Mgeja amchana Sitta, kumbe alishachapwa viboko na Nyerere kwa kuongoza maandamano!!!

Kuna Member alileta thread hapa akisema CDM imejiingiza kichwa kichwa , eti Six atakuja na silaha za maangamizi dhidi ya Dokta Slaa na CDM. Mkuu njoo utuambie sasa kama sio SIx imekuwa Zero. ohhhh
 
Ukilikoroga ni lazima ulinywe!!! CCM endeleeni kumalizana!!! Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi!!
 
Sita hawezi kushindana na mvua.kwisha habari yake.....,.
 
Sita alikuwaga raisi wa chuo kipindi hicho (kama sikosei). Na aliendesha mgomo kupinga serikali kwenye maamuzi fulani fulani. Inaelekea ndio kipindi hicho alichopatishwa bakora. Kwa information za watu wakaribu yake wa kipindi hicho (serikali ya wanafunzi) inasemekana alikuwa mtu jasiri lakini vile vile ni mtu ambaye akianza jambo hamalizi e.g. anakuwa na ideas nyingi; put into action lakini anaziacha kabla hazija-mature. Nahisi ndio maana CCJ haikufanikiwa. Inaonekana walianza na moto lakini wakashindwa kufanikisha. Labda wananchi wa jimboni kwake wanaweza pia kutuelezea if that is true.
 
SIKU moja baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa kumrushia kombora zito Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Hamis Mgeja amemtaka waziri huyo na wabunge wengine 55 wapime, watafakari na hatimaye wachukue hatua kwa kuondoka ndani ya CCM.
Mgeja ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, amesema tuhuma zilizotolewa na Dk. Slaa dhidi ya Sitta na wabunge hao, zinathibitisha jinsi kiongozi huyo na wenzake walivyo wasaliti ndani ya chama chao na serikali, na kwamba kitendo cha kuigeuza ofisi ya spika kuwa kijiwe cha kupanga uhaini na usaliti ndani ya CCM hakivumiliki hata kidogo.
Mgeja alitoa kauli hiyo jana jijini Mwanza, alipozungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kumpongeza Dk. Slaa kwa kufichua uozo wa Waziri Sitta na wenzake hao. Alisema Dk. Slaa ameisaidia CCM kutambua viongozi wake wanaokisaliti.
"Nianze kwa kumpongeza Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Slaa kwa kufichua madhambi ya Samuel Sitta. Huyu mtu (Sitta), ni hatari sana katika maendeleo ya chama chetu.
"Dk. Slaa ametueleza jinsi Sitta alivyotumia ofisi ya spika kama kijiwe cha kutaka kukisaliti chama chetu na kuanzisha CCJ. Huyu mtu ni hatari sana... tunaomba CCM imtose yeye na wabunge hao 55 maana uroho wao wa madaraka unaweza kuigharimu CCM.
"Kwa kashfa hii nzito dhidi yao, namshauri wapime, watafakari na hatimaye wachukuwe hatua. Pia nawashauri kwanza watubu na kuomba radhi chama na wana CCM wote, au wajiengue kwa hiari yao bila shuruti, ili walinde heshima yao. Wasingoje kuhukumiwa na wanachama," alisema.
Mjumbe huyo wa NEC na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga aliyejipambanua kupiga vita ufisadi na vitendo viovu ndani na nje ya CCM, alisema historia ya Waziri Sitta inajionesha wazi kwamba ni 'mkorofi na msaliti mkubwa', kwani mwaka 1966 akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alishiriki maandamano hadi Ikulu kupinga sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Alisema katika harakati zao hizo za kupinga sheria hiyo iliyotaka kila mwanafunzi wa Chuo Kikuu lazima ajiunge na Jeshi la Kujenga Taifa, Baba wa Taifa wakati huo akiwa Rais wa nchi na mkuu wa chuo hicho, alilazimika kumchapa viboko Sitta kutokana na usaliti wake huo kwa serikali.
Mgeja alisema mbali na kufanya maandamano hayo, Sitta na wenzake ambao wengine ni marehemu kwa sasa walikuwa na mabango yenye ujumbe mkali kwa serikali, ukiwemo uliosema 'Onyo kali na la mwisho kwa serikali', na kwamba alikuwa akiipinga pia Serikali ya Baba wa Taifa huku akiusifu uongozi wa kikoloni.
"Huyu Sitta ambaye leo hii anawadanganya watu, kipindi hicho akisoma Chuo Kikuu alikuwa akiipinga serikali na kudai afadhali serikali ya kikoloni. Tusipoamini leo usaliti wake huu tunasubiri hadi aje shetani atuambie usaliti wa Sitta ndipo tuamini?
"Za mwizi ni 40, ndiyo maana tumeambiwa toka mwaka 2005 hadi 2010 huyu Sitta amekuwa akikisaliti chama chetu kupitia Bunge alilokuwa akiliongoza. Tunataka chama kimtose na kisiwaonee haya wasaliti hawa wakubwa. Wasipoondoka kwa hiari yao wataondolewa kwa nguvu ya wanachama wa CCM,” alisema.
Alimtuhumu pia Waziri Sitta kwa kauli zake za kulalamikia serikali bila kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayolikumba taifa, na alimtaka ataje jinsi alivyoisaidia serikali kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, mfumuko wa bei, ufisadi na mambo mengine ndani ya chama na serikali.
Kwa mujibu wa Mgeja anayedaiwa kuanza kuundiwa mbinu chafu za kutaka kuangushwa katika kinyang'anyiro cha uenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga na kundi la kigogo mmoja anayetajwa kutaka kugombea urais mwaka 2010, tuhuma hizo dhidi ya Waziri Sitta zimekisaidia maradufu chama, kwani siyo Dk. Slaa pekee aliyewahi kumshutumu kiongozi huyo kwa usaliti ndani ya chama.
Alisema yupo tayari kusulubiwa, kutolewa kafara au kufukuzwa na chama kwa kusema ukweli daima, kwani anayasema hayo kwa kufuata kiapo cha katiba ya CCM

Sorce; Tanzania Daima

kwenye green na blue,,,,,,,,,,,
 
Sitta angekua na akili, asinge gombana na CDM. Magamba hawamtaki huyu jamaa. Sympathy ya wananchi ndio pekee inambeba kwa kujaribu kuplay fair game katika bunge lililopita. Sasa anaondoa hiyo sympathy ya wananchi kwa kugombana na viongozi wa chama kinachopendwa zaidi na wananchi kwa sasa. Mr. 6 ur digging the our own grave politically!!!
 
Nyie huyu jamaa ni chuma cha pua au mmesahau?
Ngoja aombe kipindi cha dk 45 akajisafishe na kuchafua wengine tena mshangae hapa hapa kuwa kuna mengine mengi ya wengine hamyajui. Siasaaaaaaaaa
 
Unakuwa usaliti pale unapokuwa upo ndani ya chama CCM akili yako CCJ

Lowasa aliwahi kusema kwamba wakati wao wanapiga kampeni za CCM 2010 Sitta na wenzake walikuwa busy kusajili CCJ nadhani ndio maana kwenye uspika walimchomoa.
sitta walimtoa uspika kwasababu alileta usawa kwa wabunge wote. si unakumbuka wakina slaa na zitto walikua free. ccm ilitaka spika kama huyu mama makinda ambaye anaweka chama mbele ya maslahi ya nchi. vile vile kipindi chake cha uspika kiliwabana mafisadi na serikali.
 
SIKU moja baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa kumrushia kombora zito Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Hamis Mgeja amemtaka waziri huyo na wabunge wengine 55 wapime, watafakari na hatimaye wachukue hatua kwa kuondoka ndani ya CCM.
Mgeja ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, amesema tuhuma zilizotolewa na Dk. Slaa dhidi ya Sitta na wabunge hao, zinathibitisha jinsi kiongozi huyo na wenzake walivyo wasaliti ndani ya chama chao na serikali, na kwamba kitendo cha kuigeuza ofisi ya spika kuwa kijiwe cha kupanga uhaini na usaliti ndani ya CCM hakivumiliki hata kidogo.
Mgeja alitoa kauli hiyo jana jijini Mwanza, alipozungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kumpongeza Dk. Slaa kwa kufichua uozo wa Waziri Sitta na wenzake hao. Alisema Dk. Slaa ameisaidia CCM kutambua viongozi wake wanaokisaliti.
"Nianze kwa kumpongeza Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Slaa kwa kufichua madhambi ya Samuel Sitta. Huyu mtu (Sitta), ni hatari sana katika maendeleo ya chama chetu.
"Dk. Slaa ametueleza jinsi Sitta alivyotumia ofisi ya spika kama kijiwe cha kutaka kukisaliti chama chetu na kuanzisha CCJ. Huyu mtu ni hatari sana... tunaomba CCM imtose yeye na wabunge hao 55 maana uroho wao wa madaraka unaweza kuigharimu CCM.
"Kwa kashfa hii nzito dhidi yao, namshauri wapime, watafakari na hatimaye wachukuwe hatua. Pia nawashauri kwanza watubu na kuomba radhi chama na wana CCM wote, au wajiengue kwa hiari yao bila shuruti, ili walinde heshima yao. Wasingoje kuhukumiwa na wanachama," alisema.
Mjumbe huyo wa NEC na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga aliyejipambanua kupiga vita ufisadi na vitendo viovu ndani na nje ya CCM, alisema historia ya Waziri Sitta inajionesha wazi kwamba ni 'mkorofi na msaliti mkubwa', kwani mwaka 1966 akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alishiriki maandamano hadi Ikulu kupinga sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Alisema katika harakati zao hizo za kupinga sheria hiyo iliyotaka kila mwanafunzi wa Chuo Kikuu lazima ajiunge na Jeshi la Kujenga Taifa, Baba wa Taifa wakati huo akiwa Rais wa nchi na mkuu wa chuo hicho, alilazimika kumchapa viboko Sitta kutokana na usaliti wake huo kwa serikali.
Mgeja alisema mbali na kufanya maandamano hayo, Sitta na wenzake ambao wengine ni marehemu kwa sasa walikuwa na mabango yenye ujumbe mkali kwa serikali, ukiwemo uliosema 'Onyo kali na la mwisho kwa serikali', na kwamba alikuwa akiipinga pia Serikali ya Baba wa Taifa huku akiusifu uongozi wa kikoloni.
"Huyu Sitta ambaye leo hii anawadanganya watu, kipindi hicho akisoma Chuo Kikuu alikuwa akiipinga serikali na kudai afadhali serikali ya kikoloni. Tusipoamini leo usaliti wake huu tunasubiri hadi aje shetani atuambie usaliti wa Sitta ndipo tuamini?
"Za mwizi ni 40, ndiyo maana tumeambiwa toka mwaka 2005 hadi 2010 huyu Sitta amekuwa akikisaliti chama chetu kupitia Bunge alilokuwa akiliongoza. Tunataka chama kimtose na kisiwaonee haya wasaliti hawa wakubwa. Wasipoondoka kwa hiari yao wataondolewa kwa nguvu ya wanachama wa CCM," alisema.
Alimtuhumu pia Waziri Sitta kwa kauli zake za kulalamikia serikali bila kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayolikumba taifa, na alimtaka ataje jinsi alivyoisaidia serikali kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, mfumuko wa bei, ufisadi na mambo mengine ndani ya chama na serikali.
Kwa mujibu wa Mgeja anayedaiwa kuanza kuundiwa mbinu chafu za kutaka kuangushwa katika kinyang'anyiro cha uenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga na kundi la kigogo mmoja anayetajwa kutaka kugombea urais mwaka 2010, tuhuma hizo dhidi ya Waziri Sitta zimekisaidia maradufu chama, kwani siyo Dk. Slaa pekee aliyewahi kumshutumu kiongozi huyo kwa usaliti ndani ya chama.
Alisema yupo tayari kusulubiwa, kutolewa kafara au kufukuzwa na chama kwa kusema ukweli daima, kwani anayasema hayo kwa kufuata kiapo cha katiba ya CCM

Sorce; Tanzania Daima
wazee kama huyu mgeja ni mapumbavu sana. kuna watu wana kashfa za ufisadi ccm mbona simjamsikia hakitaka wafukunzwe kwenye chama. hii story ya ccj inajulikana mda mrefu. alivyokua **** [mgeja] anajifanya ndo anaisikia leo kwa slaa . mpaka sasa sijasikia mtu yeyote serious ccm akiongea hii ishu ya sitta Vs slaa..
 
sitta walimtoa uspika kwasababu alileta usawa kwa wabunge wote. si unakumbuka wakina slaa na zitto walikua free. ccm ilitaka spika kama huyu mama makinda ambaye anaweka chama mbele ya maslahi ya nchi. vile vile kipindi chake cha uspika kiliwabana mafisadi na serikali.

Hamna usawa wowote aliyouleta spika Sitta zaidi ya kuboresha mtandao wake. Akiona hoja inatoka upinzani ya kuwakandamiza maadui zake ndani ya CCM ndio anaiachia.
 
maundumula unataka kusema bunge la mama makinda na lile la sita ni sawa kweli. mimi naona kama bunge ili wabunge wa upinzani wamebanwa zaidi.
 
wanaomuona sitta ni muadilifu labda hawamjui vizuri wamesahau ndie aliekuwa mkurugenzi wa CDA ikafia mikononi mwake na amefanya kazi tokea serikali ya mwalimu mpaka kikwete ameifanyia nini tz cha kukumbukwa mnafiki sitta
 
Binafsi naamini Mzee Sitta sio tu kamalizwa kisiasa bali kateswa sana kwanza (tortured) Dr. Slaa hakutakiwa kwenda mbali kiasi kile maanake hizi ndio siri za chama na tunaweza tu kumweka wazi mtu ambaye kenda nje kutengenza deal la kukiua CDM sio CCM japokuwa ni Unafiki wake ulomponza. Aloyasema Sitta kuhusu Mbowe hayakuwa na uzito wowote zaidi ya propaganda za kisiasa lakini hili la Sitta, duh... Dr. Slaa sio tu kwamwacha uchi mzee wetu bali kahakikisha ndio mwisho wake kisiasa. Haya ndio malipo ya UNAFIKI usipotimiza ahadi fahamu yatakukuta ya Sitta.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom