Gottee
R I P
- Sep 7, 2008
- 174
- 1
Ndugu zangu, Watanzania wenzangu, hawa kina Maggid ni wengi sana kwa sasa. Wametapakaa kila kona. Ukifuatilia vyombo vya habari vilivyoripoti leo kuhusu ile 'TV Show' ya Dk Slaa unaweza kusikia kichefuchefu na hasa magazeti ya Habari Leo, Jambo Leo na lile la Uhuru. Ameibuka mtu mmoja anayeitwa Ngeleja kujaribu kujibu hoja za Dk Slaa zinazohusu madini. Msomaji wa Magazeti pale TBC Taifa yeye ndiye alienda mbali kwa kusema, "Gazeti la Mtanzania Daima limeandika Slaa aumbuliwa" Sina uhakika kama upotoshaji huu ulikuwa wa makusudi au 'ukanjanja' wa mtangazaji huyo maana toka nizaliwe sijawahi kuliona gazeti la Mtanzania Daima.
Kuhusu Maggid, kama mtakuwa mmefuatilia tangu wiki iliyopita alianza kumtajataja Profesa Lipumba. Kwenye makala yake katika gazeti la Raia Mwema aliandika 'Mbio za Urais: Lipumba anakuja, chupa ya maji mkononi!' Aliandika mengi lakini akionyesha kuwa Watanzania wamemsahau Lipumba na kujikita zaidi kwa wagombea wengine, humo ndani akimpa 'misifa' Prof Lipumba. Maggid anacheza na akili za watu kujifanya yeye si mshabiki wa CCM. Nadhani lengo lake ni kuwa wale ambao hawataki kusikia 'madudu' ya Meneja Miradi wa CCM ambaye pia ni mgombea Urais kupitia chama hicho wamwone mbadala wake ni Profesa Lipumba na kwa kuwa huyu mgombea wa CUF sio 'dili' zaidi ya kupunguza kura za Slaa kutoka kwa wapinzani.
Kwenye Blogu yake Maggid ameshaandika mkataba wake wa kazi anayofanya sasa unaisha mwezi wa 12 mwaka huu. Maggid hata kama unafukuzia 'u DC' ndugu yangu macho yako yawe na aibu! Kuna faida gani kushusha Integrity na credibility yako kwa vivyeo vya 'kipuuzi' Maggid inaonekana Makala hii ya mdahalo wa Slaa ulishaiandika kabla hata Slaa hajaongea na kibaya zaidi hukufuatilia hata ule mjadala kwenye TV. Laiti kama ungefuatilia nina imani usinge post hiyo 'Makala Uchwara' yako. Kinachoendelea hivi sasa ni wewe kung'ang'ania kuwa ule haukuwa mdahalo na unachotaka watu wajadili kuwa ule ulikuwa mdahalo au la! Na kwa hakika umefanikiwa kwa sababu humu ndani tumeacha kujadili mambo ya muhimu aliyoyaongea Dk Slaa juzi.
Maggid kwa kuacha kumsikiliza Dk Slaa umepitwa mengi ikiwemo majibu ya yale maswali aliyoiliza yule 'mpuuzi' kwenye Blogu yako kuhusu Makaratasi Feki ya Kura kule Tunduma. Dk Slaa alijibu kwa ufasaha. Maggid nani asiyejua sasa hivi kuna mbinu chafu zimekuwa zikifanywa ili kuzuia yale anayoyasema DK Slaa kwenye mikutano yake yasiripotiwe?.
Maggid wewe endelea na ushabiki wako kwa CCM lakini ungewaonea huruma wale ndugu zako wa kule Kinyeregete. Ambao umekuwa ukitoa picha zao mara kwa mara kwenye Blogu yako wakiwa wamevaa 'masempele' na vile vijumba vyao ambavyo unajiuliza ni mabanda ya kuku au ni mapango ya kufugia ndezi. Wale wanao machotara uliowapeleka kule Kinyeregete huwezi kuniambia maswali waliyokuuliza lakini nadhani waliona kama vile wako 'Mikumi' ya wanyama wanaoitwa Binadamu! Picha zako zote za kule Kinyeregete sijawahi kuona nyumba yako au hata ya baba yako zaidi ya zile za wale unawaita shangazi zako, wajomba zako. Niambie mara ya mwisho ulimaliza usiku mzima pale Kinyeregete lini kama sio kupita dakika moja na kuwaachia ndoo za vitunguu na nyanya zile unazotuonyesha kila siku! Acha bana! Halafu najiuliza huku kwa JK umekuja lini? Najua mwaka 1995 ulikuwa wapi na mgombea wako unakumbuka alivyochafuliwa jina na hawa 'wahuni' Jamani!
Maggid wanao wanasoma International School na huenda hata maisha yao ya baadaye yanaweza yasiwe pale Kinyeregete au hata Kinondoni Biafra. Sasa mwache Slaa aje asomeshe watoto wa Kinyeregete bure na kuangalia afya zao bure, sio kuwapiga picha na vitambi vyao huku wakiwa na umri mdogo wa miaka sita na kwenda kuziuza Sweden. Acha bana!