Mgomo wa wafanyakazi wasitishwa kwa muda

Viongozi wa tucta wajinga na nchi hii itaendelea kuendeshwa kibabe milele.raisi kuwatisha kidogo wamenywea.raisi anakwambia mshahara wa 315000 haiwezekani laniki bilioni 16 ya chai kwenye wizara inawezekana.kwa stahili hii bora ccm watangazwe rasmi kuwa wafalme wa nchi kama wananchi hatuna sauti.sababu kubwa ya ccm kutoheshimu kura ya wananchi ni kwa vile inanunulika na hela wanayo ya kununua.kama kura ingekuwa haununuliki tanzania basi raisi ange heshimu malalamiko ya wananchi waliomuajiri.
 
Hamna hotuba isyo enda shule kama ya jana. Hivi wale walikuwa ni wazee wa Dar es salaam au walikuwa wanachama wa CCM?

Sidhani kama walikuwa wazee wa Dar, nahisi ni wazushi tu wa CCM. Kama kweli ni wazee wa Dar basi wamewasiliti wazee wenzao waliostaafu Afrika Mashariki ambao wangali wakipigania viinua mgongo vyao hadi leo (wengine hadi kaburini), shame on the so called 'wazee wa Dar' kwa kushangilia hotuba kama ile...
 
Baada ya kusikia mbwembwe za mwajiri mkuu jana jioni ndugu wafanyakazi wenzangu mgomo utakuwepo au tuachane nao na tukubaliane na ushauri wa mwajiri mkuu????
BREKING NYUUUUUUZZZZZ: TUCTA YASITISHA MGOMO WA KESHO

SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NCHINI (TUCTA) LEO LIMETANGAZA KUSITISHA MGOMO WAO ULIOPANGWA KUFANYIKA KESHO NCHI NZIMA.
VIONGOZI HAO WA TUCTA WAMETOA TAMKO HILO MUDA MFUPI ULIOPITA KATIKA OFISI ZA SHIRIKA LA KAZI LA KIMATAIFA (ILO) MTAA WA MAKTABA STREET JIJINI DAR, AMBAPO RAIS WA TUCTA BW. OMARY AYOUB JUMA, AKIWA NA NAIBU KATIBU MKUU BW. NICHOLAUS ERNEST MGAYA WALIPOKUTANA NA WANAHABARI NA KUTOA TAMKO LA KAMATI YA UTENDAJI TAIFA KUHGUSU MGOMO SHINIKIZI WA WAFANYAKAZI NCHI NZIMA (PROTEST ACTION).
"TUNAWARIFU KUWA MGOMO (PROTEST ACTION) YA KESHO IMESITISHWA KWA MUDA", INASEMA TAARIFA HIYO, NA KUONGEZEA KWAMBA "TAARIFA KAMILI KUHUSU SHUTUMA ZILIZOTOLEWA NA MHESHIMIWA RAIS KWA VIONGOZI WA TUCTA ZITATOLEA HIVI KARIBUNI..." ILIMALIZIA
HATUA HII INAKUJA SIKU MOJA BAADA YA JK KUWATAKA WASIGOMEWAKATI AKIWAHUTUBIA WAZEE WA DAR ES SALAAM UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE HALL.

KATIKA HOTUBA HIYO JK ALITANGAZA KUFUKUZA KAZI YEYOTE ATAKAYEGOMA, AKAWAITA TUCTA KUWA NI WAONGO NA WANAFIKI WAKUBWA, NA KUWATAJA KAMA WACHONGANISHI NA WATU WENYE HIANA.


PAMOJA NA KUSEMA YUKO TAYARI KUKOSA KURA KATKA UCHAGUZI MKUU UJAO KULIKO KUDANGANYA KUHUSU HALI HALISI ILIVYO, JK PIA ALIONYA KUWA ATAYEFANA FUJO ATASHUGHULIKIWA NA KUNAINISH KWAMBHA KIMA CHA MISHAHARA CHA SH. 315,000 KILICHOPENDEKEZWA NA TUCTA HAKILIPIKI NA MKUMFANANISHA BW. MGAYA NA NDEGE KONG'OTA KWA KUTAKA KUCHUUZA WENZIE.

HABARI KAMILI NA TASWIRA BAADAYE KIDOOOOGO....

ILA HABARI NDIYO HIYO
.......Kwa hisani ya globu ya Michuzi.....
 
Mimi nashauri sisi Ngangari wa JF tukaandamane badala ya hao wafanyakazi wa serikali. Mbele yetu awe mzee wetu Dr. Slaa.

Viboko vya FFU vitageuka kuwa soda.
 
Niligoma nikiwa nasoma Chuo sikupata Chochote... zaidi nilijipotezea muda wangu wa kusoma.... Sasa na kazini tena nigome???? Hata! Namuheshimu Raisi wangu!

Mbona huonyeshi kama ulikuwa chuo hata kidogo katika maelezo yako, labda ulisindikiza weingine au ulienda kutalii tu!!!
 
FFU (na JWTZ) hawawezi kuingia kwenye mgomo kirahisi wakati maboss wao wanashinda Ikulu wakila kuku. Ni vigumu kuyashawishi majitu yaliyoko jeshini kwani siku yakikubali kazi inakuwa imeisha. Siyo kitu rahisi.


Ndugu yangu wanajeshi wa sasa ndo makondoo ile mbaya, bora raia! Wana hali ngumu ile mbaya lakini ndo hamna anayeweza kuchukua risk yoyote bora wa zamani. Hata training yao sasa ni too dilute kuliko zamani. Ukitaka kujua tofauti yao jaribu kuongea na ofisa mkubwa yeyote halafu linganisha ufahamu wake na akina Capt Hatty McGhee na wenzie waliotaka kufanya mapinduzi 1984 akili zao zilikuwa juu na walijua wanachofanya. Wa leo wanalia matatizo yao chini ya miti tu na kumuomba Mungu, hamna lolote kule kwenye makambi ndugu yangu.

Ndio maana wanakuja kumaliza stress zao kwa raia wanapopata nafasi kwa manguvu yasiyo na msingi
 
Tuwe wakweli, CHADEMA walikuwa wanachochea huu mgomo kwa chini chini, ila sasa wamefulia!

Wao wanashindwa kuandamana kupinga katiba, wanawaambia wafanyakazi wagome kupinga mishahara midogo?
 
Mbona huonyeshi kama ulikuwa chuo hata kidogo katika maelezo yako, labda ulisindikiza weingine au ulienda kutalii tu!!!
wachana na huyo mchafuzi wa mazingira tu......am afraid hakujua hata alichokuwa anagomea huko chuo, sasa atajuaje mgomo ulimnufaisha vipi
 
Ni bora tu hiyoTUCTA imebarikiwa na viongozi waoga,hiyo ndiyo ponea ya JK otherwise wazoefu wa migomo kama sie tungekua huko basi nchi ingekuwa Ndogo.We ngoja tu,nasema ngoja!

Kaka unasema tu but asili ya watanzania ni waoga kama kuku anavyoogopa mwewe na vifaranga vyake. Ukikaa na watu kusikiliza wanachokizungumza baada ya kuchimbwa mkwara unakuta wanakusikilizia wewe utasema nini. Bwana watanzania sote tumekaaa kinafiki nafiki na kiwoga na ndio maana haki zetu hata siku moja tutazipata labda mwaka 3000
 
Hapana Mkuu. TUCTA wametumia busara na akili sana. JK na serikali walitumia nguvu nyingi kwa hiyo hapa ingekuwa hatari. Kwa hiyo naamini TUCTA wamefanya jambo la busara.

Hata hii hatua ya kufanya JK aongee kama jana siyo ndogo. Hapo tayari tuko hatua moja mbele.[/QUOTE]

hakika!!ukiweza kumfanya mtu alipuke kama jana basi ujue umemgusa haswaa,muoga na hekima sifuli
hatua zingine zitafata tu sio lazima tuandamane barabarani i
 
Niligoma nikiwa nasoma Chuo sikupata Chochote... zaidi nilijipotezea muda wangu wa kusoma.... Sasa na kazini tena nigome???? Hata! Namuheshimu Raisi wangu!

rejao
  • profile.png
    View Profile
  • forum.png
    View Forum Posts
  • message.png
    Private Message
  • article.png
    View Articles
  • add.png
    Add as Contact
user-online.png

Junior Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
Join Date Tue May 2010
Posts 4
Thanks 0 Thanked 0 Times in 0 PostsRep Power 0Wakuu mnashangaa nini, huyu ni kabaraka wao!!!!
 
MGAYA NI NANI NA TUCTA NI NANI???????????.
Kwa mawazo yangu,Mgaya anapewa jukumu la kuongoza ujumbe wa wafanyakazi Tanzania nzima.
Hata JK jana kakosea kumtaja Mgaya kama issue ni ya mtu binafsi.
Mgaya katumwa na wafanyakazi wote.

SUBIRI HIYO KESHO UTAONA KILICHOMKIMBIZA JAMAA WA SYSHELIS.

Sishangai, wewe ni pupet tu......
mbona sijawahi kukuona humu? Wale wale tu....
 
Ndugu yangu wanajeshi wa sasa ndo makondoo ile mbaya, bora raia! Wana hali ngumu ile mbaya lakini ndo hamna anayeweza kuchukua risk yoyote bora wa zamani. Hata training yao sasa ni too dilute kuliko zamani. Ukitaka kujua tofauti yao jaribu kuongea na ofisa mkubwa yeyote halafu linganisha ufahamu wake na akina Capt Hatty McGhee na wenzie waliotaka kufanya mapinduzi 1984 akili zao zilikuwa juu na walijua wanachofanya. Wa leo wanalia matatizo yao chini ya miti tu na kumuomba Mungu, hamna lolote kule kwenye makambi ndugu yangu.

Ndio maana wanakuja kumaliza stress zao kwa raia wanapopata nafasi kwa manguvu yasiyo na msingi[/QUOTE]

Hakuna mapinduzi yanaendeshwa na majenerari. Daima mapindizi viongozi wake ni wanajeshi wa rank za chini hasa makaptain!
 
I did not get a chance to hear the JK's Speech. But from what I have gathered it was not a good one, at least to the employees. Some of what has angered lots is JK's statement that there is plenty of people looking for jobs out there. I think that is a heavy threat to make. I can only image if only all medical personnel will stay home for a day! Sketch at picture at Muhimbili. Not a good! I hope a solution is reached before the strike.

This strike will work if the whole labor force will 'sing the same song' and in harmony, in that if all are striking then all strike. If its a strike, I hope its one of those calm strikes where the employees just stay at home, no street match as 'virungu' may be used.

But all in all I hope a solutions is reach before all hell goes loose.

May God help us on this one.
 
Hivi ule mgomo wa maprof wa vyuo umeishia wapi?

Mgomo wa maprof umeisha baada ya kupewa kauli za kwamba eti PM yuko pamoja nao katika kutafuta solution ya matatizo yao. Ila kutokana na move hii ilivyokwisha nimeamini wasomi wengi ndio maana sio matajiri. Maana hawataki ku-take risk, kama umeamua kugoma weka mambo ya sheria nyuma na songa mbele. Hata siku moja mgomo hautaweza kuwa wa halali endapo unapingana na maslahi ya serikali. Hivyo mkiamua kuingia vitani mswiogope kifo.
 
Nafikiria tena kwamba pengine JK alijiandaa kwa awamu moja tu..Haya majibu yake yaliniacha hoi. Hivi JK anaposema Mgaya ametumwa alikuwa na maana gani? katumwa na kina nani hili swali waandishi wa habari jamani tafuteni ukweli wa statement hii. Kaitoa yeye mwenyewe inatakiwa atoe maelezo zaidi maanake inatisha zaidi kufikiria kwamba Mgaya katumwa kuwatumia Wafanyakazi wasiojua undani wa issue nzima.
 
Mgomo wa maprof umeisha baada ya kupewa kauli za kwamba eti PM yuko pamoja nao katika kutafuta solution ya matatizo yao. Ila kutokana na move hii ilivyokwisha nimeamini wasomi wengi ndio maana sio matajiri. Maana hawataki ku-take risk, kama umeamua kugoma weka mambo ya sheria nyuma na songa mbele. Hata siku moja mgomo hautaweza kuwa wa halali endapo unapingana na maslahi ya serikali. Hivyo mkiamua kuingia vitani mswiogope kifo.

Kimsingi wafanyakazi ndo wanafanya makosa kuwapata viongozi wao, ni makosa yaleyale tunayofanya wananchi kuchagua viongozi.

Sifa za kiongozi zinatakiwa
1.Awe bandidu
2.Awe maisha yake hayategemei sana huo mshahara.
Hata kama wewe ni jasiri lakini maisha yako na familia yako inategemea ajira za namna hiyo, lazima utie adabu. Unaweza jiuliza sawa mie wakinizuia kufanya kazi na kunizuia kutoka nje ya nchi, hawa watoto nani atawalea ? wataomba kwanani mhugo ama chipsi dume. Kiongozi lazima awe na sifa za ziada zaidi ya ubandidu tu.
 
kwa namna yoyote ile hata kama tucta hawatarudisha mgomo mi nadhani hakuna kurudi nyuma...at least it was something. Utawala wa kikwete umetaabika kwa namna moja au nyingine, kuja kutoa hotuba ya namna ile ni desperations!! Watanzania waoga sawa lakini woga ndo unaisha kidogokidogo hivo. Kuenzi nguvu zilizotumika katika hili ni kuwa tayari kusapoti mara swala kama hili litakaporudi. Pia tukumbuke haya yoooooooote hadi oktoba...maana hatukawii kusahau tena wadanganyika wenzangu!! zidumu fikra za kizazi kipya!!
 
Back
Top Bottom