Negotiator
JF-Expert Member
- Aug 9, 2010
- 303
- 44
mdharau mwiba mguu huota tende. chonde chonde serikali
Pinda amekamilisha mkutano na waandishi wa habari hivi punde na meseji ya kubwa kwa madaktari ni kuwaambia kuwa serikali haiwezekani kushinikizwa na madaktari na kuwafukuza mawaziri Mponda na Nkya. Hivyo, kama wanataka kugoma, wagome tu
kuna tetesi serikali imeomba madakitari 350 kutoka india na 300 kutoka china wanaweza wakaingia muda wowote kuanzia kesho.
Pinda akumbuke wananchi wanauwezo wakumfukuza rais licha ya waziri eg egypt,tunisia,libya
Huu mgomo ni wa kisiasa zaidi kuliko kudai masilahi. Nina waomba vijana wetu madktari, achaneni na mambo ya kisiasa kabisa. Taaluma yenu si siasa bali ni kutibu. Msikubali kabisa kutumiwa na wanasiasa.
Mkuu kwani Serikali ni nani? Au PM anaposema Serikali haiwezi kufanya kazi kwa shinikizo ka Madaktari kuwafukuza kazi hao Mawaziri, hiyo Serikali ndiyo ipi? Ni mtu mmoja au ni Baraza la Mawaziri au ni Rais au ni PM? Ni nini hiki kinachoitwa Serikali? Je ni kweli Serikali nzima ndiyo inakuwa na kigugumizi ktk suala hili la Madaktari? Labda nikukumbushe kitu kidogo, tu kwa uelewawangu mdogo, Serikali ni Wananchi, kwa hiyo wakiamua leo Serikali itoke madarakani wanaweza kufanya hivyo. Kuna mifano mingi ambayo haihitaji hata kuitaja. Hembu fungueni macho na akili zenu.
.......baada ya hapo, ama kweli we nunda!!!!!!!!!Nakuunga mkono mheshimiwa Pinda, wacha madaktari wagome.
Kwani wakigoma anayeumia nani? si babu zao, bibi zao, shangazi zao ,kaka zao wa Namtumbo, Nachingwea, Tandahimba, Kilindi na Kahama?
hii kesho inaweza ikauzika kwenye mafazeti