Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

Huku Bukoba nako kimenuka nipo Bukoba mjini hakuna walimu walioenda kazini na sekondari ndo kabisa hazina watu
:israel:
 
Safi sana mbeya fungeni na mpaka wa tukuyu,mpaka kieleweke hakuna kulala yeye mwacheni alale kwenye majamvi na mkeka huko msoga na bado mgomo wa wafanyakazi wote nchi nzima.
 
kama tunavyofahamu kuwa leo walimu kote nchini wameanza mgomo wao kuishinikiza serikali kuwatatulia matatizo yao taarifa kutoka sehemu mbalimbali zinaonyesha kwamba walimu wameamua kufanya kweli,bravo all teachers.
 
Katika mkoa wa Kilimanjaro:

Katika shule za msingi walimu wakuu wameonekana wakiwahi shuleni huku wakiwa hawaelewi mgomo upo vipi "Mi siwezi kugoma nimebakiza mwaka mmoja kustaafu" mwalimu mkuu mmoja alisema.

Hali hii inaonekana kuwa mgomo huu hauna nguvu walimu wakuu wanawalazimisha walimu wao kufundisha..

Nako mkoani Arusha hali ni tete, nikiwa Karatu Mjini shule nazo hazina walimu, wanafunzi; wapo walimu wakuu hasa wale wenye umri wamekuwa waoga kugoma
 
Naambiwa ofisi za mkuu wa wilaya na halmashauri ya wilaya ya Mbozi (Vwawa) zimezingirwa na wanafunzi kutoka shule za Mwenge, Hhaloli, Ichenjezya, Isangu, Mbimba, Ilolo, Makatani n.k!

Kazi kwelikweli, halafu naambiwa Tunduma wazazi nao wameungana na wanafunzi geti la kuingilia Zambia limefungwa na wamechoma boma ndogo ya Tunduma!
 
goma goma goma goma gomaaaa!!! mgomo mgomo mgomo mgomo!! yap hil ndo lugha unayosikka na wanasiasa wetu!! goma mkuu goma..gomeni tuuuuuuuuu!!!!
 
Naambiwa ofisi za mkuu wa wilaya na halmashauri ya wilaya ya mbozi(vwawa) zimezingirwa na wanafunzi kutoka shule za mwenge,haloli,ichenjezya,isangu,mbimba,ilolo,makatani etc! Kazi kwelikweli,afu naambiwa Tunduma wazazi nao wameungana na wanafunzi geti la kuingilia zambia limefungwa na wamechoma boma ndogo ya Tunduma!

Msaada tafadhali maana ya boma.
 
Serikali ya awamu ya nne ndo pekee haikubahatika kuwa na viongozi wenye busara na hekima licha ya akili tu za kuzaliwa na ndio maana badala ya kutatua matatizo ki-professional inatumia mbinu dhaifu za kwenda mahakamani. Ubinafsi na uchu wa kupenda utajiri ndio unaotumaliza itabidi ifike mahali tuwaite wazungu warudi tena kututawala.
 
Shule ya Secondary St Francis Mbeya wao wamekataa kugoma wamegundua ni upuuzi tu wa walimu wa Serikali kwani wao madai ya mishahara haiwahusu wanalamba mpaka netpay za 2M
 
wakuu sasa tujipange kwenda kulinda msitu wa mabwepande usiku huu Mkoba rais wa cwt anaweza akatia timu,bado kuna walimu wasaliti hasa hawa wa vodafasta na diploma ndio wanatuangusha degree wanaonyesha ushirikiano mzuri kumtia displini 3Dr Jk.
 
DHARAU HAIFAI,SERIKALI INAWADHARAU WALIMU! KAZI ZA WALIMU:
- Kufundisha/kuelimisha
- Kulea
_ Kusaidia serikali katika sensa
- Kusaidia serikali katika uchaguzi mkuu
HAPO SERIKALI YA CCM IACHE KUWADHARAU,LA SIVYO UTAWALA WAKE UNAKARIBIA KIKOMO!
 
Shule ya Secondary St Francis Mbeya wao wamekataa kugoma wamegundua ni upuuzi tu wa walimu wa Serikali kwani wao madai ya mishahara haiwahusu wanalamba mpaka netpay za 2M

...wa shule binafsi haya hayawahusu.
 
Shule zote wilaya ya serengeti walimu hawajafika, madaftari ya kusaini maudhurio yamefichwa. Naambiwa baadhi ya shule maeneo ya Musoma walimu waliofika mashuleni wamerushiwa mawe na viongozi wa CWT.
 
Back
Top Bottom