zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,910
Leo ni ya pili mgao wa umeme umelikumba jiji La Daresalam na Zenji ni ya tano hakuna umeme , maji yamekatika jeneretor zinanguruma ,mifuko ya plastiki mali kwa wanaokaa magolofani hutumia kujazia haja kubwa ,na kuirusha madilishani kwa hasira.
Je huku si ndio kushindwa kwa serikali au watasingizia mtikisiko wa uchumi huko ulimwengu wa kwanza ? Maana ikiwa mtikisiko ni hivi je ukianguka ?
Labda kuna sehemu tu za Dar zilizokatika umeme, leo ya pili nipo maeneo ya Sinza, umeme kaa kazi, na ushahidi ni post kibao nilizotuma jana na leo. Maeneo mengine ya Dar sina uhakika.