk uchaguzi ujao.. of which sio kuvunja sheria.

Pili hili ni swala la ndani ya chama, ndani ya Chadema wanaweza kabisa kuunda kundi la kumwondoa Mbowe ktk Uenyekiti na pengine kusimama kwa tiketi ya chama uchaguzi wa 2010. Hawavunji sheria yoyote isipokuwa sisi sote tunatazama ni kina nani wanaotaka kufanya hivyo kutoa hukumu zetu..jambo la muhimu ni wanachama wa CCM kujihadhali na kundi hili litakalo wawakilisha..Kikwete mwenyewe alijiandaa hivyo hivyo kwa miaka kibao kupingana na wana CCM wengine watakao simama kugombea Urais, Nyerere aliweza kuwatangaza kina Mwinyi na Mkapa ktk mbinu kama hizi kuhakikisha mtu fulani (kikwete na Lowassa) hawachukui kiti cha Ikulu.

Iweje hili swala liwe la kitaifa la lenye kuhitaji nguvu ya kituo cha Usalama hali ni mambo ya ndani ya chama!.. Magazeti yetu yaliandika mengi kuhusiana na mbinu hizi hasa wakati wa uchaguzi wa mwaka 1995 - Kikwete vs Mkapa, mbona sikuona mtu akitafutwa!
 
Upumzike mahali pema kaka kubenea - bado hujaandika na kuwajibu tanzania kuhusu tuhuma zako za kutembea na mke wa mtu , tuko na wewe bado -- wengine ni wanaharakati wa ukimwi na haki za wanawake

MOD tafadhari hebu hakikisha status ya Shy ni yeye au amekuwa hacked?
 
Whaaaat? JF bwana!

Wakuu heshima mbele sana, so far bado hatuna habari za uhakika sana kuhusu Kubenea, either mahali alipo au kama ni mzima, lakini kama kawaida tuko on top of this ishu na soon tutakua na something on it,

Sasa hivi na toka jana tumekwua tunapekua kila mahali na tumeshawaarifu wote wanaohusika na amani nchini kuwa tunawa-hold responsible kwa 100% na this, kwa sababu tayari tunajua nani aliyeonekana naye dakika za mwisho kabla hajapotea, na jina tunalo.

Na ushaidi upo wa wazi, wa nini aliambiwa na Rostam, na pia alichoambiwa na Lowassa aliyedai kuwa ametumwa na muungwana kumfikishia huo ujumbe, yes kama hakuonekana ina maana kuna uhusiano wa hayo maneno na kupotea kwake, kwa sababu tunazo records.

Ninaamini kuwa Shujaaa Kubenea, ni mzima na yupo salama tena kwa 100%.

Ahsante Wakuu

Mkulu, I hope haya mambo wanayotaka kushinikiza yafichuke hayatapelekea kukamatwa kwa 'informers'. Taifa letu liko kwenye wakati mgumu ambapo skendo baada ya skendo zinazidi kufichuka. Bila the likes of Mwanahalisi, Kulikoni na ThisDay, mengi tusingelijua. Hivyo basi ni muhimu sana kwa watu kama SK kuhakikisha sources za information zao hazi-leak na kuhatarisha maisha ya hao informers.

Mamlaka za Dola ni sharti zielewe kuwa, whatever hizi critical media zimekuwa zikichapisha ni representation kubwa sana ya hali halisi kuakisi kile jamii inachotaka kukijua, kukikemea na kukitatua kwa ajili ya maisha bora wanayotarajia na wangelipenda kuwa nayo.

Leo hii wakifungia MwanaHalisi, 3months down the line, naamini kutajitokeza MwanaHalisi nyingine ku-cover demand hii ya jamii katika kufichua maovu ambayo yamevunda na kunuka mpaka sasa yanashindwa hata kufunikwa kwa zuria.

SteveD.
 
Wako jengo la mbao lililopo nyuma ya jengo kubwa la Wizara ya Mambo ya Ndani, eneo ambako kuna kitengo cha intelijensia ya polisi.

Mkuu wa timu inayomhoji Kubenea anasema anasubiri wenzake ambao wako mbali kidogo, anafika mmoja, anasema bado mwingine yuko Temeke anakuja.

Wakili Marando anawaambia kwanini wasifanye mahojiano yao kesho baada ya yeye kutoka Mahakamani, wanasema wasubiri tu atawajibu. Watu wengine wawili wanatolewa nje, anabaki Kubenea na Marando.
 
mmmh, naona kama mpango ulikuwa kumchukuwa kubenea kimya kimya ili waweze kumminya vizuri basi wamenoa.
 
Yaani hapo nasema wakilifungia wahakikishe hawalifungulii tena,maanke wakilifungulia watakua wamelitangaza kwa bei bure na watazidi kuumbuka.Hata kesi yenyewe watakua wameikuza sana,au Jk nae kashtukia itakua hivyo ili Watanzania wasikie waone Rais anawindwa na watu wabaya?
 
Upumzike mahali pema kaka kubenea - bado hujaandika na kuwajibu tanzania kuhusu tuhuma zako za kutembea na mke wa mtu , tuko na wewe bado -- wengine ni wanaharakati wa ukimwi na haki za wanawake

Nikijaribu kupata real image yako shy,Naona unafanana na avatar
 
Mkulu, I hope haya mambo wanayotaka kushinikiza yafichuke hayatapelekea kukamatwa kwa 'informers'. Taifa letu liko kwenye wakati mgumu ambapo skendo baada ya skendo zinazidi kufichuka. Bila the likes of Mwanahalisi, Kulikoni na ThisDay, mengi tusingelijua. Hivyo basi ni muhimu sana kwa watu kama SK kuhakikisha sources za information zao hazi-leak na kuhatarisha maisha ya hao informers.

Mamlaka za Dola ni sharti zielewe kuwa, whatever hizi critical media zimekuwa zikichapisha ni representation kubwa sana ya hali halisi kuakisi kile jamii inachotaka kukijua, kukikemea na kukitatua kwa ajili ya maisha bora wanayotarajia na wangelipenda kuwa nayo.

Leo hii wakifungia MwanaHalisi, 3months down the line, naamini kutajitokeza MwanaHalisi nyingine ku-cover demand hii ya jamii katika kufichua maovu ambayo yamevunda na kunuka mpaka sasa yanashindwa hata kufunikwa kwa zuria.

SteveD.

Mkuu Steve D,

Heshima mbele mkuu, maneno mazito sana mkuu na tupo ukurasa mmoja.
 
Wanamtisha hao, hawana chochote cha maana kwani kama wangekuwa serious wangekwisha mpeleaka mahakamani, unless wameona ukweli wanataka kupata more information
 
Mpaka sasa SK yupo makao makuu, kuna wadau wamefunga safari kuelekea huko, watatuhabarisha kinachoendelea.
 
Back
Top Bottom