Membe vs January Makamba

Vijana wa Membe kuweni na subira humu yaani mtu wenu asiguswe ila ninyi kazi kushambulia wengine humu.
 
hivyo hivyo kiaina lisukume February hata kama mikono itachubuka poa tu usiwe kama baba yako
 
Weweeeee,ebu muaache afanye kazi zake bana!
Sasa ajilekibishe ili iweje?
ionekane mmevua gamba kweli?

Kazana kijana,i hope mzee kakurithisha kila kitu
sasa ukivua magamba kama kobe si utabaki uchi?
icon8.png
 
membe sio kilaza kama JM bali ni muongo kuanzaia hapo alipopinga Mapank Mwanza, Siraha kwenda Congo akiituhumu UN, OIC kuingiza kinyemea alafu hajisimamii anatumika tu, Makamba kumjibu Mwana Mama wa kimarekani kuhusu hatima ya tazania na umaskini wakati wahisani kupitia aids zao wanatoa pesa nyingi zinaishia mifukoni mwa JM na JK akatoa mfano wa mkate kutoka 400 -800 na nk , makamba kwa kutumia ukilaza wake alimjibu huyo mtoa misaada kuwa ya nchi yetu hayamhusu wakati JK uenda Marekani na ka bakuri kila mara, inaonesha wote hawana busara hawafai, samahani mama huyu jina lake nimelisahau aliyesoma makala ya face book hatukumbushe, sijui ni rockfer
 
Kwanini uachiwe upumzike wakati umechangia katika kutuharibia nchi yetu!? Huna tuhuma za kujibu kule mahakamani katika ufisadi mbali mbali ulioshiriki kutuibia/kutudhulumu Watanzania?
 
Makamba Jr anaonekana mtu mwenye uwezo wa kujenga hoja, ngoja tuendelee kumpa muda
 
Ukweli unabaki, January just didnt think. His support to kiswahili was ill timed!

Ill timed to support Kiswahili? When is it the right time? Hivi kweli unamshutumu Januari hata kwa hilo? Suala sio kwamba hakuelewa Kanuni za kuchagua wabunge wa AU (hilo lazima analifahamu). Suala ni kutaka Kanuni itazamwe upya ili kukuza lugha yetu ndani ya shughuli za kimataifa. Na hiyo ni hoja sahihi kuitoa. Badala ya kujadili hili la kukuza lugha yetu nje, mnajadili nani kati ya Januari na Membe mwenye akili na nani kamuumbua mwenzake! The Home of great thinkers. Chuki ikizidi maarifa bwana...
 
Hivi kweli unamshutumu Januari kwa jitihada za kukuza lugha ya Taifa? Suala sio kwamba hakuelewa Kanuni za kuchagua wabunge wa AU (hilo lazima analifahamu). Suala ni kutaka Kanuni itazamwe upya ili kukuza lugha yetu ndani ya shughuli za kimataifa. Na hiyo ni hoja sahihi kuitoa. Badala ya kujadili hili la kukuza lugha yetu nje, mnajadili nani kati ya Januari na Membe mwenye akili na nani kamuumbua mwenzake! The Home of great thinkers. Chuki ikizidi maarifa bwana...
 
Huyu JM naona anapandishwa ngazi kwa kasi ya ajabu; nahisi atakuwa anaandaliwa post nzito sana ndani ya dola in the near future
 
January bwana! Eti alikuwa mfanyakazi wizara ya mambo ya nje na walikuwa wanatumia pesa nyingi kupromote kiswahili hivyo wagombea wahojiwe kiswahili. Yeye alikuwa mfanyakazi wa wizara wakati membe ndiye bosi wa wizara hiyo sasa sielewi january anataka kutueleza nini! Kwamba membe hatimizi majukumu yake ipasavyo kukikuza kiswahili na hivyo yeye apewe nafasi hiyo?
 
Hivi kweli unamshutumu Januari kwa jitihada za kukuza lugha ya Taifa? Suala sio kwamba hakuelewa Kanuni za kuchagua wabunge wa AU (hilo lazima analifahamu). Suala ni kutaka Kanuni itazamwe upya ili kukuza lugha yetu ndani ya shughuli za kimataifa. Na hiyo ni hoja sahihi kuitoa. Badala ya kujadili hili la kukuza lugha yetu nje, mnajadili nani kati ya Januari na Membe mwenye akili na nani kamuumbua mwenzake! The Home of great thinkers. Chuki ikizidi maarifa bwana...

Safi sana Mbegu. Lugha yetu ni nzuri sana na nashindwaga kabisa kuelewa kwa nini hatuikuzi na badala yake tunashobokea lugha ya kigeni. Januari alikuwa sawa kabisa na kwa hilo mimi namuunga mkono. Tutaendelea kuathirika na ukoloni mamboleo hadi lini?
 
Kanuni zetu ni za kipumbavu sana. Kwa mgombea ubunge anambiwa awe na sifa ya kujua kusoma na kuandika, enough, haikusema vidato.. sasa nijuavyo mimi wapo wabunge wengine sekondary hawakugusa, sasa sijui wanawasaidiaje, yaani kanuni moja inapingana nanyingine, shida tupu.
 
Huyu JM naona anapandishwa ngazi kwa kasi ya ajabu; nahisi atakuwa anaandaliwa post nzito sana ndani ya dola in the near future
Ameanza na nafasi za chama, bado uwaziri na huenda urais huko mbeleni!!
 
Hapa hakuna kitu kama Membe v/s January. Why not Halima v/s January? Au Mna- chovya karatasi ya litimasi muone miitikio au ushabiki wa watu?


1.Hawa unaowajadili ni marafiki na hawana bifu lolote. Aidha, wawakilishi kutofautiana katika mitizamo na maelezo bungeni ni jambo la kawaida sana na kama sivyo basi mnataka tujiandae kuwa na Bunge la ajabu lisilo na mijadala bali kupitisha tu hoja kwa ndiyooooooooooooo!
Membe anatetea Kanuni na mazoea ya Bunge, January anatetea mchakato wa kuanza kubadilisha hayo mazoea; no big deal of the so called timing and what not!!

2. Suala la wigo wa matumizi ya Kiswahili bado ni la mjadala katika medani na nyanja mbalimbali nchi mwetu kwa siku nyingi.
Mimi naungana na wote ambao hawashabikii matumizi ya Kiingereza kila mahala, nataka kuona Kiswahili kinatumika hata mashuleni, vyuoni katika Mahakama n.k. Wajapani, Wachina, Wajerumani n.k si maskini na wala hawajifunzi au kujadiliana kwa Kiingereza. Ukisikiliza Kiingereza cha Balozi wa Japani nchini kwetu unaweza kukodoa macho tu na kuanza kusukuma cha kwako popote kwa kujiamini kama above good user katika viwango vya mitihani ya kiingereza duniani.
Tuache kuendeleza kujiningíniza katika Utumwa. Kiingereza kibaki kama lugha ya pili au ya tatu ukithamini lugha ya kabila lako pia!

2. Hakuna kipengele wala kanuni inayoeleza kuwa Waziri wa Mambo ya nchi za nje ndiye lazima apewe kuongoza Idara hiyo katika CCM, haya ni mazoea tu ambayo yanaweza kubadilishwa. Kwa hakika mimi napenda Viongozi wa juu wa CCM wasiwe watendaji wa juu katika Serikali na sababu zake nzuri zipo ambazo zimesha jadiliwa humu.

3. Nawapa pole na pengine onyo watu wenye uwanja finyu sana wa kufikiri. Tz na hapa niseme CCM ina watu kibao (hata walio nje ya Halmashauri kuu au hata Kamati Kuu) wenye uwezo na sifa nzuri sana kugombea Urais na kuajibika ipaswavyo kwa kiwango cha juu wakifanikiwa. Kwa nini tunazunguka katika kamzunguko ka sampuli ya watu wachache tu hivi? Ni nani ametoa hiyo sampuli. Unafikiri watu ni wajinga toka wakati wa Nyerere (pamoja na kura ya ndiyo na hapana) hakuna mahala paliandikwa kuwa sifa ya Mgombea Rais ni kuwa lazima awe mjumbe wa Kamati Kuu au Halmashauri kuu ya Chama au awe Waziri?

Mazoea si kanuni na hata kanuni hubadilishwa endapo zinapwaya! Hiki ni kizazi kingine na upeo wa watu ni mkubwa sana.

MwanaJF makini ni yule anayemaliza kwa kushauri kubadili kichwa cha mada hii kuwa, "Wigo Matumizi ya Kiswahili na Kiingereza nchini Tanzania".
 
Safi sana Mbegu. Lugha yetu ni nzuri sana na nashindwaga kabisa kuelewa kwa nini hatuikuzi na badala yake tunashobokea lugha ya kigeni. Januari alikuwa sawa kabisa na kwa hilo mimi namuunga mkono. Tutaendelea kuathirika na ukoloni mamboleo hadi lini?


Mbegu na NN, nadhani suala pia ni January kutenda anayohubiri. Kwa bahati kidogo nawafahamu wote hawa wawili. Ukiongea nao utaona utofauti mkubwa katika hili suala la Kiswahili vs Kingereza.

Ukiongea na January katika kila maneno 10, saba au zaidi ni kiingereza na wakati mwingine anaenda sentesi mfufulizo bila kuchomeka kiswahili. Kwa uzoefu wangu nimeweza kujua kuwa anafanya hivyo kutegemeana na nani anazungumza naye, na uwezo wa mtu katika lugha.

Ukiongea na Membe katika kila maneno kumi, labda matatu yatakuwa ni kiingereza, na hii ni kwa wote, tangu alipokuwa Canada.

Kwa January kutetea Kiswahili wakati kitabu chake, blog na website zake (January Makamba.com au Politics, Society & Things) zinazowalenga wapiga kura wake wa Bumbuli zimeandikwa Kingereza, nadhani ni unafiki wa aina fulani.

Muswada wa Mabadiliko Ya Katiba umeandikwa Kingereza na kusambazwa kwa wananchi, pamoja na wapiga kura wa Bumbuli, waujadili. Kamwe hatukusikia January kuungana na akina Zitto, Lema, Mnyika, UDASA na wengineo waliotaka na bado wanataka kuwa muswada huo uchapishwe kwa Kiswahili kabla ya kuzambazwa kwa wananchi wote. Na serikali ya CCM imegoma kufanya hivyo, na badala yake wanasema wataweka wakalimani.........go figure!!!

Ni nini kimebadilika hadi leo hii January amekuwa mtetezi mkubwa wa Lugha ya Taifa kuliko lugha mbadala iliyopo kwenye kanuni za Bunge?
 
Back
Top Bottom