Mchango wa rais kwa CHADEMA ni kujipendekeza?

Rais Haitajiki kutoa pesa mfukoni kwake, hizo ni fedha ambazo amezipata kutoka kwenye kodi zetu,
hivyo mchango hauna tija yoyote ile, tunachokitaka kutoka kwake ni uongozi bora na imara, utakao
simamia maendeleo ya elimu tanzania.

tumempa mamlaka na nguvu kubwa sana za kutekeleza wajibu huo tunataka azifanyie kazi
Mkuu Kwahiyo unataka kusema yale mamilioni aliyoyatoa kama rambi rambi kwa familia ya yule Mchawi wa Magomeni mwembe chai ni kodi zetu? Nijibu haraka ili nijue kama niandae maandamano au la!
 
Gazeti la Mwananchi limeandika kuwa rais Kikwete ametoa mchango wa sh. mil.10 kwenye harambee iliyoandaliwa na Chadema kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu katika Jimbo la Nyamagana ambalo linawakilishwa bungeni na Ezekiel Wenje mbunge kupitia tiketi ya Chadema.

Katika harambee hiyo iliyofanyika juzi jijini Mwanza na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe, jumla ya Sh47 milioni zilikusanywa.

Wadau hii inatoa ujumbe gani toka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.

wameanza kukua kisiasa.
 
Kwa hili jamani tumpongeze..... Amechangia kwa manufaa ya taifa sio chama. Chadema tuongeze juhudi ya kufanya harambee kama hizi katika majimbo tofauti.
 
Mkuu Kwahiyo unataka kusema yale mamilioni aliyoyatoa kama rambi rambi kwa familia ya yule Mchawi wa Magomeni mwembe chai ni kodi zetu? Nijibu haraka ili nijue kama niandae maandamano au la!

Mkuu leo sikuwa na mawasiliano kabisa kutokana na tatizo la umeme, ebu nijuze huyu JK ametoa rambi rambi ya shillingi ngapi kwa familia ya huyu mchawi mfuga majini?
 
Hata RA huwa anachangia kwaya, ingawa hata huko masjid kwake haendi kuswali!
 
Watu kweli hamna wema, asingetoa mngesema anawabagua, ametoa mnasema amejipendekeza sasa kwenu jema ni lipi ? na ww umeisha sema ni RAIS, kama hivyo ndivyo, ni Rais wa watu wote bila kujali itikadi zao wakiwemo chadema ndio Rais wao

Ni bora umewaelimisha, Kikwete ni Rais bora, mlezi wa watu wote hana ubaguzi,mcheshi,mwenye huruma. wao wanataka rais wa namna gani, Tukamfufue Idd amini aje awatawale?
 
Gazeti la Mwananchi limeandika kuwa rais Kikwete ametoa mchango wa sh. mil.10 kwenye harambee iliyoandaliwa na Chadema kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu katika Jimbo la Nyamagana ambalo linawakilishwa bungeni na Ezekiel Wenje mbunge kupitia tiketi ya Chadema.

Katika harambee hiyo iliyofanyika juzi jijini Mwanza na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe, jumla ya Sh47 milioni zilikusanywa.

Wadau hii inatoa ujumbe gani toka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.

JK atakuwa amekuwa amefanya jambo bora kama tu, mchango huo hautatumika katika majukwaa ya kisiasa. Nashauri kama CCM wataanza kutumia majukwaa kuuzungumzia mchango huu, basi CDM waurudishe. Otherwise inaonesha wazi kuwa JK amegundua kuwa CDM ni wananchi na si kina Dr Slaa, hivyo yeye kama rais wa nchi na mtanzania ana haki ya kuchangia in good faith.
 
Nafikiri linapokuja suala la maendeleo kwa watanzania hatuna budi kuweka itikadi zetu pembeni. Kwenye mazuri tutamsifu na kwenye mabaya tutamsema na kumuwajibisha. Pamoja na kuchangia huo mfuko bado CHADEMA watampelekesha palipo na kasoro. Kama yeye JK alifikiri kuwa huo mchango unaweza kupunguza mashambulizi kutoka kwa CHADEMA, hapo alikuwa wrong. Lakini siamini kama hiyo ndiyo ilikuwa sababu.
 
wasiwasi wangu ni hiyo simu aliyopigiwa na zitto,..how many times do they talk??eti ni rafiki yake!!hivi sio hela ya kifisadi cdm wanapokea hiyo,..haukawii kesho kumsikia nape anasema" kama jk yupo kwenye list ya mafisadi mbona wamempigia simu kumwomba mchango"???ccm hawatabiriki lets wait...zitto naye controversial!!leo ataandamana ruvuma kesho anampigia simu jk...mmh!!
 
na Sitta Tumma, Mwanza

RAIS Jakaya Kikwete ametoa sh milioni 10 kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa Maendeleo ya Elimu katika Jimbo Nyamagana jijini Mwanza.

Hatua ya Rais Kikwete kutoa kitita hicho cha fedha, imeonyesha kufungua milango kwa wanasiasa wengine kushiriki kuchangia maendeleo ya wananchi bila kujali itikadi zao za kisiasa.

Rais Kikwete alichangia fedha hizo juzi usiku, wakati wa harambee ya ufunguzi wa mfuko huo katika jimbo hilo linaloongozwa na mbunge Ezekiel Wenje (CHADEMA), iliyofanyika jijini hapa.

Harambee hiyo ambayo iliongozwa na mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (akiwa ni mgeni rasmi) ilifanikiwa kupata zaidi ya sh milioni 50 huku Zitto akiipiga mnada saa yake na kununuliwa kwa sh milioni 1.7.

Mbali na Rais Kikwete kutoa mchango huo, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa alichangia sh milioni tano, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, sh milioni mbili, Zitto sh milioni moja na Wenje milioni tatu.
Baadhi ya wabunge wengine wa CHADEMA waliotuma michango yao kwa kupitia kwa mgeni rasmi, Zitto ni pamoja na Gres Kiwelu sh 300,000, Muhonga Saidi sh 200,000, Rayah Ibrahim sh 200,000, na wengine wengi, huku Naibu Meya wa jiji la Mwanza, Charles Chinchibela (CHADEMA), akichangia sh 200,000.
Baadhi ya wafanyabiashara wa jijini Mwanza waliochangia kufanikisha harambee hiyo ni pamoja na mfanyabiashara maarufu Joseph Madirisha ambaye alitoa sh milioni moja pamoja na wengine kadhaa waliochangia kupitia mtandao wa Facebook ya Zitto ambao walitoa euro 1,000 na sh 600,000. Akizungumza katika harambee hiyo ya kuchangia Mfuko wa Maendeleo ya Elimu jimbo la Nyamagana, Zitto aliwataka wanasiasa kuacha hulka ya kususia shughuli za maendeleo, kwani wakati huu si wa siasa bali ni kupigania maendeleo ya wananchi wote kwa ujumla.
 
Kuna jamaa mmoja ali comment kuwa J.K. anaikubali CHADEMA moyoni lakini anashindwa kusema wazi wazi. Nimekubaliana naye maana naona sasa Bwana mkubwa ameshindwa kuvumilia sasa ameanza kuonyesha kwa matendo. Huu ndio uungwa mtu akifanya mazuri hata awe anatoka chama gani CCM msiwe na hofu kuiga. Mkuu wenu ameonyesha njia natumaini mtafuata nyao. Hongera J.K.
 
Sio kitu cha ajabu nampongeza rais kikwete kwa uamuzi huo maana yeye ni rais wa tanzania na wakazi wa nyamagana ni watanzania licha ya kwamba jimbo linaongozwa na chadema. Natumaini mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na RAS nao watachangia vilevile ili kufuata mfann wa bosi wao.
 
Gazeti la Mwananchi limeandika kuwa rais Kikwete ametoa mchango wa sh. mil.10 kwenye harambee iliyoandaliwa na Chadema kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu katika Jimbo la Nyamagana ambalo linawakilishwa bungeni na Ezekiel Wenje mbunge kupitia tiketi ya Chadema.

Katika harambee hiyo iliyofanyika juzi jijini Mwanza na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zitto Kabwe, jumla ya Sh47 milioni zilikusanywa.

Wadau hii inatoa ujumbe gani toka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.

Somo hapa ni kwamba... mkuu wa kaya amekubali kuwa cdm haishikiki na amekubaliana na maamuzi sahihi ya wananchi!!!
 
Back
Top Bottom