Mchungaji Gwajima na tabiri zake: 'Tanzania Mpya' inakuja

Hivi akisema siyo muunini wa ccm zengwe litaanza nara aondoke ktk eneo, vifaa vya dini havina ushuru ni njia ya kulipa fadhira. Haipendezi kiongozi wa dini kuwa na chama cha siasa anatukwaza waumini. Bora iwe siri yake je! Atatendaje haki ktk kutolea maamuzi kauli za serikali ikikosea wakati ni mwanachama hata akitoa maoni yake yatakuwa ya kisiasa tu, ni mtizamo tu.

Siasa bila dini ni uendawazimu'

Na Lilian Nyenza


Kanisa halitaacha kutoa mwongozo kwa watu wake hata kwa mambo ya kisiasa ukiwamo uchaguzi kwa kuwa, siasa bila dini ni sawa na uendawazimu.



Aidha, imedaiwa kuwa tabia ya kuwalaghai vijana kuwa ni taifa la kesho, ndiyo inayowadumaza kiakili na kuwafanya watumiwe na wanasiasa kufanya fujo, badala ya kujitokeza kuongoza kwa kufuata taratibu za nchi.



Mkurugenzi wa chama cha kifamilia cha Undugu Association Tanzania, Padri Baptiste Mapunda, alitoa kauli hiyo katika sherehe za kuuaga mwaka 2004 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2005, zilizofanyika katika ukumbi wa Parokia ya Mt. Yosefu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.



Mkurugenzi huyo wa UNDUGU ASSOCIATION TANZANIA alisema kuwa, Tanzania imeanza kuonesha dalili mbaya za machafuko kutokana na baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa kuweka mbele ubinafsi.

"Tukikaa kimya huku mambo yanaharibika katika jamii; eti tuwaachie wanasiasa wafanye watakavyo, tutakuwa hatutendi wajibu wetu na hivyo, Kanisa halitaacha kusema ukweli kwa maslahi ya umma hata kama unamkera mtu. Hii ni kwa kuwa tunajua wazi kuwa siasa bila dini, ni uendawazimu ambao mtu hajui akifanyacho kwa kuwa akili yake haijatimia kiroho." alisema.


Aliitaka jamiii ya Kitanzania ijifunze thamani ya amani na siasa safi kutokana na hali ya amani na usalama katika nchi jirani za Rwanda na Burundi ambayo ni hatari na inasikitisha.


Alisema vita na mauaji yanayoendelea katika nchi hizo, yanasababishwa na uroho wa madaraka wa watu wachache ambao hawajali utu wa wengine.

Aliongeza kuwa, "Siku zote tunapaswa kukumbuka kuwa, amani na mapendo ambayo Mungu ametujalia, tunapaswa kuyaenzi sisi sote kwa kuwa siasa bila dini, ni sawa na uendawazimu."


Padri Mapunda aliiasa jamii kuendelea kumuomba Mungu ili azidi kuwajalia amani,upendo na utulivu uliopo sasa, kuwa uwepo hata baada ya Uchaguzi Mkuu kupita.

Amewataka Waamini kuwaombea viongozi wanyanyasaji kama Herode, wabadilike na hivyo, kuongoza nchi kwa haki na akawasihi Watanzania kuyashinda maovu kwa kutenda yaliyo mema.



Hata hivyo, Padri Mapunda amewatahadharisha vijana kujiepusha kutumiwa na baadhi ya viongozi wa siasa, kwa nia ya kufanya fujo katika uchaguzi.

"Vijana mara nyingi wamekuwa wepesi wa kurubuniwa na vijizawadi vidogo vidogo, ili wafanye kile wanachokitaka wanasiasa wabinafsi. Sasa mimi nasema mkae chini na mlitafakari hilo kwa makini. Mtakao angamia ni ninyi na si wao," alitahadharisha.



Alisema vijana ni Taifa la leo na Taifa bila vijana limekufa, hivyo aliwasihi kuwaheshimu wazazi na walezi ili wapate kuishi maisha marefu na yenye heri duniani, kama walivyojaliwa kuuona mwaka huu mpya.



Naye Mwenyekiti wa Umoja huo, Bw. Benjamini Komba alisema, lengo la Shirika la Undugu, ni kuiunganisha jamii, ikiwa ni pamoja na kuimarisha Ukristo katika kupata hamasa katika kazi ya umisionari, ili ijengeke roho ya umisionari wa kweli nchini Tanzania.



Bw. Komba alisema kuwa, Shirika limekuwa na mchango mkubwa kwa jamii, kwa kuwa ni chombo cha kuelimisha jamii na kuendeleza mawasiliano na wamisionari wa Afrika ambao wapo ndani na nje ya nchi kwa lengo la kusukuma mbele kurudumu la Injili katika Taifa hili.



Umoja huo haujishughulishi na mambo ya siasa na hauna ubaguzi wa dini, rangi, imani wala itikadi.


Katika sherehe hizo, Wanaundugu na watu wengine walialikwa na kuhudhuria pamoja na familia zao.
 
CCM Bana

Wamekodisha Vifaa Kanisani Halafu Wakavitumia Kuwatukana Uamsho. Astakafilulah
 
Huyu Gwajima atakuwa na damu ya Kikenya manake huko Kenya ndio siasa zinatamalaki makanisani. Nimekuwa nikisikia viongozi wa kisiasa hasa wa CCM wakikaribishwa huko kanisani kwake na kutoa maneno ya kisiasa wakati wa Ibada. Nimewahi kuwasikia makamanda dhidi ya ufisadi, nikamsikia Nape na juzi ilikuwa zamu ya Sumaye sijui jumapili hii ilikuwa zamu ya nani. Watu si waende wasali kama tunavyozoea kwenye makanisa mengine. Manake tunaweza kuanza kusikia wanasiasa wanapewa nafasi wakati wa swala misikitini; mwisho itakuwa vurugu tu. Gwajima haitakii mema nchi hii. Hivi ana tofauti gani na Kakobe ama Mwingira au Mzee wa Upako?
 
Hili linajulikana kwamba ccm siku zake zinahesabika, kizuri ambacho na msifu ni kati ya wanaccm wachache wanao ujua ukweli huu kwamba ccm basi
 
kwanini asiwe yeye wa kwanza kutoka na anaona ufahari gani kujiita eti mwa ccm? uku ndo kujipendekeza CCM wanamavyombo chungu mzima ata mwaka 2010 walinunua system mpya za music na matangazo kila mkoa asitudandanye huyu ccm ni taasisi kubwa huyu kajipendekeza kwa serikali ya magamba kwani nae ni mcheza dili chafu anaweza kufilisiwa anytime akiwa against nao....meli ikiwa inazama utawashauri vipi wenzako wajiokoe na wewe ufe km sio unafiki?
 
Hii ni saa ya Ufufuo na Uzima. Mmewafanya watu kuwa misukule kwa miaka 50. Sasa nyota zao zimerudi. Tanzania mpya inakuja. Neno la hekima sasa litoke M4C.
 
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Kawe, Mch.Josephat Gwajima amesema Tanzania mpya yenye matumaini inakuja.

Akihubiri Kanisani hapo leo alisema ingawa yeye ni mwana CCM na vyombo vyote vilivyotumika kwenye mkutano wa ccm Jangwani jana vilitoka Kanisani kwake, alisema chama cha siasa cha ccm kipo katika wakati mgumu na kimepoteza kabisa mwelekeo na uwezo wa kuongoza dola.

Amewaonya wanasiasa wanaojiona ni wasafi na bado wanang'ang'ania ccm, wajue mwisho wao kisiasa upo ukingoni, aliwaonya Mwakyembe, Sita na wanasiasa wangine kuwa hali ya ccm ilivyo sasa ni sawasawa na samaki aliye ndani ya bwawa na maji ambalo linakaribia kukauka.

"Tanzania mpya inakuja" ulikuwa ndio ujumbe wake wa leo.

Tanzania yenye uwezo wa kukomesha rushwa inakuja.

Tanzania yenye uwezo wa kujali afya za wananchi wake inakuja.

Tanzania yenye uwezo wa kukomesha wizi wa mali za uma inakuja.

Tanzania yenye uwezo wa kuwapatia vijana wake elimu bora inakuja.

Tanzania yenye uwezo wa kuwalisha wananchi wake inakuja.

Amewatakia wananchi wote afya njema, wapate kuipokea Tanzania mpya.

Tanzania mpya inakuja - AMINA.

Aaaaameeeeeen!!!!!!!!!!!
 
sipendi kuyaamini haya niliyoyasoma hapa, kumbe magamba walienda kuazima vipaza sauti kanisani?? kweli magamba ni magamba tuuu
 
R i p ccm mafuriko yanakuja yatasomba kila aina ya uchafu ndani ya nchi yetu nayo itakua safi
 
Kaona ishu za misukule hazilipi kaamia kwenye siasa: HIVI LILE ZOEZI LAKE LA KUMFUFUA AMINA CHIFUPA LILIFANIKIWA?
 
Anakiri kuwa mwanaCCM ingawa anawaonya kina Mwakyembe wasing'ang'anie huko! Yeye anahofia nini, kwa nini asianze yeye kutoka ?

wewe unadhani na yeye anatumia kamasi kama nyie magamba,yaaani aseme hayuko ccm ili mbomoe kanisa lake kuwa liko kwenye njia ya umeme au ni hifadhi ya barabara..........thubutuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Gwajima ndio mkodishaji wa vyombo vya muziki na matangazo kwaajili ya mkutano wa CCM?

HAKUKODISHA VYOMBE BALI ALIWAPA CCM bure tena akatoa angalizo kwa CCM kuwa CHADEMA wakija kuazima vyombe yeye atawapa kwa ahiyo CCM wasilalamike
 
Treni la ufufuo na uzima sasa linataka kufufua watanganyika. Kumbukeni ushirikina umezidi huko magambaz. Hii nchi ilizindikwa kuzimu. Saa ya Ufufuo na uzima imefika, Treni le ufufuo limeweka gea ya M4C, na bahati mbaya breki zimekata. CCM kaeni mkao wa Baru.
 
Back
Top Bottom