Uchaguzi 2020 Meneja Kampeni CUF: Adui wa CUF ni adui wa CHADEMA na adui wa CHADEMA ni adui wa CUF hivyo hakuna sababu ya kuhitilafiana

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,280
Akizungumza kabla ya kuanza kwa mkutano, Meneja Kampeni wa CUF, Miraji Mtibwiriko katika viwanja vya viwanja vya Fatuma Mkoani Kagera aliwataka wanachama kuwa watulivu kwa kuwa bado wanahitaji kuwa kitu kimoja.

Meneja kampeni huyo alitumia nafasi hiyo kuwaeleza wafuasi hao kuwa adui wa CUF ni adui wa Chadema na adui wa Chadema ni adui wa CUF hivyo hakuna sababu ya kuhitilafiana.

Amesema wao kama wapinzani wanapaswa kujitafakari na kujiangalia kwani inawezekana kuna eneo wanapishana lakini lengo lao ni moja inawezekana wakahitalifiana leo lakini kesho wakawa kitu kimoja.

''Tuweni watulivu sana hawa watu watatuchezea miaka nenda miaka rudi tusipokuwa watulivu ndugu zangu kwahiyo utulivu wenu ndio utakaoamua kuwa tunakwenda au hatuenda na ili tufanikiwe kwenye taifa letu tunahitaji tafakari ya kina kwani Taifa hili ni letu sote mikwaju tunachapwa sote ndugu zanguni.

"Aliongeza kuwa tunatakiwa tafakari ya kina sisi tulitakiwa kuwepo hapa lakini tumekutana na ndugu zetu wa chadema ambao nao wanataka kukiondoa chama cha mapinduzi hivyo hatuna sababu ya kuendelea kuumana,''

''Sisi kama wapinzani kila mmoja ana Sera yake itikadi yake na kila mmoja ana utaratibu wake tuliungana mwaka 2015 wote tulikuwa kitu kimoja na tulikuwa na mgombea mmoja yule ambaye mwisho was siku alipata bakora akarudi kulekule ametunanga ametukashifu na kusema kuwa amerudi nyumbani,''alisistiza.

Akiwahutubia wananchi wa Muleba katika viwanja, Profesa Lipumba amesema endapo chama hicho kitapata ridhaa kitaboresha maisha ya wakulima na wafugaji wa mkoa huo. Amesema ni lazima kuwekeza kwenye kilimo,viwanda na ufugaji ili kukuza viwanda na uchumi wa wananchi.

"Endapo tutaoata ridha tutahakikisha tunaboresha maisha ya mwananchi mmoja mmoja ili kukuza uchumi wa nchi,pamaoja na kuongeza kipato"amesema Profesa Lipumba.

Amesema katika ilani ya chama icho imeainisha kuwa tume ya haki za binadamu ili kuhakikisha wananchi wanaishi bila kuvunjiwa haki zao.

" Wapo baadhi ya watumishi wa umma wanaonyanyasa wananchi kwa kuvunja haki za bindamu, chama kimekuja na sera ya haki sawa na furaha kwa wote"amesema.

Aidha Profesa Lipumba amesema kila mwanachi nilazima aishi kwa kufwata misingi ya haki sawa na furaha kwa wote,tutakapoingia madarakani tutahaikisha jambo la kwanza ni kupata katiba mpya.


IPPMedia
 
Lipumba baada ya nakuona mziki ni nzito kwake sasa ameanza kutaka kutembelea nyota ya Lissu..

Mzee ni oppotunist vibaya mno!! Mze wa Dhamira imenisutaa!!
 
Kuna wakati unapoona chama Kama CUF na Lipumba wanaamini kwamba kuna watanzania wanawaamini kuwa nao ni wapinzani unaanza kujiuliza kama kweli unaishi na watu kwenye dunia moja au upo kiroho na sio kimwili.
 
... hakuna kitu kiliniuma CUF kama kumtimua Maalim Seif mtu aliyekitumikia chama kwa uaminifu mkubwa na kwa nguvu zake maisha yake yote ya utu uzima! Hivi Lipumba, Sakaya, na wapambe wao walikuwa na akili kweli? Ni aibu sana.
Ndo laana inayoitafuna cuf na itaitafuna hd kaburini
 
Lissu akikosa urais aende kuomba hifadhi ulaya
WA chato anayaandika yote anayosema
 
Back
Top Bottom