Mgomo wa Wahadhiri na Wanafunzi UDOM 2011

Mbona thread nyingine inasema wahadhiri walimsubiri chimwaga lakini pinda akachelewa na kuomba radhi na kuwataka wakutane kesho sa tano?????? wewe unasema wamegoma kuongea nae sasa tuamini lipi?????????????

Nami wamenichanganya kabisa. MwanaJF mwenye ukweli wa suala hili atujuze tafadhali.
 
Gud. kumkataa kwao ni sawa. coz hapo pinda tasema nitaishauri serikali. na udom wanamtaka mtendaji mkuu wa serikari sio mwenyejina la utendaji mkuu anayeishia kushauri na si kutekeleza. gud udom. udsm we are coming!
 
Yote haya yanayotokea UDOM kabla sijalaumu naangalia ni nani anayestaili pongezi na ni nani anayestaili kukosolewa na kukimbiwa kama sio kuonywa kwa dhati kabisa.
Nawahurumia sana wadogo zangu wa Udom kwa kujionyesha sana kuwa mnaweza na mnaijua siasa kumbe hata definition ya siasa hamuijui! Poleni sana ila kueni muyaone. Nadhani kwa yaliyotokea hamtarudia tena kosa. Najua kwa sababu ya uchanga wenu na uduni wa uelewa wa mambo sauti za CCM za kampeni ziliwaponza mkajikuta mnakuwa vipaza sauti wa CCM bila kujua hatima yake baadae. Naomba kuwauliza swali moja kuwa, HIVI KWELI MLIZALIWA TANZANIA AU NI WAKIMBIZI? KAMA MLIZALIWA TANZANIA NA MKAONA UTENDAJI WA CCM MKAPA LEO HII NADHANI KAMA NINYI SIO VIPOFU BASI NI ZUZU. NATILIA SHAKA UTENDAJI WENU BAADA YA KUMALIZA MASOMO YENU NA SIDHANI KAMA MTATUFAA KWA MAENDELEO YA TAIFA KAMA LETU. LABDA MKATAFUTE TAIFA LA MAZEZETA KAMA MLIVYO! NIKIANGALIA WANAZUONI WAJANJA NA WAELEWA NADHANI WANAWEZA KUWA UDSM AMBAO KILA KUKICHA WANA MIJADALA YENYE MBEGU ZA MAPINDUZI YA MAENDELEO!
Mlimchangia fomu ya urais Mkwere mlidhani ni mjomba wenu?
Sasa ni haki yenu kuvuna matunda ya ujinga wenu!
Mkome kabisa kutuongezea uozo nchini kwetu! hamna adabu wala nidhamu!
 
Sasa wataweza vipi kukiendesha hicho chuo idadi ya wanafunzi itapokuwa imefikia hiyo 40,000 kama wanashindwa na hiyo idadi ndogo ya sasa??
 
kama sinema vile pinda amefika udom na ving'ora vyake kwenye ukumbi ili aongee na wahadhiri wa udom kuhausu mgomo wao wahadhiri wamegoma kuingia kuongea naye wanamtaka rais sio pm kuona hivyo pinda akajinda kwenda kuongea na serikali ya wanachuo hali wanachuo waliisha kubaliana kuwa aongee na wanachuo wote basi wakati pinda anaongea na viongozi huku wanachuo wakakutana na kuwang'oa madarakani haraka wakasimika serikali mpya wakamwapisha rais mpya na mawaziri wapya hapo patamu serikali yetu imechanganyikiwa huku makamba yuko arusha,mbeya kunafukuta.kila kona ya nchi yetu wananchi wameivimbia serikali naona ya tunisia yanakaribia DOWANS,ARUSHA,UDOM.KATIBA.UDSM nasikia j3 wanaanza kugoma,IRINGA,KIU sasa wameelemewa

Habari za kuaminika ni kwamba anachotakiwa ni kuweka fedha kwenye account za waadhiri na si vinginevyo ndio maana wakasema Pinda ni njia ya kumtaka JK endapo atatoa kauli ya mwisho. Kama hatatoa iyo kauli mgomo upo pale pale.
 
Udom semeni jamani. Karibu mtoke huko kwenye kata muwe nasi wanamapinduzi wa ukweli
 
jamani hawakugoma kuongea nae, mtoa mada hayupo DOM. Alichelewa kumaliza mambo yake katika sehemu fulani ya ziara yake UDOM kwani hadi saa kumi na mbili jioni malikuwa na maongezi na serikali ya wanafunzi- udoso. alituma waziri wa elimu kuomba radhi, wanataaluma walimuelewa, na akaomba akutane nao kesho saa tatu asubuhi.
 
Pinda ameogopa kuongea na wanafunzi wa COeD, kapitiliza kiasi cha kuzua taflani na kuzuia gari la mkuu wa Wilaya na baadhi ya magari ya polisi. Gari la mkuu wa wilaya limetolewa upepo kwenye matairi na ikamlazimu kukaa ndani ya gari kwa masaa kadhaa. Uongozi wa UDOSO - COeD umepinduliwa mbele ya mkuu wa wilaya. Na baada ya kuchagua viongozi wa serikali ya mpito mkuu wa wilaya aliombwa kutoa speech but alishindwa kuongea kama alivyoombwa.
Hali bado ni tete.
 
jamani hawakugoma kuongea nae, mtoa mada hayupo DOM. Alichelewa kumaliza mambo yake katika sehemu fulani ya ziara yake UDOM kwani hadi saa kumi na mbili jioni malikuwa na maongezi na serikali ya wanafunzi- udoso. alituma waziri wa elimu kuomba radhi, wanataaluma walimuelewa, na akaomba akutane nao kesho saa tatu asubuhi.
Tujuze yaliyojiri katika maongezi na serikali ya wanafunzi.
 
kama sinema vile pinda amefika udom na ving'ora vyake kwenye ukumbi ili aongee na wahadhiri wa udom kuhausu mgomo wao wahadhiri wamegoma kuingia kuongea naye wanamtaka rais sio pm kuona hivyo pinda akajinda kwenda kuongea na serikali ya wanachuo hali wanachuo waliisha kubaliana kuwa aongee na wanachuo wote basi wakati pinda anaongea na viongozi huku wanachuo wakakutana na kuwang'oa madarakani haraka wakasimika serikali mpya wakamwapisha rais mpya na mawaziri wapya hapo patamu serikali yetu imechanganyikiwa huku makamba yuko arusha,mbeya kunafukuta.kila kona ya nchi yetu wananchi wameivimbia serikali naona ya tunisia yanakaribia DOWANS,ARUSHA,UDOM.KATIBA.UDSM nasikia j3 wanaanza kugoma,IRINGA,KIU sasa wameelemewa
mtalalamika sana. mkileta fujo ni vurungu tu kwa kwenda, kudadadek. Hata mkiwatumia hao maaskofu wenu. watanzania wengine tunaangalia maslahi ya taifa kwanza na si masinagogi. Ni virungu tu kwa kwenda mbele, mpaka muelewe maana ya maslahi ya taifa kwanza.
 
Back
Top Bottom