Mchumba wangu ana matatitizo ya kizazi hawezi kuzaa, kumuacha namuonea huruma, nifanyeje?

mahwela

Member
Aug 18, 2011
5
2
Jamani naomba ushauri,

Mimi nina mchumba wangu ambae naishi nae lakini hatujafunga nae ndoa, huu ni mwaka wa 3, hajapata mimba na baada ya kwenda hospitali amegundlika kuwa ana matatizo na hawezi kuzaa! Kumuacha namuonea huruma kwani si kosa lake, nifanye nini?

Ushauri, matusi no plz!
 
Pole sana, ishi nae usimwache ila baadae mtaongelea swala la mtoto ukimwacha utakua unamwonea
 
Fanya kile moyo wako umeridhia. Usiendeshwe na huruma.
Dunia ya leo sio ya huruma tena.
 
miaka mitatu unagegeda 24hrs bila ndoa mkuu hyo mkeo hakuna namna nyingine ya kumuacha .awe anazaa au hazai ila sio tija.
 
Pole kwa changamoto... Hakuna kinachoshindikana. Angalia hio video hapo na nyingine then ukiona cha kukufaa nirudie (come back to me).

kwenda hospitali amegundlika kuwa ana matatizo na hawezi kuzaa! Kumuacha namuonea huruma kwani si kosa lake, nifanye nini?
 
Last edited by a moderator:
Pole sana . Usimwache watoto ni matokeo tu . Angalia furaha yako na watoto mnaweza mkawapata kunanjia nyingi sasa hivi elimu imeongezeka na maarifa nayo yamekua . Watoto ni wazuri but mungu ndie anapanga!
 
Huyo ni mkeo tayari
kwa kushi naye muda wote huo!!?
Hili tatizo ni dogo sana, kama utaelewa watoto wanatoka wapi....
Watoto ni zawadi toka kwa Mungu.
Kama hujapewa zawadi utalalamika?

Na wewe pamoja na mkeo ni walezi tu.
 
Lengo lako la ndoa ni nini????? (Kwa nini wataka kuoa (ingawa najua huyo ni mchumba))

Pia tatizo ni nini? La uoelekea kutokuzaa???? Maana maratizo mengine yanatatulika hata kwa ivf etc etc
 
mbona kama story katoa nusu halafu anataka ushauri usio na mipaka?siyo kosa lake kutozaa ni kosa la nani??ni nani alisababisha hayo??
 
Jamani naomba ushauri,

Mimi nina mchumba wangu ambae naishi nae lakini hatujafunga nae ndoa, huu ni mwaka wa 3, hajapata mimba na baada ya kwenda hospitali amegundlika kuwa ana matatizo na hawezi kuzaa! Kumuacha namuonea huruma kwani si kosa lake, nifanye nini?

Ushauri, matusi no plz!

Inawezekana tatizo liko humo nilimopigia mstari.
Hebu kamilisha taratibu halali za kukaa na mwanamke kisha ujaribu uone.
Matatizo mengine hutatuliwa unapoamua kupita kwenye mistari minyoofu.
Kawaombe rehema wazazi kwanza kisha muendelee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom