Mchemsho wa TANESCO? Nchi nzima haina umeme

Magogoni, Upanga (JWTZ), Kijitonyama (TISS), Muhimbili, Pugu Road (RTD), Mtaa wa Ghana (Mambo ya Ndani), suites za mabalozi, hawatakiwi wategemee umeme wa TANESCO. Backup power za kwenda usiku kucha inabidi ziwepo.

Kama Invisible ameweza ku back up power kwa servers zake umeme ulipokatika nchi nzima nategemea security functionaries wa Ikulu wana backup pia. I really hope so.

Usije kushangaa tu kuambiwa kwamba hawana back-up power kwenye hayo maeneo nyeti, wala si ajabu kwa nchi hii!
 
Kama Singida watazalisha umeme kwakutumia windmills kwanini wanyalukolo pale makambaku nao pia wasizalishe umeme kwa kutumia upepo kwani kuna sehemu pale yenye upepo mkali sana mwaka mzima; hii itapunguza adha hii ya kutegemea umemme kutoka kwenye grid kubwa.

..............kweli aisee....hata kule kwetu Same they can go for windmills to generate power.............
 
Eheheheheheheee...typical Miafrika!! Ndivyo Ilivyo!!!

Halafu eti sijui usalama wa taifa....usalama wa taifa gani? Heheheheheheheee....Miafrika bana inachekesha sana wakati mwingine. Umeme utakatikaje nji nzima?
 
Hali ya umeme kwa Dar bado haiko sawa.

Nafahamishwa hata sasa hakuna umeme maeneo mengi (sina hakika kama jiji zima).

........kwa hiyo tutegemee hata hali ya water supply itakuwa pungufu!!......
 
........kwa hiyo tutegemee hata hali ya water supply itakuwa pungufu!!......

ahahahahahahahahaaaa....ilitakiwa uwe umeshaji-condition kutegemea rumba kali unless wewe umezaliwa kiwanja....lakini kama umezaliwa bongo sijui unachoshangaa ni nini......
 
Jamani Wahindi hawajauza generator zao pale mtaa wa kitumbini mjini kwahiyo inabidi mkanunue generator kwanza ndio umeme ukae sawa.

Any feedback kutoka TANESCO au wamekuwa mabubu kama kawaida yao, Badra Masoud anasemaje?
 
Any feedback kutoka TANESCO au wamekuwa mabubu kama kawaida yao, Badra Masoud anasemaje?
Feedback ninayoweza kukupa ni kuwa LEO Jiji limekosa umeme (katikati ya jiji kote) kutwa nzima na mpaka naandika hivi sasa naambiwa bado umeme kuwaka.

Ukweli ni kuwa kukosekana kwa nishati kwa muda mrefu kiasi hiki (zaidi ya masaa 8 sasa) ni hatari kwa maendeleo ya taifa.

Sijui nini tatizo haswa...
 
Hii balaa umeme umekatika night kali nilikua nacheki Super Bowl! Hado mida hii saa kumi na mbili usiku!! Na battery ndo inayoyoma!!!!
 
Shauri yenu, mmemshambulia Idrisa kwamba ni fisadi, sasa kaamua kulipiza. Usimshambulie aliyeshika mpini, utaipata fresh kwi kwi kwi!!!!

Wakati wengine mnafaidi giza, sisi tunafaidi snow ambayo imeanguka nchi nzima. Watu tumepata kisingizio cha kulala. London leo imekuwa Siberia
 
Lazima kwa mwendo huu mitambo ya Dowans inunulike tu!

Nchi nzima haina umeme ninapoandika dakika hii...

Kaazi kwelikweli
 
Lazima kwa mwendo huu mitambo ya Dowans inunulike tu!

Nchi nzima haina umeme ninapoandika dakika hii...

Kaazi kwelikweli

Mkuu Invisible,

Ni kweli au utani tu. Poleni sana. Mbona kuna vyanzo vingi vya umeme, iweje nchi nzima ikose umeme?
 
Ni kweli kwetu Kanjunjumele kulikuwa hakuna umeme, ndo umerudi sasa hivi dakika kama 20 tokea jana jioni.

Makamba naye yuko kwenye giza leo Kyela.
 
Lazima kwa mwendo huu mitambo ya Dowans inunulike tu!

Nchi nzima haina umeme ninapoandika dakika hii...

Kaazi kwelikweli

...Si bure, mkono wa serikali huo! wao wamekamata mpini, sie wananchi tumekamata makali...

hiyo ni kuonyeshwa, tukubali kununua mitambo ya Dowans, au tusote na umeme wa mgao!!! kaazi kweli kweili wallahi,....jana nilikuwa nazungumza na Tanzania, dah, athari za kuishi bila umeme...pump za maji hazifanyi kazi na maji hakuna, foleni barabarani bila mataa ya kuongozea magari, biashara hata ya fotokopi hakuna bila umeme, ...halafu Joto, mbu! ...Kero tupu!

Haya serikali, NUNUENI HIYO MITAMBO YA DOWANS, Tushakoma!!!!!
 
Wakati huu bado umo kwenye awamu yao,bado wana uhuru na nguvu za kufanya kile watakacho bila kujali kelele zetu.
Wakati unakuja, ambao awamu yao itakuwa historia kama ilivyo historia ya utawala wa wajerumani na ule wa waingereza.

Gharama ya kuushikilia utawala wa CCM imekuwa kubwa mno haibebeki.
Wananchi tumeshindwa kabisa kubeba gharama hiyo kwa sababu hatuna uwezo wa kuibeba.
Tumetumia damu na na sehemu ya uhai wetu kubeba gharama ya kuishikilia CCM hapo ilipo.
Tukiendelea kuibeba CCM hatutakufa sisi tu vitakufa vizazi vyetu vyote.
Kwa hiyo ni bora kutumia uhai wetu mdogo ulobakia kuimaliza CCM ili kujinusuru kama taifa na jamii ilo huru.
Ni lazima CCM ionje mauti ili kuinusuru jamii ya Tanzania na umauti kwa sabau hata tukitoa uhaiwetu Watanzania wote bado hatuwezi kulipia gharama ya kuibeba CCM.
Ni rahisi kwetu Watanzania kulipia gharama zote za kuiendesha kuzimu kuliko kulipia sehemu ya gharama ya kuibeba CCM.
 
Umeme umekatika nchi nzima. Masaa mawili sasa.

Msimlaumu Idrissa Rashid wala TANESCO, na Kikwete kama alivyokwishatwambia Comical Salva hahusiki kabisa na issue ya umeme, Richmond na Richmond. Maskini nchi yetu!!! Inafanywa kama kichwa cha mwendawazimu kila kukicha!!! :(
 
Dar nabagamoyo bado...leo balaa isije kuwandio kutukomoa ili tununue dowans?? Haya dr idrisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom