Mdahalo ITV Bila Profesa Lipumba Na Wengine, Kwanini?

Miye nilishamshtukia siku nyingiiiii kwamba fani ya uandishi si fani yake kakurupuka na kuivamia tu lakini hana uwezo nayo kabisa maana huishia kujikanyagakanyaga tu na msomaji kushindwa kabisa kuelewa alikuwa anataka kusema nini.

Kuna kipindi aliandika makala kuwalaumu TTCL na gharama za mtandao, yes gharama za mtandao ziko juu Tz, lakini upupu na uwongo alioandika, ningekuwa mwanasheria wa TTCL ningepeleka hii kitu mahakamani mara moja.
 
Kaka huu haukuwa mdahalo, mbona hufuatilii habari, ushaambiwa kina lipumba watahojiwa vilevile na mkwere akikubali? Ni mahojiano tu wala si mdahalo!
 
Rufiji,
Hakuna anayelazimishwa kujadili. Ukiwaona wenzako wanajadili, basi, ujue wanalojadili lina umuhimu kwao. Ndio maana na wewe umetumia muda wako kuingia humu na kuchangia mawazo yako.
Hili la kuwekana sawa juu ya dhana ya mahojiano/mazungumzo na mdahalo lina umuhimu. Tusifike mahali hata mikutano ya ndani ya vyama nayo ikaitwa midahalo. Ni pale anayehojiwa anaingia studio na wapambe wake wakiwa na bendera na matarumbeta. Watamshangilia kila anapomaliza sentesi moja. Nadhani tukisoma mawazo ya wengine na kuwa na utayari wa kuelewa, basi, tumeshaelewa, kuwa wa jana haukuwa mdahalo kwa maana ya mdahalo tunaouelewa wengi wetu. Na haina maana ya kudharau kilichoongewa na Dr Slaa kwenye mahojiano/mazungumzo yale na mwendesha kipindi ambaye jana alitambulishwa kama ' Mwenyekiti wa Mdahalo'.

I dont care which name you give to that TV Show last night, i have to say Dr. Slaa proved to as many Tanzanians that he is a true leader. Watu walikuwa wanashangilia as if it was a football match. Sababu kubwa ni kuwa watanzania for a long time hawajakutana na kiongozi mwenye charisma yenye mfano wa Dr. Slaa.

I think now Tanzania tunaweza kujivuna kwamba tunaenda kumpata kiongozi bora na si bora kiongozi the likes of Jakaya Mrisho Kikwete.

No wonder Kikwete will never agree to stand with Dr. Slaa kwenye mdahalo and i support him for that decision.
 
Kuna kipindi aliandika makala kuwalaumu TTCL na gharama za mtandao, yes gharama za mtandao ziko juu Tz, lakini upupu na uwongo alioandika, ningekuwa mwanasheria wa TTCL ningepeleka hii kitu mahakamani mara moja.
sasa wewe ndio unachangia kudumaza maendeleo, mbona hujatuambia wanasheria wa ttcl...

huwa sisom makala zake hadi ziwe JF, ni mchemfu, kwani alisema nin?
 
quoted as a fair user

once you marriage get a crap out of you... the rest follow suit

no harm intended
 
Bwana Maligwa,
Umenena, na nashukuru umenielewa. Naamini waandaaji hawajachelewa kutukusanyia wagombea Urais zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja kwenye mdahalo halisia. Katika wakati huu ni vema tukawekana sawa juu ya nini maana ya mdahalo, mahojiano na mazungumzo. Narudia, tulichokiona jana si mdahalo kwa maana ya mdahalo tunayoifahamu wengi. Yawezekana mahojiano au PR tu, kutangaza sera za chama husika. Binafsi sina tatizo na ujumbe alioutoa Dr Slaa, isipokuwa, ingekuwa na maana zaidi kama angekutanishwa na hoja kinzani kutoka kwa wagombea wengine. Isifike mahali, hii tunayoiiita sasa midahalo ikawa ni midahalo inayotokana na mikutano ya ndani ya vyama- Pale ambapo, mgombea anakutana na tabasamu za wapambe na washabiki wa chama chake wakiwa wameshika bendera na hata matarumbeta. Watamshangilia kila anapomaliza sentesi. Inahusu mambo muhimu kwa taifa letu. Kama Lipumba atahojiwa Ijumaa akiwa peke yake, basi, set up ya mahojiano irekebishwe, na usiitwe mdahalo. Ni mtazamo wangu tu.

kumbe hoja yako unataka kuthibitisha kwamba waliokuwa wanamshangilia ni wanachadema nataka kukufahamisha kwamba mimi nilikuwepo na ni mwanachama wa CCM MFU na wengine wengi mambo ya kitaifa Maggid usiwe unayeletea mzaha kwa kisingizio cha uchambuzi wa masuala nimegundua wewe ni mtu mwenye dharau sana kwa mambo usioyaamini na huo ndio ujinga wako wa maisha
 
Kwenye video clip, inasema Kipindi Maalumu : Ana kwa Ana na mgombea Urais Chadema wala haisemi Mdahalo wa wagombea Urais........hivyo tusipotoshane kusema mbona wengine hawapo maana huu ulikuwa mahsusi kwa Mgombea wa Chadema.
 
I dont care which name you give to that TV Show last night, i have to say Dr. Slaa proved to as many Tanzanians that he is a true leader. Watu walikuwa wanashangilia as if it was a football match. Sababu kubwa ni kuwa watanzania for a long time hawajakutana na kiongozi mwenye charisma yenye mfano wa Dr. Slaa.

I think now Tanzania tunaweza kujivuna kwamba tunaenda kumpata kiongozi bora na si bora kiongozi the likes of Jakaya Mrisho Kikwete.

No wonder Kikwete will never agree to stand with Dr. Slaa kwenye mdahalo and i support him for that decision.
Kutokuwepo kwa Kikwete ni statement kubwa kuhusu rais wetu. Umebakiza siku nane tu za kampeni na wewe na wabunge wa chama chako mnakataa mdahalo - yaani mbinu thabiti wa kisasa kutimiza kusudi la msingi la zoezi la Uchaguzi?!?

This was, of course, to be expected, maana ingekuwa political suicide: ni kitu rahisi kuhotubia wakulima na wasio na mazoea ya kusoma huko majimboni, na suala lingine kuulizwa maswali na watanzania wenye muamko, wenye kutazama kwa macho ya kupambanua matendo yako na kukumbuka yaliyopita. Mdahalo kati ya Slaa na JK may have turned into one of TZ's most memorable TV incidents (kama vile Kanumba's classic Big Brother Blooper ya ku"close" ["kufunga"]), ndio maana haikutokea, na haitatokea. Voter base wa JK ni the poor and ignorant (wajinga ndio waliwao - as usual) for whom his speeches are tailored.

Ninamsifu Dr. Slaa kwa kuwa mwenye msimamo hadi kuweza kutingisha wale waliojiona untouchable. Money, not even US$ 1.5 million worth of CCM posters from Canadian capitalist brothers can buy you everything - especially not the trust of your people! Well, ngoja nisiwe too strict: most gov'ts are not to be trusted, so ours is no exception, uongo?

Dr. Slaa: rest assured: he/they may have feared nothing in his life more than you, and maybe the God of the Heavens to Whom all leaders and kings belong and Who sets up kingdoms and tears them down just as He pleases may bless the goodwill of TZ people!
 
Kwenye video clip, inasema Kipindi Maalumu : Ana kwa Ana na mgombea Urais Chadema wala haisemi Mdahalo wa wagombea Urais........hivyo tusipotoshane kusema mbona wengine hawapo maana huu ulikuwa mahsusi kwa Mgombea wa Chadema.

Hata mimi nilijua kuwa kile kilikuwa ni kipindi maalum akama ambavyo kuna vipindi vingine vya Kiti moto na vitu vya namna hiyo. Nimesikia kuwa baada ya kumhoji silaha, Ijumaa au Jumamosi ijayo kuna mgombea mwingine atakeyojiwa kati kiwete na lpumba
 
Njilembera na Wengine,

Nimechokoza mjadala huu kwa nia njema kabisa. Tuwekane sawa, kwamba kuna tofauti ya embe na chungwa, kwa mwonekano na ladha pia. Kilichokuwa kikitangazwa kabla ya jana ni " Mdahalo". Tulichokiona si mdahalo, na sisi ni watu wazima. Wasije wajukuu zetu wakaja kutushangaa watakaposoma historia. Watahoji upeo wetu wa kufikiri . Kinachoonekana hapa ni ukweli, kuwa wa jana haukuwa mdahalo. Swali linabaki, jana tuliona nini? Mazungumzo, mahojiano au PR? Hivi set up ya mahojiano inatakiwa iweje ili yaitwe mahojiano? Na kwanini aliyeendesha shughuli ile alitambulishwa kama ' Mwenyekiti wa Mdahalo?". Hebu 'Great Thinkers ' tuumize vichwa tuweke hili sawa.

Q/A Full stop! Hio ndio tulikuwa tunataka tumwone laivu anavyojibu maswali papo kwa papo. Suala la mdahalo, mahojiano, et al. ukawaulize waliogoma kushiriki toka mwanzo mpaka wakavuruga utaratibu. Samahani.
 
Hata mimi nilijua kuwa kile kilikuwa ni kipindi maalum akama ambavyo kuna vipindi vingine vya Kiti moto na vitu vya namna hiyo. Nimesikia kuwa baada ya kumhoji silaha, Ijumaa au Jumamosi ijayo kuna mgombea mwingine atakeyojiwa kati kiwete na lpumba

Kichuguu,
Kumbe, ilikuwa ni ' Kipindi Maalum'! Jumamosi asubuhi niliona tangazo kwenye ITV, kuwa kungekuwa na ' Mdahalo' wa Dr Slaa utakaongozwa na Jenerali Ulimwengu na Rosemary Mwakitwange. Ilipofika saa moja usiku nilikuwa mbele ya tv. Nilichokiona ndicho hicho nilichokianzishia mjadala. Haukuwa mdahalo kwa maana ya mdahalo.
 
Maggid, unaonaje sasa tuzinguzumzia kilichonenwa humo katika hayo 'mahojiano' ambayo kikwete amekataa kuhudhiria na kusababishwa usiuite mdahalo. Hivi katika mantiki ya kawaida kwa kipindi hiki, mpenda maendeleo unataka kujua kuwa ule ni mdahalo au la? Yaani fikra zako ndo ziishie hapo kweli? Kwanini sasa usianze kuzungumzia kilichosemwa?

Wkati mwengine nafika wakati wa kuamini kuwa ukileta hoja humu, zingine wala hazina interest ya taifa kwa sasa then ili mradi watu wakae wachambuane tuuuu. Hivi sasa tunajadili kama ule ulikuwa mdahao au la? C'mon u people
 
kumbe hoja yako unataka kuthibitisha kwamba waliokuwa wanamshangilia ni wanachadema nataka kukufahamisha kwamba mimi nilikuwepo na ni mwanachama wa CCM MFU na wengine wengi mambo ya kitaifa Maggid usiwe unayeletea mzaha kwa kisingizio cha uchambuzi wa masuala nimegundua wewe ni mtu mwenye dharau sana kwa mambo usioyaamini na huo ndio ujinga wako wa maisha

Froida,
Umeniita mjinga, hewallah! Iweje wewe mwerevu unajiita mwanachama wa CCM Mfu badala ya kwenda CHADEMA ukashangilie ukiwa mwanachama wa CHADEMA Hai? Kipi kinachokufanya uendelee kusubiri ukiwa mfu ndani ya CCM?
 
Kichuguu,
Kumbe, ilikuwa ni ' Kipindi Maalum'! Jumamosi asubuhi niliona tangazo kwenye ITV, kuwa kungekuwa na ' Mdahalo' wa Dr Slaa utakaongozwa na Jenerali Ulimwengu na Rosemary Mwakitwange. Ilipofika saa moja usiku nilikuwa mbele ya tv. Nilichokiona ndicho hicho nilichokianzishia mjadala. Haukuwa mdahalo kwa maana ya mdahalo.

Kama kweli ulikuwa unaangalia kipindi hicho, hutakuwa umekosa kuona image ya aina hii :

attachment.php

kipindimaalum.JPG
 
Hata mimi nilijua kuwa kile kilikuwa ni kipindi maalum akama ambavyo kuna vipindi vingine vya Kiti moto na vitu vya namna hiyo. Nimesikia kuwa baada ya kumhoji silaha, Ijumaa au Jumamosi ijayo kuna mgombea mwingine atakeyojiwa kati kiwete na lpumba

Badilika kaka acha kuandika ujinga
 
Ni Wapi tunapoelekea?Tujifunze kukubali au kutokubali mitazamo tofauti kwa Hoja.Haiyumkiniki wanadaamu wote kuwa na uwezo sawa wa kufikiri au kutoa hoja zinazoshahabiana.Dharau,Kejeli,Matusi si ungwana.
 
Non sense!! Maggid usifanye maisha yako kuwa magumu. Take note, jukwaa hili si pahala pa watu wa kushikiwa akili. Find out kwanini hao unaowataka hawakushiriki kisha urudi hapa jukwaani ukiwa umejiandaa na hoja za msingi. Mambo ya kukariri inakuwa shida tupu ktk real life. Unataka kujadili na nani kuhusu maana ya mdahalo? Kajielimishe kwanza wewe kisha utajua kuwa mahojiano ni sehemu ya mdahalo. Nikukumbushe pia kuwa thread hii inazungumzia uchaguzi 2010.

This says a lot about Wanademokrasia wetu.......
 
Kama kweli ulikuwa unaangalia kipindi hicho, hutakuwa umekosa kuona image ya aina hii :

Kichuguu,

Nimeandika, kuwa ITV Jumamosi asubuhi ilirusha tangazo kuwa jioni hiyo kungekuwa na ' mdahalo' wa Dr Slaa utakaoongozwa na Jenerali Ulimwengu na Rosemary Mwakitwange. Na umakini uanzie kwa waandaaji kuweka wazi ni kitu gani wametuandalia. Mpaka magazeti na TV yanapotoa matangazo ina maana waandaaji wanajua nini umma umetangaziwa, kama hilo hawakuwa na taarifa nalo ni tatizo kubwa. Nadhani, baada ya mkanganyiko wote huu, wahusika walipaswa kiungwana kutuomba radhi tulioletewa taarifa zisizo sahihi na kutuambia nini kilicho sahihi maana bado kuna wanaodhani walichoona ni mdahalo. Na gazeti la Tanzania Daima siku moja kabla Ijumaa Oktoba 22 liliripoti kama ifuatavyo;
Mdahalo wa urais kesho

na Mwandishi wetu

amka2.gif
TAASISI ya East Africa Business and Media Training Institute kwa kushirikiana na Vox Media Centre imeandaa mdahalo wa mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.
Mkurugenzi wa Vox Media, Juvenalis Ngowi, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa mdahalo huo utafanyika kesho kuanzia saa 12 jioni na kurushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV.
Alisema mdahalo huo utafanyika katika Hoteli ya Movenpic na wananchi wataweza kuuliza mashwali moja kwa moja.
Ngowi alieleza kuwa mdahalo huo unatarajiwa kuhudhuriwa na watu 200.
Wagombea urais kwa Tanzania Bara mbali na Dk. Slaa ni Jakaya Kikwete (CCM), Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Peter Mziray (APPT-Maendeleo), Fahmi Dovutwa (UPDP), Mugahywa Muttamwega (TLP) na Hashimu Rungwe (NCCR - Mageuzi).
Huu ni mdahalo kwa pili kuandaliwa na Vox, baada ya ule wa kwanza kufanyika mwanzoni mwa mwaka huu visiwani Zanzibar ambao uliwakutanisha wagombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.
 
Bwana Maligwa,
Umenena, na nashukuru umenielewa. Naamini waandaaji hawajachelewa kutukusanyia wagombea Urais zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja kwenye mdahalo halisia. Katika wakati huu ni vema tukawekana sawa juu ya nini maana ya mdahalo, mahojiano na mazungumzo. Narudia, tulichokiona jana si mdahalo kwa maana ya mdahalo tunayoifahamu wengi. Yawezekana mahojiano au PR tu, kutangaza sera za chama husika. Binafsi sina tatizo na ujumbe alioutoa Dr Slaa, isipokuwa, ingekuwa na maana zaidi kama angekutanishwa na hoja kinzani kutoka kwa wagombea wengine. Isifike mahali, hii tunayoiiita sasa midahalo ikawa ni midahalo inayotokana na mikutano ya ndani ya vyama- Pale ambapo, mgombea anakutana na tabasamu za wapambe na washabiki wa chama chake wakiwa wameshika bendera na hata matarumbeta. Watamshangilia kila anapomaliza sentesi. Inahusu mambo muhimu kwa taifa letu. Kama Lipumba atahojiwa Ijumaa akiwa peke yake, basi, set up ya mahojiano irekebishwe, na usiitwe mdahalo. Ni mtazamo wangu tu.

Maggid ngoja nikusaidie.....

Mdahalo ule uliandaliwa na VOIX Media wakishirikiana na TCMB na kufadhiliwa na Civil Society Foundation...

Nakupa zoezi utafute who is VOIX Media....
 
Na gazeti la Tanzania Daima siku moja kabla Ijumaa Oktoba 22 liliripoti kama ifuatavyo;

Mdahalo wa urais kesho

na Mwandishi wetu

amka2.gif
TAASISI ya East Africa Business and Media Training Institute kwa kushirikiana na Vox Media Centre imeandaa mdahalo wa mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.
Mkurugenzi wa Vox Media, Juvenalis Ngowi, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa mdahalo huo utafanyika kesho kuanzia saa 12 jioni na kurushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV.
Alisema mdahalo huo utafanyika katika Hoteli ya Movenpic na wananchi wataweza kuuliza mashwali moja kwa moja. Ngowi alieleza kuwa mdahalo huo unatarajiwa kuhudhuriwa na watu 200.
Wagombea urais kwa Tanzania Bara mbali na Dk. Slaa ni Jakaya Kikwete (CCM), Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), Peter Mziray (APPT-Maendeleo), Fahmi Dovutwa (UPDP), Mugahywa Muttamwega (TLP) na Hashimu Rungwe (NCCR - Mageuzi).
Huu ni mdahalo kwa pili kuandaliwa na Vox, baada ya ule wa kwanza kufanyika mwanzoni mwa mwaka huu visiwani Zanzibar ambao uliwakutanisha wagombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.

.......................
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom