Mgomo wa madaktari na kiburi cha watawala wetu, nani anaumia?

Ehh Mungu Mwenyezi, mwingi wa huruma epusha maskini wa nchi hii na vifo vitakavyotokana na kukosa huduma za madaktari. Kuna wachache wetu ambao ndio wenye maamuzi nini kifanyike bahato mbaya sana wao wana madaktari wao hivyo hawategemei huduma za afya za umma, hao wafanye waone tatizo lililoko mbele yetu na uwape hekima na busara ya kufanya maamuzi yenye maslahi kwa uhai wa maskini wa Tanzania..AMEN
 
Awasikilize hao Madaktari.Kiuhalisia pia ni vyema hao Mawaziri wakajiuzuru kwani lazima kuna jambo na madhara ya mgomo uliopita tuliyaona hivyo ni vyema wakajiuzulu na hapo hapo serikali itimize ahadi zake kwa hao madaktari.Madaktari sio walimu jamani
 
Mlisema serikali haifanyi maamuzi magumu haya sasa wameamua kuacha madaktari wagome.

Lete Wachina na wa Cuba hapa mtu 200 zinapiga kazi ya watu 1000.
 
Alosema Jk wa kwanza na kafulila kuwa hii ni serikali legelege, sasa hatimaye leo yametia na tunashuhudia so ni vyema serikali isome majira na wakati.
 
Kwa hiyo kwa lugha nyingine ni kwamba huyu 'mtoto wa mkulima' ni kwamba hivi sasa KATOA LESENI wananchi tusiokua na uwezo kwenda Appolo Hospital kule India sasa kufa ni haki yetu tujijue sio?
 
Madaktari wanaonyesha Immaturity and hooliganism ya hali ya juu. Wacha wagome ila wasidai mshahara kwa siku watakazokuwa kwenye mgomo.
 
Nawauliza enyi madaktari, naomba mnijibu. je mgomo wenu unahusu na kwa akina mama wajawazito wajao kujifungua?
 
Ikumbukwe kwamba maslahi ya nchi lazima yawekwe mbele,mawaziri kujiuzulu ni ukomavu na uwajibikaji,come on Mponda & Nkya,achieni mchuma huo ili wananchi wahudumiwe na madaktari wao bila kinyongo,
 
Hivi huyu PM Pinda hakuwa na maneno mengine ya kidiplomasia ya kuelezea ugumu wa utekelezaji wa dai la madakatari la mawaziri kujiuzulu?! Halafu ili pia apate reputation na public support Je, ameeleza kwamba madai mengi kama ilivyoahidi serikali yametekelezwa? Kasoro hilo la kujiuzulu kwa mawaziri?

I'm doubting Thomasi "Pinda kasema Kama madaktari kama wanataka Kugoma basi wagome"
 
Nakuunga mkono mheshimiwa Pinda, wacha madaktari wagome.

Kwani wakigoma anayeumia nani? si babu zao, bibi zao, shangazi zao ,kaka zao wa Namtumbo, Nachingwea, Tandahimba, Kilindi na Kahama?
Eh ndugu yangu mbona unasikitisha kwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa hao kaka,dada,bibi au shangazi wa madaktari namtumbo pinda na serikali hawawahusu,mimi naamini serikali ipo kwa maslahi na ulinzi wa kila raia kumbe kuna wengine hawaihusu.so sad kwa hii poor reasoning yako.
 
Pinda amekamilisha mkutano na waandishi wa habari hivi punde na meseji ya kubwa kwa madaktari ni kuwaambia kuwa serikali haiwezekani kushinikizwa na madaktari na kuwafukuza mawaziri Mponda na Nkya. Hivyo, kama wanataka kugoma, wagome tu

Kama ni kweli PM wetu ametoa kauli iliyopo hapo juu, basi amekosea. Madaktari ni raia wa Tanzania kama walivyo raia wengine. Wana haki zao za msingi kama Watanzania wengine. Tatizo lililopo ni Viongozi wa Tanzania kutokutambua kuwa wako katika uongozi kwa ajili ya Watanzania na si vinginevyo. Sasa kama unayemuongoza hataki kuongozwa na wewe kuna ubaya gani?? Haiingii akilini mtu kung'ang'ania kuwaongoza watu wasiotaka kuongozwa naye.

Hebu Watanzania tuamke usingizini na tuache mabavu katika mambo ya msingi. Tujifunze kuwajibika pale ambapo tunaona wazi kuwa tumeshindwa kutekeleza wajibu wetu.
Hivi, kuna raha gani ya kuwa kiongozi mahali watu hawakutaki?? Utafanya kazi kwa amani kweli wakati unaowaongoza hawatakupa ushirikiano.

Tuache mawazo mgando eti ukiwaondoa hao mawaziri itaonekana ni kwa ajili ya shinikizo la Madaktari. Kwani Mheshimiwa Waziri Mkuu haoni ukweli ulivyo?? Mbona hata yeye kwenye kikao chake na madaktari aliliona hilo na akasema kuwa liko nje ya uwezo wake kwa maana ya kwamba angekuwa na uwezo angewaondoa??? UNAFIKI KWENYE AFYA ZA WALIOWAWEKENI MADARAKANI SI MZURI. Mjue Mungu anaona na adhabu yake mtaipata hapahapa.
 
Looh...?!What kind of shit is this?Mbona kwa Blandina na Mtesimwa iliwezekana?Kuna nini kwa hawa wawili?...
 
hawa madaktari ni wajinga wanataka kuanzisha mchezo mbaya leo wao shinikizo lao likipitshwa kesho walimu pia watakuja na shinikizo lao sasa serikali gani? Mwisho utasikia na rais asipojiuzulu tunagoma bora wawapotezee tu
hii ndio ninayoitaka........kwanza nashauri wananchi tuandmane mkweere aachie ngazi...
 
Nakuunga mkono mheshimiwa Pinda, wacha madaktari wagome.

Kwani wakigoma anayeumia nani? si babu zao, bibi zao, shangazi zao ,kaka zao wa Namtumbo, Nachingwea, Tandahimba, Kilindi na Kahama?
We babu yako si yuko Masaki bana, akijisikia homa check up Nairobi, Mafua India, Jipu London. Sisi tunaoishi Gengelegengele ndio wenye shida.
 
Pinda amekamilisha mkutano na waandishi wa habari hivi punde na meseji ya kubwa kwa madaktari ni kuwaambia kuwa serikali haiwezekani kushinikizwa na madaktari na kuwafukuza mawaziri Mponda na Nkya. Hivyo, kama wanataka kugoma, wagome tu

Kuna kila dalili hii nchi kuja kuingia kwenye mgogoro mkubwa sana kwa sakata ili,nafikiri hawa watawala hawajuhi wananchi walivyochoka na kukata tamaha huku uraiani,wawe makini ili jambo ndio linaweza kua chanzo ya kuiingiza nchi kwenye mgogoro kwa ajili ya kuwakingia kifua Nkya na Mponda,hawatokuja kuamini!
 
Natamani lowassa angekuwa pm . Sijui kungekuwa na mgomo au ? Najiuliza sana.
 
Back
Top Bottom