Mgomo wa wafanyakazi wasitishwa kwa muda

Dalili za kujilipua hizo!

Si kweli mkubwa, nimesikia RWANDA inawajali sana wafanyakazi na inawalipa vizuri na kutoa maslahi muhimu kwao. Kuna watu kibao wanatimkia huko jaribu na wewe acha kukaa huko Zanzibar.
 
Si kweli mkubwa, nimesikia RWANDA inawajali sana wafanyakazi na inawalipa vizuri na kutoa maslahi muhimu kwao. Kuna watu kibao wanatimkia huko jaribu na wewe acha kukaa huko Zanzibar.

Nimekusoma kiongozi, wacha nimshawishi mzenj wangu....sijui kama tutapata bata huko!
 
Je itakuwaje kama hata hao FFU wa JK nao watajiunga kwenye mgomo wakidai maisha mazuri kama ya wenzao kule Mwenge??????

Toka lini mbwa akamgomea boss wake! hao FFU ni kama mbwa aliyetolewa mfano na JK jana kuwa hata kama Master wake hayupo anarekodi tu sauti kwenye grammerphone na mbwa husikiliza.

Mimi sielewi, Mgaya anasema wamesitisha mgomo kupisha mazungumzo ya tarehe 8, wakati anatangaza kuwa mgomo uko paleplae ile juzi hakujuwa kama kuna hayo mazungumzo! kwanini amesubiri hadi JK kasema juu ya mkutano huo na yeye ndio atangaze, yaani kwa hili amethibitisha maneno ya JK kuwa wao ni wanafiki na walikuwa wanaongea ili wapigiwe makofi. Kifupi kwa hili kampa JK credit na domo la kusema kwa wananchi! aaaaaaaah No wonder JK alikuita WOZOZA!
 
Zipo taarifa zinazoonyesha kwamba TUCTA wameaamua kusitisha mgomo wao kwa muda kuona majadiliano ya tar 8 mei 2010 yatazaa nini?
 
This is what we call the "picha kamili", watanzania bado ni wadanganyika na mwamko bado haujawa ule wa kufanya lolote kwa sasa. Mnajua Mkwere na Intelligence yake ingawa hawana akili lakini huo ujinga walionao umeweza kuwasaidia kuzima hii noma iliyokuwa ianze kesho. Anyway, nadhani moto haujazimika kabisa kwahiyo kuna haja ya kutafuta kuni kavu za kutosha pamoja na oil chafu kama sikosei (nimesema oil chafu ili iwake kwa muda wa kutosha maana petrol italipuka ikwishe haraka) kabla ya kuwakisha tena
 
Sio tuu asitishe, bali afungashe na virago, hiyo TUCTA ifilie mbali, hakuna haja kuendeleza majadiliano na mtu aliyesema kwamwe hawezi kulipa hiyo pesa.
 
Nikiwa Dar nawafahamu zaidi ya wasomi sita waliotimkia Rwanda na wawili waliondoka kwenda Botswana ambako pia kuna kundi kubwa la wasomi wamehamia huko. Sijui JK na utawala wake wanafikiri kitu gani haswa.... lakini kwa kuisoma hotuba ya JK jana nadhani kuna beef baina ya JK na mtu fulani ambaye hadi sasa hivi sinfahamu. Inaonyesha wazi kwamb JK anaamini Mgaya ametumwa na watu fulani kuanzisha vurugu hizi na kwamba sio swala la haki za wafanyakazi. Hii imani sijui JK kaitoa wapi hali ukweli upo wazi kabisa.
Maisha ya wafanyakazi nchini yanatisha.. Ni mashirika binafsi toka nje ndiyo pekee yanalipa mishahara mizuri kwingine kote zuga...Kila mfanyakazi anategemea kupokea rushwa -Nisaidie Nikusaidie, hii ndio mbiu ya wafanyakazi wote wa serikali na mashirika.. Kweli tutafika?
 
Hakuna jipya hapo ndo kwishney....... Warundi wanasema karahezeh... Imekwisha hakuna mgomo. Nani hamuogopi mwajiri mkuu?????????
 
Haya bandugu, yetu masikio.......Na huyo ndo atakaepigiwa kura na wazalendo wa nchi hii... aah watanzania bwana
 
Hawa mabwege kweli nilitegemea hili kama ilivyo lol Tanzania zaidi uijuavyo
 
Mwaka jana Mkoba Aliitisha Mgomo wa CWT akageukwa sijui sasa yuko wapi, hapa inawezekana kila chama kimeshachukua Msimamo wake, TUGHE wana msimamo wao, COTWU, CWT nk, Nguvu ya TUCTA inategemea zaidi uthabiti na Uimara wa Vyama Shirika
 
Kwa yale aliyoongea, tusubiri tarehe nane ifike kisha tutajua mbivu na mbichi

Kingi umesema sawa kabisa, mbwa mkorofi mpe kamba ndefu ajinyonge atatulia. Hatujui nani ni nani kwa sasa na mimi sitaki kutoa hukumu ingawa kimsingi tumepata picha kwamba ubabe, matusi na vitisho vimetumika waziwazi na rais wa nchi hii kwa kuogopa kuona nchi nzima inagoma wakati wa mkutano mkubwa kama huu uliopo sasa. Naamini TUCTA walijua kuhusu huu mkutano. kama nia yao ilikuwa ni kuwaonyesha wageni kwamba tuna matatizo basi lengo lao la kwanza hapo limegoma. Mengine naombeni nisubiri tarehe 8 maana sio mbali, vinginevyo naomba ijulikane Tanzania ni maarufu kwa siasa za danadana kiasi kwamba hata wanasiasa wengine huwa wanakuja kuomba ushauri jinsi ya kupiga danadana..!

Kingine naomba niangalize kwa haraka, nadhani hatujaamka sawasawa, uchaguzi kwa sasa sio issue tena maana CCM walishamaliza mambo siku nyingi. Kama mtakumbuka vyema Chadema haina mgombea, CUF haina kitu maana Lipumba kwa taarifa nilizo nazo amepewa kazi UN na JK (mshauri wa uchumi), Sharif huko Zanzibar ndio hivyo, TLP wanajulikana maana Mrema kasema mwenyewe, Mbatia hagombei urais ingawa ni shogake JK na anamfanyia kazi, Zitto Kabwe ndio hivyo tena, Slaa hapo hagombei nadhani kaambiwa asubiri zamu nyingine, KWA SASA HAKUNA UPINZANI KWAHIYO JK ATAWAFANYA ANACHOTAKA, NA AMESHASEMA KWAMBA MSIMPE KURA MAANA HAHITAJI KURA ZENU KUSHINDA, ALISHASHINDA SIKU NYINGI KINACHOSUBIRIWA NI PROCEDURES AMBAZO NI ZA KAWAIDA KILA BAADA YA MIAKA 5. HATA MKIKAA MAJUMBANI ZOTE SIKU HIYO, ATASHINDA TUU..! Mwenye data anikatalie..!
 
[QUOTE=Mfamaji;900143]Hatugombani ,wala hatutishiani nyau. Yeye atumie mipasho sisi tutatumia akili. Full stop.[/QUOTE]



....hivi nyie kawaambia nani that you have akili. Brains aint synonymous with akili. Even the retards have brains!. Akili zingekuwepo basi zingeonekana pia kwenye nyanja zingine. So far hakuna. What can you show for it? What??? Ubishi na ushabikitu na mineno. Kamwe hamtashinda hata ng'o!
 
Wewe Charity acha hizo wewe. Mgomo baridi mgomo baridi. Tukikupata we will fire you. Alaa!!
 
Hamna hotuba isyo enda shule kama ya jana. Hivi wale walikuwa ni wazee wa Dar es salaam au walikuwa wanachama wa CCM?

wale ni wazee wa DSM na ni wazee wa chama pia ...mie siwezi kuvaa green green kama si mwanachama ..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom