Mgogoro ndani ya CHADEMA!?

Sasa ni dhahiri kuwa kuna mgogoro wa chini kwa chini ndani ya CHADEMA kati ya viongozi wake, ingawa viongozi wake wamekuwa wakifanya kila jitihada kuficha

Tukio la hivi karibuni viongozi wake wamekuwa wakifanya kila njia kuhakikisha suala la Mnyika kumtumia sms za vitisho Mh. Mwigulu Nchemba linamalizwa nje ya vyombo vya usalama, viongozi wamekuwa wakimshutumu sana Mnyika kwa uamuzi alioufanya wa kutuma sms za vitisho kwa Nchemba hali inayokifanya chama kutumia nguvu kubwa kushughulikia suala hilo, pia wamekuwa wakimshutumu kwa uamuzi wake wa kwenda kufanya mkutano huko Singida hadi kusababisha mauaji.

Pia umetokea msuguano kati ya Mbowe na Zitto kutokana na uamuzi wa Zitto kususia kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge pamoja na wabunge wengine wa CHADEMA baada ya kutokea msuguano kati Tundu Lissu na Werema, inasemekana siku hiyo Mbowe ambaye hakuwepo Bungeni alimtumia sms Zitto akimshutumu Zitto kwa uamuzi wake wa kubaki ukumbini wakati wenzake wanatoka nje, hata hivyo inasemekana Zitto alimjibu Mbowe kuwa suala lile lilikuwa kati ya Lissu na Werema hivyo lilikuwa halimhusu yeye,

NOTE: Kama hali iko hivi mapema itakuwaje wakikabidhiwa nchi, si watachinjana hawa

Nawasilisha!!!?


Unawasilisha RUBISH
 
Hapa ndugu yangu naona umetumia neno mgogoro vibaya, hapo hakuna mgogoro hayo ni mambo ambayo yametokea na watu wanatafuta namna ya kuayamaliza siyo mgogoro hata kidogo, na hii ndiyo siasa inavyokwenda. Mnyika kateleza basi anaambiwa hivi sivyo, kwa upande wa Zitto alichokifanya siyo kigeni, kama mbowe alimtumia ujumbe ni katika kumwambia tu tumeona unakosimamia na inajulikana wazi. Zitto anayo hiyo historia ya misimamo ya hivyo hajaanza leo na anjua mwenyewe anachokifanya.


Kwa mtazamo wako unafikiri ni kwa nini Zitto hakutoka nje ya ukumbi?
 
Yaani mleta hoja hapo kwenye CHADEMA ungeweka CCM watu wote wangekuunga mkono lakini ukishaiongelea CDM tu tegemea matusi hata kama ukiweka vyanzo vya kuaminika.Hili si jukwaa huru tena bali ni jukwaa la kukisifia chama.Hili linanikera sana,binafsi sina chama maana kwangu siasa za bongo ni za waganga njaa tu lakini kama tunaongelea siasa jamani tukubali na kukosolewa au vinginevyo yaanzishwe majukwaa ya vyama kimoja kimoja ndani ya Jamiiforum kwamba nikiingia jukwaa la CCM nikaisema vibaya nitukanwe na vivi hivyo kwa CDM.


ni kweli mkuu, hawa CHADEMA wanataka kusifiwa tuu, kama wao ni malaika vile
 
kweli midomo itatuponza, huyu mtu kaandika vitu hana information but out of whims, atakuwa ni mkereketwa wa magamba. Watu wa hivi huwa wana maisha magumu, wanaishi pabovu, wanakula hovyo af wanajifanya chama cha magamba ni chao.
 
kweli midomo itatuponza, huyu mtu kaandika vitu hana information but out of whims, atakuwa ni mkereketwa wa magamba. Watu wa hivi huwa wana maisha magumu, wanaishi pabovu, wanakula hovyo af wanajifanya chama cha magamba ni chao.


hongera wewe mwenye maisha mazuri
 
Swali langu naona limekuwa gumu sana, ngoja nilibadili, Zitto hajambo? Josephine nae hajambo, tayari au bado?


Namuonea huruma sana Josephine, huyu mzee lazima atampiga chini baada ya muda mfupi
 
Kuna Bendi illimba kwamba " hata mapacha ufika wakati wakaacha kuelewana" Hakuna la ajabu hapa.
 
CHADEMA tunawapenda tu hata kama wakiwa na migogoro, jamii isiyo na migogoro ni jamii iliyokufa kiakili
 
Hakuna mgogoro wowote ndani ya Chadema, huu unauzusha wewe ni upuuzi usio na mashiko, chadema ni chama makini na huendesha siasa zao kwa umakini zaidi
 
Hakuna mgogoro wowote ndani ya Chadema, huu unauzusha wewe ni upuuzi usio na mashiko, chadema ni chama makini na huendesha siasa zao kwa umakini zaidi
TUNTEMEKE unamjuwa au unajisemea tu? ingawa mmemlamba ban lakini nna-uhakika ukimuudhi atakuja kivingine, shauri lako.

Vipi software ya kudhibiti mahesabu ya chama iliyowekwa na Josephine wa mzee Slaa, imesharekebishwa maana ilitowa hesabu za mapato "0" za bajeti. Umesahau sakata lake?
 
Last edited by a moderator:
hata vikombe kabatini hugongana. Kikubwa wakitofautiana basi suluhu iwepo.
 
mawazo yako potofu. Hivi wewe hujawahi suguana na nduguyo hata siku moja? Hata mke na mume hutofautiana.
 
Back
Top Bottom