Membe kuwania urais 2015...

Hii habari wala haikukaa sawa zaidi ya kuzungumzia maudhi ya Mudhihir..
Yes Membe anaweza kuwa na mapungufu yake kama kiongozi...
I'm for Membe....
Ni kweli kuwa habari hii ni malicious. Hakuna kiongozi asiye na mapungufu, na inawezekana kuwa mapungufu ya Membe ni afadhali kuliko hao wengine.
 
Kama kweli atagombea,basi ni pandikizi la 'uovu'
membe-kama-membe is not independent of his own!watakuwa wamemuweka wahuni hawa,ili asijekufikiria kuirevise katiba!

tunamtaka rais ambae akiingia tu,anaanza na kuirevise katiba
 
Lakini Membe hawezi kugumbea Urais,kwa sababu ana uhusiano na Kikwete,uhusiano wa aina fulani,shemeji or something.
Inashangaza kuona kwamba Waziri wa Mambo ya Nje Tanzania sasa anakuwa Crown Prince.Lakini ni kwa ajili ya zile big,big,fat bags wanazopitisha airports. Umeyaona mabego yao hawa diplomats? It is xxxxx unbelievalable,yale mabegi yalivyokuwa makubwa.
 
Makubwa hayo. Kila la Kheir Membe katika mbio zako.........



Dr Hamza.
Doha
 
Hao ndio aina ya watu wanaotaka kutuongoza katika nchi hii. Tutaendelea kusema pasipo vitendo hadi kiama. Jamaa kapania kuwa Rais kwa gharama yoyote ile. Lakini tukikataa asiwe Rais nani kwa mtazamo wako unadhani anafaa kuwa Rais wetu ajaye ndani ya CCM.

Hili ni Swali zuri sana ma tunatakiwa tuwe tunauliza maswali haya mapema kabla muda haujatufikia usoni. Nani tunamtaka awe rais wetu? Na kwa nini tunazungumzia 2015, kwani hatuna uchaguzi 2010, au ndo kusema...?
 
Mie nina khabari kuwa mheshimiwa hana 'digrii', sasa CCM si hawaitaki hiyo kitu ya kutokuwa na angala shahada1!!! itakuwaje? au ameisha andaa ya chonga!!?
 
kwani kuba ubaya Membe kugombania urais?

mbona Mbowe tayari keshajipitisha kugombea Urais na hakuna anayetia neno?
 
Mimi ningependekeza kama na mbwai na iwe mbwai. Kwa kuwa nchi imekumbatia ubepari uliokithiri kwa viongozi wetu na hali ni mbaya sana kwa wanyonge, na kwa kuwa kuzuia hali hiyo nguvu ni kidogo, ningependekeza fomu ya urais mwaka ujao ada yake iwe ya kifisadi yaani bilioni 220 za kitanzania. Ili kama mbwai na iwe mbwai. Ama! Hapa nchi ni Masokorokwinyo tuuu, kila kukicha!
 
Integrity ya gazeti hili lililoandika hii habari nina wasiwasi nayo, ni yale yale ya wanaopigana vikumbo kuelekea Urais 2015 na hata ikilazimu 2010.
 
Jamani,Membe na mudhihir wote wanajuana..hapa kuna issue moja tu...Kiwanda cement.Membe ana watu wake wanataka kujenga Mtwara mjini hicho kiwanda...Mudhihir nae ana watu wake (TioT)wanataka wajenge Mchinga,ila malighafi iko mchinga.....sasa hapo wanatakiwa kwenda na hoja zao kwenye kamati ya mkoa...sio bungeni.......ila mwaka ujao MM hana lake...ubunge anataka labda atokee hapo....kwenye kiwanda
Mkuu bado hata hii haileti mantiki.. Membe akijenga kiwanda cha saruji Mtwara na Mudhihir akijenga kwao Mchinga kuna ubaya gani kuwa na viwanda viwili.. Hii ni dunai aya utandawazi ambapo soko ndilo linatawala supply kisha hakuna mipaka kwani saruji inahitajika kusini kote kwa Afrika iweje Membe amzuie mtu kujenga kiwanda cha saruji wakati sii cha serikali.

Membe hatoi vibali vya ujenzi, walla huu sii mradin wa kitaifa kusema kwamba kuna mkopo hawa jamaa wanagombania..ndio maana nikasema huyo Mudhihir atueleze vizuri Membe anahusiaka vipi na kuzuia mradi huo, pengine mimi nachjoweza kufikiria ni wapi kiwanda kijengwa kati ya wilaya mbili wanazowakilisha watu hawa.. ndipo utata ulipoanza kwani kila mmoja wao anataka kura za wananchi wake..Na ugonvi kama huu bungeni Hilo linawezekana kabisa, ni jambo la kawaida fahari wawili kugombea uwekezaji ktk wilaya zao..
 
Membe hafai kuwa kiongozi wa nchi hii maa hana sifa yoyote ile. ni mnafiki mkubwa, hajiamini,hana uwezo wa kuongea mbele ya watu, anatumia akiliza za wenzie kufanya maamuzi.
kuwa waziri wa mambo ya nje si kigezo. kwa hali tuliyonayo hv sasa akishika nchi 20015 hakuna jipya.
Kuwa Mkatoliki hakusaidii kuwa rais,hana sifa kabisa maana ana tofauti kidogo sana na huyu wa sasa. unafiki mwingi sana nchi hii.MEMBE HAFAI
 
The point is hiyo limestone iko wilaya nzima ya Lindi. Ndiyo maana Mudhihir haelewi kama andiko la mradi lilisema kiwanda kijengwe jinbo la Mchinga kwa nini lihamishiwe sehemu nyingine? Hata mimi sielewi na siamini kama Membe anaweza kufanya kitu kama hicho. Ninahisi Mudhihir ana agenda nyingine. Na yeye ameishakatika mkono bado hajajifunza tu? Akae kimya na ashukuru kiwanda kuja Lindi iwe jimbo la Mtama au Mchinga bado ni Lindi.
 
Mkandara,

..Membe anataka kumzidi mahesabu mwenzake kwa kulazimisha kiwanda kijengwe jimboni kwake -- Mtama.

unaendelea.

Joka Kuu, huu Uongo 100%. Kiwanda kitarajiwa kujengwa Lindi mjini, Lindi mjini sio jimbo la Membe wala la Mdhihiri. Na ni Membe aliyefanikisha ujenzi huu.

Mdhihiri ni mfa maji na anatumiwa na mafisadi. CCM haimtaki kwani uchaguzi uliomweka Kikwete madarakani alishindwa vibaya sana katika jimbo lake na kusababisha JK kupata 3% ya kura zote kwenye jimbo la Mdhihir. Mchinga ni jimbo la CUF na CCM wanakiri kuiba kura na Mdhihir anajuwa hili fika.
 
mgonjwaUkimwi said:
Joka Kuu, huu Uongo 100%. Kiwanda kitarajiwa kujengwa Lindi mjini, Lindi mjini sio jimbo la Membe wala la Mdhihiri. Na ni Membe aliyefanikisha ujenzi huu.

Mgonjwa,

..what i wrote was my own interpretation of what was on the newspapers. thanks for the correction.

..Mudhihiri analilia kiwanda kijengwe jimboni kwake, na anahisi Membe "nyoka wa mdimu" anamuwekea roho mbaya ktk suala hilo.

..kwa tafsiri yangu wanamtandao ni mafisadi, na Membe kuwa kinara ktk kundi hilo ni fisadi pia.

..hizi mbinu anazotumia Mudhihiri sasa hivi ndiyo mbinu alizotumia Membe na wanamtandao wenzake kuwachafua wenzao kabla ya uchaguzi wa 2005.

..it is now Membe's turn to taste his own medicine.

..kwa upande mwingine sidhani...sidhani kama Bernard Camilius Membe is a Presidential material.

..inawezekana kwamba Mudhihir anatumiwa na mafisadi, lakini ktk hili la kumshughulikia Membe, nadhani mafisadi wanafanya jambo la mbolea kwa taifa letu.
 
Back
Top Bottom