BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
Rais Mstaafu wa Awamu ya 4 Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana wamemwandikia Barua Saed Kubenea na Gazeti lake la Mwana Halisi wakimtaka kutimiza madai yao mawili ambayo ni 1. Kufuta Kashfa Dhidi yao na Kuomba Radhi 2. Kuahidi Kuacha Kuwakashifu kutokana na chapisho la kuwahusisha na kupinga Uwekezaji wa Dubai katika Bandari za Tanzania.
Kwa mujibu wa Barua ya Ofisi ya Mawakili ya Eric S. Ng'maryo Advocates, Kubenea na Kampuni yake hiyo wanadaiwa kuchapisha taarifa katika Gazeti Namba 413 Alhamisi ya Julai 20, 2023 mpaka 26 Julai likiwa kashfa zilizoelezwa kuwafedhehesha, kutweza na kuwashushia hadhi viongozi hao.
Aidha, barua hiyo imesema Gazeti la Mwana Halisi limechapisha taarifa kuwa Kikwete na Kinana wamekuwa wakiwalipa watu fedha ili waendelee kupinga uwekezaji wa Bandari.