Mchumba wangu ana matatitizo ya kizazi hawezi kuzaa, kumuacha namuonea huruma, nifanyeje?

Kuishi bila kyfunga ndoa ni dhambi Mbele za Mungu coz hapo Mnafanya uzinzi.. Pengine dhambi hii ndio inafunga Asipate Mtoto haijalishi report ya Doctor imesemaje.. Tubuni na Msizini tena Fungeni/barikini Ndoa.. Mtoto Atakuja kwa wkt sahihi na Mazngra sahihi. Kwaoneni pia Watumishi Wa Mungu kwa Msaada Zaidi.
 
Umekaa naye miaka 3, huyo tayari mkeo.
Ukimwacha unataka nani amchukue? Upendo huwa hauletwi na watoto.
Kama ungekuwa wewe huwezi kumpa mimba, je angekuacha ungejisikiaje?
 
Mkuu kwanza pole,alafu ningekuomba husimame kwenye maombi zaidi,mwenyezi Mungu ni mwenye heri na anaweza kila kitu ni wewe tu kuwa na imani naye.Pili nakuomba umuoe na mungu utaona maajabu yatatokea.Utapata watoto wazuri na mtakuwa na furaha na amani kwenye nyumba yenu.Ninaomba Mungu wa yakobo,Mungu wa Ibrahim asimamamie hili tatizo ambalo ni dogo sana,naomba katika jina la bwana yesu kristu wa nazareth aliye hai.tuwasiliane mkuu.
 
Imani yako msingi wako. Mtangulize MUNGU watafute wataalamu waeleze tatizo lake
 
Utaishije na mchumba jamaniii unatakiwa uishi na mke apo umeshabugi unaishi na msichana miaka 3 halaf bado ni mchumba?
 
mahwela

Ishu si kumuhurumia,ishu ni kujua kwamba kuzaa au kutozaa ni mipango ya Mungu.Kama hajapangiwa kuzaa sio ticket ya wew kumuacha
 
Last edited by a moderator:
Pole ndugu mm nawiwa kukushaur kwa kufuata maandiko ya kidini, so unahiyari niambie ww u dini gani??
 
Kuishi bila kyfunga ndoa ni dhambi Mbele za Mungu coz hapo Mnafanya uzinzi.. Pengine dhambi hii ndio inafunga Asipate Mtoto haijalishi report ya Doctor imesemaje.. Tubuni na Msizini tena Fungeni/barikini Ndoa.. Mtoto Atakuja kwa wkt sahihi na Mazngra sahihi. Kwaoneni pia Watumishi Wa Mungu kwa Msaada Zaidi.

Washauri waboreshe ndoa tu sio kuwaambia ni dhambi eti ndio maana hawapati mtoto.Mwogope Mungu coz kwan wangapi walozaa bila ndoa leo Mungu kawaita na wanamtumikia?
 
Washauri waboreshe ndoa tu sio kuwaambia ni dhambi eti ndio maana hawapati mtoto.Mwogope Mungu coz kwan wangapi walozaa bila ndoa leo Mungu kawaita na wanamtumikia?

Wewe ndio umuogope Mungu..Mimi si Afiki hiyo dhambi.. Ya Uzinzi Maandiko yanesema huo ni Uzinzi na ni dhambi sijui kwako labda imani yako inasema sio Uzinzi kulala pamoja bila ndoa au sio dhambi.. Sijasema hyo ndio Sababu pekee japo in Moja ya sababu.. Ila nimesema pengine inaweza ikawasababu kuu Wakifuatilia kwa kina coz kuna laana au adhabu inayoambatana na Dhambi ya uzinzi hvyo wachunguze hapo pengine z a wayout au wanaweza kupata suluhisho Who knows?
Najua wapo waliopata watt kabla ya ndoa lkn kesi au chanzo cha kesi kimetofautiana pia adhabu zao zmetofautiana usicrame maisha ndugu..Ushauri wangu kwako usicrame njia moja ya kusolve matatizo yanapotokea unatafuta zaid ya njia Moja ili kuyatatua. Matatizo yanaweza kufanana ila njia zakutoka kwenye hayo matatizo zikatofautiana na kila mmoja Mungu akamuokoa kwa njia yake ingawaje wote tumepitia matatizo yanayofanana.
 
nendeni FOREPLAN CLINIC muonane na DR MWAKA ipo ILALA BUNGONI KATIKATI YA ILALA (BOMA/HOSPITAL) NA BUGURUNI MALAPA ni daktari mzuri sana wa magonjwa ya kina mama (uzazi) na kikubwa mumwamini MUNGU, hakuna mgumba wala tasa mbele zake!!!
 
Jamani naomba ushauri,

Mimi nina mchumba wangu ambae naishi nae lakini hatujafunga nae ndoa, huu ni mwaka wa 3, hajapata mimba na baada ya kwenda hospitali amegundlika kuwa ana matatizo na hawezi kuzaa! Kumuacha namuonea huruma kwani si kosa lake, nifanye nini?

Ushauri, matusi no plz!

Watoto ni majaliwa ndg. Mungu alimuumba Eva ili ampe KAMPANI Adamu, sio kumzalia watoto. Watoto walizaliwa baada ya wao kula tunda kimakosa. Usimwache Huyo mchumba
 
mahwela

Kwanza na kushauri haya maswala usiwambie wazazi wako kabisa!
Pili fikiri kama ndio ungekuwa wewe umepimwa na kukuta kuwa mbegu zako haziwezi kutunga mimba na mwanamke wako akwambie ana kuacha utajisikia vipi?

Mimi naamini bado unaweza kujaribu kwa madaktari tofauti tofauti kutatua ili tatizo!

Nakuomba utulie kabisa huu ni wakati mgumu sana kwako usichulue uamuzi wa kumuacha haraka hivi na ukumbuke huyu mtoto wa watu umekaa naye miaka mitatu leo hii umtupe?

Hebu jaribu kufikiri mara mbili na ukae nae umuulize mfanyeje kupata mtoto..sikiliza maoni yake kwanza!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom