Mgomo wa Wahadhiri na Wanafunzi UDOM 2011

Nikisikia vitoto vya UDOm natamani kuwahi Uani. kwani hawa siyo waliomchangia Jua kali fedha za kununua fomu? leo wanataka pesa kwa ajili gani? Wamefungua shina la wakereketwa chuoni (aibu)na walikuwa wa kwanza kulaani CDM kususia hotuba ya Jua kali. Afande Yapige mabomu hayo yakiaandamana au yakigoma.
 
Hayo madai ni madai gani? Kwa nini hao wanataaluma hawafungui kesi mahakamani ? Au wanalengo ya kuchafua jina la UDOM na mafanikio ya serikali kujenga Chuo Kikuu kizuri kwa muda mfupi tu ?
Naushauri uongozi wa UDOM uchukue hatua za kisheria dhidi ya hao wanataaluma wa UDOM wanaleta “migomo-siasa” ambayo haifuati sheria za kazi za Tanzania. Mfanyakazi ana haki ya kugoma, lakini utaratibu unaeleweka kisheria. Ninavyofahamu chama cha wanataaluma sio chama cha wafanyakazi (Trade Union) kinachoweza kuitisha mgomo. Hata kama wanataaluma wamefikia uamuzi wa kugoma lazima wafuate sheria za kazi.
Huu utamaduni wamigomo isiyofuata sheria ni kansa mbaya sana inayotafuna utawala wa sheria. Imefikia wakati sheria za kazi zitumike dhidi ya migomo-siasa na hao wanataaluma watakuwa ni mfano mzuri sana wa utawala wa sheria.
Basi kawafukuze wote wewe juha.
 
udom ata wakiandamana wapigwe mawe ata wafe! Ni wanafiki. Ndo waliomchangia jk fedha za kuchukulia form.wangeziweka zingewafaa muda huu.
 
udom ata wakiandamana wapigwe mawe ata wafe! Ni wanafiki. Ndo waliomchangia jk fedha za kuchukulia form.wangeziweka zingewafaa muda huu.
mkuu talk like a great thinker, umeambiwa mara ngapi kwamba waliomchangia kikwete ni mamluki wachche waliopo ndani ya Uom na sio wote?
wanafunzi wa Udom wapo wangapi? na kama wote wangechanga si pesa zingekuwa zaidi ya hizo milioni mbili? nakubali kwamba kuna mamluki wa ccm pale, lakini sio wote, do not genersalise issues. mbona hata vyuo vingine nako wapoa makada wa ccm na wa vyama vinine pia?
acha kuhukumu kishabiki, talk with facts ndg yangu wewe ni great thinker
 
1. UDOMASA

University of Dodoma, Chimwaga Complex, P.O. Box 259,Udom, Cell +255 755 210310 +255 755 210310 ,
+ 255 784 855444 + 255 784 855444 , + 255 712 792561 + 255 712 792561 , Email: khamismkanachi@yahoo.com

TAARIFA YA MATATIZO YANAYOWAKABILI WAFANYAKAZI WANATAALUMA WA CHUO KIKUU CHA DODOMA

Utangulizi

Tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) mwaka 2007 kumekuwa na maendeleo makubwa ya miundo mbinu mbalimbali hasa majengo na barabara. Chuo kimepanuka kwa kiwango cha kuridhisha na hii ni hatua ya kupongezwa na mpenda maendeleo yeyote.

Sanjari na ujenzi wa miundo mbinu kutokana na kuongezeka kwa udahili wa wanafunzi watumishi wa fani mbalimbali wamekuwa wakiajiriwa tangu kuanzishwa kwa chuo. Katiba ya Chuo (University Charter) imeweka wafanyakazi katika makundi makuu mawili. Moja ni kundi lenye wafanyakazi wanataaluma ambao pamoja na mambo mengine kazi yao kubwa ni ufundishaji, utafiti na ushauri; na pili ni kundi la wafanyakazi wa upande wa utawala. Hata hivyo chuo kinakua kwa haraka sana na hivyo kuhitaji idadi ya wafanyakazi iendanayo na kasi ya ukuaji wa chuo.

Matatizo ya Wafanyakazi Wanataaluma UDOM

Pamoja na jitihada nzuri ya kuajiri wafanyakazi ili kukidhi mahitaji ya chuo, kumekuwapo matatizo mbalimbali yanayowakabili wafanyakazi katika Chuo Kikuu cha Dodoma. Matatizo makubwa yanaegemea katika swala la malipo ya stahili mbalimbali pamoja na mishahara kama inavyoelekezwa katika nyaraka mbalimbali za serikali. Mkutano wa 4 wa UDOMASA umeainisha matatizo hayo ni kama yafuatavyo:

Mosi, wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma hawajapata mishahara mipya tangu kutangazwa kwa ongezeko la asilimia 20-30 mwezi Julai 2010 kupitia Waraka wa Msajili wa Hazina namba 4, wa mwaka 2010 uliotolewa 3 Agosti 2010. Ushahidi toka Hazina umeonesha kwamba mishahara mipya ililipwa mwezi Novemba 2010 kwa vyuo vikuu vyote vya umma ikiwamo Chuo Kikuu cha Dodoma. Mkutano umeazimia kwamba fedha hizo za mishahara ambayo menejimenti ya UDOM imekata kupitia mishahara mipya ya Hazina zilipwe kwa wahusika mara moja wakati mkutano wa wanataaluma unaendelea.

Pili, Hazina imekuwa ikilipa mishahara ya juu katika ngazi husika lakini menejimenti ya UDOM inapunguza kwa visingizio mbalimbali. Kwa mfano, mfanyakazi mwenye Check No 11818320 (PUTS 15), Hazina mwezi Novemba na December ilimlipa 2,269,890/=, Chuo kilimlipa 1,605,310/= jambo linaloashiria udanganyifu. Payroll ya Hazina inaonesha kuwa fedha inayotoka hazina ni tofauti na fedha anayolipwa mwanataaluma hapa UDOM. Wanataaluma wana wasiwasi kuwa tabia hii ya kupunguza mishahara imekuwa ikiendelea kwa muda sasa. Hivyo, mkutano umeazimia kuwa fedha zote ambayo menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dodoma imekuwa ikikata zilipwe.

Tatu, upunguzwaji wa mishahara inayotoka Hazina kimsingi umeathiri uchangiaji wetu katika mifuko ya hifadhi ya jamii (NSSF, LAPF, PPF, PSPF n.k.), pamoja na michango yetu katika vyama vya wafanyakazi kama vile RAAWU. Hali hii ya upunguzwaji mishahara pia umeathiri uchangiaji wa mwajiri katika mifuko ya hifadhi ya jamii kama inavyotakiwa na sheria husika. Mfano mfanyakazi anayelipwa 853,300/= badala ya 1,248,070/= kama ilivyo katika payroll ya hazina anachangia LAPF kiasi cha 42,665/= (asilimia 5) kwa mwezi badala ya 62,403.3/= kwa mwezi. Pia uchangiaji wa mwajiri unapungua hali ambayo itaathiri mafao ya uzeeni. Mkutano umeazimia kuwa kiasi chochote ambacho kilipunjwa katika mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na vyama vya wafanyakazi ilipwe mara moja wakati wanataaluma wanaendelea na mkutano wao.

Nne, Chuo Kikuu cha Dodoma kimekuwa kikitoa salary slips zake badala ya kutoa salary slips zinazotka Hazina. Aidha menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dodoma imedai kuwa Hazina haitoi salary slips. Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na uongozi wa UDOMASA umeonesha kuwa salary slips zimekuwa zikichukuliwa kutoka hazina na maafisa wa UDOM. Madai ya menejimenti ya UDOM kuwa hazina haitoi salary slips yanaashiria mbinu inayotumiwa kupunja mishahara ya wafanyakazi inayotoka Hazina. Mkutano umeazimia kuwa kila mfanyakazi apatiwe salary slips zake tangu Hazina waanze kutoa.

Tano, fedha za kujikimu wakati wa kuanza ajira pamoja na usafirishaji wa mizigo wakati wa kuja kuanza kazi hatujalipwa. Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dodoma imeripotiwa mwaka 2008 ikisema kuwa zaidi ya asilimia 95 ya wafanyakazi wa taasisi hii hawakustahili kulipwa fedha za kujikimu. Mazungumzo ya hivi karibuni yamepelekea menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dodoma kukubali kuwa fedha za kujikimu ni stahili ya mfanyakazi yeyote anapoanza kazi, ingawa wamesema kinagaubaga kuwa haitaweza kulipa stahili hizo kwa sasa kwa kisingizio kuwa ni fedha nyingi sana. Mkutano umeazimia kuwa Chuo Kikuu cha Dodoma kilipe stahili hizi kwa wafanyakazi wote. Zoezi hili la malipo ya fedha ya kujikimu lifanyike mara moja wakati wanataaluma wakiendelea na mkutano wao.

Sita, katika kikao cha tarehe 29 Desemba, 2010 kati ya menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dodoma na viongozi wa UDOMASA iliripotiwa na menejimenti ya chuo kuwa wafanyakazi 409 hawajasajiliwa katika payroll ya Hazina. Aidha menejimenti imeshindwa kutoa sababu za msingi kwa tatizo hili licha ya kuwa wafanyakazi hao wameshafanya kazi kwa miezi kadhaa sasa. Mkurugenzi wa Rasilimaili Watu katika Chuo hiki alitoa sababu zisizoweza kuaminika kuwa Hazina ndiyo yenye matatizo. Aidha, uongozi wa UDOMASA imeuliza swala hili Hazina lakini lawama zilirudishwa menejimenti ya UDOM. Hali hii ya kutoingizwa wafanyakazi katika Payroll ya Hazina, pamoja na mambo mengine unapelekea wafanyakazi wa UDOM kuishi kwa mashaka makubwa kwa kuwa menejimenti ya UDOM imekuwa ikitenda kazi zake si kwa kuzingatia kanuni bali kwa vitisho. Mkutano umetoa umeazimia kuwa wafanyakazi wote ambao mpaka sasa walikuwa hawajaingizwa kwenye payroll ya Hazina wawe wameingizwa ifikapo mwisho wa mwezi Januari, 2011. Aidha, ofisi iliyohusika na uzembe huu ndani au nje ya menejimenti ya UDOM iwajibike.

Saba, Chuo Kikuu cha Dodoma kimeandaa Sera ya Mazishi ambayo inafanya mwajiri kukwepa wajibu wake wa kisheria. Menejimenti ya UDOM kwa miezi kadhaa sasa imekuwa ikikata 3,000/= kwa wafanyakazi kila mwezi bila idhini ya waajiriwa. Na uwajibikaji wa fedha haupo wazi. Hali hii inaashiria kuwa menejimenti ya chuo inafanya kazi nje ya kanuni na sheria zinazosimamia makato ya fedha. Mkutano umeazimia kuwa chuo kisimamishe ukataji huo na timu huru iundwe na isimamie fedha hizo, wakati wadau wakifanya mchakato wa kuijadili upya kuhakikisha inakidhi mahitaji yao, na mwajiri hakwepi jukumu lake.

Nane, lingine ni kutokuwepo kwa samani katika ofisi za wanataaluma na wengine hawana ofisi kabisa. Tatizo hili la samani na vitendea kazi vingine limefanya mazingira ya kazi kuwa magumu mno kwa utendaji wa wanataaluma kama vile ufundishaji na pia wanafunzi wameathirika kwa kuwa wanawakosa walimu wao maofisini. Vitendea kazi kama vile kompyuta na printer zipo katika baadhi ya ofisi ya wakuu wa idara pekee. Pia ukubwa wa madarasa unaadhiri utendaji wa walimu kwa kuwa baadhi ya madarasa yana idadi kubwa ya wanafunzi (mfano zaidi ya 1200 katika ukumbi mmoja). Mkutano umeazimia kuwa wanataaluma wote wapatiwe ofisi zenye samani (meza, viti, makabati, dustbin n.k), pamoja na vitendea kazi vingine kama kompyuta, projector ili kuweza kurahisisha mazingira ya kazi.

Juhudi zilizofanywa na UDOMASA kutatua matatizo tajwa

Matatizo yaliyoanishwa hapo juu ni ya msingi na yamekuwepo tangu kuanzishwa kwa chuo mwaka 2007. Jumuiya ya wanatalaamu (UDOMASA) imefanya juhudi mbalimbali bila mafanikio. Juhudi hizo ni kama ifuatavyo

Tarehe 17 Novemba, 2008 ulifanyika mkutano mkuu wa kwanza wa UDOMASA kwa ajili ya kujadili mambo ya msingi likiwemo suala la fedha za kujikimu. Jambo hili lilijadiliwa tena katika mkutano mkuu wa pili tarehe 18 Novemba, 2008. Pamoja na juhudi za uongozi wa UDOMASA kuongea na menejimenti ya chuo walijibiwa kuwa asilimia kubwa ya waajiriwa UDOM hawastahili fedha za kujikimu. Hali hii ilipelekea wanataaluma kugoma kufanya kazi, na baadaye wanataaluma watatu kusimamishwa kazi kwa kisingizio cha kuchochea mgomo huo. Waliosimamishwa kazi ni pamoja na Dr Kisanga, Titus Mpemba, na Rajab Chipila. Kutokana na kusimamishwa kwa wanataaluma hao umoja wao uliyumbishwa au kusambaratishwa kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja hadi hali ya umoja ilipofufuka mwishoni mwa mwaka jana, 2010 baada ya uongozi wa kwanza wa UDOMASA kumaliza muda wake kufuatia uchaguzi uliofanyika tarehe 19 Oktoba, 2010.

Tarehe 10 Novemba, 2010 uongozi mpya UDOMASA ulikwenda kuonana na menejimenti ya UDOM kwa ajili ya utambulisho lakini menejimenti ikawakataa kwa kisingizio kuwa hawakuwa na sifa za wanataaluma. Hata hivyo viongozi wapya wa UDOMASA waliiambia menejimenti ya UDOM kuwa wapo tayari kuachia ngazi iwapo menejimenti itatoa barua kueleza kutowatambua na kuthibitisha si wanataaluma, jambo ambalo halikutekelezwa. Siku chache baadaye mwenyekiti mpya wa UDOMASA, Paul Loisulie, alipokea barua kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo ambayo ilishauri kuwa viongozi wapya wa UDOMASA wanatakiwa kutumia muda mwingi ili kujiendeleza kimasomo na si kujiingiza katika siasa za UDOMASA. Barua hii ambayo kimsingi haikurejea kauli ya Makamu Mkuu wa Chuo ya kuwa viongozi wapya wa UDOMASA hawakuwa na sifa zinazotakiwa ilitafsiriwa na wana UDOMASA kuwa ni dhamira ya chuo kudhoofisha umoja wa wanataaluma hapa chuoni.

Baada ya muda si mrefu uongozi mpya wa UDOMASA uliomba kibali cha mkutano mkuu kutoka kwa DVC-PFA na kukubaliwa. Hivyo mkutano mkuu wa tatu ukafanyika tarehe 4 Desemba 2010 ambao pamoja ulijadili fedha za kujikimu, mishahara mipya kama inavyoelekezwa na waraka wa Hazina namba 4, 2010, na sera ya mazishi. Mkutano uliamua kuwa viongozi wa UDOMASA wafanye uchunguzi wa kinachoendelea kwa masuala ya fedha ya kujikimu na mishahara mipya.

Ufuatiliaji ulifanyika kwa kwenda Ofisi ya Utumishi wa Umma; Hazina; na Wizara ya Elimu. Hazina ilikiri kuwa mishahara mipya ilishapelekwa katika vyuo vikuu vyote kikiwamo Chuo Kikuu cha Dodoma. Aidha, Hazina iliongeza kuwa fedha ya kujikimu inatakiwa kulipwa kupitia Other Charges (OC) ya taasisi husika, kwa hiyo UDOM pia ilitakiwa kulipa fedha ya kujikimu kupitia OC.

Viongozi wa UDOMASA walipokwenda Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma waliambiwa kuwa ofisi hiyo inahusika na sera na kwamba masuala ya taasisi za umma yanashughulikiwa na Msajili wa Hazina. Wakaahidi kuwa wangetafuta utaratibu wa kuzungumza na Hazina. Jitihada za kuonana na Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu hazikuzaa matunda kwa kuwa wahusika hawakuwepo.

Baada ya kurudi kutoka katika ofisi za juu, uongozi wa UDOMASA ulifanya jitihada kuonana na Msaidizi wa Makamu Mkuu wa Chuo (Mipango, Fedha na Utawala) na Mkurugenzi wa rasilimali watu UDOM ambao walidai kuwa mishahara mipya imeletwa lakini ilikuwa na makosa makubwa. Pia walikiri kuwa fedha ya kujikimu zinatakiwa kutoka ndani ya chuo (OC) lakini ikadaiwa kuwa fedha hazitoshi kulipa wafanyakazi kwa kuwa ni wengi sana kwa sasa.

Tarehe 29 Desemba, 2010 uongozi wa UDOMASA ulikutana na menejimenti ya UDOM ambapo taarifa ya mishahara kuanzia 2007 hadi Novemba 2010 ilisomwa na Mkurugenzi wa rasilimali watu. Pia iliripotiwa kuwa wafanyakazi 409 hawakuwapo katika payroll ya hazina. Menejimenti ya chuo ilitoa lawama kwa hazina kwa matatizo yanayohusiana na mishahara, fedha ya kujikimu pamoja na wafanyakazi 409 kutokuwapo katika orodha ya hazina. Hivyo, baada ya majadiliano kikao kiliunda timu ya watu watano (Mkurugenzi rasilimali watu, Msarifu, Wawakilishi wawili wa UDOMASA, na mwakilishi mmoja wa RAAWU) ili kuweza kufuatilia matatizo hayo. Pia ilikubaliwa kuwa fomu ziletwe ili ziweze kujazwa na wafanyakazi ambao hawapo katika payroll ya hazina ili timu iweze kwenda nazo wiki ifuatayo. Aidha, ilikubaliwa pia Makamu Mkuu wa Chuo asionane na wafanyakazi kwa ajili ya kutakiana heri ya mwaka mpya mpaka hapo timu itaporudi kutoka Dar es Salaam.

Kinyume na makubaliano, Mkurugenzi rasilimali watu pamoja na Msarifu walikwenda Dar es Salaam siku iliyofuata hali ambayo iliwapa taabu viongozi wa UDOMASA pamoja na wafanyakazi kwa ujumla. Kutokana na hili viongozi wa UDOMASA walikwenda kumuuliza Naibu wa Makamu Mkuu wa Chuo (Mipango, Fedha na Utawala) kuhusu safari ya ghafla ya watu waliotakiwa kuwa katika timu ya kufuatilia matatizo, lakini alieleza kuwa safari ile ilikuwa ya mambo ya bajeti. Tuliamini kimsingi, bila ushahidi wowote.

Mwenyekiti na Katibu wa UDOMASA pamoja na Mwenyekiti wa RAAWU tawi la UDOM waliweza kuondoka tarehe 4, Januari 2011 kwenda Dar es Salaam kuungana na Msarifu na Mkurugenzi rasilimali watu kwa ajili ya kutatua matatizo yanayowakabili wafanyakazi kama ilivyokubaliwa katika kikao cha tarehe 29 Desemba, 2011.

Wakati tunaendelea kusubiri majibu kutoka timu iliyokwenda Dar es Salaam tuliona matangazo yaliyobandikwa katika mbao mbalimbali za matangazo yakidai kuwa Makamu Mkuu wa Chuo alitaka kuongea na wafanyakazi tarehe 6 Januari, 2011 saa nane mchana. Mkutano huu wa Makamu Mkuu wa Chuo na wafanyakazi ulikwenda kinyume na makubaliano ya kikao cha tarehe 29 Desemba, 2010. Hivyo, Makamu Mkuu wa Chuo alipomaliza kutoa taarifa katika mkutano wake na wafanyakazi, Makamu Mwenyekiti wa UDOMASA alimtaka ajibu madai ya msingi ya wafanyakazi (fedha za kujikimu, mishahara mipya) kwa kuwa alifanya mkutano kinyume na makubaliano. Aidha, Makamu Mkuu wa Chuo pia alitakiwa kueleza habari zilizozagaa kuwa chuo kililetewa mishahara mipya kuanzia Novemba, 2010 lakini chuo hakikuwa tayari kulipa kama ilivyoletwa kutoka hazina. Makamu Mkuu wa Chuo hakuweza kujibu. Aidha, katika mkutano wa Makamu Mkuu wa Chuo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Mipango, Fedha na Utawala) alieleza kuwa amepokea barua ikimshauri kuanza kupunguza deni la fedha ya kujikimu kupitia OC.

Tarehe 8 Januari, 2011 wanataaluma walifanya mkutano mkuu wa nne ikiwa pamoja na mambo mengine kupokea taarifa ya maswala muhimu ya stahili za wafanyakazi. Baada ya kujadiliana kuanzia saa nane mchana hadi saa 12 jioni mkutano uliahirishwa kwa masharti ya kuendelea siku ya Jumatatu ya tarehe 10 Januari, 2011.

Hitimisho

Kwa kuwa uongozi wa UDOMASA umefanya jitihada za kufuatilia utatuzi wa matatizo haya yanayohusiana na fedha katika Hazina; Wizara ya Elimu; na Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na kuonekana kuwa matatizo yapo hapa ndani ya chuo; na kuwa menejimenti ya UDOM mpaka wanataaluma wanakwenda kwenye mkutano haikuwa tayari kushughulikia matatizo haya, Mkutano Mkuu wa nne wa UDOMASA wa tarehe 8 Januari, 2011 uliamua umwombe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aingilie kati suala hili. Pia wanataaluma wameamua kuendelea kufanya mikutano mpaka hapo matatizo yatakapopatiwa ufumbuzi.

Paul Loisulie,

Mwenyekiti
UDOMASA.
 
colgate umefanya vizuri kuliweka huku, mimi ninashangaa mpaka hapa thread zinachakachuliwa sijui ni kwa nini au taarifa za UDOM zinausiri upi, nianomba moderator airudishe thread isemayo madai ya wahadhili udom lipi kati ya haya hapa ni ya msingi? ninaomba sana kwani kinyume na hapo nitajenga hisia hasi
 
kwa kweli tumechoshwa na ubadhilifu wa namna hii, halafu ni kwa nini vyombo vya habari havitangazi hii habari? hao viongozi kwa nini wasiwajibishwe, hebu wapeni haki yao ya msingi, wanafanya kazi kwa kweli kwa uvumilivu mkubwa, ningekuwa mm nisingeweza ningeacha kazi! Hongereni kwa mapambano, kilio chenu kitafika tu, 'KELELE ZA CHURA HAZIMZUII CHURA KUNYWA MAJI' msitishwe na kelele za chura nyinyi endeleeni kunywa maji
 
Vyombo vya habari vimeamua kutowatendea haki wafanyakazi hao, kwani wameenda kuongea nao na bado madai yao hawajayafikisha kwa umma, Taifa la Tanzania linaelekea wapi? kama vyombo vya habari vinafanya hivi watanzania tukimbilie wapi?
 
kwa kweli mkuu wa chuo na makamu wake wanatakiwa kukamatwa na kufungwa kabisa bila hata kufikishwa mahakamani,haiwezekani kabisa kikundi cha watu wachache wakawa wananufaika kwa jasho la wanataaluma wengine chuoni hapo wanakata pesa ya mishahara halafu wanamfanya mwanataaluma akose heshima na utu kwa kumnyima ofisi na samani hivi wanafunzi watawaheshimu kweli ,mwanataaluma lazima atumi computer kuandaa masomo hivi kweli anatayarishaje notes inamaana anaandika ubaoni kama shule ya msingi,hivi sio kuwaumiza wanataaluma kisaikolojia,kwa kweli ndugu mwenyekiti musitishike na hao watawala wa chuo hawana nia njema ni wezi ,watovu wa nidhami na hawajali utu poleni sana na kazeni uzi haki haiji kwa kubweteke shurti upambane kweli kweli
 
Wacha kudanganya watu. Wewe unaelewa fika unachosema si sahihi. Na ukweli unao.

I. Mishahara mipya
Unafahamu kwa takwimu ulizopewa na Menejimeti kuwa hayumkini kuwa HAZINA walileta mishahara mipya mwezi Novemba kama unavyodai.
Taarifa nilizonazo, umepewa copies za ex-chequers kuanzia mwezi wa saba zinazoonyesha kuwa UDOM imekuwa ikipokea fedha pungufu za mishahara toka HAZINA. Copies hizo zinaonyesha kuwa mwezi Oktoba na Novemba UDOM ilipokea kiasi cha fedha kinachofanana na hakuna ongezeko kama wewe na huyo jamaa wako wa HAZINA mnavyodai. Ushahidi huo unao.

2. Malipo ya fedha za kujikimu
Makamu Mkuu wa Chuo alishatolea maelezo kwenye mkutano wake na wafanyakazi kuwa Chuo kimeamua kutoa kwa awamu. Wewe hutaki wenzio walioanza kazi mwaka 2007 wapate pesa zao ndiyo maana unawadanganya.

3. Safari ya Msarifu na Mkurugenzi wa Rasilimali Dar es Salaam
Viongozi hawa wanaripoti UDOMASA au kwa Management? Uliambiwa baada ya kikao chenu kazi zote zilisimama. Wewe ni muongo, unajua kabisa kuwa viongozi hawa walikwenda Dar es Salaam kuwasilisha bajeti za mwaka ujao wa fedha. Kwa nini unataka kudanganya wenzio? Usitumie shida za wengine kujitafutia umaarufu.

4. Ulipwaji wa mishahara
Hakuna wizi kama unavyodai. Kama data clerk wa hazina alifanya makosa unataka na Menejiment ifanye makosa pia? Wewe una barua ya ajira inayoonyesha mshahara wako, unapopaswa kuanzia, nyongeza ya kila mwaka na kadhalika. Wewe mwenyewe umetia saini kukubali mkataba huo. Bila shaka unalipwa kulingana na barua yako ya ajira. Kama kuna kiasi kinazidi kutoka Hazina, Menejiment ya UDOM inapaswa kurudisha kinachozidi HAZINA. ukidai ulipwe haki si yako ni ufisadi. Mbona huzungumzii wafanyakazi wanaoletewa fedha pungufu za mishahara yao toka hazina kama wewe ni mkweli? Unavyowadanganya wenzako kuwa waendelee kudai tofauti ya kiasi cha mshahara unaotoka Hazina na unaolipwa na UDOM kwa mujibu wa mikataba yenu ya ajira unawapotezea muda. Hili haliwezekani hata kama utadai miaka 1000 wacha siku 2. Kulipwa tofauti unayodai ni kuvunja sheria na wewe unalijua hilo. Kwa kuwa serikali haiwezi kuvunja sheria, hata ukidai kwa rais wa jamhuri hawezi kusikilia upuuzi wako. Wewe unatia aibu wasomi wa nchi hii. Kumbe hujui hata sheria ndogo ndogo za kazi?

Sera ya Mazishi
Leo nimeona tangazo linalowataka wafanyakazi wasiotaka kuendelea na sera ya mazishi wajitoe, mbona hili husemi.

Bwana Paul Loisulie, wewe ulitumwa kwenda Dar kufuatilia masuala ya mishahara, umeshaieleza Menejimenti kilichojiri huko? Mmefikia muafaka gani na menejiment? Mbona husemi kama ulilipwa pesa za kwenda Dar kwa masuala hayo? Wewe ni mwizi, kwa nini umechukuwa michango ya wanachama wa UDOMASA wakati Menejimeti ya UDOM imekulipa zaidi ya laki nne kwa safari yako ya Dar kama posho ya kujikimu na nauli?

Sisi tunaipenda UDOM, tunataka watoto wetu wasomeshwe. Serikali ilishatangaza mishahara mipya na italipwa tu. Migogoro ya nini?
Mishahara kulipwa tofauti iachie Menejiment na HAZINA. Wewe kama ni Mzalendo kweli ifahamishe HAZINA ufisadi wa uongozi wa UDOM kisha waachie wenyewe washughulikiane. Kama una ushahidi zaidi wa ufisadi peleka TAKUKURU wafanye kazi zao. Mbona hili hufanyi?

Wewe umepoteza siku mbili bila kufanya kazi, je ukatwe mshahara? Kama sivyo, huu nao si ufisadi?

Menejiment ya UDOM ikikuchukulia hatua za kisheria utalia na nani? Usiwaponze wenzio bila sababu za msingi.

WEWE HUFAI KUWA MWENYEKITI WA UDOMASA. ACHIA WATU WENYE UWEZO NA UPEO NAFASI HIYO. KWA NINI HUTAKI KUJIFUNZA KUTOKA KWA MZEE SHIVJI AU MAREHEMU CHACHAGE ENZI ZA UDASA. HAWA HAWAJAHI KUWA NA MADAI YA KIPUUZI KAMA HAYA YAKO.
 
Yote yawekwe hadharani Watanzania walipakodi tujue. Na sasa tukipeleka ufisadi hadi mashuleni na vyuo vikuu hivi sasa tutakua tunategemea kuwapata wahitimu wa aina gani mwisho wa siku?

Mtu uzaliwe katika minyanyaso, macho yafunguke unakuta wazazi wako wako katika minyanyaso mtindo mmoja kwa serikali dhalimu, usome kiminyanyaso sasa kule kazini ndio utaweza kutenda haki kwa wengine kweli?

Kama taifa tunakwenda kubaya sasa, wapeni walimu kwa wanafunzi UDOM na vyuo vikuu vingine vyote nchini haki zao. Mpaka karibia kila taasisi inalia na kugoma nchini maana yake ni kwamba hakuna haki na kwamba kuna uwezekano mtu fulani mahali anakula haki za wengine kifichoni.
 
WE MAMKWE kibaraka mkubwa huna hoja vielelezo vyote UDOMASA wanavyo na copy zimeshatumwa TAKUKURU NA katika wizara zote husika. Hakuna mjadala hawa mafisadi lazima wafikishwe mahakamani. Umeona wapi mhahara wa serikali ukatofautiana kwa watu wa daraja moja???? Kashfa hii haikwepeki kirahisi tunajua uongozi wa UDOM umekua na kawaida ya kuwapatia bahasha baadhi waandishi wa habari wa dodoma ili wasiandike mambo mazito yanayohatarisha nyazfa zao lakini kwa hili la ufisadi ukweli utabainika.
 
Wacha kudanganya watu. Wewe unaelewa fika unachosema si sahihi. Na ukweli unao.

I. Mishahara mipya
Unafahamu kwa takwimu ulizopewa na Menejimeti kuwa hayumkini kuwa HAZINA walileta mishahara mipya mwezi Novemba kama unavyodai.
Taarifa nilizonazo, umepewa copies za ex-chequers kuanzia mwezi wa saba zinazoonyesha kuwa UDOM imekuwa ikipokea fedha pungufu za mishahara toka HAZINA. Copies hizo zinaonyesha kuwa mwezi Oktoba na Novemba UDOM ilipokea kiasi cha fedha kinachofanana na hakuna ongezeko kama wewe na huyo jamaa wako wa HAZINA mnavyodai. Ushahidi huo unao.

2. Malipo ya fedha za kujikimu
Makamu Mkuu wa Chuo alishatolea maelezo kwenye mkutano wake na wafanyakazi kuwa Chuo kimeamua kutoa kwa awamu. Wewe hutaki wenzio walioanza kazi mwaka 2007 wapate pesa zao ndiyo maana unawadanganya.

3. Safari ya Msarifu na Mkurugenzi wa Rasilimali Dar es Salaam
Viongozi hawa wanaripoti UDOMASA au kwa Management? Uliambiwa baada ya kikao chenu kazi zote zilisimama. Wewe ni muongo, unajua kabisa kuwa viongozi hawa walikwenda Dar es Salaam kuwasilisha bajeti za mwaka ujao wa fedha. Kwa nini unataka kudanganya wenzio? Usitumie shida za wengine kujitafutia umaarufu.

4. Ulipwaji wa mishahara
Hakuna wizi kama unavyodai. Kama data clerk wa hazina alifanya makosa unataka na Menejiment ifanye makosa pia? Wewe una barua ya ajira inayoonyesha mshahara wako, unapopaswa kuanzia, nyongeza ya kila mwaka na kadhalika. Wewe mwenyewe umetia saini kukubali mkataba huo. Bila shaka unalipwa kulingana na barua yako ya ajira. Kama kuna kiasi kinazidi kutoka Hazina, Menejiment ya UDOM inapaswa kurudisha kinachozidi HAZINA. ukidai ulipwe haki si yako ni ufisadi. Mbona huzungumzii wafanyakazi wanaoletewa fedha pungufu za mishahara yao toka hazina kama wewe ni mkweli? Unavyowadanganya wenzako kuwa waendelee kudai tofauti ya kiasi cha mshahara unaotoka Hazina na unaolipwa na UDOM kwa mujibu wa mikataba yenu ya ajira unawapotezea muda. Hili haliwezekani hata kama utadai miaka 1000 wacha siku 2. Kulipwa tofauti unayodai ni kuvunja sheria na wewe unalijua hilo. Kwa kuwa serikali haiwezi kuvunja sheria, hata ukidai kwa rais wa jamhuri hawezi kusikilia upuuzi wako. Wewe unatia aibu wasomi wa nchi hii. Kumbe hujui hata sheria ndogo ndogo za kazi?

Sera ya Mazishi
Leo nimeona tangazo linalowataka wafanyakazi wasiotaka kuendelea na sera ya mazishi wajitoe, mbona hili husemi.

Bwana Paul Loisulie, wewe ulitumwa kwenda Dar kufuatilia masuala ya mishahara, umeshaieleza Menejimenti kilichojiri huko? Mmefikia muafaka gani na menejiment? Mbona husemi kama ulilipwa pesa za kwenda Dar kwa masuala hayo? Wewe ni mwizi, kwa nini umechukuwa michango ya wanachama wa UDOMASA wakati Menejimeti ya UDOM imekulipa zaidi ya laki nne kwa safari yako ya Dar kama posho ya kujikimu na nauli?

Sisi tunaipenda UDOM, tunataka watoto wetu wasomeshwe. Serikali ilishatangaza mishahara mipya na italipwa tu. Migogoro ya nini?
Mishahara kulipwa tofauti iachie Menejiment na HAZINA. Wewe kama ni Mzalendo kweli ifahamishe HAZINA ufisadi wa uongozi wa UDOM kisha waachie wenyewe washughulikiane. Kama una ushahidi zaidi wa ufisadi peleka TAKUKURU wafanye kazi zao. Mbona hili hufanyi?

Wewe umepoteza siku mbili bila kufanya kazi, je ukatwe mshahara? Kama sivyo, huu nao si ufisadi?

Menejiment ya UDOM ikikuchukulia hatua za kisheria utalia na nani? Usiwaponze wenzio bila sababu za msingi.

WEWE HUFAI KUWA MWENYEKITI WA UDOMASA. ACHIA WATU WENYE UWEZO NA UPEO NAFASI HIYO. KWA NINI HUTAKI KUJIFUNZA KUTOKA KWA MZEE SHIVJI AU MAREHEMU CHACHAGE ENZI ZA UDASA. HAWA HAWAJAHI KUWA NA MADAI YA KIPUUZI KAMA HAYA YAKO.

Mkuu,
Naona unayazungumza haya kwa ufasaha mkubwa. Yaonesha ni mmoja ya viongozi wa UDOM..nimefuatilia posts zako, zina mlengo wa kufungana na serikali ya UDOM.

Ningependa kujua kama hayo yaliyoandikwa yana mantiki au hayana kuhusu madai ya walimu.
Kama wewe ndo shabani mlacha, kwanini toka 2007 watu hawajalipwa, wakati deni la dowans la juzi mnataka kwenda kulipa..Priority iko wapi??
 
Wacha kudanganya watu. Wewe unaelewa fika unachosema si sahihi. Na ukweli unao.

I. Mishahara mipya
Unafahamu kwa takwimu ulizopewa na Menejimeti kuwa hayumkini kuwa HAZINA walileta mishahara mipya mwezi Novemba kama unavyodai.
Taarifa nilizonazo, umepewa copies za ex-chequers kuanzia mwezi wa saba zinazoonyesha kuwa UDOM imekuwa ikipokea fedha pungufu za mishahara toka HAZINA. Copies hizo zinaonyesha kuwa mwezi Oktoba na Novemba UDOM ilipokea kiasi cha fedha kinachofanana na hakuna ongezeko kama wewe na huyo jamaa wako wa HAZINA mnavyodai. Ushahidi huo unao.

2. Malipo ya fedha za kujikimu
Makamu Mkuu wa Chuo alishatolea maelezo kwenye mkutano wake na wafanyakazi kuwa Chuo kimeamua kutoa kwa awamu. Wewe hutaki wenzio walioanza kazi mwaka 2007 wapate pesa zao ndiyo maana unawadanganya.

3. Safari ya Msarifu na Mkurugenzi wa Rasilimali Dar es Salaam
Viongozi hawa wanaripoti UDOMASA au kwa Management? Uliambiwa baada ya kikao chenu kazi zote zilisimama. Wewe ni muongo, unajua kabisa kuwa viongozi hawa walikwenda Dar es Salaam kuwasilisha bajeti za mwaka ujao wa fedha. Kwa nini unataka kudanganya wenzio? Usitumie shida za wengine kujitafutia umaarufu.

4. Ulipwaji wa mishahara
Hakuna wizi kama unavyodai. Kama data clerk wa hazina alifanya makosa unataka na Menejiment ifanye makosa pia? Wewe una barua ya ajira inayoonyesha mshahara wako, unapopaswa kuanzia, nyongeza ya kila mwaka na kadhalika. Wewe mwenyewe umetia saini kukubali mkataba huo. Bila shaka unalipwa kulingana na barua yako ya ajira. Kama kuna kiasi kinazidi kutoka Hazina, Menejiment ya UDOM inapaswa kurudisha kinachozidi HAZINA. ukidai ulipwe haki si yako ni ufisadi. Mbona huzungumzii wafanyakazi wanaoletewa fedha pungufu za mishahara yao toka hazina kama wewe ni mkweli? Unavyowadanganya wenzako kuwa waendelee kudai tofauti ya kiasi cha mshahara unaotoka Hazina na unaolipwa na UDOM kwa mujibu wa mikataba yenu ya ajira unawapotezea muda. Hili haliwezekani hata kama utadai miaka 1000 wacha siku 2. Kulipwa tofauti unayodai ni kuvunja sheria na wewe unalijua hilo. Kwa kuwa serikali haiwezi kuvunja sheria, hata ukidai kwa rais wa jamhuri hawezi kusikilia upuuzi wako. Wewe unatia aibu wasomi wa nchi hii. Kumbe hujui hata sheria ndogo ndogo za kazi?

Sera ya Mazishi
Leo nimeona tangazo linalowataka wafanyakazi wasiotaka kuendelea na sera ya mazishi wajitoe, mbona hili husemi.

Bwana Paul Loisulie, wewe ulitumwa kwenda Dar kufuatilia masuala ya mishahara, umeshaieleza Menejimenti kilichojiri huko? Mmefikia muafaka gani na menejiment? Mbona husemi kama ulilipwa pesa za kwenda Dar kwa masuala hayo? Wewe ni mwizi, kwa nini umechukuwa michango ya wanachama wa UDOMASA wakati Menejimeti ya UDOM imekulipa zaidi ya laki nne kwa safari yako ya Dar kama posho ya kujikimu na nauli?

Sisi tunaipenda UDOM, tunataka watoto wetu wasomeshwe. Serikali ilishatangaza mishahara mipya na italipwa tu. Migogoro ya nini?
Mishahara kulipwa tofauti iachie Menejiment na HAZINA. Wewe kama ni Mzalendo kweli ifahamishe HAZINA ufisadi wa uongozi wa UDOM kisha waachie wenyewe washughulikiane. Kama una ushahidi zaidi wa ufisadi peleka TAKUKURU wafanye kazi zao. Mbona hili hufanyi?

Wewe umepoteza siku mbili bila kufanya kazi, je ukatwe mshahara? Kama sivyo, huu nao si ufisadi?

Menejiment ya UDOM ikikuchukulia hatua za kisheria utalia na nani? Usiwaponze wenzio bila sababu za msingi.

WEWE HUFAI KUWA MWENYEKITI WA UDOMASA. ACHIA WATU WENYE UWEZO NA UPEO NAFASI HIYO. KWA NINI HUTAKI KUJIFUNZA KUTOKA KWA MZEE SHIVJI AU MAREHEMU CHACHAGE ENZI ZA UDASA. HAWA HAWAJAHI KUWA NA MADAI YA KIPUUZI KAMA HAYA YAKO.

Hebu tufafanulie huu mgomo ni wa mwenyekiti pele yake au ndio strategy za kumtisha kwa kumcall out naona tuhuma unaelekeza kama vile aliyoandika hayakuamuliwa na wanataaluma wote ebu tuweke wazi
 
Sera ya mazishi imeamuliwa na uongozi wa juu bila kuwashirikisha wafanyakazi tena wakuu wa vyuo wamejipa nafasi ya mwenyekiti na katibu bila kuchaguliwa. Shilingi 3000 kwa mwezi kwa wafanyakazi wapatao 1000 ni sawasawa na sh. milioni tatu, zinakwenda wapi zote hizo kama sio wizi. Leo baada ya uongozi kushikwa pabaya wanasema wanaotaka kujitoa kwenye sera ya mazishi wajitoe mbona hawakusema wanaotaka kujiunga sera ya mazishi wajiunge??????? wakaamua wao wenyewe na kukata pesa za watu bila idhini yao??????
 
Wacha kudanganya watu. Wewe unaelewa fika unachosema si sahihi. Na ukweli unao.

I. Mishahara mipya
Bwana Paul Loisulie, wewe ulitumwa kwenda Dar kufuatilia masuala ya mishahara, umeshaieleza Menejimenti kilichojiri huko? Mmefikia muafaka gani na menejiment? Mbona husemi kama ulilipwa pesa za kwenda Dar kwa masuala hayo? (1) Wewe ni mwizi, kwa nini umechukuwa michango ya wanachama wa UDOMASA wakati Menejimeti ya UDOM imekulipa zaidi ya laki nne kwa safari yako ya Dar kama posho ya kujikimu na nauli?

Sisi tunaipenda UDOM, tunataka watoto wetu wasomeshwe. Serikali ilishatangaza mishahara mipya na italipwa tu. Migogoro ya nini?
(2) Mishahara kulipwa tofauti iachie Menejiment na HAZINA. Wewe (3) kama ni Mzalendo kweli ifahamishe HAZINA ufisadi wa uongozi wa UDOM kisha waachie wenyewe washughulikiane. Kama una ushahidi zaidi wa ufisadi peleka TAKUKURU wafanye kazi zao. Mbona hili hufanyi?

Wewe umepoteza siku mbili bila kufanya kazi, je ukatwe mshahara? Kama sivyo, huu nao si ufisadi?

Menejiment ya (4) UDOM ikikuchukulia hatua za kisheria utalia na nani? Usiwaponze wenzio bila sababu za msingi.

WEWE (5) HUFAI KUWA MWENYEKITI WA UDOMASA. ACHIA WATU WENYE UWEZO NA UPEO NAFASI HIYO. KWA NINI HUTAKI KUJIFUNZA KUTOKA KWA MZEE SHIVJI AU MAREHEMU CHACHAGE ENZI ZA UDASA. HAWA HAWAJAHI KUWA NA MADAI YA KIPUUZI KAMA HAYA YAKO.

Wana jf kwa kuwa jamvi hili ni la Great Thinkers naomba hili swala la UDOM lijadiliwe nukta kwa nukta ili tuweze kuwatendea haki wenzetu walioonelea vema kuliwashilisha hapa kwetu.

Pamoja na yote huyu MaMkwe mpaka sasa keshaninyima kabisa raha kwa kumshambulia mtu ambaye anamjua peke yake kichwani bila kujali kuchambulia hoja baada ya hoja. Dalili hiyo si nzuri, kuna jambo hapo.

Lugha chafu na vitisho kama inavyoonekana kwenye wino mwekundu hapo juu ni ishara ya mtu kuelekea kupoteza kitu, keshapoteza au anapoteza katika mgogoro wa waalimu UDOM

Kusema kwamba baraza la waalimu wa chuo kikuu Dodoma (UDOMASA) kikae tu pembeni na kuacha watu wengine wizarani na menejimenti UDOM kuwaamulia maslahi yao siku watakapopenda wenyewe nao naiwekea bendera nyekundu. Kama hali halisi ndio hivyo basi hakuna haja ya baraza hilo kabisa chuoni hapo.

Kusema uzalendo wa mtu kwa taifa lake litaonekana tu kwa kufichaficha yanayowasibu na hasa ukiwa ni kiongozi si sahihi. MaMkwe kama alikua na mawazo mazuri kiasi hicho namna gani maslahi ya waalimu hapo chuoni kuboreshwa alikuwa na fursa nzuri sana wa kumshirikisha kiongozi wake huyu ndani ya vikao vyao vya UDOMASA na wala si kuja kutaka kumnyang'anya mwenzie kiti kinafiki hapa jukuani.

Nilivyoona mimi, waaalimu wasiyotendewa haki kuto kutokana na mtandao mpana wa tangu wizarani, UDOM menejimenti na hata pandikizi ndani ya vikao vya UDOMASA chenyewe ni vigumu sana wakajidanganya kudai 'kukipenda chuo chao na kutaka WOTOTO WAO wasome' kwa mtaji wa tumbo lililowazi na familia nyumbani isiyopata huduma sawa.

Wana jf, naona UDOM kuna tatizo kubwa kuliko tunavyofikiri hivyo tusiwabeze wanafunzi wala waalimu wao wanapogoma. Huyu MaMkwe ni kuogopwa kama ukoma na familia ya UDOM kwa sababu maelezo yake yaonyesha yeye anacheza kote kote tangu wizarani, UDOM uongozini na UDOMASA na pengine hata ndani ya serikali ya wanafunzi pale wakati yaonyesha wazi yeye ndio mzizi wa kilio chao. Jamii hiyo itakapombaini hivyo UDOM patakua hapatoshi.

Nachelea kusema kwamba huyu MaMkwe huenda asiwe RAFIKI SANA WA FAMILIA YA UDOM isipokua ni sehemu ya kupe inayozalisha shida kwao, leo na kesho.

Na kabla sijarudi kwa uchambuzi zaidi wa mada hii kwanza naanza kupitia michango yote ya MaMkwe ya tangu huko nyuma ndio nipate picha halisi hapa.
 
Wacha kudanganya watu. Wewe unaelewa fika unachosema si sahihi. Na ukweli unao.

I. Mishahara mipya
Unafahamu kwa takwimu ulizopewa na Menejimeti kuwa hayumkini kuwa HAZINA walileta mishahara mipya mwezi Novemba kama unavyodai.
Taarifa nilizonazo, umepewa copies za ex-chequers kuanzia mwezi wa saba zinazoonyesha kuwa UDOM imekuwa ikipokea fedha pungufu za mishahara toka HAZINA. Copies hizo zinaonyesha kuwa mwezi Oktoba na Novemba UDOM ilipokea kiasi cha fedha kinachofanana na hakuna ongezeko kama wewe na huyo jamaa wako wa HAZINA mnavyodai. Ushahidi huo unao.

2. Malipo ya fedha za kujikimu
Makamu Mkuu wa Chuo alishatolea maelezo kwenye mkutano wake na wafanyakazi kuwa Chuo kimeamua kutoa kwa awamu. Wewe hutaki wenzio walioanza kazi mwaka 2007 wapate pesa zao ndiyo maana unawadanganya.

3. Safari ya Msarifu na Mkurugenzi wa Rasilimali Dar es Salaam
Viongozi hawa wanaripoti UDOMASA au kwa Management? Uliambiwa baada ya kikao chenu kazi zote zilisimama. Wewe ni muongo, unajua kabisa kuwa viongozi hawa walikwenda Dar es Salaam kuwasilisha bajeti za mwaka ujao wa fedha. Kwa nini unataka kudanganya wenzio? Usitumie shida za wengine kujitafutia umaarufu.

4. Ulipwaji wa mishahara
Hakuna wizi kama unavyodai. Kama data clerk wa hazina alifanya makosa unataka na Menejiment ifanye makosa pia? Wewe una barua ya ajira inayoonyesha mshahara wako, unapopaswa kuanzia, nyongeza ya kila mwaka na kadhalika. Wewe mwenyewe umetia saini kukubali mkataba huo. Bila shaka unalipwa kulingana na barua yako ya ajira. Kama kuna kiasi kinazidi kutoka Hazina, Menejiment ya UDOM inapaswa kurudisha kinachozidi HAZINA. ukidai ulipwe haki si yako ni ufisadi. Mbona huzungumzii wafanyakazi wanaoletewa fedha pungufu za mishahara yao toka hazina kama wewe ni mkweli? Unavyowadanganya wenzako kuwa waendelee kudai tofauti ya kiasi cha mshahara unaotoka Hazina na unaolipwa na UDOM kwa mujibu wa mikataba yenu ya ajira unawapotezea muda. Hili haliwezekani hata kama utadai miaka 1000 wacha siku 2. Kulipwa tofauti unayodai ni kuvunja sheria na wewe unalijua hilo. Kwa kuwa serikali haiwezi kuvunja sheria, hata ukidai kwa rais wa jamhuri hawezi kusikilia upuuzi wako. Wewe unatia aibu wasomi wa nchi hii. Kumbe hujui hata sheria ndogo ndogo za kazi?

Sera ya Mazishi
Leo nimeona tangazo linalowataka wafanyakazi wasiotaka kuendelea na sera ya mazishi wajitoe, mbona hili husemi.

Bwana Paul Loisulie, wewe ulitumwa kwenda Dar kufuatilia masuala ya mishahara, umeshaieleza Menejimenti kilichojiri huko? Mmefikia muafaka gani na menejiment? Mbona husemi kama ulilipwa pesa za kwenda Dar kwa masuala hayo? Wewe ni mwizi, kwa nini umechukuwa michango ya wanachama wa UDOMASA wakati Menejimeti ya UDOM imekulipa zaidi ya laki nne kwa safari yako ya Dar kama posho ya kujikimu na nauli?

Sisi tunaipenda UDOM, tunataka watoto wetu wasomeshwe. Serikali ilishatangaza mishahara mipya na italipwa tu. Migogoro ya nini?
Mishahara kulipwa tofauti iachie Menejiment na HAZINA. Wewe kama ni Mzalendo kweli ifahamishe HAZINA ufisadi wa uongozi wa UDOM kisha waachie wenyewe washughulikiane. Kama una ushahidi zaidi wa ufisadi peleka TAKUKURU wafanye kazi zao. Mbona hili hufanyi?

Wewe umepoteza siku mbili bila kufanya kazi, je ukatwe mshahara? Kama sivyo, huu nao si ufisadi?

Menejiment ya UDOM ikikuchukulia hatua za kisheria utalia na nani? Usiwaponze wenzio bila sababu za msingi.

WEWE HUFAI KUWA MWENYEKITI WA UDOMASA. ACHIA WATU WENYE UWEZO NA UPEO NAFASI HIYO. KWA NINI HUTAKI KUJIFUNZA KUTOKA KWA MZEE SHIVJI AU MAREHEMU CHACHAGE ENZI ZA UDASA. HAWA HAWAJAHI KUWA NA MADAI YA KIPUUZI KAMA HAYA YAKO.

Ndugu kutokana na mada zako katika jamvi tumekufahamu wazi kwamba wewe ni mwalimu mwenzetu na ambaye ni junior staff na kutokana na mazungumzo yako ya kila siku na misimamo yako ya ajabu hata mada zote ulizochangia zinakubainisha wazi misimamo yako kama ifuatavyo wewe ni mdini uliyekubuhu, unajipendekeza kwa utawala, ili ujue kwamba tunakufahamu ni kwamba wewe upo informatics college, na ni mwenyeji wa bukoba hivyo basi katika mkutano wetu ujao tunakujadili na hatua kali dhidi yako za kinidhamu zitachukuliwa
 
inawezekana wamesusa kutokana na mwandishi wa mwananchi kupigwa na wanafunzi jana. Lakini pamoja na hayo waandishi walisema hawatafanya kazi na wanafunzi wa udom kitu cha ajabu wameamua kugoma kuripoti hata habari ya mgomo wa waalimu ambao una madai mengi ya msingi na una ibua ufisadi mkubwa unaofanywa na uogozi wa udom. Kwa mujibu wa mdau aliyekua kwenye kikao hicho kitendo cha wanafunzi kumpiga mwandishi wa habari kilikemewa vikali na walimu kwenye kikao hicho mbele ya waandisi wa habari ambao walikua wakuchukua picha lakini leo hakuna hata TV moja iliyorusha habari hiyo. Hata hivyo kumekua na habari kwamba uongozi wa UDOM kwa kipindi kirefu umekua na tabia ya kuwaonga baadhi ya waandishi wa habari ili wafunike maovu yanayofanywa na uongozi wa chuo hicho. Tunaomba kubenea na raia mwema pamoja na tanzania daima na mwananchi wafanye hima wakaanike ufisadi huo naamini watu hawa hawadanganyiki.
 
Back
Top Bottom