Mgomo wa wafanyakazi wasitishwa kwa muda

Lord

Member
Feb 13, 2009
91
26
Baada ya kusikia mbwembwe za mwajiri mkuu jana jioni ndugu wafanyakazi wenzangu mgomo utakuwepo au tuachane nao na tukubaliane na ushauri wa mwajiri mkuu????
 
Mkwala wa jana sidhani kama hata bana mkubwa MGAYAaweza kushika tena MIC hadharani!!!
 
Kwanza sisi tunafanya mambo yetu kwa kutumia akili na vilevile tuna busra zetu.Hatuna haja ya mipasho,taarabu na jazba.Tunajipanga then tutatoka na solution itakayoleta Historia hapa TZ.Na isitoshe kwa taarifa yako migo ya kimyakimya na baridi ilishaanza kitambo na hiyo ndio mibaya zaidi kuliko huu wa kuonekana huwa unaisha haraka.
 
Tunasubiri kwanza tamko la Mgaya na TUCTA

Kweli TUCTA wanatakiwa kutoa tamko. Ila nadhani wamefanya jambo la maana kutokimbilia kujibizana na JK. Wanatakiwa kukaa chini na kutoa tamko ama kujibu hotuba ya mkulu yenye vitisho vya ajabu ajabu na kusistiza kuwa mgomo uko pale pale au kutangaza kurudisha majeshi nyuma. Lazima watoe tamko leo vinginevyo hakuna mtu atawaelewa. Pia watampa JK nafasi ya kusherehekea na wageni wake akijinywea wine au juice!
 
WanaJF nimesikia tetesi kwamba Mgaya ataitisha Press conf. leo mchana kutoa tamko la TUCTA mwenye more news please
 
Hatugombani ,wala hatutishiani nyau. Yeye atumie mipasho sisi tutatumia akili. Full stop.
 
WanaJF nimesikia tetesi kwamba Mgaya ataitisha Press conf. leo mchana kutoa tamko la TUCTA mwenye more news please

Hilo ndilo wengi wetu tunasubiri. Labda wamkamate kabla ya kusogelea mic. Lazima TUCTA itoe maelekezo kwa wanachama wake. Vinginevyo tutasambaratika kwa aibu kama Ma-Profesa wetu walioshindwa kuhimiri vishindo vya kuku. Shame on them!!
 
Kasema hivi ............nini? Hamna mtoto mdogo hapa .Kama umesikia na ni mchana subiri tutamsikia 2
 
Hilo ndilo wengi wetu tunasubiri. Labda wamkamate kabla ya kusogelea mic. Lazima TUCTA itoe maelekezo kwa wanachama wake. Vinginevyo tutasambaratika kwa aibu kama Ma-Profesa wetu walioshindwa kuhimiri vishindo vya kuku. Shame on them!!

Hivi ule mgomo wa maprof wa vyuo umeishia wapi?
 
Kwa mtu mweny busara, akiona kwamba akienda vitani atashindwa, hurudisha majeshi nyuma na kujipanga upya.
Nawashauri wafayakazi kama wanaona wameshikwa pabaya waairisha mgomo na wajipange upya.
Kwa kauli za JK, inaonesha kuna msukumo toka nje unaowafanya wafanyakazi wagome, sijui ni homa ya wapinzani wa CCM au vipi.

Hivyi viongozi wa vyama vya siasa wanasemaje wao kuhusu huu mgomo?
 
tunasubiri tamko la TUCTA, nafikiri kabla ya saa 11 tutakuwa tumesikia msimamo ni upi? ingawa so far mgomo upo palepale sababu hakuna changes tunachotaka tu kusikia Rais wetu wa TUCTA anasemaje kuhusu madongo ya mkwere ya jana.
 
Hamna hotuba isyo enda shule kama ya jana. Hivi wale walikuwa ni wazee wa Dar es salaam au walikuwa wanachama wa CCM?
 
Hii kwani lazima uite press conf. Mnarekodi tamko lenu mnalilipia mnarusha BBC, CCN, Deuste Welle na kwa internet, let start using the technology for our benefits
 
Hamna hotuba isyo enda shule kama ya jana. Hivi wale walikuwa ni wazee wa Dar es salaam au walikuwa wanachama wa CCM?

Wengi wao walikuwa wajumbe wa halmashauri ya ccm ya wazee.Na nadhani waliandaliwa maalumu kwa ajiri ya kupiga makofi na kuitikia chorus ya mipasho/taarabu.
 
Hivi ule mgomo wa maprof wa vyuo umeishia wapi?

Umesitishwa hadi mwezi wa sita. PM aliwaomba wafanye hivyo. Sasa sijui kipi kitafuata. Sijui watafukuzwa kazi au laa. Ila yote ni tisa, hili la MIGOMO kama Kikwete akirudi tena madarakani, basi atashuhudia MIGOMO isiyo na kichwa wala miguu. Nampa pole.
 
Back
Top Bottom