Mchemsho wa TANESCO? Nchi nzima haina umeme

Wakulu;

Umeme bado haujaja mpaka sasa . . .

Ingawa hapa kwetu madongo kuinama tuna ka-Generator lakini huko nje hali inasikitisha. Kama vile enzi za Ujima zimerudi.

Na hapa ndo huwa nakumbuka Majuu . . . .
 
Singida inapata umeme toka chanzo gani?
Singida wanategemea kuanza kutumia umeme wa nguvu za upepo muda wowote katika mwaka huu. Jumla ya windmill 24 zinasimamishwa ambazo zitakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 50 za umeme, sawa na asilimia 10 za matumizi ya umeme wote wa Tz kwa siku.
 
Nimeulizia Bukoba ambako wanapata umeme toka Uganda nao kama saa 12 ulikatika na ukarudi baada ya nusu saa hivi.
Tanesco wanalo la kutuambia?
 
Kunapo kuwa na giza mkuu, si rahisi sana kulinda maeneo nyeti....

Magogoni, Upanga (JWTZ), Kijitonyama (TISS), Muhimbili, Pugu Road (RTD), Mtaa wa Ghana (Mambo ya Ndani), suites za mabalozi, hawatakiwi wategemee umeme wa TANESCO. Backup power za kwenda usiku kucha inabidi ziwepo.

Kama Invisible ameweza ku back up power kwa servers zake umeme ulipokatika nchi nzima nategemea security functionaries wa Ikulu wana backup pia. I really hope so.
 
Hii ni kampeni ya Rostam kupitia kwa Rashid kuweka shinikizo ili ionekane kuwa ni lazima mitambo ya Dowans inunuliwe kwa bei wanayotaka wao ili kuepukana na adha hii!! Hawa mafisadi si wamchezo ni Mafia babu kubwa!
 
Kama Singida watazalisha umeme kwakutumia windmills kwanini wanyalukolo pale makambaku nao pia wasizalishe umeme kwa kutumia upepo kwani kuna sehemu pale yenye upepo mkali sana mwaka mzima; hii itapunguza adha hii ya kutegemea umemme kutoka kwenye grid kubwa.
 
Si umemsikia Mchukia ufisadi anasema hata wale wanaopata umeme toka Uganda nao ulikatika so! ilikuwa ni kuzuia watu wasione taarifa za habari ili kuficha aibu/madudu yanayoendelea katika udahili wa wanafunzi pale UDSM.
 
Si umemsikia Mchukia ufisadi anasema hata wale wanaopata umeme toka Uganda nao ulikatika so! ilikuwa ni kuzuia watu wasione taarifa za habari ili kuficha aibu/madudu yanayoendelea katika udahili wa wanafunzi pale UDSM.


Kama serikali wamekuwa waoga kiasi hichi... then hali yetu mbaya sana!! Tumekwisha

BTW, siamini lakini
 
Sumbawanga haukukatika kabisa, umeme wao wanachukua Zambia. Tusubiri kusikia Ngeleja atasema nini!
 
La kujiuliza kwa sasa ni hili: Mashirika/Taasisi za UMMA kama TANESCO, DAWASA, DAWASCO, TRA, ... wanaweza kutoa huduma hizi katika mazingira haya tuliomo ya rushwa, ufisadi, kulindana, teuzi za kishikaji, uwajibikaji mdogo, hakuna uwazi katika utendaji, mkaguzi ni NAO; taasisi nyingine ya umma....
 
Hali ya umeme kwa Dar bado haiko sawa.

Nafahamishwa hata sasa hakuna umeme maeneo mengi (sina hakika kama jiji zima).
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom