Mjue adui yako wa karibu usiyemdhania

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,110
22,563
Salaam, shalom!!

UTANGULIZI.

Wote tunao maadui, uwe MWEMA au Mwovu, lazima maadui watakuwepo na ni wa karibu nawe.

Leo, siwazungumzii hao maadui unaowajua wa kazini kwako, Jirani zako unayoishi nao, au maadui katika biashara, hapana!!

MADA: NANI ALIYE ADUI WAKO WA KARIBU USIYEMDHANI?

Maadui naowaongelea ni wale wa karibu Yako kabisa,

Maadui ninaowangelea Leo ni watu ambao katika mwili ni ndugu wa Damu, dada, kaka, mjomba, shangazi, bibi Yako, Babu, mtoto,mume, baba Mkwe ,mama mkwe nk nk.

Fuatana nami ujue watu hao wa karibu, wanawezaje kuwa maadui zako?

(Mathayo 10:34-35) says:

34:Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta Amani duniani, la! Sikuja kuleta Amani, Bali Upanga, Kwa maana nalikuja kumfitinisha mtu na babaye, na Binti na mamaye, na Mkwe na Mkwe mtu, na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.

35:Apendaye baba au mama kuliko Mimi hanistahili, Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.

JINSI GANI WATU WAKO WA KARIBU WANAWEZA KUKUGEUKA NA KUWA MAADUI?

Kuokoka, Kuzaliwa mara ya pili, kuamua kuishi maisha matakatifu ni kuchora mstari ambao unakutenga hata na watu unaowapenda na kiwategemea.

Wote waliopiga hatua ya kiimani ya kumpokea Yesu kuwa BWANA na Mwokozi wa maisha Yao wamejikuta katika uadui na ndugu zao wakaribu.

MKE ndani ya NDOA akiamua kuokoka kuacha DHAMBI kuanza kuamka kuomba usiku, au kwenda Kanisani, lazima adui yake wa kwanza atakuwa mumewe ikiwa mume huyo hajaokoka.

Mtoto wa kwanza katika familia, ukikutana na YESU Kweli Kweli na kuamua kuacha kufuata Mila za kwenu, ukiacha kwenda kwenu katika Ibada na shughuli za KIMILA za kiukoo, adui Yako wa kwanza, ni baba ,mama na ndugu zako wa Damu, ikiwa hawajaokoka.

Ikiwa umeokoka Leo ukagundua mkeo ni mchawi, jua wazi lazima uadui utakuwepo Kutoka Kwa aliye karibu zaidi Yako. Na uadui huo Si katika mwili, ni WA kiroho, KIMWILI ni mke, kiroho ni ADUI.

Siku mke utakapookoka na kugundua kuwa utajiri alioupata mumeo umetokana na makafara, lazima utajikuta katika vita ya karibu kabisa usoidhania. Ni mume katika mwili, katika Ulimwengu wa Roho, ni adui anayekuvizia akule KICHWA.

Siku binti utakapoamua kumkabidhi Yesu maisha Yako, uwe na HAKIKA, Adui Yako wa kwanza ni Baba na mama na familia Kwa ujumla ikiwa hawajaokoka.

SOLUTION YA KUKABILIANA NA MAADUI WA KARIBU YAKO WA DAMU.

Wengi waliookoka, waliposoma mstari huo wa (Mathayo 10:34) wamejikuta katika uchaguzi mbaya wa kuwatenga ndugu zao wasiookoka wakidhani ndivyo mstari ulivyomaanisha.

Wameacha kuhudhuria hata misiba, wanapofiwa, wameacha kuhudumia wazazi wao Kwa Sababu kuwa hawajaokoka na kukosa baraka za wazazi na maisha marefu duniani, wameshindwa kuwaonyesha Upendo ndugu zao ilhali Si sawa kufanya hivyo.

ZIFUATAZO ni suluhu kukabiliana na Hali hiyo.

1. MAOMBI.

Mwombe Mungu awavute pia waokoke Ili wasiwe tena adui zako. Mungu ameahidi akikuokoa Si pekeako tu, afuatilie pia na familia na ndugu zako wa Damu Ili waokoke. Afuatilie pia uzao wako pia uokolewe.

Unapowaombea, wataje Kwa Kila Mmoja Jina lake na usichoke kuomba na upendekeze muda ambao ungependa Mungu awaokoe.

Vita yetu ni ya kiroho Si ya kimwili, hivyo, hakikisha mahusiano yanaendelea kuwepo wakati ukiendelea kuwaombea, Mungu ni MWEMA atawaokoa.

2. WAONYESHE UPENDO.

Kamwe usionyeshe kuwachukia, jizungushie ulinzi wa Damu ya Yesu, endelea kuwapenda wakati ukiendelea kuwaombea Ili wabadilike.

3. PAMBANA NAO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.

Tenga na tafuta muda wa Kupambana na Roho za Giza katika Ulimwengu wa Roho zilizowashika Ili kuua nguvu za Giza ndani Yao. Ukiwashinda na kufanikiwa kuua nguvu za giza ndani Yao, ni Rahisi kuwavuta katika Wokovu.

Ikiwa ndugu zako ni washirikina, hakikisha unapambana nao bila huruma katika Ulimwengu wa Roho na hakikisha unashinda vita hiyo, maana aliyeokoka ni mshindi hata kabla ya kuingia vitani.

Maana imeandikwa: (Isaya 54:17).

Kila silaha itakayofanyika juu Yako, haitafanikiwa, na Kila Ulimi utakaoinuka juu Yako katika HUKUMU, utauhukumu kuwa mkosa.

Huo ndio URITHI wa watumishi wa BWANA na HAKI Yao inayotoka kwangu Mimi, asema BWANA.

Omba Kwa Imani ukiamini kuwa ukitamka Jina la YESU, radi hupiga ngome za waovu,

Ukisema Damu ya Yesu, jua kuwa katika Ulimwengu wa Roho, Damu huenda na kufungua vifungo na mikataba yote.

Ukitamka moto, jua moto utaenda kuwaunguza, ukitamka ninakata, jua kuwa Kweli Hilo litatokea,

Tumia silaha hizi, (Ephesians 6:11) says:

Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kizipinga Hila za shetani, Kwa maana, kushindana kwetu sisi, Si juu ya Damu na nyama, Bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa Giza hili, juu ya majeshi ya Pepo wabaya katika Ulimwengu wa Roho.

Katika Ulimwengu wa Roho, ndipo ulipo uwanja wetu wa vita.

Silaha zote zipo kule, vipo vifaru, Risasi, panga, mikuki, yapo makombora ya masafa marefu na mafupi, yapo mabomu ya KUTEGWA, zipo darubini na silaha zote za kivita uzijuazo katika Ulimwengu wa mwili, zipo pia huko katika Ulimwengu wa Roho.

4. WATOLEE SADAKA.

Ndugu zako wanapoenda kukuroga katika Ulimwengu wa Giza huenda na sadaka,

Pia tunapowaombea Kwa kuwataja Majina na kutumia Damu ya Yesu kuvunja mikataba na kuwanunua, ni vizuri Kutoa sadaka ya shukrani katika madhabahu ya BWANA.

NB: Ikiwa unayo dini Yako, na unashiriki kufanya Mila za ukoo au kabila Kwa miungu,una dini na unaenda Kwa Waganga, unayo dini, na pombe unakunywa kama kawaida, una dini na unatoka nje ya NDOA, nk nk, neno KUOKOKA hujalijua na kuliishi Bado.

HITIMISHO.

Sisi ni wapitaji Duniani, hatuna muda wa kupoteza, siku zote mchana na usiku tunahitaji Kupambana, kulitafakari neno la Mungu na kudumu katika Maisha ya utakatifu.

Mungu awabariki. Amen
 
upuuzi huu, sadaka haijawahi kumsaidia chochote binadamu, zaidi ya kumnufaisha mpokeaji, ndio maana makanisa mengi waumini ni masikini wa kutupwa, huku wachungaji wakiwa ni matajiri kupindukia
 
Mathayo 10:34-35) says:

Mie huu mstari sijawahi kuuelewa kabisa, anaejua anifafanulie.
 
Rudi kusoma thread nimefafanua.

Kumpokea Yesu Kweli Kweli ni kuwa Adui wa Dunia.

Wazazi ikiwa hawajaokoka, ni waabudu miungu, walevi nk nk, watasema umechanganyikiwa.

Mama atamkataa Binti akisema ameokoka na alikuwa katika uislamu nk nk, ndo uadui aliousema Yesu.

Ubarikiwe
 
upuuzi huu, sadaka haijawahi kumsaidia chochote binadamu, zaidi ya kumnufaisha mpokeaji, ndio maana makanisa mengi waumini ni masikini wa kutupwa, huku wachungaji wakiwa ni matajiri kupindukia
Usipotoa sadaka ni sawa na MKULIMA anayekula mbegu.

Mungu hukupa kipato Kwa ajili Yako, Kwa ajili ya maskini na mbegu ya kuendelea kubariki flow Yako ya pesa.

Rudi kutafuta ujue nguvu ya sadaka.

Usizidiwe akili na wapagani.
 
Amen mkuu!

Barikiwa sana..
 
Usipotoa sadaka ni sawa na MKULIMA anayekula mbegu.

Mungu hukupa kipato Kwa ajili Yako, Kwa ajili ya maskini na mbegu ya kuendelea kubariki flow Yako ya pesa.

Rudi kutafuta ujue nguvu ya sadaka.

Usizidiwe akili na wapagani.
Sawa..sasa kwa nini wachungaji wanakuwa matajiri kwa sadaka zetu sisi tunabaki masikini wa kutupwa? ndiyo Mungu alivyopanga?
 
Swali lako ni nje ya MADA.

Soma Yakobo 4:3 Pana majibu ya swali lako.

Pia Angalia Kwa Makini Mungu wa madhabahu inayoitolea sadaka ni Kutoka juu au chini.
 
upuuzi huu, sadaka haijawahi kumsaidia chochote binadamu, zaidi ya kumnufaisha mpokeaji, ndio maana makanisa mengi waumini ni masikini wa kutupwa, huku wachungaji wakiwa ni matajiri kupindukia
Wanasema wanaotoa sadaka wanabarikiwa sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom