Mchumba wangu huwa hataki nimpigie simu wala SmS bosi wake wa kiume akiwepo

Yisen

Member
Aug 6, 2023
6
10
Mimi na mchumba wangu tuna mahusiano ya miezi 5, anafanya kazi katika familia ya watumishi wa selikali nikimaanisha baba na mama ni wafanyakazi serikalini.

Shida ni kwamba bosi wake wa kike asipo kuwepo akawepo wa kiume huwa hataki tuchati wala kupigiana simu (Hasa usiku) , akidai hataki boss wake ajue kwamba tupo kwenye mahusiano, vilevile amekuwa akiniambia boss wake huyo amekuwa akiikagua simu yake mara kwa mara!

Wanajamvini naombeni Ushauri wenu.
 
Una umri gani mpaka uombe ushauri jambo la wazi hivi?
 
Mkuu unafichwa kama bangi !! Sio sawa ongea nae muyaweke sawa !! Na wewe usikute una tabia za kujipigisha simu mida ya kazi ! Kwanini usitenge muda mzuri wa kuongea na mtu wako !! Pia kuna watu hawajisikii vizuri kujadili mambo yao ya ndani kama mahusiano na mafanikio au changamoto wanazopitia !!

Na muache kuogopa kuchapiwa hakuna last seen huko !!
 
Back
Top Bottom