EWGM's
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 1,521
- 2,109
Ahsante mkuu nimekuelewa!
Lakini katika kuandika bankable business plan,baadhi ya vipengele vinakuwa ndani ya title moja,kwa mfano; marketing plan...hapa kama nilivyoeleza mwanzo,kuna vpengele viko katika title hii. Pia business description ni title ambayo utaandika jina la biashara,sehemu ilipo,bidhaa,umiliki,aina ya biashara.
Kumbe basi tunashauri,unapoandika plan ni vizuri ukaweka title kama zingine ulizozitaja,mfano financial plan....hii ni title inayojitegemea!
Hebu twende taratibu,tutafika tu na nakaribisha michango na maswali pia
Nimekupata mkuu vizuri mkuu!
Pia kwenye Market Plan, kwa uzoefu wangu sidhani kama a banker atakuwa na shauku ya kutaka kujua 2.1 nadhani hii inahusu zaidi mwenye biashara siyo banker. Sababu banker anaangalia return of investment na si kingine hivyo atakuwa na shauku kuanzia 2.2 sababu hapo ndipo unanza kuonyesha vipi utadumu vipi kwenye hiyo biashara? vipi unalijua soko unalotaka kuuza bidhaa/huduma yako? je kuna uwezo wa wewe kudumu kwenye soko hilo?
Pia a banker mwelevu anaweza soma kwa umakini executive summary halafu juu juu kwenye yanayofuata na kuweka nguvu na mawazo yake kwenye financial plan isipokuwa kama biashara iko kwenye start up level, sababu business ratios zinanguvu kuliko maneno mengi kwenye vipengele vingine vya business plan.