Mdahalo ITV Bila Profesa Lipumba Na Wengine, Kwanini?

Basi bongo hakuna waandishi,huyu Maggid mimi simujui vizuri ,ila kama mnamwita muandishi wa habari hamna kitu hapo.

Unakurupukaje kuja kuandika huo upupu ,kipindi wanakiita kipindi maalum,mahijiano ya ana kwa ana na mgombea wa urais chadema
Slaa.
Wewe unadai " ndugu zangu tumesikiliza" kumbe ww hajasikiliza nadhani moa kwa moja kungesikiliza na kuonga usingeleta huo upupu ,unaonekana unatumwa tu la kusema na kabla ya kuandika ukiwa kama mwanahabari ulitakiwa kufanyia utafiti unachoandika sio kuja na excuse za tanzania daima walisema hili wakati shutuma zako unazipeleka kwa waandaaji.
 
Bwana mdogo Maggid Heshima Mbele,

Nashukuru sana kwa jitihada zako za kupotosha ujumbe ulio tolewa na Dr Slaa kwa mtindo wa kujiuliza maswali kwamba mahojiano yalikuwa ni Mdahalo au kitu gani.!!?

Kwa kutumia Busara ya Mtanzania wa kawaida, pia kwa kutumia mtindo wako wa kawaida wa kuhoji ujumbe na maneno yasemwayo na wana siasa,bila kujadili wametumia usafiri gani kufika pale au nani kafika pale kuwasikiliza, nilitegemea ungeuliza swali la ule ulikuwa ni Mdahalo au la kisha ukajadili majibu yote ya Dr Slaa kwa mtizamo wako utokanao na , imani yako kwa nchi yako, upeo wako wa kielimu na zaidi hali halizi ya Tanzania.
Kifupi umeamua kupindisha somo zima na lengo zima la kipindi cha ITV kwa kutoa uzito mkubwa katika jambo dog,setup, na kuyapa kisogo maelezo ya Dr Slaa.
Maggid! Umeshindwa hata kudodosa kiduchu tu kile alicho kisema Dr Slaa umebaki kulalama na Mdahalo Mdahalo tu.
Hata katika Mdahalo watu hujibu maswali.
Katika mahojiano ya ITV Dr Slaa hakujibu swali lolote kwa niaba ya chama chochote kile kikiwemo chama tawala. Dr Slaa alijibu Maswali kuhusu chama chake kwa Umahiri mkubwa sana. Yote hayo MH umeona ni bure kabisa na ni upuuzi kiasi cha kujenga hoja yako kwenye mdahalo kuliko kile Watanzania wengi walichokisubiri kwa hamu yaani Majibu ya Dr Slaa na ufafanuzi wa sela za chama chake.

Wewe umeishi Sweden Miaka mingi na hata mama watoto wako ni mzaliwa wa huko.
Sweden ni nchi ya ulimwengu wa kwanza na wengi waishio huko kutoka Dunia za Tatu kama Tanzania angalau baada ya kukaa huko kwa Muda hujipangusa Matongotongo ya dunia ya tatu na kuanza kijibidisha kujifunza hali halisi ya kidunia na hasa dunia ya kwanza.

Huwezi kuandika hapa kana kwamba majiji makubwa ulowahitembelea ni Lujewa huko Mbaralali na Mbeya,pia shule kubwa ulo wahi kusoma ni Sangu Sec?

Kuna maswali kadhaa umeuliza, Maswali hayo ingefaa uwaulize ITV na pengine kabla ya kuuliza maswali hayo ingefaa uwasiliane na wasemaji wa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi kwa ngazi ya urais wakupe ukweli wa vipi wagombea wao hawakutinga kwenye uwanja wa mbigili mwitu??

Mwandishi wa Makala kama wewe ni vema ufanye uchunguzi wa kina kabla ya kuandika makala yeyote.

Maggid Soma alama za nyakati, si muda mrefu ujao hatutaandika habari za kujikomba kwa mtu yeyote awe mkuu wa Wilaya ,IGP,CDF au Rais wa nchi mwenyewe. Kazi kubwa ya muandishi yeyote wa habari itakuwa ni kupeleka ujumbe kwa usahihi wote kupitia chombo chake cha habari na kutoa maoni yake kadri ya ufahamu na uelewa wake bila kuwa biased. Zaidi kila mwandishi atwajibika kwa asilimia miamoja juu ya kile alichokiandika kama ilivyodunia ya kwanza.

Sasa ninakushauri kama kweli una nia nzuri na uzalendo wa kweli wa kuona Tanzania ikianza kuchanja mbuga katika nyanja zote kiasi kwamba nawe una njozi kwamba siku moja nasi Tuwe na uwezo wa kujenga viwanda, vyuo vikuu barabara na hospitali kama zila za Sweden jadili,bila woga wala upendeleo, majibu ya Dr Slaa katika mahojiano ya jumamosi!! Vinginevyo sitakutofautisha wewe na waliopokea zawadi za Khanga,fulana na kofia kwa dhiki au woga wa kuogopa vivuli vyao na kudhani wanafaidi matunda ya Uhuru na maendeleo ya nchi.
 
Maggid!!

Najua na ninaamini hizi habari za huu mdahalo ulishaziona hapa JF siku nne kabla.

Set up yake ilijulikana Tangu Mwanzo, Kwanini hukukosoa Set up yake kabla ya Mdahalo wenyewe.

Umekosa La kukukosoa Katika yale aliyoyaongea Slaa ukaamua Kukosoa Set up ya ule mdahalo.

But nashukuru Nimejua wewe ni m2 wa aina Gani. Hongera sana, nimeona kule kwenye Kablogu kako kuwa jana Kikwete alikupungia mkono Pale Mikumi. I really dont think wheather this is such an important information.

Safi sana kaka kumbe umegundua kuwa jamaa ni cheap journalist. Eti kapungiwa mkono na raisi.. sasa si anatafuta kula.. so cheap.
 
Maggid,

Good observation! Ki-ukweli kuita kile kilichofanyika jana mdahalo ni misnomer - haukuwa mdahalo. Sifahamu sababu za lipumba kutokuwepo lakini hata kama angekuwepo value added isingekuwa worth the effort. Iko wazi kuwa mpambano wa uraisi sasa umebaki kuwa wa watu wawili Dr. Slaa na Raisi Kikwete na kwa kuwa kikwete kapigwa marufuku na makamba kushiriki midahalo hakukuwa na uwezekano wa kumpata so waandaaji wakaamua kufanya walichokifanya. Unaweza ukawa unaamini kuwa Kina Dovutwa na mzee Rungwe pia walitakiwa washirikishwe, I beg to differ. Mimi naamini ubora wa mdahalo unapimwa na uwezo wake wa ku-influence outcome ya election na sio idadi ya washiriki. Nimalizie kwa kusisitiza kuwa mdahalo ambao utaamua mshindi wa uraisi ungekuwa kati ya kikwete na slaa; we both know that that debate will never be held!!!!

Asante.
denis_79tz.

Nakubalina nawe ndugu yangu 100%. Kama kweli Maggid angekuwa na dukuduku hilo angelitoa siku ya kwanza kampeni zilipo anza, lakini si sasa. Hata huku kwenye nchi zilizoendelea si kila mgombea Uraisi eti ana thamani sawa na mwingine linapokuja kwenye suala la debate kwenye national TV audience.
Network zinalipiwa mamillion ya fedha sasa kwa nini ulete mtu ambaye amesha onyesha utayari wa kushindwa.Uchaguzi huu mpka dakika ya sasa ni Kikwete na Dr Slaa tu. Wanaofanya majaribio waendelee kwa wakati wao.
 
Maggid ngoja nikusaidie.....

Mdahalo ule uliandaliwa na VOIX Media wakishirikiana na TCMB na kufadhiliwa na Civil Society Foundation...

Nakupa zoezi utafute who is VOIX Media....

Omar,
Ahsante sana. Utafiti mdogo niliofanya umenipa matokeo haya yanayotutaka tufikiri kwa bidii. Chini hapa ni habari katika Tanzania Daima ya Jumapili, Julai 4, 2010;

Nahodha akacha mdahalo Z'bar
• Wagombea kumi kuwekwa kiti moto leo

na Shabani Matutu

amka2.gif
WAKATI taasisi huru ya habari nchini ya Vox Media Centre Ltd imeandaa mdahalo kwa wagombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, amekacha mdahalo huo.
Nahodha ambaye ni mmoja wa wagombea hao 11, wanaowania uteuzi wa nafasi hiyo, amekacha mdahalo huo wa kwanza kufanyika visiwani Zanzibar tangu kuanza kwa harakati za kuwania urais, kwa madai ya kutingwa na shughuli za Baraza la Wawakilishi.
Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari jana, Nahodha alifafanua kuwa hatoweza kuhudhuria mdahalo huo kutokana na kuendelea kwa shughuli za Baraza la Wawakilishi visiwani Zanzibar.
Taarifa hiyo iliyosainiwa kwa niaba yake na Kaimu Katibu wa Waziri Kiongozi, Mohamed Muombwa, ilisema kuwa Nahodha anaungana na taasisi hiyo kimawazo katika kufanikisha mdahalo huo na yuko tayari kushiriki wakati wowote mwingine.
"Mheshimiwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar amepokea kwa furaha mwaliko wako kushiriki katika mdahalo wa wagombea urais Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi. Hata hivyo kutokana na kuendelea kwa shughuli za Baraza la Wawakilishi hivi sasa, tunasikitika kukuarifu kuwa hataweza kuhudhuria," ilisema taarifa hiyo.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Vox Media Centre Ltd, Ansbert Ngurumo, alisema wanaendelea na maandalizi ya mdahalo huo kama ulivyopangwa.
Hata hivyo inawezekana waziri kiongozi huyo hakutaka kuhudhuria mdahalo huo kwa sababu za kisiasa, kwani unafanyika leo, ambapo hakuna shughuli zozote za Baraza la Wawakilishi visiwani humo.
Mdahalo huo utakaorushwa hewani na kituo cha televisheni cha Star TV, ulipangwa kuwashirikisha wagombea 11 wanaoomba uteuzi wa kuwania kiti cha urais Visiwani Zanzibar, kinachoshikiliwa na Rais Amani Abeid Karume.
Kwa mujibu wa Ngurumo, mdahalo huo unatarajiwa kufanyika leo, katika Hoteli ya Ocean View Hotel, Zanzibar kuanzia saa 3:30 asubuhi hadi saa 7:00 mchana.
Alisema mdahalo huo utarekodiwa kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 7 mchana na unatarajiwa kurushwa na kituo cha Star Tv mwanzoni mwa wiki ijayo katika siku itakayotangazwa baadaye.
Lengo la mdahalo huo ni kuwapatia fursa wagombea hao kujieleza mbele ya wanahabari na umma utakaohudhuria, na utakaotazama kipindi hicho kwenye televisheni ili kuwawezesha wananchi kuwajua wagombea ikiwa ni pamoja na kuwapima nia na uwezo wao kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Mdahalo huo unafanyika wakati ambapo CCM inaelekea kufanya vikao vya mwisho vya uteuzi, siku moja baada ya Kamati Kuu Maalumu ya chama hicho kufanya kikao cha kupendekeza majina kwenye Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM vitakavyofanyika mjini Dodoma, wiki ijayo.
Wagombea hawa wataulizwa maswali kuhusu masuala yote muhimu ya siasa, uchumi na ya utawala Zanzibar, na itakuwa fursa adhimu kwao kuwashawishi wanachama na viongozi wenzao kuhusu maono yao katika nchi hiyo.
Mbali ya Nahodha ambaye hatashiriki, wagombea waliothibitisha kushiriki ni pamoja na Waziri Kiongozi mstaafu, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein, Balozi Ali Karume, Ali Juma Shamuhuna, Hamad Mshindo, Haruna Suleiman, Mohammed Yusuf Mshamba, Omar Sheha Mussa na Mohammed Aboud.
 
Ndugu Zangu,
Jana tumesikiliza mdahalo, au labda mazungumzo au mahojiano kati ya Dr Slaa ( CHADEMA) na Rosemary Mwakitwange. Mahojiano yaliyoruhusu wengine kuchangia kwa njia ya simu pia.
Tunawapongeza walioshiriki kufanya jitihada zile. Ilitoa fursa kwa sisi wapiga kura kumsikiliza Dr Slaa. Hata hivyo, pungufu kubwa kabisa lililoonekana ni namna waandaaji walivyoandaa mdahalo wa upande mmoja bila kuwashirikisha wagombea wengine wa Urais waliopitishwa na NEC. Maana, ni vema pia tukatofautisha maana ya mdahalo na mahojiano. Kama yale ya jana yalikuwa ni mahojiano tu, hakuna tatizo kwa mgombea mmoja tu kuhojiwa. Lakini kama unaitwa mdahalo, basi, tujadili maana ya mdahalo.

Kama ni mdahalo, basi, ingekuwa ni vema na busara kwa wagombea wengine wa Urais kushiriki. Bila shaka, wagombea wengine nao wana haki za msingi za kupewa nafasi ya kuelezea sera zao na kujibu maswali ya wapiga kura. Hata kama chama tawala, CCM kimeweka wazi kuwa mgombea wao hatashiriki mdahalo, lakini hatujasikia vyama vingine vitoa misimamo kama hiyo.

Wengi wetu tungependa kuona wagombea wengine wa Urais nao wakialikwa, hivyo basi, kupewa fursa ya kuelezea sera za vyama vyao na kuulizwa maswali. Kungetoa fursa ya wagombea hao kushindana kwa hoja pia. Labda kama kuna maelezo ya kuwa wagombea hao walialikwa lakini hawakuitikia mwaliko wa kwenda studioni. Au kuwa gharama za muda wa kurusha hewani mdahalo ziligharamiwa na chama cha mgombea aliyefika kwenye mdahalo/mahojiano. Kama sivyo, basi, waandaaji watakuwa hawakuwatendea haki wagombea na wapiga kura kwa ujumla wao.

Maana, tukianza sasa kujenga tabia ya kubagua wagombea itakuwa ni jambo la hatari sana. Ikumbukwe, tangu Uchaguzi Mkuu wa 1995, tulianza kujenga misingi mizuri ya wagombea kupewa fursa sawa. Kwenye uchaguzi wa mwaka 1995 wagombea wote wa Urais walialikwa kwenye mdahalo uliofanyika kwenye iliyokuwa Kilimanjaro Hotel. Kama inavyoonekana pichani, kulikuwa na Profesa Lipumba, Augustino Mrema, Benjamin Mkapa na Bwana Cheyo. Historia ni mwalimu mzuri. Tujifunze.

Maggid,
Iringa, Jumapili, Oktoba, 24, 2010

Jambo la msingi ni kupata ujumbe. Kama wewe ulitaka wengine wawepo itisha na wewe mdahalo basi!
 
maggid hadi leo hujui maana ya mdahalo, mdahalo unaweza kufanyika baina ya pande mbili bila kujali idadi ya watu.
 
mimi naona hakuna kosa lolote hapo...hata hivyo kuweka mdahalo kwenye upande wa upinzani tena sio ishu...maana tushaona ni nani anaweza kuibadilisha hali chafu ya tanzania. Ila lipumba sijui hata huo u professa wake ni wa aina gani..maana kama angekuwa ni mtu mwenye uwezo angewapa hata chadema tafu..maana hapo yeye anapoteza time...ataishia tu kusema SAWA SAWAAAAA!
 
Uwe mdahalo au yawe mahojiano sidhani kama kuna jambo lolote baya as long as ule ujumbe ulitoka kufikishwa mbele ya watanzania umefika na kama suala la kuwepo kwa wagombea wengine mbona mdahalo wenyewe ulijulikana utakuwepo siku nne kabla na sidhani kama kikwete anaweza kukubali kufanya mdahalo na slaa na ndio maana anawatuma wakina kinana ambao mwisho wa siku wanaishia kusema watashinda kwa kishindo badala ya kutetea sera zao.by the way ile airtime ya masaa matatu aliyopewa dk slaa naona itakuwa imekuuma sana anywayz pole ile ni itv sio tbc
 
Whatever you call mdahalo au majadiliano. swala tunaloangalia ni vipi Dr. Slaa ameweza kufikisha ujumbe kwa ufasaha kwa wapiga kura.

Hili halina mjadala kwa sababu Dr. Slaa siyo tu ameweza kufikisha ujumbe bali pia ameweza kusambaratisha hoja nyepesi za CCM walizozitoa wakihoji ahadi zake hasa ya elimu bure mpaka kidato cha sita na katiba mpya ndani ya miaka mitano. Nadhani hii ndio sababu mtoa hoja Ndugu Maggid hakuongelea suala hili badala yake amejikita kwenye kuhoji kama ule ulikuwa mdahalo au mahojiano.
 
Mod Peleka hii mada kwenye Jukwaa la lugha, maana kumbe tunataka kujua ni nini mahojiano na ni nini mdahalo, kule kwenye Jukwaa la Lugha ndo kuna wataalamu wa Kiswahili haswaa. hii issue siyo ya kisiasa itakaaje kwenye jukwaa la siasa?

Gamba la Nyoka nakuunga mkono kwa hoja yako hii. Naona hapa tuna tatizo la lugha kujua kwanza mdahalo maana yake ni nini na kama ule ulikuwa mdahalo au siyo mdahalo. Hakuna hoja yoyote ya kisiasa ya kujadiliwa hapa. Ningemshauri mtoa hoja ajielimishe zaidi ili ajue maana ya neno mdahalo kwani itamsaidia kuelewa kama ule ulikuwa mdahalo au la.
 
u r right BUT, Dr Slaa ndie anaonekana kuwa na chance kubwa ya kuleta ukombozi. siku zimekwisha hakuna muda wa kupoteza, huu uchaguzi umesha julikana ngoma ni kikwete au Dr Slaa, sasa kama kikwete hanafyata mdahalo yanini kuleta wengine walio na 5% na siku zimebaki 6? nikukandamiza kwa Dr tuu. wagombea wengine wakauke tu time is up and they r still way behind. BIG UP ITV FOR A GREAT BROADCAST
All in all sisi kama wapiganaji tusha jua nani ni mshindani wa ukweli na nani ni mvurugani wa wengine wakati Chadema inapigania kuikomboa Tanzania CUF na CCM lao moja baada ya muafaka wa Zanzibar walikubaliana kubebana Bara na Zanzibar ndio maana wenye akili wamesha liona hilo kazi kubwa aliyopewa Lipumba ni kupunguza kura za Upinzani ili kuipa nguvu CCM Bara.ole wenu CUF siku zenu ninahesabika kuwepo bara.
 
Ndugu Zangu,
Jana tumesikiliza mdahalo, au labda mazungumzo au mahojiano kati ya Dr Slaa ( CHADEMA) na Rosemary Mwakitwange. Mahojiano yaliyoruhusu wengine kuchangia kwa njia ya simu pia.
Tunawapongeza walioshiriki kufanya jitihada zile. Ilitoa fursa kwa sisi wapiga kura kumsikiliza Dr Slaa. Hata hivyo, pungufu kubwa kabisa lililoonekana ni namna waandaaji walivyoandaa mdahalo wa upande mmoja bila kuwashirikisha wagombea wengine wa Urais waliopitishwa na NEC. Maana, ni vema pia tukatofautisha maana ya mdahalo na mahojiano. Kama yale ya jana yalikuwa ni mahojiano tu, hakuna tatizo kwa mgombea mmoja tu kuhojiwa. Lakini kama unaitwa mdahalo, basi, tujadili maana ya mdahalo.

Kama ni mdahalo, basi, ingekuwa ni vema na busara kwa wagombea wengine wa Urais kushiriki. Bila shaka, wagombea wengine nao wana haki za msingi za kupewa nafasi ya kuelezea sera zao na kujibu maswali ya wapiga kura. Hata kama chama tawala, CCM kimeweka wazi kuwa mgombea wao hatashiriki mdahalo, lakini hatujasikia vyama vingine vitoa misimamo kama hiyo.

Wengi wetu tungependa kuona wagombea wengine wa Urais nao wakialikwa, hivyo basi, kupewa fursa ya kuelezea sera za vyama vyao na kuulizwa maswali. Kungetoa fursa ya wagombea hao kushindana kwa hoja pia. Labda kama kuna maelezo ya kuwa wagombea hao walialikwa lakini hawakuitikia mwaliko wa kwenda studioni. Au kuwa gharama za muda wa kurusha hewani mdahalo ziligharamiwa na chama cha mgombea aliyefika kwenye mdahalo/mahojiano. Kama sivyo, basi, waandaaji watakuwa hawakuwatendea haki wagombea na wapiga kura kwa ujumla wao.

Maana, tukianza sasa kujenga tabia ya kubagua wagombea itakuwa ni jambo la hatari sana. Ikumbukwe, tangu Uchaguzi Mkuu wa 1995, tulianza kujenga misingi mizuri ya wagombea kupewa fursa sawa. Kwenye uchaguzi wa mwaka 1995 wagombea wote wa Urais walialikwa kwenye mdahalo uliofanyika kwenye iliyokuwa Kilimanjaro Hotel. Kama inavyoonekana pichani, kulikuwa na Profesa Lipumba, Augustino Mrema, Benjamin Mkapa na Bwana Cheyo. Historia ni mwalimu mzuri. Tujifunze.

Nijuavyo mimi, initially organisers walitaka kuwashirikisha wagombea watatu - Kikwete, Dk Slaa na Prof. Lipumba. Badala yake ikaamuliwa kwamba ashiriki mgombea mmoja mmoja. Wameanza na Dk Slaa, atafuata Prof. Lipumba na mwisho Kikwete kama hatimaye ataondoa woga na kukubali kushiriki. Ila taarifa kutoka kwa organisers zinasema CCM wanahaha kuhakikisha kwamba mahojiano na Prof. Lipumba hayafanyiki ili wasiendelee kuwekwa uchi katika wiki hii ya mwisho kuelekea Oktoba 31. Wakati huo huo, taarifa zinasema Kikwete amekataa katakata kutokea kwenye luninga na kujibu maswali.
 
Ndio, kwani tatizo lilikuwa nini kutowakutanisha wagombea wote pamoja. Mbona Zanzibar ilikuwa hivyo ingawa alihudhuria mmoja tu. Mwaka 1995 Baregu alikuwa mshauri wa Mrema na alikuwepo kwenye mdahalo wa akina Mrema, Mkapa, Lipumba na Cheyo. Baregu ni meneja wa Kampeni za Slaa mwaka huu.
 
Great Thinkers.

This should not be an issue. Tujali zaidi alichokiongea Dr. Slaa kwa sababu kama ni mdahalo au ni mahojiano, Dr. angetumia ilani ya uchaguzi ile ile. Kwa maana nyingine, angesema maneno yale yale. Inawezekana kabisa kuwa waandaaji walikosea kuuita mdahalo, so what? It couldn't have changed anything. Kwamba Professor au fulani hakuitwa, hatujui. Labda waliitwa lakini wakatoa udhuru kwa sababu ya kubanwa na ratiba zao za kampeni. Vilevile, labda waandaaji hawakutaka kuwaita kutokana na matakwa yao au ya sponsor wao, au Professor na wengine nao wataitwa kila mmoja kwa wakati wake.

Mie nilifurahia 'maongezi' ya Dr. Slaa.
 
kaka majid,lakini si nimesikia kwamba wagombea wengine wataitwa pia ili kumwaga sera zao,manake ule sio mdahalo ki ukweli,lakin fursa nzuri kwa wagombea kusikika watatufanyia nini, jana mwanawane dr. Waukweli katema vitu mpaka nikawa naona muda hautoshi,acha tumsikie dr. Kinana nae atawaambia nini wananchi ikifika zamu yake.
dr. Slaa aliongea kama mgombea wa urais kupita chadema. Huyu kinana akiongea atakuwa mgombea kupitia chama gani vile????. Mimi sitaki kumwona kabisaa tena akome kabisaa
 
Ndugu Zangu,
Jana tumesikiliza mdahalo, au labda mazungumzo au mahojiano kati ya Dr Slaa ( CHADEMA) na Rosemary Mwakitwange. Mahojiano yaliyoruhusu wengine kuchangia kwa njia ya simu pia.
Tunawapongeza walioshiriki kufanya jitihada zile. Ilitoa fursa kwa sisi wapiga kura kumsikiliza Dr Slaa. Hata hivyo, pungufu kubwa kabisa lililoonekana ni namna waandaaji walivyoandaa mdahalo wa upande mmoja bila kuwashirikisha wagombea wengine wa Urais waliopitishwa na NEC. Maana, ni vema pia tukatofautisha maana ya mdahalo na mahojiano. Kama yale ya jana yalikuwa ni mahojiano tu, hakuna tatizo kwa mgombea mmoja tu kuhojiwa. Lakini kama unaitwa mdahalo, basi, tujadili maana ya mdahalo.

Kama ni mdahalo, basi, ingekuwa ni vema na busara kwa wagombea wengine wa Urais kushiriki. Bila shaka, wagombea wengine nao wana haki za msingi za kupewa nafasi ya kuelezea sera zao na kujibu maswali ya wapiga kura. Hata kama chama tawala, CCM kimeweka wazi kuwa mgombea wao hatashiriki mdahalo, lakini hatujasikia vyama vingine vitoa misimamo kama hiyo.

Wengi wetu tungependa kuona wagombea wengine wa Urais nao wakialikwa, hivyo basi, kupewa fursa ya kuelezea sera za vyama vyao na kuulizwa maswali. Kungetoa fursa ya wagombea hao kushindana kwa hoja pia. Labda kama kuna maelezo ya kuwa wagombea hao walialikwa lakini hawakuitikia mwaliko wa kwenda studioni. Au kuwa gharama za muda wa kurusha hewani mdahalo ziligharamiwa na chama cha mgombea aliyefika kwenye mdahalo/mahojiano. Kama sivyo, basi, waandaaji watakuwa hawakuwatendea haki wagombea na wapiga kura kwa ujumla wao.

Maana, tukianza sasa kujenga tabia ya kubagua wagombea itakuwa ni jambo la hatari sana. Ikumbukwe, tangu Uchaguzi Mkuu wa 1995, tulianza kujenga misingi mizuri ya wagombea kupewa fursa sawa. Kwenye uchaguzi wa mwaka 1995 wagombea wote wa Urais walialikwa kwenye mdahalo uliofanyika kwenye iliyokuwa Kilimanjaro Hotel. Kama inavyoonekana pichani, kulikuwa na Profesa Lipumba, Augustino Mrema, Benjamin Mkapa na Bwana Cheyo. Historia ni mwalimu mzuri. Tujifunze.

Maggid,
Iringa, Jumapili, Oktoba, 24, 2010

Bwana MAJIDI,
Mimi nadhani kwanza ungerekebisha title ya thread yako bila kumtaja 'mgombea' wako Prof Lipumba.
Halafu je kama hao wengine hawakuhitaji kusiriki huo mdahalo walazimishwe? Vipi kama wao nao wameamua kuwa wafuasi wa Dr Slaa(ukiacha CCM ambao wameingia mitini anyway) na hivyo kuamua kushiriki kusikiliza badala ya kupambana nae? Au labda kampeni zimewabana wanaona hakuna umuhimu wa kushiriki? Sasa kama Dr Slaa ameona anayo nafasi basi asishiriki kwa kuwa Majidi et al hawataki iwe hivyo?
Tumeshajifunza
 
Maggid, unaonaje sasa tuzinguzumzia kilichonenwa humo katika hayo 'mahojiano' ambayo kikwete amekataa kuhudhiria na kusababishwa usiuite mdahalo. Hivi katika mantiki ya kawaida kwa kipindi hiki, mpenda maendeleo unataka kujua kuwa ule ni mdahalo au la? Yaani fikra zako ndo ziishie hapo kweli? Kwanini sasa usianze kuzungumzia kilichosemwa?

Wkati mwengine nafika wakati wa kuamini kuwa ukileta hoja humu, zingine wala hazina interest ya taifa kwa sasa then ili mradi watu wakae wachambuane tuuuu. Hivi sasa tunajadili kama ule ulikuwa mdahao au la? C'mon u people

Spot on RayB.

Anachojaribu kukifanya Maggid ni kuwatoa watu kwenye contents ili wajadili meaning ya maneno (rubbish). Nakubaliana na wewe kuwa lets talk about what was said na sio whether ni mjadala au mahojiano. Jamani msikubali awatoe kwenye nondo za Dr. Slaa, alikuwa anatoa shule kwa watanzania on Saturday bila chenga wala mikwaruzo

The good thing is wengi tumemuelewa.
 
Back
Top Bottom