Mchungaji Gwajima na tabiri zake: 'Tanzania Mpya' inakuja

Anakiri kuwa mwanaCCM ingawa anawaonya kina Mwakyembe wasing'ang'anie huko! Yeye anahofia nini, kwa nini asianze yeye kutoka ?

Huyu ni mchungaji wa watu anapenda kutanguliza wanakondoo wake naye atfuta baada ya kuwatoa wote zizini. Tunamtakia kazi njema ya ukombozi wa Taifa hili.
 
Bila ya kuiondosha CCM madarakani hizi zitakuwa ni ndoto za alinacha
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Kawe, Mch.Josephat Gwajima amesema Tanzania mpya yenye matumaini inakuja.

Akihubiri Kanisani hapo leo alisema ingawa yeye ni mwana CCM na vyombo vyote vilivyotumika kwenye mkutano wa ccm Jangwani jana vilitoka Kanisani kwake, alisema chama cha siasa cha ccm kipo katika wakati mgumu na kimepoteza kabisa mwelekeo na uwezo wa kuongoza dola.

Amewaonya wanasiasa wanaojiona ni wasafi na bado wanang'ang'ania ccm, wajue mwisho wao kisiasa upo ukingoni, aliwaonya Mwakyembe, Sita na wanasiasa wangine kuwa hali ya ccm ilivyo sasa ni sawasawa na samaki aliye ndani ya bwawa na maji ambalo linakaribia kukauka.

"Tanzania mpya inakuja" ulikuwa ndio ujumbe wake wa leo.

Tanzania yenye uwezo wa kukomesha rushwa inakuja.

Tanzania yenye uwezo wa kujali afya za wananchi wake inakuja.

Tanzania yenye uwezo wa kukomesha wizi wa mali za uma inakuja.

Tanzania yenye uwezo wa kuwapatia vijana wake elimu bora inakuja.

Tanzania yenye uwezo wa kuwalisha wananchi wake inakuja.

Amewatakia wananchi wote afya njema, wapate kuipokea Tanzania mpya.

Tanzania mpya inakuja - AMINA.
 
Ukikalia kuti kavu watu watakuambia utaanguka nahuo sio utabiri ila nimwonekano wa hili halisi inlivyo
 
Unacheza na dhambi ya wizi, rushwa na ukandamizaji nini!!??
Mwizi aliyekubuhu huwaibia majirani zake weee...mpaka kuna siku hujikuta kajiibia yeye, yaani kaiba mali yake mwenyewe. Mali inayomilikiwa na CCM haiwezi kubaki salama...ipo hatarini kuibiwa na wezi ambao ni hao hao wana CCM wenyewe. Ni sawa na desturi ya manyang'au ya kuanza kutafunana wenyewe kwa wenyewe mzoga unapokwisha!
 
Huyo Gwakima ana tofauti gani na Sita, Mwakyembe Kama ndiye aliyetoa vifaa vya kuwaongopea Watanzania?
 
Huo ni uongo. Huyu ni mzushi na muongo. Anachosema ni cha kutunga ili kufurahisha watu. Hebu toa ushahidi zaidi.

Acheni bwana kutufanya sisi kama hatujui vitu. Watumishi wa Mungu wanautaratibu wao wa kuongelea viongozi.

Eti ametaja na majina ngoja tumuulize yeye maana na yeye yumo humu.

siamini kama jana ulikali kiti cha ngwajima na kupewa rushwa ya sh 5000!

Leo nyinyiemu yako yenye mafisadi kumbe haina vyombo mpaka mka kope kanisani! Kama asingekuwepo? Kweli mnapenda kujionesha! Kwan mkikaa chini kuna tatizo? Angalia ngwajima anatoboa siri zenu, kumbe hata kumlipa hamjamlipa! Kweli mna laana.

Najua hata posho hamjapewa.
Tambo nyingi kumbe mliaharibu utaratibu wa ibada ya ngwajima.

Aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah
 
Ina maana alikuwa amekoswa hata msitari mmoja toka Bible hadi awalishe siasa waumini wake?.
The unseen is illustrated by the seen.
 
mimi ninasikitika sana kuona kila siku watu wanazidi kumtabiria marehemu ccm kifo. It something which is impossible, keshakufa labda watabiri mazishi yake yatakuaje na si kifo chake. RIP CCM
 
CCM na matapeli ni kama pete na chanda,kwani mpaka aseme hivyo vyombo ni vyake?misifa mingine bana
 
Tunaisubiri kwa hamu kubwa sana siku hiyo Tukufu...itakuwa ni sawa na kuupata uhuru wetu kwa mara ya pili...Watanzania wengi naamini watatoa machozi mengi yaliyochanganyika na furaha na majonzi kwa kunyanyasika kwa miaka chungu nzima chini ya utawala dhalimu na wa kifisadi wa magamba ambao umeifanya nchi yetu kuwa nyuma sana kimaendeleo pamoja na utajiri mkubwa sana tuliojaliwa na Muumba wetu.
 
Well said.Tanzania mpya inakuja na ndiyo tunayosubiria.Mungu atupe afya sote hadi 2015 ili tuweze kusimika kabisa Tanzania yetu huru na watanzania wote kufaidi matunda ya nchi yetu
 
parapanda italia kila kona wakati wa ukombozi wa pili.....nafurahi kuwa miongoni mwa watu watakaokuwa wameileta Tanzania mpya.....Tanzania mpya itakuja pale ambapo watu wa mataifa watakapolisikia neno la ukombozi....nafurahi sana kuona makamanda wangu slaa, lema na wengine wakiunguruma nyikani wakitoa maelekeza ya kuyoosha mapito ya ukombozi wa pili.....wao wana pesa sisi tuna Mungu kwani Mungu awezi changamana na fisadi,mdini,,,,na mdharimu.....naiona kwa mbali nchi ya ahaadi Tanzania....Mungu tuvushe salama tuweze ifika ingawa natambua wapo wengi ambao hawataiona nchi hii lakini tone lao litakuwa wino usiofutika katika kuipata Tanzania
 
nchi yetu ndo inapoelekea ni pazur tu coz ccm wanaenda kufa huo ndio ukwel uyo ni mchungaj ananena kiroho c kimwil ccm nyie neneni kimwil t mtaona wat wa mungu wana mamlaka wamepewa
 
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Kawe, Mch.Josephat Gwajima amesema Tanzania mpya yenye matumaini inakuja.

Akihubiri Kanisani hapo leo alisema ingawa yeye ni mwana CCM na vyombo vyote vilivyotumika kwenye mkutano wa ccm Jangwani jana vilitoka Kanisani kwake, alisema chama cha siasa cha ccm kipo katika wakati mgumu na kimepoteza kabisa mwelekeo na uwezo wa kuongoza dola.

Amewaonya wanasiasa wanaojiona ni wasafi na bado wanang'ang'ania ccm, wajue mwisho wao kisiasa upo ukingoni, aliwaonya Mwakyembe, Sita na wanasiasa wangine kuwa hali ya ccm ilivyo sasa ni sawasawa na samaki aliye ndani ya bwawa na maji ambalo linakaribia kukauka.

"Tanzania mpya inakuja" ulikuwa ndio ujumbe wake wa leo.

Tanzania yenye uwezo wa kukomesha rushwa inakuja.

Tanzania yenye uwezo wa kujali afya za wananchi wake inakuja.

Tanzania yenye uwezo wa kukomesha wizi wa mali za uma inakuja.

Tanzania yenye uwezo wa kuwapatia vijana wake elimu bora inakuja.

Tanzania yenye uwezo wa kuwalisha wananchi wake inakuja.

Amewatakia wananchi wote afya njema, wapate kuipokea Tanzania mpya.

Tanzania mpya inakuja - AMINA.

watamkolimba
 
Hivi akisema siyo muunini wa ccm zengwe litaanza nara aondoke ktk eneo, vifaa vya dini havina ushuru ni njia ya kulipa fadhira. Haipendezi kiongozi wa dini kuwa na chama cha siasa anatukwaza waumini. Bora iwe siri yake je! Atatendaje haki ktk kutolea maamuzi kauli za serikali ikikosea wakati ni mwanachama hata akitoa maoni yake yatakuwa ya kisiasa tu, ni mtizamo tu.
 
Back
Top Bottom