Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

Wanaenda kufungua kesi juu wenzao walio maliza mwaka jana.wakafaulu lakini hawajui kusoma...

waenda mahakani kufunga kesi........??? siku POLICE WAKIGOMA itakuaje nasiku MAHAKAMA wakigoma itakuaje ???kweli kuishi kwingi utaona mengi poleni wa TZ.....
 
hata me nina wasiwasi sana unajua kuna mtaalamu simkumbuki alisema makundi matatu ya watu wanaoreact kama vichaa ni wanafunzi,washabiki wa mpira na police.sasa leo naogopa hasa hawa wa Primary
 
Huku Wilaya ya Same nako kimenuka.

Nimepita shule za Njoro, Ishinde, Majevu, Kisima, Makanya na Nkwini hakuna waalimu shuleni wanafunzi wametelekezwa
 
Nimekutana na walimu wa shule ya msingi kongowe kibaha wanarudi nyumbani wanasema mgomo upo hadi kieleweke shuleni wamemuacha mwl mkuu pekee yake. Hivyo hivyo walimu wa mwambisi na tandau kata ya kongowe
 
Nchi inatengeneza jamii ya kesho inayojifunza kudai haki kwa maandamano!....serikali timizeni ahadi zetu za kuwatumikia wananchi na kuwapa haki yao
 
Tunduma wanafunzi wakati wanaandamana, FFU wamewapiga bomu la machozi, sasa watu wakubwa wameingilia, gate la kwenda Zambia limefungwa kwa muda hakuna gari kuvuka!
 
Nipo huku Tabora, shule nyingi za mjini zimefungwa waalimu wamegoma, isipokua shule moja tu ya Msingi Mtendeni wapo waalimu wawili tu..

Nitaendelea kuwajuza..
 
Manispaa ya Shinyanga nako wamegoma, shule wameachiwa walimu wa field walimu wako vijiweni wanajadili mechi ya Yanga na Azam
 
wanaongozwa na nani si rahisi wanafunzi wa shule ya msingi kujikusanya na kufanya kitu kama hicho
Hizi siyo zama ambazo ulisoma wewe, Mwanafunzi wa chekechea anaweza kupembua Mchele na Pumba, waacheni wawaburuze Walimu wao mahakamani kwani nao wanayohaki hiyo.
 
Mgomo wa waalimu hautaiathiri sana serikali bali watoto wanaosoma shule za St. Government ambao pia wataathirika walimu wao watakapoenda kufanya sensa. Wenzao wa za kulipia wataendelea kula kitabu kama kawa. Matokeo yake, hawa wa serikali watakapokuwa wakubwa watatawaliwa na hawa akina Riz 1...
 
Back
Top Bottom