Mchungaji Gwajima na tabiri zake: 'Tanzania Mpya' inakuja

Watu wengine hovyo kabisa, hivi kuna tofauti gani kati ya dini na siasa, Akina Ibrahimi, akina Musa na wengine hawakufanya siasa? Manabii hawkuwa wanaonya na kuwapa misaada viongozi. Someni vitabu vya Muumba. Vimejaa mambo ya haki na watu wa mwenyezi Mungu. Kwa taarifa yenu Amriza Muumba ndizo nguzo kuu za sheria na kulinda haki za raia. Uswatani ndio unataka kuwatoa viongozi wa dini katika siasa. wasikilizeni hao mpate mafanikio, ama sivyo mtalaanika.
 
Toka lini huyu pastor amekuwa mwana siasa?. Si vyema kuchanganya dini na siasa na pia si vyema kutumia majukwaa ya dini kusemea siasa.
 
Kukipiga tafu Magamba ni Bonge la Usaliti kwa Yesu Kristo Mchukia dhambi, ufisadi, rushwa, fitna, matusi etc. Na vyombo vya waumini waliojitoa kusikiliza mahubiri na kusambaza injili kutumika katika sherehe ya watu wa namna hiyo ni kuwatia NAJISI. Nasisitiza ni NAJISI.. vyombo vinunuliwe na watu safi waende wakakalie mafisadi, wala rushwa, wasema uongo, mafisadi etc??. Gwajima amekosea ...Kweli Tanzania Mpya inakuja kuwaondoa watu walaghai wa dizaini hii. Na wote tuseme AMINA.
 
Sawa tanzania mpya inakuja lakini nyinyiemu wamemlipa?
 
"Tanganyika mpya inakuja" Naongezea Msumari zaidi.

Tanganyika yenye uwezo wa kukomesha rushwa inakuja.

Tanganyika yenye uwezo wa kujali afya za wananchi wake inakuja.

Tanganyika yenye uwezo wa kukomesha wizi wa mali za uma inakuja.

Tanganyika yenye uwezo wa kuwapatia vijana wake elimu bora inakuja.

Tanganyika yenye uwezo wa kuwalisha wananchi wake inakuja.

Amewatakia wananchi wote afya njema, wapate kuipokea Tanganyika mpya ndani ya Jamuhuri ya Muungano.

Tanzania mpya inakuja - AMINA.
 
Kwa wale mnaomfahamu mchungaji Gwajima mtakubaliana nami kuwa ni moja ya wachungaji wenye upako wa ajabu Tanzania na wanaozungumza mambo yaliyofunuliwa kwao na Mungu.

Katika mahubiri yake ya Jumapili na jana jioni alisema kwamba amefunuliwa kuwa Sitta na Mwakyembe kwakuwa ni watu waadilifu watashindwa ku-survive ndani ya CCM maana watakuwa wanachukiwa sana na kuwekewa mizengwe na hivyo watajiunga CHADEMA kabla ya uchaguzi mkuu 2015. Pia alitabiri CCM inakwenda kuanguka na utawala utakaojali maslahi ya nchi kuundwa.

Natamani mwaka 2015 ufike haraha ili tushuhudie unabii ukitimia! Ili ukubaliane na Mchungaji kuwa CCM inakwenda kuanguka, angalia kadi za CHADEMA zinavyotafutwa kama dhahabu mitaani. Kila mtu anaulizia kadi zinapatikana wapi, maji yamebadili mkondo, hakuna anayevutiwa tena na CCM
 
Huyu pastor huwa anaona mbali sio kama wale wachumia tumbo wengine. Ubarikiwe pastor.

Ngoja nisubiri comment ya Tume ya katiba then ntarudi soon.
 
Hata Kakobe alisema hivi hivi enzi zile za Mrema Augustino, tuache utabiri tupige kazi jamani..
 
Mbona hili halihitaji utabiri? Mara ngapi hapa JF tumesema kuwa CCM kwishney?
 
Hakuna jambo kabla hilo,huyo kasoma alama za nyakati anajaribu kutabiri,muongo sana huyo.
 
Back
Top Bottom