Sungi
Senior Member
- Apr 29, 2009
- 149
- 47
Kuna tafrani ya kutupiana maneno kati ya mzee Mudhihiri na Membe kuhusu kujengwa kwa kiwanda cha saruji kilomita 35 kutoka eneo lenye malighafi ambalo ni Mchinga ambapo Mudhihiri ndio Mbunge.
Kitu ambacho kinanishangaza ni hili la kwamba Membe ana nia ya kugombea urais mwaka 2015 (ana haki kama mtanzania kufanya hivyo).
Alipoulizwa (Membe) iwapo anahisi matamshi ya Mudhihir yana msukumo wa maadui wake kisiasa ambao wanahisi anaweza kugombea urais 2015, Membe alisema kwa vyovyote itakuwa hivyo.
Hivi kuwa waziri wa mambo ya nje ndio ticket Tanzania kuwa rais?
(Source: Mwananchi Mwananchi Communications Ltd)
Kitu ambacho kinanishangaza ni hili la kwamba Membe ana nia ya kugombea urais mwaka 2015 (ana haki kama mtanzania kufanya hivyo).
Alipoulizwa (Membe) iwapo anahisi matamshi ya Mudhihir yana msukumo wa maadui wake kisiasa ambao wanahisi anaweza kugombea urais 2015, Membe alisema kwa vyovyote itakuwa hivyo.
Hivi kuwa waziri wa mambo ya nje ndio ticket Tanzania kuwa rais?
(Source: Mwananchi Mwananchi Communications Ltd)
Je anazo qualities zote za kiongozi? Ni zipi? Je ni kweli ana hasira? na itakuwaje watu ambao aliwakosea au walimkosea siku za nyuma? Maana mmoja kati ya sifa kuu za kiongozi ni kuwa mvumilivu ama sivyo itakuwa kila kukicha unanyonga watu.
Je wanaompinga wana mawazo gani kuhusu huyu mheshimiwa? Nazungumzia kuanzia akina Mudhihir mpaka waliopo madarakani juu.
Je tangu aingie Foreign kuna mabadiliko gani makubwa kashafanya?
Nauliza kwa sababu inaonekana kuwa kuna kila dalili anaweza kuwa rais wetu 2015 lakini je watanzania wategemee rais wa namna gani na presidency yake itakuwa ya namna gani?
Membe akiri kuwania urais 2015*Aelezwa kuiga mbinu alizotumia JK
*Kombora la Mudhihir lamshusha nguvu
*Aelezwa ni nyoka anayemaliza wenzake kwa rais
Na Mwandishi Wetu, Dodoma-UMMA Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Kimataia, Bernard Membe amekuwa ni kiongozi wa kwanza kukiri kuwa ana nia ya kuwania urais mwaka 2015 ikiwa ni siku chache baada ya Mbunge wa Mchinga, Mudhihir Mudhihir kumtaja kwa mafumbo bungni mjini hapa wiki hii.
Membe alinukuliwa na vyombo vya habari siku moja baada ya Mudhihir kisha kombora lilikuwa likimtaja Waziri mmoja anayetokea mkoa wa Lindi kuwa amekuwa mbinafsi na fisadi kutokana na tabia yake ya kutumia jina la rais Jakaya Kikwete kukwamisha ujenzi wa kiwanda cha saruji katika jimbo la Mudhihir.
Mudhihir ambaye inalezwa kabla ya kutoa kombora hilo aliwasiliana na wabunge wenzake kutoka Lindi, alifafanua kuwa ubinafsi wa waziri huyo ambaye sasa imefahamika wazi kuwa ni Membe, unalenga kumdhohofisha yeye kisiasa kwa kuwa tu, anaonekana kupingana na harakati za Membe kuwania urais mwaka 2015 kwa kutumia mbinu kama alizowahi kuzitumia rais Kikwete miaka zaidi ya kumi iliyopita.
Membe safari hii licha ya kukubali kuwa na nia ya urais anaelezea kuwa, alichokizungumza Mudhihir kinatokana na wabaya wake wasiomtakia mema katika harakati zake za kuutaka urais na kutumia wizara ambayo ilitumiwa na rais Kikwete kupata urais mwaka 2005.
‘Bila shaka, bila shaka. Mudhihir ninayemfahamu asingeweza kutoa matamshi ya aina ile, lakini nasema sihitaji kulumbana naye, namheshimu sana," alinukuliwa Membe na gazeti moja la kila siku, akifafanua kuhusu dhana ya Mudhihir kutumiwa na watu kumlipua.
Lakini kombora la Mudhihir linaelezwa kuwa kali kupita yote katika maisha ya kisiasa ya Membe. Maisha ya kisiasa ya Waziri huyu yanaelezwa kuwa yale ya kutumia migongo ya wengine kupandia na mara kadhaa waziri huyu ametazama wapi panaweza kumanyua na kuangusha kila anayedhani anaweza kuwa mwiba kwake.
Watu wengi waloongea na Gazeti hili wamekuwa wakijiuliza hao maadui wa Membe ni kina nani? Amewafanyia nini? Wana chuki gani dhidi yake? Na kwanini yeye ahusishwe na hili? Na ni kipi kilichomfanya ajibu juu ya hoja hii wakati kuna waziri mwingine anayetoka Lindi? Haya na mengine ni maswali ambayo membe anatakiwa kuwajibu watanzania ambao walistushwa na kauli iliyotolewa na Mudhihiri nay eye kuijibu.
Ni katika mbinu za aina hiyo, Waziri huyu anaeleza kumteka Rais Kikwete kwa kuwa ananufaika na kuwa naye katika ziara nyingi za ughaibuni, ziara zinazoelezwa hapa ndani kuwa haziendani na kunyanyua uchumi wananchi na badala yake kuliingiza taifa katika madeni ya siku zijazo.
Waziri Membe anatumia kigezo cha yeye kuwa Mkatoliki kama mtaji wa kisiasa na mbinu hii anaamini ndiyo itakayomnyanyua ili kushinda kiraisi katika uchaguzi ujao. Hata hivyo hivi karibuni inaelezwa kuwa, alijiiingiza katika mgogoro mkubwa na madhehebu ya Kikirstu, baada ya kujiingiza kutetea suala la Tanzania kujiunga na OIC na lile la kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi.
Kujiingiza kwa Membe katika mambo haya tata, kunatafsiriwa kulilenga kumfurahisha rais Kikwete kwa kuwa mambo hayo yameandikwa katika ilani ya uchaguzi na yanaonekana hayatatekelezwa kwa kuwa wakristo wana msimamo mkali.
Pia kuna dhana kuwa, kujiingiza kwa Membe katika mambo haya tata, kuna lengo la kusaka misaada hasa ya kifedha kwa mataifa yenye asili ya Kiarabu, ili kumsaidia katika kampeni zake za kuwania urais mwaka 2015, jambo ambalo yeyeamkuwa akilipinga.
Membe kwa siku za nyuma alikuwa miongoni mwa kundi la Mtandao, kundi linalofahamika katika kumuingiza madarakani rais Kikwete. Inaelezwa sasa baada ya kundi hilo kugawanyika, sasa hivi Membe ameungana na kundi jingine linalojumuisha viongozi wakubwa katika sehemu nyeti kama Bunge na pia wafanyabiashara ambao wara kadhaa wamekuwa akijiibua kama wasemaji wa watanzania.
Hata hivyo, kuna taarifa kuwa, waziri huyu amekuwa akijionesha kuwa ni shushushu wa Uasalama wa Taifa, mbinu anayoitumia kutanua mtandao wake ambao sasa unaonekana kuanza kupata ushindani hasa baada ya Mudhihir kuamua kwa makusudi kuulipua.
Wachunguzi wa mambo ya Kisiasa wamediriki kukubali kauli ya Mudhihiri kuwa Membe ni Nyoka aina ya MDIMU ambae sifa yake kubwa ni ubinafsi na roho mbaya, Membe itakumbukwa kuwa alihusika kwa kiasi kikubwa kumaliza wenzie hata wakati wa awamu ya Tatu aliwamaliza kina Hans Kitine, Malecela, kwa kutumia ushushu wake aliweza kumtokomeza swahiba wake wa Sasa Sitta asipate nafasi baada ya kushindwa 95 huko Urambo, alitumia uzandiki aloutaja Mudhihiri kufanikisha wenzie wanamtandao wasipate nafasi ktk awamu ya kwanza ya Mzee mkapa ambae alimstukia na Kumuondoa na kumpeleka nje ya Nchi.
Last edited: