Membe vs January Makamba

Mbegu na NN, nadhani suala pia ni January kutenda anayohubiri. Kwa bahati kidogo nawafahamu wote hawa wawili. Ukiongea nao utaona utofauti mkubwa katika hili suala la Kiswahili vs Kingereza.

Ukiongea na January katika kila maneno 10, saba au zaidi ni kiingereza na wakati mwingine anaenda sentesi mfufulizo bila kuchomeka kiswahili. Kwa uzoefu wangu nimeweza kujua kuwa anafanya hivyo kutegemeana na nani anazungumza naye, na uwezo wa mtu katika lugha.

Ukiongea na Membe katika kila maneno kumi, labda matatu yatakuwa ni kiingereza, na hii ni kwa wote, tangu alipokuwa Canada.

Kwa January kutetea Kiswahili wakati kitabu chake, blog na website zake (January Makamba.com au Politics, Society & Things) zinazowalenga wapiga kura wake wa Bumbuli zimeandikwa Kingereza, nadhani ni unafiki wa aina fulani.

Muswada wa Mabadiliko Ya Katiba umeandikwa Kingereza na kusambazwa kwa wananchi, pamoja na wapiga kura wa Bumbuli, waujadili. Kamwe hatukusikia January kuungana na akina Zitto, Lema, Mnyika, UDASA na wengineo waliotaka na bado wanataka kuwa muswada huo uchapishwe kwa Kiswahili kabla ya kuzambazwa kwa wananchi wote. Na serikali ya CCM imegoma kufanya hivyo, na badala yake wanasema wataweka wakalimani.........go figure!!!

Ni nini kimebadilika hadi leo hii January amekuwa mtetezi mkubwa wa Lugha ya Taifa kuliko lugha mbadala iliyopo kwenye kanuni za Bunge?

Una hoja nzuri.

Tatizo kubwa ni kwamba hata hatujui tufuate lugha ipi.

Hivi leo hii kuna Mtanzania anayeweza kweli kuongea Kiswahili bila kuchanganya na Kiingereza?
 
i concur with you llombe kwanza nilikuwa naona kinyaa wakati huyo januari anatetea upupu shame upon him analeta siasa za kitoto na kiswahili kwenye isue serious kweli mtoto wa nyoka hawezi kuwa kenge .
 
How could you not distinguish between informal language, official language and national language?

Unataka wawakilishi wawe wanatembea na mashine za kutafsiri lugha na dictionary?

I have confirmed once a rattle snake always a rattle snake!

========

Kilichojiri ni kwamba January Makamba ametoa taarifa kwa Spika kwamba kiswahili ni lugha ya taifa na pia moja ya lugha ya AU tujivunie na kutaka wagombea wa uwakilishi wa Bunge la Africa wajieleze kiswahili na si kiingereza kama kanuni inavyoelekeza.

Membe akasema uzoefu na kanuni vifuatwe. Wajieleze kiingereza kwa sababu kiswahili ni wakati wa mkutano, nje wajumbe watakuwa wanatumia kiingereza kuinteract.

Halima Mdee alitoa hoja kwamba kanuni ni kujieleza kwa kiingereza. Hoja ikapita

Nahisi kinyume chake ndio ukweli
 
Sidhani kama ni msuguano mkubwa sana jamani....ni hoja za kawaida sana zile..nothing valuable pale..
 
ya JM ni sawa na L Masha.......tutayaona na kuyasikia mengi kama hatajirekebisha
 
Mbegu na NN, nadhani suala pia ni January kutenda anayohubiri. Kwa bahati kidogo nawafahamu wote hawa wawili. Ukiongea nao utaona utofauti mkubwa katika hili suala la Kiswahili vs Kingereza.

Ukiongea na January katika kila maneno 10, saba au zaidi ni kiingereza na wakati mwingine anaenda sentesi mfufulizo bila kuchomeka kiswahili. Kwa uzoefu wangu nimeweza kujua kuwa anafanya hivyo kutegemeana na nani anazungumza naye, na uwezo wa mtu katika lugha.

Ukiongea na Membe katika kila maneno kumi, labda matatu yatakuwa ni kiingereza, na hii ni kwa wote, tangu alipokuwa Canada. ?

Kutetea matumizi ya Kiswahili sio lazima imaanishe kupinga matumizi ya Kiingereza. Namaanisha katika uendelevu wake lugha hizi sio "mutually exclusive", lakini sijui neno la Kiswahili la kutumia hapa! LOL. Na nikifanya hivi, yaani kutetea matumizi ya Kiswahili halafu kuwa mjuzi wa lugha ya Kiingereza haimaanishi kutokutenda ninachohubiri hata kidogo. Jamani, mbona Nyerere mtetezi na mjenzi mkubwa wa Kiswahili ndiye pia alitafsiri Shakespeare "Mabepari wa Venisi". Leo hii Januari kutetea Kiswahili wakati ni mzungumzaji sana wa Kiingereza inachukuliwa kuwa ni nongwa? Lugha zote hizi mbili zina nafasi ya kuendelezwa bila ya moja kulazimika kuwekwa juu ya nyingine kisera.

Kwahiyo basi, kutumia Kiingereza kutegemeana na mtu unayezungumza naye ni sahihi. Kwahiyo anachofanya Januari ni sawa. Hoja sio kwamba Kiingereza kisitumike; bali ufahamu mahali pake pa kukitumia. Januari hatumii Kiingereza mbele ya wananchi wa Bumbuli hata kidogo. Kule anapiga Kiswahili au Kisambaa (sio jukwaani). Lakini akiwa anabadilishana mawazo na vichwa kama nyie, haidhuru tena ni muhimu sana kutumia Kiingereza maana hiyo ndio lugha ambayo ni rahisi kujenga nayo hoja za kisasa katika dunia ya leo.

Kwa January kutetea Kiswahili wakati kitabu chake, blog na website zake (January Makamba.com au Politics, Society & Things) zinazowalenga wapiga kura wake wa Bumbuli zimeandikwa Kingereza, nadhani ni unafiki wa aina fulani.

Muswada wa Mabadiliko Ya Katiba umeandikwa Kingereza na kusambazwa kwa wananchi, pamoja na wapiga kura wa Bumbuli, waujadili. Kamwe hatukusikia January kuungana na akina Zitto, Lema, Mnyika, UDASA na wengineo waliotaka na bado wanataka kuwa muswada huo uchapishwe kwa Kiswahili kabla ya kuzambazwa kwa wananchi wote. Na serikali ya CCM imegoma kufanya hivyo, na badala yake wanasema wataweka wakalimani.........go figure!!!

Ni nini kimebadilika hadi leo hii January amekuwa mtetezi mkubwa wa Lugha ya Taifa kuliko lugha mbadala iliyopo kwenye kanuni za Bunge?

Sio kweli kwamba blogu na wotuvi yake zimewalenga wapiga kura wake wa Bumbuli. Hiyo haiyumkiniki maana wananchi wengi wa Bumbuli hawana hata kompyuta. Mikutano ya vijiji, mikutano ya hadhara, ziara jimboni, huduma ya SMS ya bure ndio baadhi ya njia Januari anazotumia kuwafikia wapigakura wake. Tovuti na blogu ni kwa ajili yako wewe Mtanzania uliyebahatika kuwa na kompyuta, na pia kwa ajili ya kujenga mtandao wa kimataifa wa kuleta maendeleo Bumbuli. Kitabu chake nimetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.

Kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Katiba kuandikwa kwa Kiingereza, hili pia Januari amelipinga (kumbuka yeye ni mwakilishi kwanza, sio mtetezi wa Serikali kwanza.... na kuwa ndani ya CCM haimaanishi huna haki ya kuikosoa katika jambo la msingi). Vile vile alipinga hapo mwanzoni kutokupeleka mjadala wa Muswada huu kule Zanzibar.
 
Bunge ni la Tanzania lugha ya kwetu Kiswahili full spot, January was very right ni vibaraka uchwara wa lugha za wageni ndio wanamuona hakutumia busara. Yeye alitaka hata wananchi wa Bubumbuli wajue wabunge wao wanazungumza nini hilo la kupima uwezo wao wa ngeli nis suala la vyama vilivyowapitisha kuwa wabunge. Full Stop.
Hivi ndio sababu aliwaandikia kitabu katika lugha ya Kiengereza?
 
Una hoja nzuri.

Tatizo kubwa ni kwamba hata hatujui tufuate lugha ipi.

Hivi leo hii kuna Mtanzania anayeweza kweli kuongea Kiswahili bila kuchanganya na Kiingereza?

Mbona unatuvunjia heshima mkuu tupo wengi tu.
 
Kuna dalili zote za 'BIFU' baina yao, sina shaka Mh. Membe baada ya kutolewa na huyu dogo kule CC, ana wasiwasi na nafasi yake ya uwaziri.
 
membe sio kilaza kama JM bali ni muongo kuanzaia hapo alipopinga Mapank Mwanza, Siraha kwenda Congo akiituhumu UN, OIC kuingiza kinyemea alafu hajisimamii anatumika tu, Makamba kumjibu Mwana Mama wa kimarekani kuhusu hatima ya tazania na umaskini wakati wahisani kupitia aids zao wanatoa pesa nyingi zinaishia mifukoni mwa JM na JK akatoa mfano wa mkate kutoka 400 -800 na nk , makamba kwa kutumia ukilaza wake alimjibu huyo mtoa misaada kuwa ya nchi yetu hayamhusu wakati JK uenda Marekani na ka bakuri kila mara, inaonesha wote hawana busara hawafai, samahani mama huyu jina lake nimelisahau aliyesoma makala ya face book hatukumbushe, sijui ni rockfer

Anaitwa Lisa Rockerfeller, ni mtoto wa Tycoon mkubwa ambao ni miongoni mwa familia zinazotoa support kubwa hata kwa serikali ya Marekani. Ni watu wenye nguvu sana katika kutoa maamuzi (Sera) za kiuchumi. Hawa ni pamoja na watu kama Teddy Turner (CNN), Waren Buffet, Donard Trimphy, Bill Gates etc. Hawa wanaweza kuiambia serikali, Tanzania isipate misaada na ikawa. My Take: Kwa sababu za kijinga JM aliweza kumshambulia huyu mama, na si kwa ule mjadala tuliouona kwenye FB lakini alikwenda mbali zaidi kwa kupiga simu na kuongea maneno makali sana. Kwa hakika busara ilikosekana either kwa nature ya kijana mwenyewe au pressure za kisiasa hasa ikizingatiwa ilikuwa ni kipindi cha uchaguzi.
 
Hoja ni Januari kutaka wagombea wajieleze kiswahili kisa ni lugha ya AU. Hayo ya bifu yanatoka wapi? Membe awe na wasiwasi wa nafasi yake kwa sababu zipi?

Kama Januari anastahili nafasi ya Membe Raisi ataamua hivyo ila mpaka sasa kila mmoja ana nafasi yake.
 
Bunge ni la Tanzania lugha ya kwetu Kiswahili full spot, January was very right ni vibaraka uchwara wa lugha za wageni ndio wanamuona hakutumia busara. Yeye alitaka hata wananchi wa Bubumbuli wajue wabunge wao wanazungumza nini hilo la kupima uwezo wao wa ngeli nis suala la vyama vilivyowapitisha kuwa wabunge. Full Stop.

You sound like yule kiongozi wangu anayecheka cheka hovyo
 
Anaitwa Lisa Rockerfeller, ni mtoto wa Tycoon mkubwa ambao ni miongoni mwa familia zinazotoa support kubwa hata kwa serikali ya Marekani. Ni watu wenye nguvu sana katika kutoa maamuzi (Sera) za kiuchumi. Hawa ni pamoja na watu kama Teddy Turner (CNN), Waren Buffet, Donard Trimphy, Bill Gates etc. Hawa wanaweza kuiambia serikali, Tanzania isipate misaada na ikawa. My Take: Kwa sababu za kijinga JM aliweza kumshambulia huyu mama, na si kwa ule mjadala tuliouona kwenye FB lakini alikwenda mbali zaidi kwa kupiga simu na kuongea maneno makali sana. Kwa hakika busara ilikosekana either kwa nature ya kijana mwenyewe au pressure za kisiasa hasa ikizingatiwa ilikuwa ni kipindi cha uchaguzi.

Mazee umechapia majina ya hao mabwana..daaaah
 
Vikwazo, unamtenga ndugu yako kisa avatar? Je Katiba mpya atachangia kweli? Muswada ameupata? Kama taarifa za Bunge zinachelewa kumfikia je maandiko?
 
Anaitwa Lisa Rockerfeller, ni mtoto wa Tycoon mkubwa ambao ni miongoni mwa familia zinazotoa support kubwa hata kwa serikali ya Marekani. Ni watu wenye nguvu sana katika kutoa maamuzi (Sera) za kiuchumi. Hawa ni pamoja na watu kama Teddy Turner (CNN), Waren Buffet, Donard Trimphy, Bill Gates etc. Hawa wanaweza kuiambia serikali, Tanzania isipate misaada na ikawa. My Take: Kwa sababu za kijinga JM aliweza kumshambulia huyu mama, na si kwa ule mjadala tuliouona kwenye FB lakini alikwenda mbali zaidi kwa kupiga simu na kuongea maneno makali sana. Kwa hakika busara ilikosekana either kwa nature ya kijana mwenyewe au pressure za kisiasa hasa ikizingatiwa ilikuwa ni kipindi cha uchaguzi.

Mmeingizwa choo cha kike ndugu zangu! Januari hakuhusika na mjadala wa FB pamoja na Lisa. Watu tu humu JF wamemzushia ili kumchafua. Kwanza hamjui huyo Lisa, pili hizo siku za huo mjadala Januari alikuwa akifanya kampeni vijijini bila kuwa na mtandao au muda wa kubishana na huyu dada kwa siku tatu mfululizo, tatu in general huwa hana muda wa kukaa kwenye FB kiasi hicho, nne hawezi kuandika ujinga ule wala sio ile sio style yake ya malumbano au ya uandishi, tano Ernesto Sheka (ambaye alikuwa analumbana na Lisa kwenye FB) mwenyewe ni mtu anajulikana na jamii. Inashangaza kwamba amegeuzwa kuwa Januari. Sita, kuna ushahidi mwingi kwamba huyo Lisa wa FB sio Lisa Rockerfeller mwenyewe, alikuwa impostor wake. Kwa ufupi, hiyo habari ni riwaya tu ambayo inaonyesha utaalam wa maadui katika kumvunjia heshima mtu.
 
Kutetea matumizi ya Kiswahili sio lazima imaanishe kupinga matumizi ya Kiingereza. Namaanisha katika uendelevu wake lugha hizi sio "mutually exclusive", lakini sijui neno la Kiswahili la kutumia hapa! LOL. Na nikifanya hivi, yaani kutetea matumizi ya Kiswahili halafu kuwa mjuzi wa lugha ya Kiingereza haimaanishi kutokutenda ninachohubiri hata kidogo. Jamani, mbona Nyerere mtetezi na mjenzi mkubwa wa Kiswahili ndiye pia alitafsiri Shakespeare "Mabepari wa Venisi". Leo hii Januari kutetea Kiswahili wakati ni mzungumzaji sana wa Kiingereza inachukuliwa kuwa ni nongwa? Lugha zote hizi mbili zina nafasi ya kuendelezwa bila ya moja kulazimika kuwekwa juu ya nyingine kisera.

Kwahiyo basi, kutumia Kiingereza kutegemeana na mtu unayezungumza naye ni sahihi. Kwahiyo anachofanya Januari ni sawa. Hoja sio kwamba Kiingereza kisitumike; bali ufahamu mahali pake pa kukitumia. Januari hatumii Kiingereza mbele ya wananchi wa Bumbuli hata kidogo. Kule anapiga Kiswahili au Kisambaa (sio jukwaani). Lakini akiwa anabadilishana mawazo na vichwa kama nyie, haidhuru tena ni muhimu sana kutumia Kiingereza maana hiyo ndio lugha ambayo ni rahisi kujenga nayo hoja za kisasa katika dunia ya leo.

Sio kweli kwamba blogu na wotuvi yake zimewalenga wapiga kura wake wa Bumbuli. Hiyo haiyumkiniki maana wananchi wengi wa Bumbuli hawana hata kompyuta. Mikutano ya vijiji, mikutano ya hadhara, ziara jimboni, huduma ya SMS ya bure ndio baadhi ya njia Januari anazotumia kuwafikia wapigakura wake. Tovuti na blogu ni kwa ajili yako wewe Mtanzania uliyebahatika kuwa na kompyuta, na pia kwa ajili ya kujenga mtandao wa kimataifa wa kuleta maendeleo Bumbuli. Kitabu chake nimetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.

Kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Katiba kuandikwa kwa Kiingereza, hili pia Januari amelipinga (kumbuka yeye ni mwakilishi kwanza, sio mtetezi wa Serikali kwanza.... na kuwa ndani ya CCM haimaanishi huna haki ya kuikosoa katika jambo la msingi). Vile vile alipinga hapo mwanzoni kutokupeleka mjadala wa Muswada huu kule Zanzibar.

Kutetea matumizi ya kiswahili haimaanishi kupinga matumizi ya kiingereza. Hii ndio hoja ya msingi.

Ni bahati mbaya tu hii nchi inashindwa kutambua michango kama hii. Najiuliza inakuwaje huyu kijana mwenzetu anashindwa kuliona hili.
 
Kuna dalili zote za 'BIFU' baina yao, sina shaka Mh. Membe baada ya kutolewa na huyu dogo kule CC, ana wasiwasi na nafasi yake ya uwaziri.

Sijawahi kuona mawazo mgando kama haya. Hivi unadhani uwaziri unagombaniwa. Kama JM ni bora kwa nini appointing authority haikumuona? Tusifike mahali tukaukanganya umma na hoja za kitoto. Hoja ilikuwa ni kwamba wagombea wa nafasi za uwakilishi bunge la afrika lazima wapimwe proficiency yao katika kiingereza maana ndiyo lugha inayotumika huko PAP. Sasa hilo la kujifanya mzalendo na kutetea kiswahili wakati anajua kwamba si wagombea wote wanajua kiingereza na kujua lugha hiyo ni sehemu ya sifa muhimu ni unafiki uliopitiliza. Hata kama kuna wanaomu-admire JM hapa hapakuwa mahali pake maana ni wazi kwamba alichemsha.

Hata yale mawazo kwamba Membe na JM wana ushindani ni potofu maana hawa hawana chochote cha kufanana zaidi ya kwamba wote ni wabunge. Upeo, uwezo na uzoefu wa Membe ni kama mlima kilimanjaro ambao unajaribu kuulinganisha na lori moja la kifusi. Kuna watu wanasema eti kwa kuingia kwenye sekretarieti basi jamaa amepata nafasi ya kuchimba dili za Membe na waarabu. Good idea lakini hatapata chochote maana hakuna madili yoyote. Lakini kama atachunguza basi afanye hivyo na aende mbele kuchunguza zilipo fenicha za shilingi 84 milioni ambazo zilitumika wakati wa mkutano mkuu wa CCM mwaka 2010 na ambazo zilikuwa chini ya uangalizi wa Katibu Mkuu wa CCM na ambazo sasa zimetoweka na minong'ono inasema zimepeklekwa kwenye hoteli ya baba yake kule Morogoro. Huu ni ufisadi ambao kwa kweli atakisaidia chama kuutokomezwa na kupendekeza hatua za kuchukua dhidi ya baba yake. Hata huko kujigamba kwamba alifanya kazi foreign affairs ni kichekesho maana hata miezi mitatu haikufika na kwa maisha yake ya ikulu amekuwa na kazi ya kutayarisha draft speeches. Hajui chochote kuhusu international relations na the rest ni ujinga tu.
 
Back
Top Bottom